Kwa wale msioamini katika dini na miungu yake

Kwa wale msioamini katika dini na miungu yake

Wakufoji

Senior Member
Joined
Jan 15, 2019
Posts
198
Reaction score
386
{ ✍️ Simple rule BIG protection }

Mimi mwenyewe ni miongoni mwa watu wanao zikataa dini.

Ila ninacho taka kuwa kumbusha wapinga dini wenzangu ni kwamba.

Tuzikatae DINI zote na MIUNGU yao kwa uwezo wetu wote ila JITAHIDI UWE NA MUNGU WAKO KWA IMANI YAKO ... nikiwa na maana zikatae Dini ila Amini katika UWEPO wa miungu nikimaanisha MUNGU YUPO ila hayupo katika muundo sawa na ule tunao elezwa na dini.

DINI zao zinatudanganya kwa kusema kua kuna MUNGU MMOJA pia tukifa tunaenda kwake Kauli hii si sahihi .. USAHIHI NI KWAMBA Kuna nguvu nyingi ambazo zina vyeo vya KIMUNGU .. na hizi nguvu hazimhitaji mtu .. BALI sisi wanadamu ndiyo tunazihitaji ili kurahisisha maisha yetu zenyewe hazimhitaji mtu.

Kwa mfano Kama unahitaji kutoboa kwenye biashara Basi uki cheza na hiyo nguvu unatoboa chapu sana . . Nje na hapo haufiki popote...huwez kutoboa ulimwengu wa biashara ukawa tajiri bila hiyo nguvu kuihusisha...IWE KWA NJIA YA GIZA AU NJIA YA NURU.


KWAHIYO NINACHO TAKA KUWAKUMBUSHA WAPINGA DINI NI KWAMBA.

Nguvu yenye cheo cha uungu ipo na ni nguvu ambayo ipo ktk makundi mengi sana .. DINI zinatudanganya ila ijapokua nguvu yenyecheo cha Umungu ipo.

Kwahiyo hatakama unazipinga dini usiache kusali au usiache maombi .. Sali kwa imani yako HAUHITAJI UELEWA WA KIKANISA AU KI ISLAM HAPANA .. njia nyepesi ni jitulize kisha kua mpole na kwaupole jiombee nia zako.

..hasa kwakua hauamini dini basi maombi yako yaelekezee kwenye roho yako zaidi . Yaan ukiwa unasali sema roho yangu nifanyie hivi na vile...{ Roho yako hukaa kwenye uti wa mgongo bila shaka hasa usawa wa tumbo karibia na kiuno uaelekezea akili eneo hilo mda wa kusali }

✍️ila tu uwe ktk hali ya upole na unyenyekevu na omba kwa upole pia .. sala yako itatimizwa haita hitaji hadi uwataje miungu wa kwenye Dini.

{ Watu wa dini wasichikijua ni kwamba sala zao zoote na miujiza yao hupokelewa na roho zao na miujiza hutendwa na roho zao bila kujali wametumia jina gani kusali. }


.. MIUNGU WAPO ila siyo kama tunavyo aminishwa kwenye DINI.Lakini pia ukisali sala itatimizwa bila kujali umemwomba Mungu gani roho ya muuombaji hutenda.


LAKINI PIA sala zako jitahidi uwe unasali kila asubuhi na jioni. Jua linaathari linapo zama au kuchomoza sala haiwez kuvuka mda huo kama ni sala ya kulindwa. { Nina ushahidi wa hili }


✍️TUZIPINGE DINI ILA BAADHI YA MAANDIKO YA VITABU VYAKE NI SAHIHI...HAKIKISHA UNA SALI HATA MARA 10 KWA SIKU UTAOKOLEWA NA MENGI.

Omba kwa ndani, omba kwa nje — lakini jua kwamba nguvu ipo NDANI YAKO.

Hakuna binadamu atakayeishi kwa kudra ya mwili tu — bali kwa nguvu ya ndani itokayo kwa Chanzo chake."
 
Back
Top Bottom