Thomas Sankara The African Che Guevara

Mkali wa Leo

Member
May 27, 2011
85
3
Ndugu msomaji wa makala hii vuta kiti chako ujifunze kitu hapa ...
Africa Ina MASHUJAA
---

MFAHAMU MWANAMAPINDUZI HAYATI RAIS THOMAS SANKARA KUTOKA NCHINI BURKINAFASO

Kama Kuna usemi umeshawahi kuusikia ya kwamba

“wema hawafi”

Basi usemi huo una ukweli ndani yake maana Mimi na wewe msomaji wangu wa makala hii bado tunamzungumzia na tuna shauku kubwa ya kumjua na kutaka kujifunza kwa MWANAMAPINDUZI Thomas Sankara.

Sina shaka kama ni mfuatiliaji wa siasa umeshalisikia jina hili.Thomas sankara alizaliwa tarehe 21/12/1949 huko Yaakov French upper volta (Jina la zamani la Nchi ya Burkinafaso) katika familia ya Bwana Joseph na mama Margaret Sankara ambayo ni familia ya kimisionari.Thomas Sankara alifahamika kwa jina la utani la The African che Guevara kutokana na misimamo yake mikali iliyomfanya akafananishwa na mwanasiasa gwiji kutoka Amerika ya kaskazini Che Guevara.

Kabla ya kuwa Rais wa Nchi ya Burkinafaso Thomas Sankara alihudumu kama waziri Mkuu katika serikali iliyokuwa madarani hadi kufika mwaka 1983 ambapo Thomas Sankara na rafiki yake wa karibu Sana toka wapo jeshini Braise Compare waliongoza mapinduzi ya kiamani kwa kumtoa madarakani Rais aliyekuwepo madarakani kipindi hicho. Rais Thomas Sankara alihudumu madarakani kuanzia mwaka 1983 Hadi mwaka 1987 alipouawa na rafiki yake wa karibu Braise Compare.Mwanamapinduzi na mwanamwema huyu wa Afrika alitawala nchi ya Burkinafaso kwa kipindi cha miaka mitatu na miezi sita.

Katika kipindi chake alipokuwa waziri Mkuu wananchi wa Nchi ya Upper volta jina la zamani la Nchi ya Burkinafaso walikuwa wanavutiwa sana na mtindo wake wa uongozi hali iliyoelekea Rais aliyekuwa madarakani kumuwekea vizuizi Thomas sankara hadi hapo alipofanikiwa kufanya mapinduzi.

MAFANIKIO YAKE KATIKA SERIKALI YA BURKINAFASO
Thomas Sankara ni mmoja wa wanamapinduzi aliyekuwa na maono ya kipekee ya kuivusha nchi ya Burkinafaso kutoka katika mawazo ya utumwa na kuanza kujitegemea kiuchumi,kisiasa na kiutamaduni.Maono yake yalitofautiana na viongozi wengi wa Afrika wa kipindi kile ikiwemo viongozi wenzake katika nchi ya Burkinafaso.

Thomas Sankara mara baada ya kuingia madarakani kama Rais alibadilisha jina la nchi hiyo kutoka kuitwa upper volta la kikoloni na kuiita nchi hiyo jina la Burkinafaso yaani ardhi ya watu wema na wanyoofu.Aidha Thomas Sankara alibadilisha bendera ya nchi hiyo na wimbo wa taifa wa nchi hiyo.

Kwakuwa alidhamiria kuinua uchumi wa Nchi ya Burkinafaso Thomas Sankara alipoingia madarakani alisitisha matumizi makubwa ya serikali kwa vitu visivyo na tija na aliekeza serikali yake itumie gari za kawaida ambazo zitakuwa Hazitumii mafua mengi na gari hizo hazina gharama kubwa.

Rais Thomas Sankara alipoingia madarakani alifanikiwa kuinua kiwango cha ufaulu na uwezo wa kusoma kwa wananchi wa Burkinafaso kutoka asilimia 13 mwaka 1983 hadi asilimia 73 mwaka 1987.

Alianzisha kampeni kabambe ya upandaji wa miti nchi nzima hadi kufikia miti milioni kumi huku akihubiri umuhimu wa utunzaji wa mazingira.

Katika kipindi Cha uongozi wa Rais Thomas Sankara ndipo wanawake wengi zaidi walipata fursa ya kujiunga na jeshi la nchi ya Burkinafaso.

Rais Thomas Sankara alihimiza katika kilimo cha mazao ya chakula na biashara ambapo hadi kufika mwaka 1987 zaidi ya ekari 3800 zilikuwa zinavunwa mazao ya ngano na mpunga wa kutosha kulisha nchi nzima.

Thomas sankara aliamini kuwa Nchi ya Burkinafaso inaweza kuendelea bila kuchukua mikopo kutoka IMF na world bank ambapo mikopo hiyo mingi ina masharti magumu kwa ustawi wa nchi.

Mwanamapinduzi Thomas sankara hakuweza kuwavumilia wala rushwa waliobainika katika uongozi wake na aliwafukuza mara moja katika serikali.

