Tiba sahihi ya hili ni nini?

Jumakidogo

R I P
Jul 16, 2009
1,851
417
Habari ndugu zangu wapendwa katika ukumbi huu. Niliambukizwa ugonjwa unaoitwa gono miezi minne iliyopita. Nikaenda kupata matibabu na kupewa dawa zinazoitwa Cipro pamoja na sindano ambayo siikumbuki vizuri. Nikanywa dawa hizo kwa siku saba. Maji maji meupe yaliyokuwa yakitoka kwenye uume pamoja na maumivu yakakoma. Lakini baada ya siku nne hali hiyo ikarudia tena. Nikarudi kupata tiba. Mara hiyo nikaandikiwa dawa inayoitwa doxy. Nikainywa kwa siku 14 ugonjwa ukakoma kwa siku tano. Siku ya sita maji maji meupe na maumivu yakaanza upya. Sasa ndugu nitumie dawa gani maana muda mrefu sasa nimekaa bila kufanya tendo. Kama mtu ana jibu la mzaha ni bora akae kimya. Nahitaji ushauri wenye msaada.
 
Unahitajika kufanya vipimo stahiki kabla ya kuanza kutumia madawa kama unavyofanya.nadhani unaweza kuwa na matatizo mawili au zaidi.lakini ukipima nadhani utkuta una infection ya trichomonas( ambayo tiba yake ni dose ya flagyl ) hizo dawa haziwezi kumaliza hilo tatizo.fanya vipimoupate ushauri na dawa sahihi.
 
Kwa kuwa ulipata nafuu baada ya kutumia hizo dawa basi ni dhahiri kuwa ulikuwa na kisonono. Magonjwa mengine hayawezi kupona kwa kutumia dawa hizo. Ila nina wasiwasi na mambo mawili aidha bado unapata maambukizo kutoka kwa mwanamke aliyekuambukiza au mwingine, au umepata kisosono ambacho ni sugu kwa dawa hizo.
Sipendi nikushauri dawa hapa ila ninachokushauri nenda hospitali yoyote ya serikali na utoe maelezo hayo utapata huduma nzuri.
 
Ukisikia gono dume ndio hilo mkuu, huwa halina dawa mpaka unaingia nalo kaburini. Jamani, huu ukicheche noma, yaani watu wanaimba condomisation we wala huna habari, ona sasa unavyolikaribia kaburi. Gono dume halina dawa mkuu umeshakwisha wewe na ukizubaa likishafika kwenye prostate ndo hivyo tena utakuwa mwanaume suruali.

Pole sana mkuu!
 
Usikute unapopata nafuu unamrudia huyo mwanamke. Kama umekuwa unafanya hivyo hautapona, na ikibidi nendeni wote hospitali
 
Unahitajika kufanya vipimo stahiki kabla ya kuanza kutumia madawa kama unavyofanya.nadhani unaweza kuwa na matatizo mawili au zaidi.lakini ukipima nadhani utkuta una infection ya trichomonas( ambayo tiba yake ni dose ya flagyl ) hizo dawa haziwezi kumaliza hilo tatizo.fanya vipimoupate ushauri na dawa sahihi.

kamanda nashukuru sana kwa ushauri wako. Nilifuata maelekezo yako, lakini nilichukuwa maamuzi magumu. Nikaanza kupiga dose ya flgyl. Ama kwa hakika ishu imekauka haijarudi tena na sasa nipo fiti ile mbaya. Pls ntaku pm kawa mawasiliano zaidi, hata takrima ikibidi.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom