Dumelambegu
JF-Expert Member
- Jan 28, 2011
- 1,052
- 257
Ndugu zangu,
Nime-ipost thread hii kwenye Jukwaa la Siasa siyo kwa sababu sijui jukwaa lake muafaka bali ni kwa sababu naamini hili ndilo jukwaa ambalo watu wengi na hususan viongozi wetu wenye dhamana ya uongozi huwa wanasoma na kujumuika nasi. Nimeamua kuandika mambo kadhaa yanayomhusu anayejiita Dr. Ndodi kwa sababu nilivyomfahamu tangu nianze kumsikiliza kupitia kwenye TV sivyo nilivyomshuhudia mwenyewe. Kwa ufupi ni kwamba tiba ya Ndodi ina utapeli uliojificha na bahati mbaya sana Biblia imegeuzwa kuwa kichaka cha kuficha utapeli huo.
Hivi karibuni nilimsikia akiongea kwenye TV kwamba anagawa dawa ya pumu bure na aliwakaribisha wagonjwa kufika kwenye vituo vyake vya Dar, Mwz na Arusha. Mimi ni mmojawapo wa watu waliohamasika na tangazo lake hilo. Nilikwenda kwenye clinic yake ya Magomeni Mwembechai na kukutana na mambo ya ajabu. Kwanza niliambiwa kwamba dawa inauzwa kwa bei ndogo sana ya Sh. 70,000 ambayo ni sawa na bure. Halafu mgonjwa hahitaji kujiandikisha. Nilishtushwa sana na kauli ile lakini kwa sababu ya ugonjwa wa ndugu yangu mmoja ilibidi ninunue hiyo dawa. Baada ya kulipa Sh. 70,000 niliambiwa nimwone Dokta anipe maelekezo ya namna ya kutumia dawa. Hapo ndipo nilipoishiwa nguvu. Niliambiwa na dokta kuwa hiyo ni dawa ya wiki moja na dozi nzima ni wiki 10. Kwa hiyo, nitatakiwa kurudi baada ya wiki moja nichukue dozi nyingine na nitafanya hivyo kwa wiki kumi. Kwa maneno mengine, dozi ya pumu inaiuzwa Sh. 700,000. Maneno hayo yalinishtua sana. Nilimwambia dokta kwamba sitakuwa na uwezo wa kulipa dawa yote. Yeye akaniambia hawezi kurejesha hela na mbaya zaidi eti hata dawa niliyonunua haiwezi kunifikisha mbali kwani ni moja ya kumi tu ya dozi nzima.
Jambo nalojiuliza ni kwamba kwa nini Ndodi hawi mkweli anapotangaza dawa zake kuhusu dawa zake? Jambo la pili ni je, gharama hizo zinatokana na nini? Je, maandalizi ya dawa yanamgharimu kiasi hicho?!
Ukweli ni kuwa huu utitiri wa watu waojiita madokta na wanakuja kwa njia ya kidini inabidi Serikali iingilie kati. Naona kuna utapeli fulani unafanywa kwa kupitia afya za watanzania. Serikali lazima iwabane watu kama akina Ndodi ili kunusuru wagonjwa wanaofanyiwa utapeli mkubwa wa aina hii. Imefika mahali nawaza kwamba kwa nini Sekta ya Afya nayo isiwe na Mdhibiti kama ilivyo kwenye sekta zingine. Viongozi mnaosoma jukwaa hili tusaidieni tafadhali.