Thousands of fake CCM cards printed

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,007
Thousands of fake CCM cards printed

AN elaborate ’internal’ plot to remove from leadership corruption-free Chama Cha Mapinduzi (CCM) members and replace them with those who embrace the vice is said to have been uncovered as the ruling party braces for next year’s presidential and parliamentary elections.

According to reports reaching THISDAY from reliable sources within CCM and also in various state organs, some leading ruling party cadres are believed to have launched an underground scheme where fake CCM membership cards are being printed in the thousands and ’strategically’ distributed in regions like Dar es Salaam, Kilimanjaro, Mbeya and the ’Lake Zone’.

The aim is to facilitate the ouster of all CCM legislators and councilors seen to be riding the anti-corruption bandwagon, and pave the way for the ’greedier’ (fisadi) elements to replace them and entrench themselves around the country, the sources say.

CCM membership cards are supposed to be sold to aspiring members, even at negligible prices. But sources say the fake cards are being given away for free, and the recipients instructed not to vote for certain candidates for parliamentary and local council seats.

State organs are understood to have been informed about this development and an undercover investigation is now underway in Kilimanjaro and Dar es Salaam regions, where the first fake CCM cards were discovered.

According to our sources, preliminary findings strongly suggest that the individuals behind the clandestine printing operation are amongst the richer CCM members.

They are believed to be taking advantage of loopholes in the internal CCM ’opinion polls’ process of selecting its contestants for parliamentary and councilorship positions.

Under the process, initiated by President Jakaya Kikwete in his capacity as party chairman, all CCM members are supposed to be given the chance of equal involvement at the nominations stage.

It is however, understood that only genuine CCM members will be allowed to vote in the primaries. Genuine members will be determined through a verification process to be done before June next year. Details of this process are not yet known.

Sought out for comment, CCM’s ideology and publicity secretary John Chiligati acknowledged that there was some truth in the reports of fake party cards having been printed, but said the only area where this had been concretely confirmed was Moshi Rural District in Kilimanjaro Region.

The district has two parliamentary constituencies: Vunjo and Moshi Rural itself. Both incumbent legislators are CCM members; Cyril Chami (Moshi Rural), who is currently Deputy Minister for Industries and Trade, and Aloyce Kimaro (Vunjo), recognized as one of the party’s more outspoken anti-corruption campaigners.

Chiligati said the fake CCM cards were found at the following locations in Moshi Rural: Kimochi, Okaoni, Uru Kaskazini and Longuo.

CCM secretary general Yusuf Makamba said when contacted for comment that he was on leave. But according to his deputy, George Mkuchika, the problem of fake membership cards being distributed around the country has been presented to relevant local government authorities for investigation, and a findings report will be released �at the conclusion of an in depth search for the truth.�

It is understood that the Moshi Rural CCM district chairman, Gabriel Masenga, is leading the probe and has vowed to take stern action against culprits who will be found, including stripping them of their own CCM membership, and written warnings sent to all party branches in the district about the presence of the fake membership cards.

But according to our sources, the fake cards are believed to have already been used in the recently-held primaries for local government leaders in the district.

According to Chiligati, legitimate party cards are henceforth to be dispatched to new members straight from CCM headquarters in Dar es Salaam, via regional party secretaries who will hand out the cards according to lists prepared by district party secretaries.

He said special member registers are currently being printed by the Government Printer, which will be used to register genuine party members to vote in next year’s primaries.

Every voter will only vote at the location where his or her name is listed in the special register, and nowhere else, Chiligati further explained.

The CCM primaries are scheduled to take place before August next year, to nominate CCM contestants for councilorship and parliamentary seats in the general election a couple of months later.
 
Kiongozi wa ufisadi huu atakuwa si mwingine bali ni Rostam Aziz ambaye ameitia CCM na Serikali mifukoni mwake.
 
Ha ha ha ha....LOL! Hii issue ni kubwa sana ya mafisadi kutaka kuiteka CCM na kuwaondoa "maadui" wao wote ambao ni wapiganaji dhidi ya Mafisadi. Hata baadhi ya wapiganaji wametishiwa uhai wao.
 
