Tigo mnatukera

peri

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
2,579
1,164
Tunawashukuru sana TIGO kwa kudhamini blog hii ya JAMII FORUM ila tunaomba wajirekebishe kwani tumewachoka na huduma zao mpaka tunafikiria kuhama mtandao huu kama huduma zitaendelea kuwa duni na dhaifu hivyo
Haya ni mambo machache tu ambayo nayaorozesha hapa
Mosi, unampigia mtu simu unaambia haipatikanbi wakati simu iko on
Pili. simu unapiga unaambia inatumika wakati haitumiki
Tatu, unapiga simu kwa mtu inaenda kwa mtu mwingine
Nne, huduma yao ya Kununua umeme Luku, unanunua halafu kwa siku 3 hawakutumii namba za kuingiza
Tano, huduma yao ya internet kila mara inakuwa haifanyi kazi.

Haya ni machache tu ambayo nimeyaorothesha kwa watumiaji wa tigo watakuwa lazima wengi wao wameshakutana na haya matatizo.
natamani sana niandike makala kwenye magazeti au japo barua ya wasomaji lakini kwa kuwa tigo ni watangazaji wa kwenye magazeti, tv na redio hata ukiwasilisha jambo kama hili haliwezi kuripotiwa

Tigo badilikeni tutahamia mitandao mingine, mmetulaza gizani mara kibao kwa luku, mmetukosesha michongo pale tutapopigiwa simu hatupatikani, simu zetu tunashindwa hata kuingia jamii forum kwa kuwa internet mara kibao haifanyi kazi. tumewachokaaaaaaaaaa.
TIGO, SOTE NI NDUGU
 
Nasi tumewachoka watumiaji wa TIGO mnavyolalamika hapa kila kukicha,hebu search threads za TIGO hapa utaona naongelea nini.
Kuna namna kadhaa ya kutatua tatizo:
-kulizoea na kulikubali
-kulitatua
-kilikimbia
 
Naunga mkono hoja! Tigo sasa hivi wamekuwa matapeli. Wanatangaza gharama za kupiga simu kwa sekunde ni sh.1 lakini gharama halisi ni zaidi ya Sh.3 kwa sekunde Tigo kwa Tigo! Huu ni utapeli mkubwa kabisa kuwadanganya wateja. Nakubaliana na Uporoto01 kwamba dawa yao ni kuwakimbia tu nasi vinginevyo!
 
Naunga mkono hoja! Tigo sasa hivi wamekuwa matapeli. Wanatangaza gharama za kupiga simu kwa sekunde ni sh.1 lakini gharama halisi ni zaidi ya Sh.3 kwa sekunde Tigo kwa Tigo! Huu ni utapeli mkubwa kabisa kuwadanganya wateja. Nakubaliana na Uporoto01 kwamba dawa yao ni kuwakimbia tu nasi vinginevyo!

hili la viwango vya kupga cm nimelishuhudia kwa 2 weeks sasa,intaneti ndo NIMEJITO KABISA!NIPO ZEINIIIÍÌ
 
ukiona tigo haikufai achana nayo mbona mitandao mingi tu??ila na ninyi TIGO jirekebisheni la sivyo mtapoteza wateja wengi.....
 
PHP:
hili la viwango vya kupga cm nimelishuhudia kwa 2 weeks sasa,intaneti ndo NIMEJITO KABISA!NIPO ZEINIIIÍÌ
Nilidhani ni mimi tu nimekereka kumbe tuko wengi. Na kuna nyingine imezuka ukimpigia simu mtu tu simu inakata kama network haipo. Hivyo vya bei ndio usiseme. We waache tu tutawaacha kwani kabla hatujajiunga si tulikua na wengine walikua viburi wa kupunguza bei tuka sepa tukajiunga kwingine. Walivyogundua wakarekebisha. Tumerudi kiaina. Na wao kama hawasikii watasikia. Tukazane tuwaeleze kama walikua hawajui tunajua sasa tunajua.
 
Tatizo mnalalamika alafu kila siku mnao............nilipata tabu sana awali kuwahama maana kuna wengi wa karibu wanatumia tigo ila nashukuru mpaka sasa wale wa muhimu wa-5 wamesha "hamia" na sasa bado kama wa-3 tu ili wote wawe wamehamia na iwe kazi ni kwetu tu....nyambafu tigo
 
kweli bana mnaboa sana juzi kidogo nikose mpira ..haina maana kuweka pesa kwa tigo pesa maana nilitaka kurecharge account yangu dstv tigo wananiambia eti nimekosea namba kwa urefu zaidi ya mara tano hadi jamaa yangu akanitumia hela kwa voda pesa yangu ukipiga customer care hamna kitu wanakata sh 50wanakuhold dkk 10 hadi nikaamua kukata wapuuzi sana mnatufanya sisi mabwege?
 
Back
Top Bottom