Tiba mbadala ni bomu linalokaribia kulipuka

Tiba mbadala ni bomu linalokaribia kulipuka

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
26,021
Reaction score
25,424
Baada ya kudorora kwa huduma za afya hapa nchini, wameibuka waganga wa kienyeji wanaojiita TIBA MBADALA na wamekuwa wakitumia kila mbinu kujitangaza kupitia kwenye vyombo vya habari kama TV, redio, magazeti, mitandao ya kijamii, nk.

Mwaka juzi nilitembelea mganga mmoja aliyeko Temeke kwa lengo la kufanya utafiti. Nilichokipata kule kinasikitisha sana. Aidha, jana nilikuwa nafanya utafiti kupitia redio ya TBCCM. Kuna mganga mmoja alikuwa anaelezea magonjwa ya ngozi akasema kwamba ugonjwa wa candiasis unaathiri hadi ngozi ya miguu na kichwa! Nilimshangaa sana. Hawa watu ni wauaji---ukiwasikia wanaongea utagundua kwamba ni 'weupe' sana....wako shallow sana na ni mbumbumbu wa kutupwa.

Inashangaza pamoja na udhaifu huu wote bado watu wanavyowashobokea. Kwao, kila mmea ni dawa na hakuna ugonjwa watakaosema wanashindwa kuutibu! Serikali inapaswa kuwa makini na makanjanja hawa wasiendelee kuupotosha umma. Dawa zao zifanyiwe uhakiki na watueleze namna dozi ya maji inavyoweza kutibu malaria.

Nawasilisha
:israel:
 
---ukiwasikia wanaongea utagundua kwamba ni 'weupe' sana....wako shallow sana na ni mbumbumbu wa kutupwa.

Inashangaza pamoja na udhaifu huu wote bado watu wanavyowashobokea.
:israel:

Uko sahihi kabisa mkuu ila ujue "mgonjwa hachagui dawa", hivyo watu kuwashobokea ni kutokana na matatizo waliyonayo, na huenda wameshajaribu kwenye hizi hosipitali zetu bila mafanikio. Jukumu la kuhakikisha ubora wa bidhaa zote zinazotumiwa na Watanzania ni la serikali na vitengo husika, lakini ndio hivyo tena tumeachwa kama watoto wa bata kila mtu ajihangaikie.
 
Wengi wao wanacheza na fursa tu sio wataalamu kabisa waliosomea mambo ya tiba asilia.
 
Tatizo Moja Hujui Lolote Unakurupuka Tu. Jiulize Mababu Zako Walitumia Nini Huko Nyuma.

Unakurupuka wewe. Hebu nambia kama mababu zetu walitumia maji (water therapy) kutibu malaria. Kila siku dr ndodi anawalaghai watu kwamba maji ni tiba ya malaria na matokeo yake wagonjwa wanaacha kumeza vidonge hadi wanakufa! Usitetee jambo usilolijua.
 
Wengi wao wanacheza na fursa tu sio wataalamu kabisa waliosomea mambo ya tiba asilia.

ni kweli kabisa mkuu. kuna mmoja nimemsikia jana akipotosha watu, yaani angesemea ule ujinga mbele yangu angepokea vitasa vya kufa mtu.
 
Uko sahihi kabisa mkuu ila ujue "mgonjwa hachagui dawa", hivyo watu kuwashobokea ni kutokana na matatizo waliyonayo, na huenda wameshajaribu kwenye hizi hosipitali zetu bila mafanikio. Jukumu la kuhakikisha ubora wa bidhaa zote zinazotumiwa na Watanzania ni la serikali na vitengo husika, lakini ndio hivyo tena tumeachwa kama watoto wa bata kila mtu ajihangaikie.

ni kweli kabisa mkuu, hawa watu wanaudhi sana....wanatumia vzr kifo cha serikali kuwapumbaza watu.
 