CCM wamezoea kuiba kura kwenye uchaguzi sasa wanajiibia wao wenyewe. Mpaka apatikane mshindi kwenye uchaguzi wao usishangae wote watakaochaguliwa wakawa ni mafisadi.
 
Ha ha ha ha....LOL! Hii issue ni kubwa sana ya mafisadi kutaka kuiteka CCM na kuwaondoa "maadui" wao wote ambao ni wapiganaji dhidi ya Mafisadi. Hata baadhi ya wapiganaji wametishiwa uhai wao.
Habari yote imekaa kufikilika tu, CCM haina lengo hilo na kamwe haitaweza kuwa na lengo kama hilo.

Hii haina maana kama hakuna baadhi ya Wanachama wake wenye mawazo kama hayo ya kutetea ufisadi at any cost, but at the end of day wataumbuka tu.

(font hizo kaka)
 
UCHAGUZI 2010

Mafisadi waibuka
na mkakati mpya

*Wachapisha kadi bandia kuwang'oa wapambanaji
*CCM yawashitukia, makachero nao waingia kazini

MWANDISHI WETU
Dar es Salaam

WATUHUMIWA wa ufisadi pamoja na kuzidi kubanwa kila kona, bado wanaendelea na mikakati yao ya kimajitaka safari hii, wakitumia mbinu ya kuingiza watu wao katika nafasi za ubunge na udiwani katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 na sasa wamebainika kuchapisha kadi bandia za CCM kutimiza azma hiyo.

Tayari vyombo vya dola vimekwishajulishwa na vimeanza kuzifanyia kazi taarifa hizo baada ya kukamatwa kwa kadi kadhaa katika mikoa ya Dar es Salaam na Kilimanjaro.

Habari za ndani ya vyombo vya dola zimethibitisha kubainika kwa mkakati huo wa kihalifu ambao ulianza kutumika katika baadhi ya maeneo ya nchi, washiriki wakielezwa kuwa na nguvu kubwa ya kiuchumi.

Ofisa mmoja mwandamizi wa serikali ameliambia KULIKONI kwamba kumekuwa na mshituko ndani ya vyombo vya usalama kutokana na uhalifu huo kuwa na nia ya kuvuruga mfumo mzima wa uongozi wa nchi.

Siku za mwanzo za uongozi wa Rais Jakaya Kikwete katika serikali yake na ndani ya CCM, alionyesha waziwazi kukerwa na utaratibu ambao unatoa mwanya wa rushwa na alianzisha mchakato wa kukabiliana na hali hiyo.

Dhamira hiyo njema ya Kikwete ilikisukuma chama hicho kubadili mfumo wake wa upigaji kura za maoni pamoja na udhibiti wa kadi za wanachama wapya wanaojiunga nacho kuepusha kuingizwa kwa ‘mapandikizi' yatakayovuruga, ukiwa unafanyiwa kazi, mafisadi wameiasi azma hiyo.

Maofisa Usalama wa Taifa wameelezwa kuingia kazini sasa baada ya kubainika kuwapo kwa kundi kubwa la wahalifu lililoanza kusambaza kadi bandia kwa nia ya kupandikiza wanachama wengi watakaoshiriki upigaji kura za maoni za udiwani na ubunge kwa matakwa ya wanaozichapisha kadi hizo ambao wana historia ya ufisadi na hata uhalifu mkubwa wakiwamo majambazi.

Kwa mujibu wa mwenendo wa kisiasa nchini, huenda mkakati huo ulilenga kuwang'oa wabunge na madiwani wa CCM ambao ni kikwazo kwa mafisadi kutokana na msimamo wao mkali wa kusimamia maslahi ya Taifa kwa kupinga rushwa na ufisadi.

Tayari wanamkakati hao walionekana kutaka kufaidika na utaratibu mpya kwa wanachama wote wa CCM wenye kadi halali ndio walioruhusiwa kupiga kura za maoni katika maeneo yao badala ya utaratibu wa zamani ambao kura hizo zilipigwa na viongozi wachache katika kata.

