Wana JF, Tutofautishe Kati ya Kusema Uongo na Kuteleza Ulimi, Rais wa TZ Hawezi Kusema Uongo, Labda Kuteleza tuu!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,467
113,570
Wanabodi,

Hii ni thread elimishi ya kuwapiga darasa wana jf kuhusu tofauti ya kitu kinachoitwa kusema uongo, lying na kuteleza ulimi, kwa lugha ya Kiingereza, a slip of a tongue, na kuwajulisha kusema uongo chini ya kiapo ni kosa la jinai, viongozi wetu wote licha la kula kiapo cha kuilinda katiba, pia wanakula kiapo cha uaminifu ambapo kwao ni kosa la jina kusema uongo wowote maana wamekula kiopo cha uaminifu, hivyo rais wa nchi hawezi kabisa kusema uongo, kwa sababu urais ni taasisi, haiwezi kusema uongo, ila taasisi hii inaongozwa na mtu aitwae rais, huyu ni binaadamu tuu kama binadamu wengine wote, anaweza kukosea, kusema uongo au anaweza tuu kuwa ameteleza ulimi, and this is not a big deal!. Tena sio wengi wanaofahamu kuwa kwa mujibu wa katiba yetu ya Tanzania ya mwaka 1977, rais wa Tanzania, hawezi kufanya makosa yoyote ya jinai na ndio maana hawezi kushitakiwa kwa sababu urais ni taasisi, tatizo kubwa ni the dividing line between rais ambaye ni mtu, binadamu na urais ambao ni taasisi ni very thin, one has to be very smart to distinguish them because they are two in one.
Darasa hili linafuatia kuibuka kwa mijadala mingi humu kuhusu nani ni muongo, kulikoibuliwa na hotuba ya rais Magufuli, kumtuhumu mwanasiasa mmoja kupika data za uongo, na rais akashangaa kwa nini hakamatwi wakati sheria zipo!.

Ndipo kukaibuka mijadala mingi kuhusu nani ni muongo, katika miijadala hiyo, ili kuthibitisha rais ni muongo, wengi wa wachangiaji wametumia kauli yake alipoingia alikuta bei ya kilo ya sukari ni ni Shilingi 5,000, kulikofuatiwa na kusambaa kwa video hii ili kuthibitisha rais ni muongo.

Baada ya kuiangalia video hii, nikaona kama mwana jf responsible, ukiona kuna watu wanachangia kitu au kushabikia kitu wasichokijua au in a wrong way, wewe kama mwana jf responsible una wajibu wa kuwaelimisha, kuwafahamisha na kuwaelewesha the right thing.

Kunatofauti ya Kukosea Kitu, Kuteleza Ulimi, Kusema Uongo na Kupika Data.

Kukosea Kutamka ni Nini, Jee Kukosea Kutamka Kitu ni Kusema Uongo?.
Kukosea kutamka kitu, ni pale mtu anapohutubia, na kusema jambo lolote kwa makosa, inaweza kuwa ni kukosea facts, kukosea majina, kukosea idadi, au kukosea kutamka jambo lolote, hii inaitwa error, kukosea kitu au kufanya error sio kusema uongo.

Jee Kuteleza Ulimi ni Nini?, na Kuteleza Ulimi ni Kusema Uongo?.
Kuteleza ulimi, au kujikwaa ulimi, ni pale mzungumzaji anapokosea kutamka jambo fulani kwa bahati mbaya akikusudia kutamka jambo fulani, lakini akatamka jambo jingine bila kukusudia. Mfano mzuri wa hili ni kule kwenye ule mkutano ambako Naibu Waziri wa Elimu aliteleza ulimi na kusema Tanzania ni muungano wa Pemba na Zimbabwe. Nilipandisha bandiko hili kuelimisha watu
Ya Mulugo: Was Only a Slip of Tongue! [Aliteleza Ulimi tuu ...
"].
Kuteleza ulimi, au kujikwaa ulimi sio kusema uongo kwa sababu huku kunafanyika bila kukusudia, ila kama kuteleza huku kunaweza kuleta madhara kwa mwingine, anaweza kufungua kesi ya madai kudai fidia, kwa kosa linaloitwa 'innuendos'.

