Tido Mhando alikosea sana

Wiyelelee

JF-Expert Member
Nov 9, 2012
1,072
1,170
Nikiwa mdau wa habari, nasikitika kusema kwamba pamoja na sifa zote alizojizolea, Bw. Tido Mhando alikosea sana kubadili jina kutoka RTD ililozoeleka sana kwenda TBC Taifa. Matokeo yake sasa, hiyo TBC Taifa imepoteza mvuto, mwelekeo na wasikilizaji wengi huko vijijini hawaipati. Wanashindwa kuitofautisha hiyo radio na FM stations!

Mi nadhani kwa mambo ya Kitaifa kama haya, siyo vizuri mtu akakurupuka tu na kuanza kubadilisha vitu ambavyo vilikuwepo hata kabla hajazaliwa. Kungelikuwa na maoni na mijadala ya Kitaifa kabla ya kufikia huo uamuzi. Napendekeza jina la RTD lirejeshwe maramoja.
 
Domhome

JF-Expert Member
Jun 28, 2010
2,493
2,000

Sidhani kama kubadili jina toka RTD kwenda TBC Taifa, ndo imeleteleza tatizo la "kutosikika", kama unavyodai wewe!!!!
 
Zogwale

JF-Expert Member
Jul 10, 2008
12,680
2,000
Tido Mhando alifanya kazi nzuri ya kufanya mageuzi RTD na TVT na kuvifanya vyombo vya mawasilioano imara kwa wananchi wote bila kufungamana na upande wowote!!! walipoona yuko neutral na akaruhusu zile debate za kuchambua kama karanga 2010 wakamtoa!!! Sasa wamemuweka anayitika YES boss na mambo si mazuri TBC kwa sasa!! Itadondoka!!
 
sifongo

JF-Expert Member
Jun 5, 2011
4,809
2,000
Nikiwa mdau wa habari, nasikitika kusema kwamba pamoja na sifa zote alizojizolea, Bw. Tido Mhando alikosea sana kubadili jina kutoka RTD ililozoeleka sana kwenda TBC Taifa. Matokeo yake sasa, hiyo TBC Taifa imepoteza mvuto, mwelekeo na wasikilizaji wengi huko vijijini hawaipati. Wanashindwa kuitofautisha hiyo radio na FM stations!

Mi nadhani kwa mambo ya Kitaifa kama haya, siyo vizuri mtu akakurupuka tu na kuanza kubadilisha vitu ambavyo vilikuwepo hata kabla hajazaliwa. Kungelikuwa na maoni na mijadala ya Kitaifa kabla ya kufikia huo uamuzi. Napendekeza jina la RTD lirejeshwe maramoja.
Hivi unajua kabla ya kuitwa Radio Tanzania ilikuwa inaitwa TBC.
 
WA-UKENYENGE

JF-Expert Member
Oct 1, 2011
2,901
1,500
Acha hivyo hivyo, hili lishirika linakera sana! kwanza watu hawataki kuambiwa wala kusikia, pale hapatakiwi siasa basi. Weka pembeni usanii wa siasa, waacheni wajiendeshe wenyewe mbona akili itawaingia! wakila hasara wanajifukuzisha kazi. Hizo pesa za mafisadi ndo zinawafanya wasahau hata miiko ya kazi zao, matokeo yake nani atangalia au kupeleka hata matangazo zaidi ya yale ya serikali na propaganda za vyama.
 
SMU

JF-Expert Member
Feb 14, 2008
8,849
2,000
..siyo vizuri mtu akakurupuka tu na kuanza kubadilisha vitu ambavyo vilikuwepo hata kabla hajazaliwa....
Tujikumbushe kidogo:

The radio station was known as Sauti ya Dar es Salaam, meaning the Voice of Dar es Salaam. In August, 1955 the British colonial government brought in new and more powerful transmitters, which covered not only Dar es Salaam but also other provinces (regions).At that time (1955) the colonial government changed the name from Sauti ya Dar es Salaam to Tanganyika Broadcasting Services (TBS). A year later on July first 1956 the station changed its name from TBS to Tanzania Broadcasting Corporation, (TBC).
Nine years later on March 17th, 1965 the National Assembly passed a bill changing the name of the broadcaster from TBC to Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD).The name was changed officially on the 1st of July, 1965 after the changes were published in the official gazette
 
kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,151
1,500
.., mkuu' mleta mada ushauri wako ni sawa kwa upande wa kubadili jina toka RTD kuwa tbc, hata mimi sikuona sababu ya kufanyahivyo, kwa mfano wa BBC tangia enzi hizo jina ni lile. Lakini kwa upande wa usikivu, yawezekana nadhani haihusiani na ubadilishaji wa jina, ni usimamizi mbovu wa viongozi wetu, unakumbuka shirika ili liliujumiwa na waziri aliyekuwa analisimamia kwa kutumia mitambo yake kukodisha shirika hilo. Pia siyo busara kuwa kila kiongozi anayeshika madaraka kubadili mifumo na taratibu nzuri tulizojiwekee: mfano, utaratibu na mfumo wa ELIMU yetu umeharibiwa sana viongozi wasio kuwa na fikra, hii inatokana na kutokuwa na utaratibu unaoeleweka wakuendesha nchi.
 