Uongozi wa juu wa CCM akiwamo Katibu wa Itikadi na Uenezi, CCM, John Chiligati, umethibitisha kupokea taarifa za kuwapo kwa kadi bandia katika baadhi ya maeneo lakini wamesema eneo ambalo kuna ushahidi ni wilaya ya Moshi Vijijini yenye majimbo mawili la Moshi Vijijini na Vunjo.

Majimbo hayo sasa yanaongozwa na Cyril Chami, ambaye ni Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko na Aloyce Kimaro, ambaye amekuwa mwiba kwa watuhumiwa wa ufisadi na wote sasa wanaandaliwa mikakati ya kung'olewa kwa gharama yoyote.

Katibu Mkuu wa CCM, Yussuf Makamba alisema kwa sasa yuko likizo na kazi zake zinafanywa na Naibu wake, George Mkuchika, ambaye kwa upande wake alidai hakuwa na taarifa rasmi kuhusiana na kuwapo kwa kadi bandia zinazosambazwa bila kufuata taratibu mpya za chama hicho tawala.

Mkuchika alionekana kutofahamu yanayoendelea katika chama kwani Chiligati yeye si tu alikiri bali alionekana kufahamu hata hatua zilizokwishachukuliwa kwa kusema tayari suala hilo limeripotiwa na linafanyiwa kazi na viongozi wa wilaya husika na majibu yatatolewa wakati wowote baada ya uchunguzi wa kina kukamilika.

Wilayani Moshi Vijijini, imebainika kwamba kadi hizo zimekamatwa katika maeneo ya Kimochi, Okaoni, Uru Kaskazini na Longuo na uongozi wa CCM wilayani humo wamekwishachukua hatua ya kufuatilia suala hilo.

Mbali ya kuchukua hatua kuhusiana na usambazaji wa kadi bandia, uongozi wa wilaya hiyo umetoa karipio kali kwa baadhi ya watu walioanza kufanya mikakati ya kuwavuruga wabunge wa sasa kwa nia ya kuwazuia kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho ya 2005.

Hatua ambazo zimeelezwa kuchukuliwa na kamati ya siasa Wilaya chini ya Mwenyekiti wa CCM Moshi Vijijini Gabriel Masenga ni pamoja na kuagiza uchunguzi ufanyike na wote watakaobainika wachukuliwe hatua kali ikiwemo kuvuliwa uanachama.

Katibu wa CCM wa Wilaya hiyo Cosmas Kasangani pia ameamriwa kuandika barua kutahadharisha kata zote kuhusu ukiukwaji huo wa taratibu na usambazwaji wa kadi bandia pamoja na kuwakemea wanachama waliotajwa kuhusika na matukio hayo.

Mbali ya uchaguzi mkuu wa mwakani, imebainika kwamba kadi hizo baadhi zimetumika katika mchakato wa kuwapata wagombea nafasi za uongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa.

Mbali ya mikoa ya Dar es Salaam na Kilimanjaro, kadi hizo bandia zimeelezwa kusambazwa katika mikoa ya kanda ya ziwa na Nyanda za Juu Kusini, kwa lengo la kuwang'oa wabunge wanaoonekana kuwa mwiba kwa mafisadi na wahalifu wengine.

Baada ya mchakato wa muda mrefu ulioanzishwa na Rais Kikwete na watendaji wake, Halmashauri Kuu ya Chama hicho (NEC) iliweka masharti ya watu kujiunga na chama hicho kabla ya uchaguzi mkuu ujao ili kuwaepuka watu watakaojiunga na chama hicho kwa lengo la kuwapitisha watu wao wakati wa kura za maoni.

Miongoni mwa masharti hayo ni pamoja na kutoingizwa mwanachama mpya yeyote kuanzia Juni 30 mwakani na pia kuandikisha majina ya wanachama wote katika rejesta kupitia matawi kuanzia mwezi huu au ujao hadi mwakani (Juni) ili kuepuka watu kuingia kiholela.

Imeelezwa kwamba uamuzi huo wa NEC ulianza kuzungumzwa tangu kikao cha mwaka jana Butiama mkoani Mara na umepitishwa ili kupunguza vurugu za kuharibu haki katika kura za maoni ambazo zingetokea kama utaratibu huo usingepitishwa.