Kusema Uongo, Ni Kudanganya Bila Kukusudia, Au Kukusudia kwa Malengo
Kusema uongo, ni kitendo cha kusema kitu ambacho sio kweli, au kwa kudhamiria, au bila kudhamiria, huku wewe mtamkaji ukijua ni kweli kumbe sio kweli. Kwenye kusema uongo, kuna uongo ambao una madhara, hivyo kusema uongo huo ni kosa, na kuna uongo ambao hauna madhara, kusema uongo huo sio kosa, ila kusema uongo chini ya kiapo ni kosa la jinai. Kwenye kusema uongo, ukipewa taarifa ya uongo na watu unaowaaminia bila wewe kujua ni uongo, na wewe ukaisoma hivyo hivyo ilivyo, baadae ikakutikana ni uongo, wewe uliosoma unakuwa huna kosa wala hujadanganya bali umetoa wrong information ulizokuwa fed, kama wewe ni kiongozi wa umma, kama uongo huu una madhara, then unawajibika, lakini kwa uongo kama ule wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anne Kilango, na akatumbuliwa, kiukweli kabisa, Kilango alionewa tuu, ila kosa lile limeisharekebishwa kwa Kilango kupoozwa na uteuzi mwingine.
Kwenye kudanganya, kuna kuna kudanganya kwa jinai, forgery, lying, false pretense na kuna kudanganya ambako sio jinai kama cheating kwenye mahusiano, etc

Kupika Data ni Kutengeneza Uongo Kwa Lengo Ovu, ni Kosa la Jinai.
Kupika data ni kutengeneza uongo dhahiri kwa nia ovu, hivyo hili ni kosa la jinai la kuhadaa jamii. Mfano hai ni hili tukio la Waziri wa Afya kasema kati ya Watanzania waliopimwa na kukutwa na Ukimwi, ambao walipaswa kutumia ARV, ni asilimia 67% tuu ndio wanaotumia ARV. mwandishi akaandika asilimia 67% ya Watanzania, wanatumia ARV. Hata hivyo hukumu iliyotolewa kwa gazeti hilo ni kubwa kuliko the motive behind kosa lenyewe. Ili kuwepo kosa la kupika data, lazima kuwe na ill motives behind upikaji huo. Mfano kwenye matokeo ya uchaguzi, unakuta jumla ya kura ni nyingi kuliko idadi ya wapiga kura.

Ubingwa na Upishi wa Mhe. Zitto Katika Kupika Data.
Kwenye hili la kupika data na kusema uongo, ni ukweli Mhe. Zitto ni mpishi mzuri wa data, mfano juzi juzi amekuja na uongo kuwa Tanzania tumekopa mkopo wa dola milioni 500 kutoka benki ya Uswisi kwa riba ya asilimia 80%, hivyo tutalipa dola milioni 900 ndani ya kipindi cha miaka 5!, kitu mbacho sii kweli. Hii chini ni mifano ya upishi wa Zitto katika kupika data
Anaandika Zitto_Kabwe.
"Mnakumbuka Hosteli za Chuo Kikuu tuliambiwa zimejengwa Kwa TZS 10bn? Ukaguzi wa kawaida tu CAG amekuta ni TZS 54bn. Serikali Hii ni HATARI." Uwongo uwongo tu
Kiukweli huu uongo wa Zitto sasa unazidi kukithiri, anaendelea kumsingizia rais kusema uongo, rais amesema ukweli kuwa ule ujenzi wa zile hostel, umegharimu shilingi bilioni 10 tuu, kitu ambacho ni kweli, kakini Zutto anamsingizia kuwa eti rais ni muongo, na kudai hosteli zimegharimu bilioni 54 kwa mujibu wa taarifa ya CAG, who is CAG mbele ya rais katika kusema ukweli?.
Nasisitiza kuwa kauli ya rais ndio kauli ya ukweli halisi na ndio kauli ya mwisho, rais wa nchi anaweza asiwe sahihi, lakini hawezi kabisa kusema uongo, rais wa nchi aseme uongo ili iweje?, kwa nini adanganye wakati kila anachosema ni sheria?, hivyo Zitto ndio muongo, kitendo cha kutoa kauli yoyote kuashiria kuwa rais ni muongo, ni uchochezi, hivyo hii ni kosa la jinai.

