Tigo Mungu anawaona

Mimi iko tofauti kidogo sasahivi Nikiweka vocha bila kujiunga haki ya mungu internet haifunguki hadi nijiunge sijajua kwanini hata pawe na salio lazima kwanza nijiunge ndo nipate huduma

Hiyo utakuwa uliweka setting ya kulimit matumizi ya Internent kwa kifurushi peke yake,hii huwa ni msg flan inakuletea hiyo option,ukibonyeza kukubali basi,kifurushi kikiisha,Internent haitumii airtime ya kawaida.Kama huhitaji unaweza kurest kuruhusu Internent kutumia airtime ya kawaida pindi Kifurushi kinapokwisha.
 
Nimelala na sh200 kwa ajili ya ku access bankmobile cha ajabu sijaweka setting za internet za tigo wala sijabip wala kupokea. Naamka hakuna hata shilingi? kweli? sasa imekuwa dasturi Tigo usilaze vocha ikiwa hujaungwa wanailamba. Haya sina pa kuwashtaki ila kwa njia moja au nyingine Mungu atanilipia
Kwa tigo hata kama hauna fedha unaweza access bank mobile na hasa NMB japo kwa CRDB sijui
 
Tigo wezi sana hasa internet ukiwasha 4G ukaingia instagram nusu saa 1GB inapotea
 
Mimi iko tofauti kidogo sasahivi Nikiweka vocha bila kujiunga haki ya mungu internet haifunguki hadi nijiunge sijajua kwanini hata pawe na salio lazima kwanza nijiunge ndo nipate huduma
Ukitaka ifunguke bila kujiunga kuna namna unachagua mwenyewe..kwenye menu unachagua matumizi bila bundle.
 
Mitandao ya simu ni matapeli wakubwa. Mimi nina router nilikua na salio baadae sikulikuta.. nilipotoa line nikaangalia nikakuta sms nimejiunga na kitu kinaitwa airtel games. Nikawapigia simu wakaniambia nimejiunga mwenyewe nikalumbana nao wakaiondoa na nikaona msg nimejiondoa.. nikakaa baada ya kama week nikacheki salio nikakuta limekatwa tena. Niliporudisha line kusoma sms nikakuta siku ile ile niliyoondolewa baada ya masaa kadhaa nilitumiwa ujumbe karibu umejiunga upya kwenye airtel games.
Hao airtel wana huo ujinga sana wakuunganisha watu kihuni nahuo upuuzi wao wanaouita Game club.Mitandao ya simu imekua na mambo ya ovyo ovyo sana.
 
Mie nlishaacha siku nyingi kuacha salio kuu kwenye simu. Ht sh 50 siachi

Pole sana Julaibibi. Ila wasamehe
Hii ni nzuri ila sasa wakati mwingine ni ngumu kama umejiunga kifurushi kupitia vocha za kawaida.Wao ndio wanaotakiwa wajirekebishe maana wateja tukibadilika tabia hasara ni yao wenyewe.
 
Back
Top Bottom