Hata hivyo taarifa rasmi ya CCM iliyotolewa na Chiligati ilikanusha kuwapo kwa kadi bandia katika mchakato wa kampeni na uchaguzi unaoendelea wa Serikali za Mitaa.

Kuhusu uwezekano wa watu kutumia mwanya huo kujiandikisha kabla ya Juni, Chiligati alisema kadi kwa ajili ya wanachama wapya zitachukuliwa makao makuu ya chama na kwamba makatibu wa CCM wa mikoa watakabidhiwa idadi ya wanachama wapya na Katibu wa Wilaya kutoka kwa Katibu wa Tawi kwa utaratibu maalumu utakaowekwa.

Chiligati alinukuliwa akisema kwamba utaratibu wa kupokea wanachama wapya utaendelea tena Agosti mwakani baada ya kura za maoni ili mambo yafanyike kwa haki na kwamba katibu wa ngazi hizo mbili (mkoa na wilaya), atakayebainika kufanya hujuma, atafukuzwa kazi au kupewa adhabu kali.

Alisema kwa sasa rejesta zinaandaliwa kwa Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali na kila mwanachama ataandikishwa katika tawi lake anakoishi na ambako mwakani atapiga kura katika tawi hilo hilo na si vinginevyo.

Kura hizo za maoni zitapigwa mwakani kabla ya Agosti na kwa mujibu wa utaratibu huo mpya wa CCM, kila mwanachama katika tawi lake ataruhusiwa kupiga kura hizo kumchagua mtu atakayesimama kuwania udiwani na ubunge kupitia chama hicho.

Kabla ya utaratibu huo, ni wajumbe wachache wa chama ndio waliohusika kupiga kura za maoni jambo lililojadiliwa katika vikao vya NEC kwamba linawanyima wanachama demokrasia na wakati mwingine inachangia kupitishwa mtu ambaye hakubaliki katika jamii.

Chanzo:KULIKONI Namba 758, Ijumaa, Septemba 25, 2009
 
Habari yote imekaa kufikilika tu, CCM haina lengo hilo na kamwe haitaweza kuwa na lengo kama hilo.

(font hizo kaka)

Sidhani kama kuna mtu anayezungumzia chama kama taasisi bali watu ndani ya chama hicho na ambao pia ni viongozi. Wanaweza wakawa si wote lakini wamo. Ndio maana nakubaliana na wewe kwamba CCM haiwezi kuwa na mpango wa kuweka mafisadi lakini wamo viongozi wenye nia hiyo.

Kuhusu habari "imekaa ya kufikilika": kama una maana ya kufikirika, nadhani umekosea maana uongozi wa CCM, Chiligati na uongozi wa CCM Moshi Vijijini umethibitisha hilo.

Hii haina maana kama hakuna baadhi ya Wanachama wake wenye mawazo kama hayo ya kutetea ufisadi at any cost, but at the end of day wataumbuka tu.

(font hizo kaka)

Hapo nakubaliana na wewe mia kwa mia kama nilivyoeleza hapo juu kwamba wataumbuka ama wameshaumbuka kwa kujulikana kwao. Lakini ujue hata wakijulikana ni vigumu sana kuchukuliwa hatua kwa sasa japo inawezekana.
 
Habari yote imekaa kufikilika tu, CCM haina lengo hilo na kamwe haitaweza kuwa na lengo kama hilo.

Hii haina maana kama hakuna baadhi ya Wanachama wake wenye mawazo kama hayo ya kutetea ufisadi at any cost, but at the end of day wataumbuka tu.

(font hizo kaka)

Ahsante Mkuu Kibunango, kama Watetezi wa Ufisadi ndani ya CCM wataumbuka basi itakuwa ni furaha kwa mamilioni ya Watanzania ndani na nje ya nchi ambao wanaona CCM imetekwa nyara na mafisadi ambao wamekuwa na nguvu ya kutisha ndani ya chama hicho. Tusubiri tuone kama kweli Watetezi wa ufisadi ndani ya CCM wataumbuliwa.
 
Kiongozi wa ufisadi huu atakuwa si mwingine bali ni Rostam Aziz ambaye ameitia CCM na Serikali mifukoni mwake.
Mkuu usifikiri haraka haraka kuwa ni huyo jamaa ndie kiongozi wa mkakati huo. Huko kwenye hiyo Kampuni (Chama) kumeoza kabisa kwa mbinu chafu kiasi huwezi kujua nani hasa Engineer wa mipango hiyo.Yeyote anaweza kwa sasa.
Mkuu BAK, Mlozi akishachoka kuloga majirani huwa anawarudia wanafamilia wake mwenyewe, ndivyo ilivyo kwa CCM sasa. Mbinu chafu zimefanywa kwa vyama vingine ktk chaguzi zilizopita sasa dhambi hiyo inaanza kula ndani ya Familia yao (chama) na huo ndio mwisho wa ukoo wa KILOZI.
SUBIRI UTASHUHUDIA
 
CCM wamezoea kuiba kura kwenye uchaguzi sasa wanajiibia wao wenyewe. Mpaka apatikane mshindi kwenye uchaguzi wao usishangae wote watakaochaguliwa wakawa ni mafisadi.

Sahihi 100%; mbinu zilezile wanazotumia kwenye uchaguzi mkuu dhidi ya vyama vingine sasa wanazitumia kuibiana wao kwa wao.
Nyerere alisema mtu akishaonja nyama ya mtu hawezi kuacha - hivyo mtu wa nje akikosa atamla mwanae; hayo ndiyo ya CCM! KIDUMU CHAMA CHA....
 
Mkuu usifikiri haraka haraka kuwa ni huyo jamaa ndie kiongozi wa mkakati huo. Huko kwenye hiyo Kampuni (Chama) kumeoza kabisa kwa mbinu chafu kiasi huwezi kujua nani hasa Engineer wa mipango hiyo.Yeyote anaweza kwa sasa.
Mkuu BAK, Mlozi akishachoka kuloga majirani huwa anawarudia wanafamilia wake mwenyewe, ndivyo ilivyo kwa CCM sasa. Mbinu chafu zimefanywa kwa vyama vingine ktk chaguzi zilizopita sasa dhambi hiyo inaanza kula ndani ya Familia yao (chama) na huo ndio mwisho wa ukoo wa KILOZI.
SUBIRI UTASHUHUDIA

Hata nyani wakishamaliza kupaamia miti yooote; wanaparamiana wenyewe kwa wenyewe, the same to CCM
 
Halisi,

Ninachojua mimi na ambacho ndicho pia nilihakikishiwa na viongozi wa chama wa wilaya ni kwamba tayari kuna utaratibu ambao unaondoa kama sio kupunguza kabisa tatizo ambalo limeongelewa kwenye makala hizo mbili.

Kadi zote CCM kuanzia sasa zunaagizwa na katibu wa CCM wa mkoa. Kama wilaya wanahitaji kadi basi wanaandika barua kwa katibu wa mkoa kuomba hizo kadi. Katibu wa mkoa ndiye anaomba hizo cards toka makao makuu.

Zikifika wilayani, zitagawiwa kwa makatibu wa kata, ambao nao watagawa kwa makatibu wa matawi.

Pia CCM wanaanda daftari la wanachama wao; daftari hilo litahakikiwa ili kuhakikisha kadi zao ni zile ambazo zimepatikana kwa njia halali. Zoezi la kuingiza wanachama wapya litasimama 30/06/2010 ili kuwe na muda wa kutosha kuhakiki daftari la wanachama.

Utaratibu huo huo nimeusoma hata juzi juzi hapa JF. Nafikiri kama ni kweli kuna watu wanachapisha kadi basi ni criminals ambao huenda hata hawajui kwamba CCM imeandaa utaratibu wa kulipunguza hili tatizo. Watu watauziwa hizo kadi fake kwa bei poa na mwishoni wala hata hawatapiga hizo kura. Siamini kwa mfano mjumbe wa NEC au CC afanye hivyo maana atakuwa anajua utaratibu ulioandaliwa.