Wiyelelee

JF-Expert Member
Nov 9, 2012
1,072
1,170
Kuna ukweli kwamba pengine kutosikika hakuna uhusiano na kubadilisha jina. Lakini, sielewi kwanini kila mtu anakuwa na madaraka ya kubadili kila kitu anavyotazama yeye bila kushirikisha watu au jamii kwa mambo makubwa ya kitaifa.
 
kipimo

JF-Expert Member
Dec 30, 2010
828
0
so reverting where we had been, implies we have exhausted all the names; however the current name gives a room for expansion and thus matches with the services provided by the corporation rather than being RTD which dictates provision of redio broadcasting alone!
 
Was it not possible for instance to have TBC as a corporate name and then have some radio stations retaining their brand names like RTD? It is really confusing me.
 
SpaceBrigade

Member
Oct 24, 2012
20
0
TBC si yetu tena......wamiliki wake ni wachina wa star times, hivi sasa naona wanakula timing tu ya kuichukua mazima.
 
Songoro

JF-Expert Member
May 27, 2009
4,127
0
TBC haisikiki kwa sababu ya kubadili jina kutoka RTD kwenda TBC!!!!!!!! sasa ni wakati muafaka tuanze kupata ma Great thinkers kwa njia ya usaili badala ya U great thinker utokanao na uwezo wa kukariri Use name na password ya ku login!
 
adolay

JF-Expert Member
Dec 8, 2011
11,099

Mkuu hilo hasa ndilo swali la kujiuliza.

Hakuna ukweli hapo, uzembe wa viongozi na kukosa ubunifu na zaidi kuendekeza majungu na fitina katika kazi ndiyo sababu ya kukosa nguvu kutoka kwa watazamaji na wasikilizaji, hivyo kupelekea kufifia na kupoteza mwelekeo.

Chombo cha taifa kinatangaza habari kwa ukada wa chama, kuficha ukweli, kushindwa kukosoa wanasiasa wanaopotosha au wanaofanya makosa, kushindwa kuandaa vipindi vyenye mvuto na msisimko kwa wasikilizaji na watazamaji, kushindwa kuibua hoja zenye changamoto, mvuto wala msisimko kwa jamii hasa katika uchumi na siasa, utawala bora, elimu na afya. Ni wapuuzi tu ndio watabaki kuwa wapenzi wa habari hewa zisizo na ukweli wala tija kwa jamii.

Kwa hili la kubadili jina nadhani si vema kubadili badili majina, hata hivyo RTD - Redio Tanzania Dar es salaam, ni shirika la kitaifa na sio based only at Dar es salaam kwahiyo TBC Tanzania broadcasting co.....Ni la kitaifa zaidi ya RTD.
 
Nkyumu

JF-Expert Member
Jun 22, 2012
332
195
Kubadilisha jina haimaanishi kushindwa kupatikanika kwa TBC Taifa nchi nzima....hivyo mimi naona hakukosea
 
Bitabo

JF-Expert Member
Sep 27, 2011
1,902
1,250
Ni kweli, najua vizuri. Lakini hilo jina halikukaa sana. Wengi walilizoea RTD kuliko hiyo TBC ya zamani
kwani watu wanasikiliza au kuangalia jina la kituo au CONTENT ZA PROGRAMS za kituo?
 
MTK

JF-Expert Member
Apr 19, 2012
8,255
2,000
Nikiwa mdau wa habari, nasikitika kusema kwamba pamoja na sifa zote alizojizolea, Bw. Tido Mhando alikosea sana kubadili jina kutoka RTD ililozoeleka sana kwenda TBC Taifa. Matokeo yake sasa, hiyo TBC Taifa imepoteza mvuto, mwelekeo na wasikilizaji wengi huko vijijini hawaipati. Wanashindwa kuitofautisha hiyo radio na FM stations!

Mi nadhani kwa mambo ya Kitaifa kama haya, siyo vizuri mtu akakurupuka tu na kuanza kubadilisha vitu ambavyo vilikuwepo hata kabla hajazaliwa. Kungelikuwa na maoni na mijadala ya Kitaifa kabla ya kufikia huo uamuzi. Napendekeza jina la RTD lirejeshwe maramoja.
TBC ni kifupi cha Shirika la utangazaji la Taifa na RTD ni kifupi cha Redio Tanzania Dar-es-Salaam, nafikiri unaweza kuiona tofauti yake.
kumbuka wakati huo RTD haikuwa na kituo cha Televisheni na sasa TBC ina televisheni huwezi kuiita redio ya dar-es salaam tena??!! AMKA.
 
Wiyelelee

JF-Expert Member
Nov 9, 2012
1,072
1,170
kwani watu wanasikiliza au kuangalia jina la kituo au CONTENT ZA PROGRAMS za kituo?
Kuna kitu tunaita "brand name". watu wakizoea kitu fulani, ukibadilisha jina lazima nao watayumba kwa muda before they finally settle their minds. Sasa leo hii jina ni tata, hata content is zero!
 
Wiyelelee

JF-Expert Member
Nov 9, 2012
1,072
1,170
TBC ni kifupi cha Shirika la utangazaji la Taifa na RTD ni kifupi cha Redio Tanzania Dar-es-Salaam, nafikiri unaweza kuiona tofauti yake.
kumbuka wakati huo RTD haikuwa na kituo cha Televisheni na sasa TBC ina televisheni huwezi kuiita redio ya dar-es salaam tena??!! AMKA.
Wewe ndo umelala kabisa! Hivi hujui kwamba kuna corporate names like IPP? Na chini ya IPP kuna Guardian Ltd, chini ya Guardian Ltd kuna magazeti chungu mzima. Yawezekana tungekuwa na TBC, yes! Lakini tukabaki na majina yaliyozoeleka. Sasa wewe amka hapo ulipo!
 
Top Bottom