magonjwa mengi yanatokana na kutozingatia usafi, kuwa na hewa ya kutosha, msongamano kwenye banda. ninalokushauri tibu maji yao ya kunywa tumia water guard ya kidonge au ya maji. hili huwa wengi wanalisahau, pia waongezee vitamin wape chakula kizuri kwa kampuni inayoaminika.
jibu yafuatayo
amprolium uliwapa kwa siku ngapi
chakula ulibadilisha au ni kile kile
je wanaonyesha dalili gani kwa sasa, choo chao kikoje
unapotoa dawa safisha banda na kila kitu vyombo nk. tumia disinfectant kali. lasivyo ugonjwa huwa unarudi. maranda yatoe na choma moto. iwe tabia yako kusafisha vyombo na dawa kila mara unapopata ugonjwa. ili ugonjwa usijirudie.