Anaandika kiongozi wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe

Taarifa yetu kuhusu ' kupikwa ' Kwa takwimu za Pato la Taifa tutaitoa mara baada ya kikao cha Kamati Kuu ya Chama cha Act Wazalendo kitakachoketi 28/10/2017. Sheria ya Takwimu aliyotaja Rais kutaka itumike kuziba watu midomo haizuii tafsiri za Takwimu zinazotolewa na Serikali.

Tunatumia takwimu za Serikali kuonyesha kuwa Serikali inadanganya Kwa kutokusema ukweli wote wa uhalisia wa uchumi na kuporomoka Kwa mapato. Ni sawa na mtu anayesema Glasi ni ' half empty or half full ' kwani anasema kitu kile kile.

Kwa mfano, Rais anaposema kuwa Serikali inatekeleza miradi mikubwa Kwa kutumia ongezeko la kodi anakuwa anadanganya Wananchi na anafanya hivyo akijua anadanganya. Rais anajua kuwa Deni la Taifa limeongezeka Kwa TZS 6.5trn katika miaka yake miwili ya urais. ( Deni la Nje limeongezeka Kwa US$1.5bn ( TZS 4.5trn) kati ya July 2016-July 2017. Deni la ndani limeongezeka Kwa TZS 2trn katika kipindi hicho.

Soma . http://www.bot.go.tz/Publications/MonthlyEconomicReviews/MER August 2017 Final.pdf ).

Pia Rais anajua kuwa Serikali inatumia, bila kufuata sheria, Fedha za Mashirika ya Umma zilizopo Benki Kuu kulipia baadhi ya Miradi yake. Kukiuka sheria za Fedha ni kosa la jinai na wakati mwengine kosa la kikatiba kwani Katiba imeweka utaratibu wa masuala ya Fedha za Umma.

Kodi inayokusanywa na TRA inaweza kulipa mishahara na kuhudumia Deni la Taifa tu. Kwanini Rais wetu hasemi kuwa tunakopa? Kukopa sio dhambi, kwanini aaminishe watu kuwa anatekeleza miradi Kwa kuwa kodi zimeongezeka? Kama Rais anaamini kuwa Mapato hayajaporomoka, aruhusu ukaguzi maalumu wa CAG kwenye Mapato ya July na Agosti 2017 na ukaguzi huo uwekwe wazi Kwa umma.

Rais akifanya hivyo NITAWAJIBIKA

Taarifa kuwa tumekopa dola milioni 500 Uswisi na tutalipa dola milioni 900 baada ya miaka mitano itakuwa ni uongo!.
Hii taarifa kuwa Deni la Taifa limeongezeka Kwa TZS 6.5trn katika miaka yake miwili ya urais, huu pia utakuwa ni uongo!.
Hii taarifa kuwa Deni la Nje limeongezeka Kwa US$1.5bn ( TZS 4.5trn) kati ya July 2016-July 2017 pia itakuwa ni uongo!. Hii taarifa kuwa Deni la ndani limeongezeka Kwa TZS 2trn katika kipindi hicho, pia itakuwa ni uongo!.
Mtu hawezi kusema uongo mkubwa kama huu tena waziwazi mchwana kweupe akaachwa tuu hivi hivi!. Kuhusu huu uchochezi wa Zitto, niliwahi kushauri hivi, Zitto Zuberi Kabwe Ni Mchochezi, Akamatwe, Ashitakiwe Kwa ...

Hitimisho
Kuteleza ulimi sio kusema uongo, kukosea katika kuzungumza sio kusema uongo, kusema uongo ni kosa, sio lazima liwe la jinai, ila kupika data zenye nia ovu ni kosa la jinai, uongo, na kuteleza ulimi, kwa lugha ya Kiingereza, a slip of a tongue, sio kusema uongo, cheating or lying na sio kosa la jina, hiyo hutokea kwa kila binadamu, lakini rais wa nchi kwa muktadha wa taasisi ya urais, hawezi kusema uongo, anaweza tuu kuwa ameteleza tuu ulimi, kwa ule ubinaadamu wa rais na sio urais, tena sio wengi wanaofahamu kuwa kwa mujibu wa katiba yetu ya Tanzania ya mwaka 1977, rais wa Tanzania, hawezi kufanya makosa yoyote ya jinai na ndio maana hawezi kushitakiwa kwa sababu urais ni taasisi, tatizo kubwa ni the dividing line between rais ambaye ni mtu, binadamu na urais ambao ni taasisi ni very thin, one has to be very smart to distinguish between the two of them because they are two in one.

