Thread ya list ya wana JF wanaohama Tigo

Lupweko

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
16,426
14,030
Si kwamba wana JF wanaotumia mtandao wa Tigo ndio wateja wakubwa, hapana! Lakini tukijitaja hapa itakuwa sample mojawapo itakayowafanya Tigo wapate takwimu fulani zinazoonyesha impact ya uamuzi wao wa kupandisha bei ya kupiga simu kinyemela. Kwa kuwa nimeona Tigo wameweka matangazo yao kwenye web hii ya JF, bila shaka ujumbe utawafikia kwamba tunahama. Nitabaki na line kwa ajili ya incoming calls, lakini nitapiga outgoing kwa line ya pili (siitaji). Naanza kujiorodhesha:

mimi ninahama
 

Asprin

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
65,930
89,012
Mi sitahama huu mtandao, kwakuwa huu sasa ni mwezi wa sita simu yangu ni kama redio tu, inapokea simu tu!
 

wilbald

JF-Expert Member
Dec 17, 2007
1,804
1,366
kwanini mnatumia tigo? Hata siwaelewi kwaheri
hata voda nao wamepandisha bei hadi sh 2.6/sec tena bila kuwaarifu wateja.
mimi kwa sasa natumia laini mpya ya ZANTEL raha sana kutumia huu mtandao. wanaJF twanga kotekote.
 

Lupweko

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
16,426
14,030
Naendelea kupata watu hapa. Ikifikia mahali nitaweka summary ili Tigo na wengine wanaoshusha bei kwa mabango makubwa lakini wanapandisha bei kinyemela, wapate message
 

juniorfeb18

Member
Apr 12, 2011
36
14
mimi pia nahama.sijajua coverage ya huu mtandao wa wapemba,kule kwenye miteremko ya mlima kilimanjaro tarakea unapatikana?
 

Likwanda

JF-Expert Member
Jun 16, 2011
3,914
1,115
Dah, Toka Mobite, Buzz hadi Tigo. Bado na imani sana na tigo hivyo siwezi kuhama kabisa maana wao ndio wakali wa promotion mtarudi wenyewe huko mlipoenda kupanga.
 

NewDawnTz

JF-Expert Member
Nov 15, 2010
1,668
362
Yaani hiyo tiGO mwenzenu nilishaachaga long time........uchaaaaaaaaaaaafuuuuuuuuuuuuuuuuuuu
 

The Finest

JF-Expert Member
Jul 14, 2010
21,615
5,966
TIGO
ZANTEL
VODACOM
AIRTEL

Na mitandao mengine yote hakuna mwenye afadhali nasema kwasababu watanzania wengi tunajua kuweka vocha na kupiga simu sidhani kama watu wana tabia ya kufanya uchunguzi baada ya kupiga ameongea kwa muda gani na kwenye simu yake alikuwa na salio kiasi gani na amekatwa kiasi gani kwa muda huo aliongea, mkiambiwa Sh 1 au Sh 2 kwa sekunde huwa mnahakikisha kuwa kweli? Hakuna tofauti yoyote ile nasema hivyo sababu niliishafanya kazi kwenye NOC (Wataalamu wa IT watakuwa wanaelewa namaanisha nini) ya mojawapo ya hawa providers and i know how the game is being played na hawa operators.
 

TEMPOLALE

JF-Expert Member
Aug 18, 2011
302
107
Mimi bado niko tigo, na ni mteja wao kwa mda mrefu sana kwa namba 071340301.. siku kadhaa zilizopita niliweka mda wa maongezi wa elfu50 nikamgawia wife elfu20 nikabakiwa na elfu30+ leo nimeangalia salio nina elf23 sikumbuki kama nimepiga simu za hivyo, nafanya uchunguzi nikikuta nimeibiwa naachana nao, naamini mimi ni mmoja wa wateja wao wakubwa.
 

Babuu blessed

JF-Expert Member
Oct 14, 2010
1,363
488
Mi wiki ya tatu sasa sijaweka salio nilikwaruza nikafuta namba bahati mbaya vocha ya buku,kuwapigia customer care wakaniambia kuongea nao inabidi niwalipe yaani unakata pesa <salio>unapoitaji msahada nikaongea nae wakasema inabdi niende offisi za tiGo watanitatulia tatizo kufika wakaleta longolongo sana mwisho mdada mmoja akaniambia nimwachie ile vocha kwa ahadi,mpaka kesho yake nitakuwa nishaongezewa salio matokeo yake paka sasa sijaona salio wala nini? Hawa jamaa ni genge la wauni,wezi nk.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

1 Reactions
Reply
Top Bottom