Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 360,000
- 828,752
Unapopata tatizo la kiafya...hamu yako ni kupona haraka, hivyo harakati na juhudi za kutafuta tiba huwa kubwa......ni katika hamu hiyo ya kutaka kutibika kwa haraka utapokea ushauri na maelekezo yoyote toka kwa matabibu unaowaamini bila kujali usahihi wa kile wanachokuambia....kidunia tunaambia nusu ya vifo duniani ni kutokana na ushauri wa tabibu.....
Kiroho pia kuna mikanganyiko yake kuanzia kwenye ardhi , makazi, miili yetu mpaka biashara na vitu tunavyomiliki...huku nako kunapata shida ya kiafya lakini kiroho....huku nako kunaugulia na kutafuta tiba...huku nako kuna vita na kuzidiana maarifa....usipokuwa kamili,usipokuwa imara kiroho unapigwa dafrau kubwa usiweze kusimama tena...epuka kuchanganya tiba za kiroho
Ulimwengu wa kiroho ni kitu kikubwa mno na kwa bahati mbaya sana wataalam wajuzi wake ni viumbe waliovaa mwili wa nyama...mwili dhaifu uharibikao...na kwa uoga wao na kutaka sifa hawako tayari kukiri kuwa jambo fulani kwake ni kina kirefu tena kipana
Tunaweka makazi yetu, biashara zetu, ofisi zetu nk juu ya ardhi yenye mambo mengi
Ardhi yenye maagano
Ardhi iliyonajisiwa
Ardhi iliyolaaniwa
Ardhi ambayo ni makazi ya viumberoho
Ardhi iliyofanyiwa kafara ama matambiko
Ardhi ilihobebeshwa roho zilizodhulumiwa, ardhi iliyotwishwa mambo ya ajabu na ya kutisha kabisa
Kwa nia safi kabisa na kwa moyo mweupe unakuja kufanya makazi kwenye ardhi ya namna hiyo ama kufanya biashara
Kwenye mambo kama haya unakumbuka ama unasahau kufanya ibada za kutakasa ardhi na makazi....unaanza biashara yako hapo....lakini pengine tayari kuna wenzako walishaanza kabla yako na kuweka mambo yao sawa
Bila kujua pale unapoingia wewe ndio dampo lililotumika kutupa kila kitu kibaya...unapoanza tu biashara changamoto zinaanza....mwishowe unashauriwa kuwaona wataalam....unakubali na kuanza harakati
Mtaalam wa kwanza anakuja na kufanya yake ...lakini kwa uwezo wake anashindwa kuondoa tatizo bali kuliongeza
Anakuja wa pili na pengine wa tatu....wote hawa kila mmoja ana formula yake...mwisho wa siku bila kujua unakuwa umetengeneza kilinge cha mapambao ya kiroho
Kitakachotokea sasa hapo ni madhara ya kiroho na kimwili kwako wewe, biashara ama makazi yako na hata familia yako kwakuwa kila roho lililopo pale litataka kupigania nafasi yake
Kwenye hizi biashara na makazi yetu, tunapoona mambo hayaendi na changamoto zinakuwa nyingi, rusikimbilie kutafuta na kubadili wataalam...