Rais Thomas Sankara aliamini katika usawa wa kijinsia kati ya wanawake na wanaume na hivyo katika serikali yake aliyoiunda aliweza kuwapatia nafasi zaidi wanawake sio tu katika wizara inayohusiana na mambo ya wanawake Bali hadi katika wizara nyeti za nchi hiyo tofauto na ilivyokuwa kwa nchi nyingi za Afrika kwa kipindi hicho.

Rais Thomas Sankara alikuwa muumini mkubwa wa uwazi na demokrasia na mara zote alipenda wananchi wa Nchi ya Burkinafaso watoe maoni yao bila woga wowote tofauti na viongozi wengi wa Afrika wa kipindi kile.

Rais Thomas Sankara alipata kuwa mwanamapinduzi msema ukweli hata katika mikutano ya Umoja wa Afrika OAU Ambapo alikuwa akiwashauri viongozi wenzake wa Afrika katika umoja huo kukataa kulipa mikopo mikubwa ya IMF na world bank na hii ni kutokana na ongezeko kubwa la riba katika mikopo hiyo na badala yake aliwashauri viongozi hao kuanza kuanzisha viwanda vya kutosha na kuchukua wataalam wetu wakasome ulaya na kisha kurudisha nyumbani utaalam wao.Thomas sankara anakumbukwa kwa maneno yake mazito na kauli mbiu yake ya “ To our homeland or death we shall win” yaani kwa ajili ya taifa letu tupo tayar kufa ili tushinde.Thomas sankara aliamini kuwa Afrika Ina masoko ya kutosha ya kuuza bidhaa zake na kama nchi hizi zitaungana basi umasikini utaisha Afrika.

Thomas Sankara ndani ya kipindi kifupi cha uongozi wake alianzisha viwanda vya nguo na alisisitiza sana wananchi wa Burkinafaso kufanya kazi kwa bidii ili kuikomboa nchi hiyo katika umasikini.

Misukosuko katika uongozi wa Rais Thomas Sankara ilianza kipindi Cha mwaka 1986 ambapo kulitokea mgomo mkubwa wa walimu na hivyo Rais Thomas Sankara aliwafukuza kazi zaidi ya walimu 1200 na kisha kuwapatia mafunzo vijana waliomaliza elimu ya juu ili wakawafundishe wanafunzi katika kipindi hiko cha mpito na hapo ndipo migogoro ilipoanza katika nchi ya Burkinafaso na wasomi wengi wakiupinga uamuzi wake huo.

KUPINDULIWA NA KUUWAWA KWA RAIS THOMAS SANKARA

Wataalam wa siasa wanasema Rais Thomas Sankara alikiona kifo chake na alikisubiri kwa sababu kipindi chote cha kutokueleweka kwake na nchi ya Ufaransa kwasababu Rais Thomas Sankara alipenda kushirikiana na mataifa mbalimbali bila kufungamana na upande wowote.Hali iliyopelekea watawala kutoka Ufaransa kukasirika kwani walitaka waendelee kulitawala taifa hilo katika ukoloni mambo Leo kwa kuhakikisha nchi ya Burkinafaso inaendelea kuwa ni soko la bidhaa kutoka Ufaransa na pia bajeti ya matumizi ya Nchi hiyo ikainufaishe nchi ya Ufaransa.Hivyo basi walimtumia rafiki wa Rais Thomas Sankara Bwana Braise Compare kuandaa mauaji dhidi ya Rais Thomas Sankara na hapo ndipo ikawa mwisho wa Rais Thomas Sankara. Tetesi za mauaji dhidi yake Rais Thomas Sankara alizipata, lakini hakuchukua hatua zozote kwani aliamini ubaya usitokee kwake bali utokee kwa wanaompinga.

Tarehe 15/10/1987 Rais Thomas Sankara aliuawa kikatili na kuzikwa usiku huo huo.Na kisha asubuhi yake Bwana Braise Compare rafiki wa karibu wa Rais Thomas Sankara alijitangaza kuwa Rais wa Nchi ya Burkinafaso.Rais Compare alitawala nchi ya Burkinafaso kwa miaka 27 hadi mwaka 2014.

Familia ya Rais Thomas Sankara ilifungua kesi ya mauaji dhidi ya Rais Thomas Sankara ambapo ilipofika mwaka 2022 ilithibitika katika mahakama ya Burkinafaso kuwa Rais Compare na wenzake 14 warishiriki katika mauaji ya Rais Thomas Sankara na Rais Compare alihukumiwa kifungo cha maisha jela.

JE UMEJIFUNZA NINI KATIKA MAKALA HII??

USIKOSE MAKALA IJAYO YA MASHUJAA WA AFRIKA

HAPA HAPA JAMII FORUM.
 

Attachments

  • thomas sankara.docx
    20.6 KB · Views: 7
Ndugu msomaji wa makala hii vuta kiti chako ujifunze kitu hapa ...
Africa Ina MASHUJAA
Acheni kukaririshwa uwongo. Dunia hii kulikuwa na Che Guevara mmoja na mmoja peke yake. Maisha ya Thomas Sankara hayana ushabihiano kabisa na harakati za Che Guevara

Msipotoshe watu, nenda ukachimbe zaidi
 
Back
Top Bottom