thanks mkuuSijawahi kupata ghadhabu kama kujadili na kuzipa uhai hoja ambazo siyo issues. Suala la Tido Mhando ni non-issue na yeye Mhando anajaribu kutafuta sympathy ya watu wakati yeye anajua kabisa kwamba mkataba wake ulikuwa for a definate period of time. Alijua kwamba kufika tarehe 15 Desemba anataikwa kuondoka, unless kun express renewal ya mkataba wake au hata express intention ya hiyo renewal. Sasa ni ajabu mtu anayejua kwamba anaondoka anaendelea kubaki akivizia kuona kama ataambiwa baki. Angekabidhi ili hata kama anarejea akabidhiwe na kuendelea. Halafu eti watu wanadai amefanya mengi. Ni sawa lakini ndiyo sababu alitafutwa mtu wa aina yake na kulipwa malipo manono kufanya hicho alichofanya (that is what he was contracted to do and that is what he was paid for).
Tido asijifanye ni indispensable. Halafu tujiulize: Huyu bwana anataka aje apumzike lini baada ya utumishi wa zaidi ya miaka 35? The guy is well in his sixties. Hakuna njama wala zengwe. Kamaliza mkataba aishie zake ili watanzania wengine waendeleze yale aliyoyaanzisha ili akumbukwe na vizazi vijavyo.
Tido asijifanye ni indispensable.
Mkuu JK ni mtu wa visasi na ktka hili hana aibu. Kumbuka alivyoingia '05, akina Mashishanga, Mangula at al walienda wapi? Ukubali ukatae huyu ndiyo JK na Visasi na vipenzi vyake ni watu wanaofikiri baada ya kusema/kutenda kama Makamba, Kombani, Shimbo na wengine wengi
Hapo kwenye red. Ni kweli kabisa huyu jamaa alijifanya mungu-mtu pale TBC akawatesa vyama vya upinzani na hasa Chadema. Sasa yamemfika watu wanamuonea huruma. Ni ajabu sana. Huyu hapaswi kuonewa huruma huyu!! Hana tofauti na wale waliomtoa kibaruani. Suala lake ni sawa na suala la majizi. Majizi yakiwa kwenye mipango ya kuiba huwa yanashirikiana sana. Lakini yakishapata nyara huwa urafiki unaisha - yanadhulumiana nyara na kuumizana hata kuuana. Mwizi mdhulumaji na mdhulumiwa hawana tofauti. Wote ni waovu. Period!..huyu si ndiyo alikuwa anawakatia mawasiliano/matangazo Chadema wakati wa mkutano wa kampeni.
..halafu akamuacha Mkapa akitamba na kutoa maneno ya ajabu-ajabu wakati wa mkutano wa CCM.
..sasa leo amefutwa kibarua tayari wananchi mnamuonea huruma.
..huyo ameshakula ameshiba na kuvimbiwa, sasa ampishe mwana CCM mwingine mwenye njaa aingie hapo.
..kutesa kwa zamu nchi hii, lakini lazima uwe CCM.
You need big help!Kimatendo mnamkubali JK ila kwenye kusema mnafanya kinyume chake na pia chuki zimewajaa.
Huyo Mwema kajiweka mwenyewe tu hapo? Sio chaguo la JK? Anatekeleza maamzi ya nani? Ndo maana wakati mwingine huwa natumia lugha ya ukali ili angalao mijitu ielewe.
JK ni muungwana sana na ndo maana uongozi wake upo tofauti sana na mtangulizi wake.
Upinzani haukua ICU kabla ya kuja JK? Kuweni wakweli otherwise shame on you.
Mkuu JK ni mtu wa visasi na ktka hili hana aibu. Kumbuka alivyoingia '05, akina Mashishanga, Mangula at al walienda wapi? Ukubali ukatae huyu ndiyo JK na Visasi na vipenzi vyake ni watu wanaofikiri baada ya kusema/kutenda kama Makamba, Kombani, Shimbo na wengine wengi
Said mwema yupo hatihati! Hakuwazuia watu kulinda kura hasa maeneo ya mijini