NB. Katika kuchangia uzi huu, zingatia Mwito Kwa Wana JamiiForums Kuhusu Ukosoaji wa Rais ...
Jumatano Njema.
Wasalaam.

Paskali
 
Wanabodi,

Hii ni thread elimishi ya kuwapiga darasa wana jf kuhusu tofauti ya kitu kinachoitwa kusema uongo, na kuteleza ulimi, kwa lugha ya Kiingereza, a slip of a tongue, na kuwajulisha kusema uongo chini ya kiapo ni kosa la jinai, viongozi wetu wote licha la kula kiapo cha kuilinda katiba, pia wanakula kiapo cha uaminifu ambapo kwao ni kosa la jina kusema uongo wowote maana wamekula kiopo cha uaminifu, hivyo rais wa nchi hawezi kusema uongo, ila yeye kama binadamu, anaweza tuu kuwa ameteleza ulimi, and this is not a big deal!. Tena sio wengi wanaofahamu kuwa kwa mujibu wa katiba yetu ya Tanzania ya mwaka 1977, rais wa Tanzania, hawezi kufanya makosa yoyote ya jinai na ndio maana hawezi kushitakiwa!.

Hitimisho
Kuteleza ulimi sio kusema uongo, kukosea katika kuzungumza sio kusema uongo, kusema uongo ni kosa, sio lazima liwe la jinai, ila kupika data zenye nia ovu ni kosa la jinai, uongo, na kuteleza ulimi, kwa lugha ya Kiingereza, a slip of a tongue, sio kusema uongo na sio kosa la jina, hiyo hutokea kwa kila binadamu, lakini rais wa nchi hawezi kusema uongo, anaweza tuu kuwa ameteleza tuu ulimi, tena sio wengi wanaofahamu kuwa kwa mujibu wa katiba yetu ya Tanzania ya mwaka 1977, rais wa Tanzania, hawezi kufanya makosa yoyote ya jinai likiwemo kosa la kusema uongo na ndio maana hawezi kushitakiwa!.
Jumatano Njema.
Wasalaam.

Paskali

Najutia kupoteza mda wangu kusoma ujinga kama huu, eti hawezi kusema uongo? Yeye ni nani mpaka asiweze kusema uongo?
Mambo mengine tutumie akili zetu za kawaida kufikiri. Kama kadanganya ni kadanganya tu, kwani yeye ni nani mpaka asidanganye?
Kadanganya mangapi tunamsikiliza na kumcheka kwa kuwaona watanzania hawajui kitu?
Mda uliotumia kuandika huu ujinga, bora ungekaa na mtoto wako ukaongea nae matatizo yanayomsibu.
 
Kuteleza ulimi mara moja sawa inakubalika kama ukikiri na kurekebisha, haiwezekani kila siku yeye tu ndiyo anateleza ulimi
ulimi wake umeubwa kwa utelezi maana kuteleza kumekuwa ni sehemu ya ulimi wake
paskali unaitwa central hata ile sred ya kusema zito akamatwe nilisoma nikajua humaanisi ulichosema hasa pale kwenye nb zako n hahahaha
 
Wanabodi,

Hii ni thread elimishi ya kuwapiga darasa wana jf kuhusu tofauti ya kitu kinachoitwa kusema uongo, na kuteleza ulimi, kwa lugha ya Kiingereza, a slip of a tongue, na kuwajulisha kusema uongo chini ya kiapo ni kosa la jinai, viongozi wetu wote licha la kula kiapo cha kuilinda katiba, pia wanakula kiapo cha uaminifu ambapo kwao ni kosa la jina kusema uongo wowote maana wamekula kiopo cha uaminifu, hivyo rais wa nchi hawezi kusema uongo, ila yeye kama binadamu, anaweza tuu kuwa ameteleza ulimi, and this is not a big deal!. Tena sio wengi wanaofahamu kuwa kwa mujibu wa katiba yetu ya Tanzania ya mwaka 1977, rais wa Tanzania, hawezi kufanya makosa yoyote ya jinai na ndio maana hawezi kushitakiwa!.

