Tigo acheni wizi

Tigo acheni wizi

Kwa nini lakini umuandikie mwenzio hivi?Kosa gani katika thread yake ambalo limekukera kiasi hiki?

hata mie nimemshangaa sana kwa kauli yake inayofanana na jina lake, #Sumu . yaani nina query yangu inayoniumiza kichwa halafu huyu mshenzy anakuja kuniongezea hasira.
 
Jana nimenunua laini ya simu ya mtandao wa tiGO, baada ya kuisajili nikatumiwa SMS ifuatayo:

Hongera! Umezawadiwa Dk 14 Tigo-Tigo, Dk 6 kwenda mitandao yote TZ, SMS 450 na MB 125 kwa kununua line ya Tigo. Tumia ndani ya masaa 24. Kwa salio piga *102*01#

Nilipopiga *102*01# nikapata ujumbe huu hapa:

Una sek 960 mitandao yote TZ, SMS 450 & 90MB hadi 12/07/2014.

KERO YANGU
Kupitia SMS hizi, mnaweza kushuhudia jinsi tiGO wanavyowatapeli wateja wao kwa kuwaahidi ahadi feki ambazo hazilingani na matangazo wanayoyatoa:

1. Mteja hudanganywa kwamba amepewa MB 125 kumbe amewekewa MB 90 tu! Huu ni wizi, uhuni na utapeli!

2. Mteja hudanganywa kwamba dk za ofa zimegawanywa, kumbe si kweli! Matokeo yake mtu akipiga simu analiwa fedha zake. tiGO acheni uti-GO wenu. Msiwafanye wateja wenu mafala kihivyo!

Watanzania mnajua sana KULALAMIKA lakini kuchukua UAMUZI ni jambo gumu sana kwenu!

Kama unaona mtandao fulani UNAKUIBIA, kinachokufanya ubaki hapo ni nini? Ni sawa na kumfungulia mlango mwizi, unamkaribisha ndani. Anachukua kila atakacho, kisha unamsindikiza nje na kumwabia, Karibu tena. Jisikie nyumbani!

Yeye anaondoka akichekelea huku akikushangaa kwa UJUHA wako!

Najua ukweli unauma lakini ukweli ndio huo!

Mnaikacha TTCL, kampuni ya nyumbani, mnaenda kwa hao wezi. Hivi mnadhani TTCL itaacha kukua bila ya ninyi wazawa kuiunga mkono? Mmeisahau ile methali ya Mdharau kwao ni Mtumwa.

Sasa umefika wakati wa kusama IMETOSHA! Tunarudi nyumbani!

Mimi nimerudi nyumbani, kwetu Moshi. Nilipadharau, lakini sasa napaona pazuri sana. Punde nitabadilisha namba na kubakia na TTCL na Zantel TU! Zantel ni kampuni iliyosajiliwa Tanzania Zanzibar kwa hiyo ni ya nyumbani vile vile. Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (ambayo, kikatiba, iko ndani ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa TANZANIA) ina hisa asilimia 49, kama sikosei, kwenye kampuni ya Zantel, ambayo jina lake halisi ni Zanzibar Telecommunications Limited. Zantel ni muungano wa herufi "Zan" na "Tel" ambazo zinatokana na maneno mawili yanayokamilisha jina halisi la kampuni hii.

Kwa taarifa yenu, Zantel na TTCL (Tanzania Telecommunications Company Limited) HAWAIBI HATA KIDOGO! Wanaosema kwamba wameibiwa, hawajaelewa vizuri huduma za kampuni hizi mbili. Tunaweza kuibadilisha taswira ya Mawasiliano ya Simu hapa nchini TUKIAMUA!

Unangoja nini kuamua kurudi nyumbani? Utawatajirisha hao mafisadi wa nchi za nje mpaka lini? Wote hao, Vodacom, Tigo na Airtel, ni wezi. Wamewaweka makuwadi wa ufisadi - mnawajua - kwenye mifuko yao, hujuma inafanyika dhidi yetu Watanzania.