Bado viongozi wa CCM wanaweza kucheza fouls lakini most likely itakuwa fouls kwa kutumia kadi halali. Watu wa kuwaangalia sana kwenye uchaguzi wa CCM mwakani ni hao makatibu wa mikoa na wilaya.

Kingunge wa CCM akitaka kadi si atawaambia makatibu waombe? Sidhani kama atakuwa na haja ya kwenda kuchapisha kadi fake.
 
I am sure hao waliochapisha hizo kadi fake wanajua wanachokifanya. Tusiwaaunderestimate mafisadi.
 
CCM laana tullah hakika . Sasa wameanza kuchoma nyumba wakiwa ndani . Dhuluma ya ccm inawapa laana na mwish utasikia makubwa zaidi ya haya .
 
Uyasemayo ni sahihi kabisa na hiyo iko:

http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=3679

Lakini tatizo kubwa katika nchi yetu ikikaribia uchaguzi na wakati wa uchaguzi kunakuwa na mambo mengi ya aibu na wengi hufanya kazi kuhakikisha wanatengeneza mazingira ya kujinufaisha kwa njia za kifisadi. Kwa mfano kwa wale wanaokusudia kuwania ubunge ama wanaotetea nafasi zao wanashawishika kuingia katika gharama za kijinga kuwalipa watu ambao kila siku wanatunga jambo jipya la kuwawezesha kuendelea kuishi ikiwa ni pamoja na mambo kama hayo ya kihalifu. Pia watu ambao waliingia madarakani kwa mbinu chafu wataendelea (wao na wenzao) kufanya mambo ya kihalifu ikibidi hata kuchapisha kadi, vipeperushi (vichafu) ili kuhalalisha mipango yao ya kisiasa. Hayo kwa sasa itakuwa vigumu sana kuyazuia lakini ni lazima tukemee kwa nguvu zetu zote ili historia ije ituhukumu kwa hilo.
 
Halisi,

Najua kwa Tanzania ujambazi wa kwenye siasa ni real and live.

Nilichokuwa na question mimi kwenye hii habari ni juu ya kwanini mtu kama huyo ambaye ni kiongozi ahangaike kuchapisha wakati anaweza kuagiza makatibu waagize kadi halali toka makao makuu?

Tatizo la TZ ni sisi wananchi ambao tumewaruhusu wanasiasa kufanya kila aina ya madudu.

Pia kuna mkongwe wa siasa aliniambia hizo kadi ni cluster bombs, zikimwagwa zinaweza kudhuru hata huyo mnunuaji mwenyewe. Alisema uzoefu unaonyesha watu wengi wameshalizwa sana huko nyuma kwenye serikali za mitaa na hao hao waliowanunulia kadi. Lets hope huyo mkongwe yuko right.

Uyasemayo ni sahihi kabisa na hiyo iko:

http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=3679

Lakini tatizo kubwa katika nchi yetu ikikaribia uchaguzi na wakati wa uchaguzi kunakuwa na mambo mengi ya aibu na wengi hufanya kazi kuhakikisha wanatengeneza mazingira ya kujinufaisha kwa njia za kifisadi. Kwa mfano kwa wale wanaokusudia kuwania ubunge ama wanaotetea nafasi zao wanashawishika kuingia katika gharama za kijinga kuwalipa watu ambao kila siku wanatunga jambo jipya la kuwawezesha kuendelea kuishi ikiwa ni pamoja na mambo kama hayo ya kihalifu. Pia watu ambao waliingia madarakani kwa mbinu chafu wataendelea (wao na wenzao) kufanya mambo ya kihalifu ikibidi hata kuchapisha kadi, vipeperushi (vichafu) ili kuhalalisha mipango yao ya kisiasa. Hayo kwa sasa itakuwa vigumu sana kuyazuia lakini ni lazima tukemee kwa nguvu zetu zote ili historia ije ituhukumu kwa hilo.
 
CCM laana tullah hakika . Sasa wameanza kuchoma nyumba wakiwa ndani . Dhuluma ya ccm inawapa laana na mwish utasikia makubwa zaidi ya haya .
Hii ni kona ya CCM, huo Uchadema wako katafute bandiko la kuuweka
 
Back
Top Bottom