Hitimisho
Kuteleza ulimi sio kusema uongo, kukosea katika kuzungumza sio kusema uongo, kusema uongo ni kosa, sio lazima liwe la jinai, ila kupika data zenye nia ovu ni kosa la jinai, uongo, na kuteleza ulimi, kwa lugha ya Kiingereza, a slip of a tongue, sio kusema uongo na sio kosa la jina, hiyo hutokea kwa kila binadamu, lakini rais wa nchi hawezi kusema uongo, anaweza tuu kuwa ameteleza tuu ulimi, tena sio wengi wanaofahamu kuwa kwa mujibu wa katiba yetu ya Tanzania ya mwaka 1977, rais wa Tanzania, hawezi kufanya makosa yoyote ya jinai likiwemo kosa la kusema uongo na ndio maana hawezi kushitakiwa!.
Jumatano Njema.
Wasalaam.

Paskali
Watakuelewa wachache sana kwa huu uzi mkuu. Sikuelewa at the first place ikabidi nirudie kusoma tena.
Kweli mkubwa hajambi
 
Ubingwa na Upishi wa Mhe. Zitto Katika Kupika Data.
Kiukweli huu uongo wa Zitto sasa unazidi kukithiri, anaendelea kumsingizia rais kusema uongo, rais amesema ukweli kuwa ule ujenzi wa zile hostel, umegharimu shilingi bilioni 10 tuu, kitu ambacho ni kweli, kakini Zutto anamsingizia kuwa eti rais ni muongo, na kudai hosteli zimegharimu bilioni 54 kwa mujibu wa taarifa ya CAG, who is CAG mbele ya rais katika kusema ukweli?.
Nasisitiza kuwa kauli ya rais ndio kauli ya ukweli halisi na ndio kauli ya mwisho, rais wa nchi anaweza asiwe sahihi, lakini hawezi kabisa kusema uongo, rais wa nchi aseme uongo ili iweje?, kwa nini adanganye wakati kila anachosema ni sheria?, hivyo Zitto ndio muongo, kitendo cha kutoa kauli yoyote kuashiria kuwa rais ni muongo, ni uchochezi, hivyo hii ni kosa la jinai.

Pascal hali yako Mkuu. Kwa hiyo kwa hili la Hostel za UDSM, unatuambia tukate shauri kuwa CAG kasema uongo ili Raisi Magufuli awe amesema ukweli?

Mie kwa hili I will beg to differ with you, kwa kuwa katika professional ethics, CAG hawezi kusema uongo katika masuala ya auditing. Na pia, katika context ya ethics za auditing, ni afadhali raisi aonekane muongo kuliko CAG.

Hata hivyo, naweza kukuelewa kwamba unaweza kusema CAG ametamka juu ya billioni 54 akimaanisha kuna ufisadi umefanyika, kwamba majengo yaliyokuwa yajengwe kwa bilioni 10 yamejengwa kwa bilioni 54. Lakini sasa, swali litakuwa, ni kichaa gani aliidhinisha bilioni 44 za ziada kwa ajili ya ujenzi wenye budget ya bilioni 10? Na alizitoa wapi hizo bilioni 44 za ziada? Na kama ni ufisadi, kwa nini hatujasikia hatua zikichukuliwa dhidi ya ufisadi huo?

Katika context nyingine, ikiwa Raisi alijua kwamba haiwezekani kujenga majengo hayo kwa bilioni 10 na bado akasema atayajenga kwa bilioni 10, basi call a spade a spade, hapo Raisi alidanganya na wala sio suala la kuteleza ulimi. Na kudanganya kunaendana na kupata manufaa fulani, hivyo hapa raisi alidanganya kwa manufaa yake binafsi ya kisiasa.

