Military Genius
JF-Expert Member
- Mar 3, 2019
- 761
- 1,480
Pichani ni Thomas Paine, huyu Alikuwa ni Mwanaharakati, Mwanasiasa na Mwanafalsafa kutoka Uingereza aliyeishi US, ni mmoja wa Wanasiasa wanaokumbukwa sana US kwa Mchango wake katika Mapinduzi ya Amerika mwaka 1775 ambapo Alikuwa anatoa hotuba na kuandika maandiko yayolikuwa na ushawishi mkubwa sana kwa Watu.
Alizaliwa January 29, 1737 Norfolk UK, akaenda Kuishi US. Inaelezwa baada ya Kutoa mchango mkubwa katika Mapinduzi ya Amerika, akaenda kuishi Ufaransa pia alikotoa mchango kama huo kuelekea Mapinduzi ya Ufaransa mwaka 1789, Alikuwa maarufu sana huyu Jamaa.
Mbali na hayo, Thomas pia Alikuwa ni mpinga Dini ambapo alikuwa akiutumia uwezo wake mkubwa wa kuwashawishi watu kuwaambia kuwa Dini zote Duniani zilianzishwa na Binadamu, lengo likiwa ni kuwafanya watu kuwa Watumwa huku wao Wakitengeneza faida, Alikuwa akisema kuwa Dini yake ni akili yake mwenyewe.
Kejeli hizi dhidi ya Dini ziliwachukiza sana watu, hata baada ya kufariki June 8, 1809 huko New York US akiwa na miaka 72, Watu na taasisi nyingi waligoma kutoa maeneo yao ili azikwe, Watu waligoma kumzika, Akarudishwa kwao UK ambako pia watu Waligona kumzika!, Alizikwa na watu 6 tuu wa Serikali, tena Porini. Alitengwa na Kila mtu kutokana na Kejeli zake kwa Dini enzi za Uhai wake.
Thomas pia Alikuwa mwandishi maarufu pia wa Vitabu, aliandika vitabu vingi sana katika Uhai wake na hivi vilitumika sana Kuhamasisha mambo mbalimbali katika Jamii, Aliandika vitabu kama vile On the origin of free-masonry, Rights of Man, The Age of Reason, Common sense na Vingine vingi.
Katika Kitabu chake cha The Age of Reason kuna kauli Aliyoandika kuwa "Ni kutoka kwenye Dini ambako mwanadamu amejifunza ukatili, ubakaji, na mauaji. kwa imani ya Mungu mkatili humfanya mtu mkatili". Akaendelea Kuandika kuwa "Akili yangu mwenyewe ndiyo Dini yangu mwenyewe.
Katika kitabu hiki hiki pia Aliandika kuwa "Msimamizi mmoja mzuri wa shule anafaida zaidi kuliko Mapadre mia", Akaendelea kuandika "Taasisi zote za Dini kwangu zinaonekana kama ni uvumbuzi wa kibinadamu uliowekwa kutisha na kuwafanya watu watumwa, Kutawala kwa nguvu na faida.