Mkuu una maana gani? Hivi unafikiri wakati Merikani ina imarisha ulizi na ku-modernise zana zao za kivita Mataifa mengine yalikuwa yamelala usingizi?? Stori zenu wakati mwingine ushangaza kidogo - nyie au USA mnajuaje Budget ya kweli ya Ulinzi wa Uchina, Urusi na say Korea Kasikazini, tangu lini Mataifa hayo yakaweka Budget zao za ulizi adharani wakati hawanunui silaha yoyote kutoka nje i.e kutoka Nchi za magharibi - wanahunda silaha zao wenyewe?
Nani kawambieni Taifa likiwa na TERA Budget ndiyo passport ya kushinda VITA - nani?Again, hapo ndipo mnakosea mahesabu kweli kweli na sijui kwa nini!! Hivi kwa akili za kawaida unaweza kweli ukalinganisha gharama za undaji ndege za vita huko Uchina, Urusi na India na hizo zinazo hundwa huko Merikani?
FYI ndege za vita za Mataifa tajwa zinaundwa kwa robo ya gharama ya kuunda ndege za Marekani, na actually ndege za kijeshi za mataifa mengine zunahundwa na viwanda ambavyo share holder mkubwa ni Serikali zao hivyo hakuna uwezekano wa kufanya ufisadi wa kufuja fedha za walipa kodi kwa ku-inflate gharama, ujanja janja wa makampuni ya USA yanayo pewa contract za kuunda zana za kivita ndiyo ufanya gharama ziwe kubwa mno au wewe hilo ulijui?? Chukulia mfano mdogo wa F-35 jetfighter, je, unajua fighter hizo zimekwisha inagharimu Taifa la Merikani kiasi gani cha fedha mpaka sasa na bado ina matatizo lukuki lakini Serikali ya USA bado inaendelea kuwapatia fedha kampuni ya Lockheed Martin kuendeleza usanii wao wa kuwaibia walipa kodi, si hilo tu hata cost of living za huko Merakani ni kubwa mno ukilinganisha na Mataifa tajwa, hivyo ni wazi mishahara ya wafanya kazi viwandani ni ya juu mno ndio maana wamiliki wa viwanda wa huko Merikani uhamishia viwanda vyao Mexico, Uchina nk wakiwa na lengo la kupunguza gharama za uzalishaji.
Dhana zenu za kujaribu ku-equate Budget za DoD ya huko Merikani na Mataifa mengine kana kwamba hicho ndicho kigezo cha kuonyesha Merikani ni zaidi katika sekta ya ulizi na uwezo kivita, in my opinion dhana hiyo inakuwa grossly misreading na sijui kwa nini wenye mawazo haya potofu hawataki kujifunza kutokana na mifano hai ifuatayo: Merikani iliwahi kuingia vitani na Korea Kaskazini mbona pamoja na Budget yao kuwa kubwa walishindwa na Wakorea Kaskazini, haya tuje vita ya VietNam mbona walitolewa mkuku na walima mpunga wa VietNam, je, Budget kubwa ya USA mnayo ipigia debe hapa iliwasaidia nini kushinda vita, haya tuje vita ya huko Afghanistani huu mwaka wa 16 na bado USA inaendelea kutolewa kamasi na Wataliban - ushahidi huu mdogo unadhilisha kwamba uwezo wa USA kivita hupo kwenye propaganda za MSM, movies za Hollywood, Video games na kijifanya paper Tiger, historia inaonyesha hawajawahi kushinda vita bila ya kusaidiwa/Shirikisha Mataifa mengine, USA ni mabingwa wa kukusanya kusanya Mataifa mengine yamsaidie kuendeleza Gun Boat Diplomacy zake zilizo pitwa na wakati, narudia - USA hawana ujasiri wala uwezo kupigana vita wakiwa pekee yao - leo hii ndiyo wajifanye wana uweza wa kupigana na Uchina, Urusi na Korea Kasikasini kwa mpigo!!!!
Tatizo kubwa la Taifa hilo linatokana na baadhi ya Ma General wa jeshi lao wanakuwaga na njozi za mchana, hawana habari kinacho endelea Duniani na wasipo kuwa makini kwa kujifunza kutokana na historia ya miaka ya nyuma basi, wakae wakijua kwamba Taifa lao litakuja kupata wakati mgumu sana wakijitia kuanzisha WW3.