Najua inawezekana Raisi Magufuli alisema atayajenga majengo hayo kwa bilioni 10 bila kujua kuwa haiwezekani yakajengwa kwa bilioni 10, kwa kuwa yeye si mtalaamu wa ujenzi. Lakini je, kuna wakati alipoelimishwa na wataalamu wa ujenzi kwamba majengo hayo isingewezekana kuyajenga kwa bilioni 10 na alikubaliana na hoja zao? Na kama alikubaliana na hoja zao, na hata kuidhinisha majengo yajengwe kwa zaidi ya bilioni 10, alirekebisha kauli yake kuwa majengo hayo yangejengwa kwa bilioni 10, hasa alipoona anasifiwa kwa kufanikisha ujenzi wa majengo hayo kwa bilioni 10 na huku akijua wazi kwamba hilo halikuwa kweli, yalijengwa kwa zaidi sana ya bilioni 10? Ni obvious hakurekebisha kauli yake ya bilioni 10, kitu kinachofanya awe alidanganya by omission, once again, kwa manufaa ya kisiasa.

Na by the way, cheo au mamlaka uliyonayo havikufanyi uongo wako uwe ni ukweli au uitwe kuteleza. Hiyo ni desturi potofu ya kuwastahi wakubwa na nahisi Pascal umelelewa katika culture hiyo na sasa unaona jambo baya kusema raisi kasema uwongo. Je tuseme Clinton hakusema uwongo juu ya Monica Lewinsky, au Trump hadanganyi? Uwongo ni uwongo tu, whether umesemwa na Raisi au mwananchi wa kawaida. Na pia, kama wanasiasa wengi kwa ujumla, maraisi wengi sana katika mambo ya siasa wana kawaida ya kudanganya - kusema uwongo. Hilo kila mtu mwenye akili timamu analifahamu.

Hivyo, hata uliangalie kwa angle ipi, hili la majengo ya hosteli za UDSM linamfanya Raisi Magufuli awe MUONGO, eidha moja kwa moja, au by omission.
 
Wanabodi,

Hii ni thread elimishi ya kuwapiga darasa wana jf kuhusu tofauti ya kitu kinachoitwa kusema uongo, na kuteleza ulimi, kwa lugha ya Kiingereza, a slip of a tongue, na kuwajulisha kusema uongo chini ya kiapo ni kosa la jinai, viongozi wetu wote licha la kula kiapo cha kuilinda katiba, pia wanakula kiapo cha uaminifu ambapo kwao ni kosa la jina kusema uongo wowote maana wamekula kiopo cha uaminifu, hivyo rais wa nchi hawezi kusema uongo, ila yeye kama binadamu, anaweza tuu kuwa ameteleza ulimi, and this is not a big deal!. Tena sio wengi wanaofahamu kuwa kwa mujibu wa katiba yetu ya Tanzania ya mwaka 1977, rais wa Tanzania, hawezi kufanya makosa yoyote ya jinai na ndio maana hawezi kushitakiwa!.

Hitimisho
Kuteleza ulimi sio kusema uongo, kukosea katika kuzungumza sio kusema uongo, kusema uongo ni kosa, sio lazima liwe la jinai, ila kupika data zenye nia ovu ni kosa la jinai, uongo, na kuteleza ulimi, kwa lugha ya Kiingereza, a slip of a tongue, sio kusema uongo na sio kosa la jina, hiyo hutokea kwa kila binadamu, lakini rais wa nchi hawezi kusema uongo, anaweza tuu kuwa ameteleza tuu ulimi, tena sio wengi wanaofahamu kuwa kwa mujibu wa katiba yetu ya Tanzania ya mwaka 1977, rais wa Tanzania, hawezi kufanya makosa yoyote ya jinai likiwemo kosa la kusema uongo na ndio maana hawezi kushitakiwa!.
Jumatano Njema.
Wasalaam.

Paskali
A slip of tongue ni direct translation! Kufa ni kufa kama ulikufa polepole ,fasta n.k Huko kuteleza ulimi kwa Mkuu wa nchi kunaweza kuwa na grave consequences kwenye maisha ya raia. Tuwe serious jamani!
 
Back
Top Bottom