Tiba zenye madhara

Unapopata tatizo la kiafya...hamu yako ni kupona haraka, hivyo harakati na juhudi za kutafuta tiba huwa kubwa......ni katika hamu hiyo ya kutaka kutibika kwa haraka utapokea ushauri na maelekezo yoyote toka kwa matabibu unaowaamini bila kujali usahihi wa kile wanachokuambia....kidunia tunaambia nusu ya vifo duniani ni kutokana na ushauri wa tabibu.....

Kiroho pia kuna mikanganyiko yake kuanzia kwenye ardhi , makazi, miili yetu mpaka biashara na vitu tunavyomiliki...huku nako kunapata shida ya kiafya lakini kiroho....huku nako kunaugulia na kutafuta tiba...huku nako kuna vita na kuzidiana maarifa....usipokuwa kamili,usipokuwa imara kiroho unapigwa dafrau kubwa usiweze kusimama tena...epuka kuchanganya tiba za kiroho

Ulimwengu wa kiroho ni kitu kikubwa mno na kwa bahati mbaya sana wataalam wajuzi wake ni viumbe waliovaa mwili wa nyama...mwili dhaifu uharibikao...na kwa uoga wao na kutaka sifa hawako tayari kukiri kuwa jambo fulani kwake ni kina kirefu tena kipana
Tunaweka makazi yetu, biashara zetu, ofisi zetu nk juu ya ardhi yenye mambo mengi
Ardhi yenye maagano
Ardhi iliyonajisiwa
Ardhi iliyolaaniwa
Ardhi ambayo ni makazi ya viumberoho
Ardhi iliyofanyiwa kafara ama matambiko
Ardhi ilihobebeshwa roho zilizodhulumiwa, ardhi iliyotwishwa mambo ya ajabu na ya kutisha kabisa
Kwa nia safi kabisa na kwa moyo mweupe unakuja kufanya makazi kwenye ardhi ya namna hiyo ama kufanya biashara

Kwenye mambo kama haya unakumbuka ama unasahau kufanya ibada za kutakasa ardhi na makazi....unaanza biashara yako hapo....lakini pengine tayari kuna wenzako walishaanza kabla yako na kuweka mambo yao sawa
Bila kujua pale unapoingia wewe ndio dampo lililotumika kutupa kila kitu kibaya...unapoanza tu biashara changamoto zinaanza....mwishowe unashauriwa kuwaona wataalam....unakubali na kuanza harakati
Mtaalam wa kwanza anakuja na kufanya yake ...lakini kwa uwezo wake anashindwa kuondoa tatizo bali kuliongeza
Anakuja wa pili na pengine wa tatu....wote hawa kila mmoja ana formula yake...mwisho wa siku bila kujua unakuwa umetengeneza kilinge cha mapambao ya kiroho
Kitakachotokea sasa hapo ni madhara ya kiroho na kimwili kwako wewe, biashara ama makazi yako na hata familia yako kwakuwa kila roho lililopo pale litataka kupigania nafasi yake
Kwenye hizi biashara na makazi yetu, tunapoona mambo hayaendi na changamoto zinakuwa nyingi, rusikimbilie kutafuta na kubadili wataalam...
Hizo ni imani tu. Our mind is so powerful, esp when our conscious mind agree with the subconscious mind. Ingawa ni binaadamu wachache sana wameweza kuoanosha hivyo vitu kwa mafanikio
 
Hizo ni imani tu. Our mind is so powerful, esp when our conscious mind agree with the subconscious mind. Ingawa ni binaadamu wachache sana wameweza kuoanosha hivyo vitu kwa mafanikio
Si kila kitu ni imani....vingine ni live bila chembe ya imani....fuatilia maeneo yenye machinjio kisha ulizia historia yake......
Fanya uwekezaji wowote sehemu ya makaburi bila kufuata taratibu uone
 
Si kila kitu ni imani....vingine ni live bila chembe ya imani....fuatilia maeneo yenye machinjio kisha ulizia historia yake......
Fanya uwekezaji wowote sehemu ya makaburi bila kufuata taratibu uone
Ila hapo kwenye makaburi ni noma. Hivi utajuaje na siku hizi kununua viwanja vya kupima.
 
Hivi Dhulma ni nini haswa? Je, ni kumkopa mtu pesa au kitu chakr na kutomrudishia?? Au ni kumpora mtu kitu na pengine hata kumpora mtu uhai wake?

Naomba kujua kama je , kumrusha mtu elfu 50 yake au laki nane yake bila kumuumiza kama ni dhuluma au sio dhuluma. Na kama ina madhara basi ina madhara gani
 
Hivi Dhulma ni nini haswa? Je, ni kumkopa mtu pesa au kitu chakr na kutomrudishia?? Au ni kumpora mtu kitu na pengine hata kumpora mtu uhai wake?

Naomba kujua kama je , kumrusha mtu elfu 50 yake au laki nane yake bila kumuumiza kama ni dhuluma au sio dhuluma. Na kama ina madhara basi ina madhara gani
Ukitenda mambo hayo na mengine yanayofanana na hayo umetenda tofauti na haki , usawa na kujali....madhara yake yanakuja kwa njia nyingi tofauti na hayana formula
 
Kuna makazi huwa yana mambo kweli kweli.
Kuna ardhi ukizichungulia rohoni unakuta zinalia, nyingine zina agano la kuondoka na mtu kila mwaka.

Nyingine ni ardhi zinazokataa watu wake na wanakuwa ni watu wa kutanga tanga.

Haya nimesyashuhudia.

Kingine ambacho wanadamu wanakipuuza ni ile laana aliyopewa Nyoka ya kula mavumbi ya ardhi maisha yake yote kipindi cha Anguko la Adam.

Kiroho laana ile inampa Nyoka(Shetani) uhalali wa kutafuna mwili wa mwanadamu(mavumbi) maisha ya nyoka yote.

Kwa hiyo ukijichanganya tu, jamaa anakuja na ana haki hiyo maana alipewa hilo, sema sisi tulipewa pia haki ya kumponda kichwa japo hatuitumii haki hii.

All in all ardhi ina kinywa cha kunena, ardhi ina sikio la kusikia.
Ardhi ikikukataa kwa sababu ya damu zilizomwagwa juu yake au dhuluma iliyofanyika hapo hata ufanye hipi hutoboi....

Na bahati mbaya sana tunamwaga uhai wa vitu(damu) katika ardhi hio hio.

Mungu atusaidie kwa kweli.
Tunayo Damu ya Mwana kondoo YESU KRISTO inatakasa Kila kitu
 
Back
Top Bottom