Tibaijuka atoa masharti mazito

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
[h=3]na Lucy Ngowi[/h]WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, amesema kuwa wizara yake haitakuwa tayari kupitisha mipango miji isiyokuwa na mtaa wenye anuani za makazi na simbo za posta.


Tibaijuka ambaye ameteuliwa kuwa Balozi maalum wa umoja wa Posta duniani katika mpango wa kimataifa wa utoaji anuani za makazi kwa kila mwananchi, alisema hayo baada ya kutangazwa kushika wadhifa huo jijini Dar es Salaam.

Alisema, moja ya faida za mfumo huo mpya wa anuani ni kutoa fursa ya kila mwananchi ya kupata anuani hiyo katika maeneo ya vijijini na ya mijini yasiyopangwa, kurahisisha utoaji wa huduma za kiuchumi na kijamii, usalama na huduma nyingine.


“Wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi ina jukumu kuu la kuhakikisha ugawaji mzuri wa ardhi kwa wananchi na hasa kuona kwamba kila mwananchi nchini anaishi katika nyumba bora,” alisema Tibaijuka na kuongeza kuwa, itakuwa ni kupoteza muda kwake katika kuhimiza nchi zingine zitekeleze mpango huo wakati kwake hakuna kinachoendelea.


Kwa upande wake, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa alisema kuwa, utekelezaji wa mfumo wa anuani za makazi na simbo za posta ni mtambuka, utekelezaji wake unahitaji ushirikiano mkubwa na wa karibu kutoka kwa wadau mbalimbali.


“Kwa mfano sera ya taifa ya posta inaelekeza uanzishwaji wa anuani za makazi na postikodi, wakati huo huo mamlaka na madaraka ya uwekaji wa majina ya mitaa na namba za nyumba, kisheria liko chini ya ofisi ya waziri mkuu, tawala za mikoa na serikali za mtaa, ambapo utekelezaji wake unafanyika katika ngazi za halmashauri,” alisema Mbarawa.


Alisema faida za anuani hizo kwa serikali ni msingi wa kutoa vitambulisho vya kitaifa kwa Watanzania, pamoja na kuongeza ufanisi katika usimamizi wa makazi ya watu.


Chanzo: Tanzania Daima
 
VIZURI kama kweli hii itawezekana... Maendeleo... Lakini ni wote wanayapenda? au baadhi ya Wananchi bado Wana DUKUDUKU MOYONI MWAO...
 
Maneno mengiiiii, wizara yake RUSHWA haina uficho, Ubabaishaji wa watendaji wa Wizara yake inaCOST watu kuvunjiwa nyumba zao.
Hao ndio Ma Profesor wa CCM wenye mipango mingi, utekelezaji wake ni ZERO
 
alisema hayo baada ya kutangazwa kushika wadhifa huo jijini Dar es Salaam
kwahiyo asingeteuliwa kuwa balozi asingefanya hayo


"Kwa mfano sera ya taifa ya posta inaelekeza uanzishwaji wa anuani za makazi na postikodi, wakati huo huo mamlaka na madaraka ya uwekaji wa majina ya mitaa na namba za nyumba, kisheria liko chini ya ofisi ya waziri mkuu, tawala za mikoa na serikali za mtaa, ambapo utekelezaji wake unafanyika katika ngazi za halmashauri," alisema Mbarawa

hapa Mbarawa amejibu ukweli wa mambo yanavyokwenda tofauti na mama tiba alivyokurupuka pale juu. Awamu hii kila mtu analopoka anapojisikia mradi tu 2015 ifike
 
nadhubutu kusema unafik wewe na mzuri rais wako watu wake wanamtumia kudhulumu ardhi za watu
Maneno mengiiiii, wizara yake RUSHWA haina uficho, Ubabaishaji wa watendaji wa Wizara yake inaCOST watu kuvunjiwa nyumba zao.
Hao ndio Ma Profesor wa CCM wenye mipango mingi, utekelezaji wake ni ZERO
 
Sasa ina maana tunataka kuvaa shati juu ya suti? Maana kwa mantiki hiyo basi ingebidi hayo yatekelezwe kwanza ndiyo vitambulisho vitolewe, Au?
 
Huu km ni mradi wa kukamua watu kwa njia ya kodi utafanikiwa maana serikali hii ya kifisadi inawaza kodi na ukandamizaji kwa wanyonge,mara utasikia eneo fulani watu wahame ili lipimwe na likishapimwa wanagawana wao mafisadi.
 
Back
Top Bottom