Hakuna haja ya kulalamika. Tupa line yako ya Tigo, Voda na Airtel. Nunua ya Zantel na/au TTCL, ule raha! Mawasilano bwerereee! Kwa upande wa data (Internet), Zantel hawashikiki. Watu wanadai kwamba eti Zantel hawana wateja wa kutosha ndio maana wana uwezo huo. Hivi, kati ya Airtel, Vodacom na Tigo, kuna HATA MMOJA aliyewekeza kiasi cha kuweka Earth Master Satellite Station (EMSS)? Hamjui ni nini hii? Nendeni makao makuu ya Zantel, Amani, Zanzibar, mtakaribishwa kujionea wenyewe jinsi zinavyofanya kazi. Zina urefu wa takriban ghorofa tatu (TATU!) na ziko MBILI!

Waulizeni Airtel, Tigo na Vodacom kama wamewekeza kwenye EMSS? Kwa taarifa yenu, wote hao watatu wanakodisha miundombinu ya TTCL (!!!!) ili kuweza kurusha mawasiliano yao kutoka mkoa na mkoa. Mnazijua zile Microwave Towers zinaonekana kwa mbali mkisafiri kwa basi njiani? Huwa zinawekwa milimani. Basi yale ndiyo madaraja ya kurusha signal za kampuni hizo. WOTE hao wanatumia miundombinu hiyo. Halafu wanawadanganya kwamba wao wako juu zaidi ya TTCL!

Anayetaka habari zaidi nitumie PM, nitakumwagia.

ACHENI UJINGA! RUDINI NYUMBANI!

TTCL na ZANTEL sasa ni nyumbani! Wekeni kapuni line za Airtel, Vodacom na Tigo. Hakuna cha SWITCH ON wala UHURU KAMILI wala SMILE YOU ARE WITH TIGO!

Mnabisha? Line yangu ya Zantel ni 0772-949577
 
isee wamekutigo,pole sana. MwanaHaki umetiririka vyema hapo juu.. ni kwel hata enternet ya ttcl na zantel zina speed sana. alafu mbona sion matangazo/campaign za ttcl? line zao kuzipata ni mbinde pamoja na vocha.
 
Last edited by a moderator:
tigo wamechachamaa kwa wizi leo wameparula kasalio kangu shs 1500/= nikiwa teyari nimeshajiunga na extreme ambayo inakwisha saa 2 usiku wamefyeka yote bila aibu hako kabalance kangu aisee "tigo hatari sana" silaumu uongozi wote hawa ni watendaji wachache ndani ya kampuni hiyo/
 
Mi najiandaa kuwashtaki tigo kwa wizi wao uliokithiri na usio vumilika
 
tigo wamechachamaa kwa wizi leo wameparula kasalio kangu shs 1500/= nikiwa teyari nimeshajiunga na extreme ambayo inakwisha saa 2 usiku wamefyeka yote bila aibu hako kabalance kangu aisee "tigo hatari sana" silaumu uongozi wote hawa ni watendaji wachache ndani ya kampuni hiyo/

hawa makampuni ni matapeli, majizi, majambazi na mafisadi wakubwa!
 
isee wamekutigo,pole sana. MwanaHaki umetiririka vyema hapo juu.. ni kwel hata enternet ya ttcl na zantel zina speed sana. alafu mbona sion matangazo/campaign za ttcl? line zao kuzipata ni mbinde pamoja na vocha.

Wapate wapi pesa za matangazo na vocha na line wakati wewe na serikali yako mmewakacha????

Mdharau kwao.....................? Jaza mwenyewe.
 
Airtel wapuuzi kweli yan,wala sikutegemea upuuzi wa dizaini hii..Yan kupiga simu huduma kwa wateja lazima ulipie sh.60??? kweli kabisa mi nilipe sh.60 kwa tatizo linalowahusu wao na kwa manufaa ya kuboresha mtandao wao? Sijawahi kuona huduma ya namna hii tokea nmeanza kutumia simu
 
Back
Top Bottom