tiGO mnatufukuza wateja wenu bila kujijua

tigo kwa dar ukiongeza elfu wanakupa dakika 6 bure za maongezi labda ndo wanathaminisha kwa kutoa dk
 
wanasema eti ukiongeza salio utapata mara mbili ya fedha ulizoongeza, kitu ambacho si kweli kabisa. Wanachokuongezea ni robo tu ya salio uliloongeza.
<br />
<br />

kwa hiyo ina maana ukiweka 1000 wanakupa 250 kama bonasi?
 
tigo=wa tz=wababaishaji=si wazalendo. nani kasema tz kuna good customer care?? so, mwana potezea tu.... kama ushasovu endelea na mishe mishe zingine tu..... mimi nikianza kueleza mambo nayokutana nayo kwenye biashara zangu katika baadhi ya ofisi ni aibu kwa tz. yaani, kuna siku nilitaka nimpige kibao secretary pale udsm nilieda kuchukua gamba langu la masters dah.
 
Vita ya kunguru.....nilihisi hii kitu itatokea tu,Jamaa wamepondwa kweli kama wadhamini kuruhusu Miss Tanzania ifanyike wakati tuna msiba mzito,nadhani ni kujibu mapigo tu kwani hilo tatizo la mleta Thread ni la kawaida sana hata kwenye mabenki yetu.
 
am kweli vya bei za chini gharama!! VOCHA tununue wenyewe kwa gharama zetu lakini tunarecharge zaidi ya masaa 3 bila mafanikio, ukipiga simu 'NETWORK BUZY', Ukipiga tigo customer care ndo kero tupu, simu inaita zaidi ya lisaa 1 kisha wakipokea hawana majibu yanayoeleweka.

duuu yaan kero tupu.
 
mbona hio kwangu si tatizo saana maana nimezoea ila kali ni juzi night ya saa tisa sikuwa nimeweka silence mara ikaingia sms kuangalia mtumaji nakuta 100 kumbe ni tigo wanataka sijui nifanyeje huko.....pambaf
 
tigo wameshindwa kumudu ushindani wa haki,...zaidi ni kero kwa wateja wao________muda si mrefu ntahamia airtel
 
TCRA inabidi wadhibiti viwango vya ubora wa mawasiliano, tigo kweli mnatukera wateja wenu!!
 
Toka juzi sipati tigo internet,
Mpaka nakua nje ya JF, shame on them!!
Imekuja kukubali muda huu,
Yaani bora hata wangekua wanasema, maana kidogo niipeleke kwa fundi nikijua nimeharibu setting za internet
 
me tigo naipenda sana natumia intaneti wiki ya pili sasa for free ,tigo yanifaa sana ila poleni sana ambao hamuipati vizuri jaribuni kuwapigia
 
Naandika nikiwa na uchungu sana. Mama yangu ana line ya tigo na amekua akiitumia siku zote na ameisajili. Kama siku mbili zilizopita, tukipiga simu yake imekua ikienda kwa mtu mwingine. Na huyo mtu amedai kwamba ameinunua hiyo number kutoka Tigo, ila ameshangaa kugundua kwamba ilikua ya mtu, na amekiri kupata usumbufu kwani mara nyingi amekua akipokea simu za mama.


Akadai kwamba atarudi Tigo kuwaeleza. Baadae simu ya mama ikawa haipatikani tena hewani. Kwa bahati, mama yupo hapa mjini (anaishi mkoani). Tuliamua kwenda Tigo (mlimani city) na kueleza tatizo tena baada ya kusubiri sana kwenye foleni. Walipoelezwa tatizo wakadai kwamba mama yangu atoe ID ili waweze kucheki.

Unfortunately hakua nayo, aliisahau kijijini, ila alikua na details za ile registration form. Waligoma kutoa msaada mpaka mama atoe ID. Kwa kweli imenimua kwani tatizo ni lao TIGO, kuuza number ya mtu ambayo inatumika na imesajiliwa, sasa wametusababishia usumbufu usio wa lazima.

Hivi nini maana ya ku register? Kwa nini wauze number kabla hawajacheki kama inatumika au la? Au kuna jambo ambalo sielewe? Wadau nisaidieni please.
 
Hata kama id muhim ila hapo tg wamechapia so theres no need ya ysajili what if hiyo namba ingekuwa misused? Wangemkamata yupi!
 
Ungetoa ID naamini usingelalamika hivi. Peleka ID uone km watakataa kukurekebishia. Pole kwa usumbufu.
 
Back
Top Bottom