Kama alivyosema mmoja wetu hapa jamaa wamatumia firsa iliyopo. Mimi nilimzuia mzazi wangu kwenda kufanya vipimo kwa hawa jamaa wa tiba mbadala tena walikuja kanisani eti wanatumia computer then magonjwa yako yote yanaonekana nikamwambia mzee hivi kama hicho kipimo kweli kingekuwa kinafanya kazi hiyo pale muhimbili si wangekuwa wamenunua hizo mashine nyingi tu kupunguza msongamano? Hivyo hawa jamaa wnajua matatizo watu waliyonayo wengi ni vidonda vya tumbo ambavyo hata muhimbili watakupa dawa za kutuliza na ukifuta masharti unapona lakini wao wanasema havitibiki hospitali za kawaida. Pia maswala ya uzazi wasichana wengi wnapokosa kwatoto wanakilbilia kwenye tiba mbadala lakini hakuna jipya huko.
 
Mliokuwa ngazi za juu fanyeni mpango muwazuie hao makanjanja
 
Mababu were knowledgeable (vastly), ethical, with high moral standards,people centred and non-money oriented!!!!!

Wa sasa wengi kanjanja tu, wanasafiria nyota ya "medical pluralism" na madhaifu ya sera!!!

Hilo ni kweli wazee walikuwa wanazielewa dawa vizuri na walikuwa wachache sana wenye kufata maadili ila hawa wa sasa wanatumia fursa ili kujipatia hela tu sasa ivi kila mtu eti anatoa tiba mbadala
 
Baada ya kudorora kwa huduma za afya hapa nchini, wameibuka waganga wa kienyeji wanaojiita TIBA MBADALA na wamekuwa wakitumia kila mbinu kujitangaza kupitia kwenye vyombo vya habari kama TV, redio, magazeti, mitandao ya kijamii, nk.

Mwaka juzi nilitembelea mganga mmoja aliyeko Temeke kwa lengo la kufanya utafiti. Nilichokipata kule kinasikitisha sana. Aidha, jana nilikuwa nafanya utafiti kupitia redio ya TBCCM. Kuna mganga mmoja alikuwa anaelezea magonjwa ya ngozi akasema kwamba ugonjwa wa candiasis unaathiri hadi ngozi ya miguu na kichwa! Nilimshangaa sana. Hawa watu ni wauaji---ukiwasikia wanaongea utagundua kwamba ni 'weupe' sana....wako shallow sana na ni mbumbumbu wa kutupwa.

Inashangaza pamoja na udhaifu huu wote bado watu wanavyowashobokea. Kwao, kila mmea ni dawa na hakuna ugonjwa watakaosema wanashindwa kuutibu! Serikali inapaswa kuwa makini na makanjanja hawa wasiendelee kuupotosha umma. Dawa zao zifanyiwe uhakiki na watueleze namna dozi ya maji inavyoweza kutibu malaria.

Nawasilisha
:israel:
Hawana tofauti na babu wa samunge huko Loliondo
 
Hilo ni kweli wazee walikuwa wanazielewa dawa vizuri na walikuwa wachache sana wenye kufata maadili ila hawa wa sasa wanatumia fursa ili kujipatia hela tu sasa ivi kila mtu eti anatoa tiba mbadala
Na kuna chaka la "spiritual healing" ila halisemwi sababu linagusa imani za wengi wakati ni mumo kwa mumo!!!!
Utapeli tuuuu
 
Mi mwenyewe ni mhanga,hawa jamaa hawajitambulishi kama ni waganga wa kienyeji wanaotumia tunguli sema ukienda kutibiwa wanazificha ila wakikuona ni mdau wa matunguli wanakuonyesha mi nilienda kwa mmoja (naomba nimtaje) yupo pale mwananyamala anaclinic inaitwa emmanuel clinic anadai anatibu mifupa,nyonga na uti wa mgongo,lakini cha kushangaza ukiingia ofisini kwake unakuta miti imetumbukizwa kwenye chupa sijui imepitaje mana imefungwa pamoja na mdomo wa chupa ni mdogo,ni kama mazingaombwe fulani hivi,wanatumia mapepo kuponya mgongo,alafu wanakuachia TB,au magonjwa mengine hatari zaidi,tuwe makini jamani na hawa watu..
 
Mganga kwa kiswahili,kwa kizungu ni daktari,usiwadharau waganga.
 
Back
Top Bottom