THRDC ni muungano wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania ambao ulianzishwa mwaka 2010 katika kipindi ambacho matukio ya uvunjaji wa haki za binadamu yalikuwa juu kwa kiasi kikubwa nchini Tanzania.
Muungano huo unafanya kazi ya kuboresha usalama na ulinzi wa watetezi wa haki za binadamu katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuhakikisha kuwa watetezi wa haki za binadamu wanaweza kutekeleza majukumu yao muhimu bila hofu ya madhara au ukandamizaji, kwa mujibu wa Azimio la Umoja wa Mataifa la mwaka 1998 kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu.
Mnamo tarehe 24 Mei, 2025 Askofu Josephat Gwajima alifanya
mkutano na waandishi wa habari ambapo alieleza mlolongo wa matukio ya watu kutekwa na kupotea hivyo kutokana na hayo, aliamua kuitisha mkutano na waandishi wa habari kuongelea kuhusu suala hilo na kisha kutoa ushauri wa namna ya kudhibiti matukio hayo.
Kutokana na mkutano huo wa Gwajima zimekuwepo taarifa nyingi ambazo baada ya akufanyiwa uhakiki ilibainika kuwa taarifa hizo si za kweli, zilitengenezwa ili kupotosha uhalisia akihushwa Askofu huyo dhidi ya kile alichokizungumza. rejea
hapa,
hapa na
hapa.
Ipo taarifa inayosambazwa mtandaoni ikidaiwa kutolewa na THRDC na kuripotiwa na Watetezi TV pamoja na ITV kuwa mtandao huo umewataka viongozi wa dini kutokujihusisha na masuala ya siasa, kipindi ambacho viongozi wengi wa dini wakikemea matukio ya utekaji, mauaji na watu kupotezwa.
Je, ni upi uhalisia wa tamko hilo?
Ufuatiliaji wa kimtandao wa JamiiCheck uliotumia utafutaji wa maneno muhimu (Key word search) ulijiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli bali ni ya kutengenezwa kwani haikuchapishwa na
THRDC.
Aidha machapisho yaliyotumika kusambaza taarifa hiyo ni ya kutengenezwa na wapotoshaji kwani yamebainika kuwa na madhaifu ambayo yanatofautisha dhidi ya machapisho rasmi ambayo hutolewa na vyanzo hivyo. Sehemu ya mapungufu hayo ni pamoja na matumizi ya fonti isiyotumiwa na
THRDC katika barua zake rasmi, Chapisho la
ITV sehemu ya kichwa cha habari inaonesha kufutwa kwa maneno ya awali na kupachika maneno hayo.
Watetezi TV kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa X,
imekanusha taarifa na kwamba si ya kweli, ni uzushi unaosambazwa na watu wenye nia ovu hivyo kuwataka wananchi waipuuze.
"Taarifa hiyo inayozunguka kwenye mitandao ya kijamii inayohusisha Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania(THRDC) ikionyesha imechapishwa na Watetezi Tv si ya kweli, ni uzushi unaosambazwa na watu wenye nia ovu. IPUUZWE!Hakuna Tamko la namna hiyo lililotolewa na THRDC mahali popote na haijachapishwa na chanel hii."