Jumakidogo
R I P
- Jul 16, 2009
- 1,851
- 417
Habari ndugu zangu wapendwa katika ukumbi huu. Niliambukizwa ugonjwa unaoitwa gono miezi minne iliyopita. Nikaenda kupata matibabu na kupewa dawa zinazoitwa Cipro pamoja na sindano ambayo siikumbuki vizuri. Nikanywa dawa hizo kwa siku saba. Maji maji meupe yaliyokuwa yakitoka kwenye uume pamoja na maumivu yakakoma. Lakini baada ya siku nne hali hiyo ikarudia tena. Nikarudi kupata tiba. Mara hiyo nikaandikiwa dawa inayoitwa doxy. Nikainywa kwa siku 14 ugonjwa ukakoma kwa siku tano. Siku ya sita maji maji meupe na maumivu yakaanza upya. Sasa ndugu nitumie dawa gani maana muda mrefu sasa nimekaa bila kufanya tendo. Kama mtu ana jibu la mzaha ni bora akae kimya. Nahitaji ushauri wenye msaada.