GE2025 Thom Mnkondya ajitosa ubunge jimbo la Tunduma

GE2025 Thom Mnkondya ajitosa ubunge jimbo la Tunduma

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,152
Kada wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Mtaalamu wa ardhi na Mjasiriamali Kijana Bw. Thom Mnkondya, Leo Jumanne Julai Mosi, 2025, amechukua rasmi fomu ya kuwania nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Tunduma kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika Ofisi za CCM Wilaya ya Momba.

1751436793594.png
Thom, ambaye amejizolea heshima kutokana na mchango wake mkubwa katika sekta ya ardhi, upimaji na uwezeshaji wa jamii kupitia elimu na uwekezaji, anaingia kwenye kinyang’anyiro hicho akiwa na ajenda ya maendeleo jumuishi na ushirikishwaji wa vijana na makundi yote ya jamii.

Kupitia taasisi alizozianzisha na kuziongoza, zikiwemo LAPEX Group Ltd na LAPEX Properties, Thom amekuwa mstari wa mbele katika kutatua changamoto za ardhi, kutoa ajira, na kuhamasisha matumizi bora ya ardhi kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Hatua yake hii ya leo imepokelewa kwa hamasa kubwa na wananchi, hasa vijana, ambao wamekuwa mstari wa mbele kumuunga mkono wakiamini kuwa ana dira sahihi kwa mustakabali wa Tunduma.
 
Moja ya vijana waliokuwa wakisubiriwa kwa hamu kubwa kuchukua fomu ya kuwania ubunge Jimbo la Tunduma ni Thom Mnkondya, ambaye leo amekamilisha hatua hiyo muhimu.

Thom ameendelea kujizolea umaarufu mkubwa miongoni mwa vijana na wakazi wa Tunduma kwa ujumla kutokana na uaminifu, uchapakazi, na mchango wake mkubwa katika sekta ya ardhi na maendeleo ya jamii.

Anatajwa kuwa kijana wa kwanza mzawa wa Jimbo la Tunduma kuchukua fomu ya kugombea ubunge tangu jimbo hilo lianzishwe — hatua ambayo wengi wanaiona kama historia mpya kwa Tunduma.

Wengi wanaamini kuwa ujio wa Thom katika kinyang’anyiro hiki ni mwanzo wa enzi mpya ya uongozi unaojali watu, wenye dira, na ushirikishwaji wa vijana katika maamuzi ya maendeleo.
 
Attachments

  • 27b55e79-ea23-4154-ad03-64c520f61053.jpeg
    27b55e79-ea23-4154-ad03-64c520f61053.jpeg
    701.2 KB · Views: 30
  • 913a5124-8aee-4118-b690-7cc837bef9c1.jpeg
    913a5124-8aee-4118-b690-7cc837bef9c1.jpeg
    595.3 KB · Views: 31
  • 08b1b39c-6b93-4a4e-9113-34ee4bc400b5.jpeg
    08b1b39c-6b93-4a4e-9113-34ee4bc400b5.jpeg
    508 KB · Views: 32
  • f34baf58-3cd2-4066-ba2c-1e3cd740edcd.jpeg
    f34baf58-3cd2-4066-ba2c-1e3cd740edcd.jpeg
    89.7 KB · Views: 30
Moja ya vijana waliokuwa wakisubiriwa kwa hamu kubwa kuchukua fomu ya kuwania ubunge Jimbo la Tunduma ni Thom Mnkondya, ambaye leo amekamilisha hatua hiyo muhimu.

Thom ameendelea kujizolea umaarufu mkubwa miongoni mwa vijana na wakazi wa Tunduma kwa ujumla kutokana na uaminifu, uchapakazi, na mchango wake mkubwa katika sekta ya ardhi na maendeleo ya jamii.

Anatajwa kuwa kijana wa kwanza mzawa wa Jimbo la Tunduma kuchukua fomu ya kugombea ubunge tangu jimbo hilo lianzishwe — hatua ambayo wengi wanaiona kama historia mpya kwa Tunduma.

Wengi wanaamini kuwa ujio wa Thom katika kinyang’anyiro hiki ni mwanzo wa enzi mpya ya uongozi unaojali watu, wenye dira, na ushirikishwaji wa vijana katika maamuzi ya maendeleo.
Muhendisamu huyu kaka Thom, nimempenda bureee
 
Back
Top Bottom