This week in Perspective: Kipindi kinamlenga nani?

Lengo la kipindi hiko ni moja tu, makomredi hukunbuka zama zao za shule/vyuo na mijadala kwa lugha ya kingereza.
 
hivi bado ulimwengu huu kuna kitu kinachoitwa tbc.

tido hakuondoka nayo kweli?!!
 
hivi bado ulimwengu huu kuna kitu kinachoitwa tbc.

tido hakuondoka nayo kweli?!!

heri yao wenye macho mpatao kuyaona ya ulimwengu huu yaliyo jaa hila na hadaa.
tbc ?!!!
napita............
 
Kuna kipindi – “This week in perspective” - kinarushwa na TBC1.

Kipindi hiki nakipenda kwani hua na mijadala mizuri ya kuelimisha jamii. Ila kwa upande wangu naona yanayojadiliwa hayawafikii watu wote, si kwa sababu watu hawana runinga, bali kwa sehemu kubwa lugha inayotumika ni ya kiingereza na watu wengi hawajui lugha hiyo.

Sasa sielewi kama kimewekwa kwa ajili ya watu wanaojua kiingereza tu au ni kwa ajili ya watu wote, kama ni kwa ajili ya watu wote, ingefaa watumie lugha ya Kiswahili ili kila mtu anayekisikiliza/tazama apate kile kilichokusudiwa.

ISIDINGO ya ITV INAMLENGA NANI?
 
Bahati mbaya mleta mada hata hajui misingi ya kuanzisha kipindi cha television, kwa faida pia ya wana jamvi, kipindi cha tv kabla ya kuanzishwa lazima kinakuwa na target audience, sio lazima kipindi kitazamwe na kila mtu, ni ajabu sana kumkuta Baba yako anasubiri kile kipindi cha wema sepetu eatv, lakini ni rahisi sana kumkuta beki tatu anasybiri kipindi cha wema au uswaz, kwa hiyo kipindi cha TWIP kinakuwa na target audiences yake ambayo ni lazima iwe inaongea kingereza, tuache jazba za kipuuzi tuangalie mambo kwa mapana kabla hatujaposti humu
 
Nimekuwa nikifuatilia mijadala mbalimbali inayoongozwa na Adam Simbeye katika kipindi cha THIS WEEK IN PERSPECTIVE kinachorushwa na TBC.Katika hivi vipindi muongozaji anajitahidi kuibua mijadala mizito sana yenye maslahi makubwa kwa taifa letu.Aidha muongozaji anajitahidi kuwatafuta washiriki(panellists)wenye uwezo mkubwa sana katika kuchambua mada husika.
Katika kufuatilia hii mijadala nimekuwa nikijiuliza sana;kwanini mambo ya msingi yanayohusu mustkabali wa nchi yetu kama katiba ya Tanzania yajadiliwe kwa lugha isiyoeleweka kwa walio wengi?Yani lugha ya kiingereza itumiwe na waswahili wachache wanaoijua ili kufikisha ujumbe kwa waswahili wenzao ambao hawajui kiingereza?Kwa nini wasitumie kiswahili ili waliowengi wafaidi mjadala unaohusu mustakabali wa nchi yao?Ni nani hasa walengwa wa ile mijadala?
Mijadala mizuri inaelimisha,inaburudisha,inatatua matatizo,inakuza akili na kuimarisha afya ya ubongo lakini sharti lugha ieleweke kwa walengwa.Walengwa wasipoelewa lugha unayozungumza hawatakusikiliza na mjadala utapoteza maana yake.
Kuna wakati nakuwa na watu wasioelewa kabisa kingereza wakati hiki kipindi kinaendelea lakini pale ninapoweza kuwaeleza tunafurahi pamoja,pale na mimi ninaposhindwa kuelewa na kuwaelezea tunahuzunika pamoja halafu tunasonga mbele pamoja.
Sio imani yangu kwamba kutumia kiingereza kwenye mijadala yetu ndio tutaonekana tunajua sana yale tunayoyajadili wala sio imani yangu kwamba ili mjadala unoge sharti tuongee kizungu pia sio imani yangu kwamba muendesha kipindi anafikiri mijadala yenye matunda mazuri au “matokeo makubwa”(BIG RESULTS) lazima kingereza kitumike.
RAI YANGU;wakati umefika sasa tuachane na lugha ya kikoloni na isiyoeleweka kwenye kujadili mambo kwa mustakabali wa nchi.
 
angalia unavyoweza kuelewa, English ni official language kwa tanzania so ni sahihi kutumia lugha hiyo
 
mtoa mada angeweza pia kuuliza magazeti ya guardian, citizen, daily news na the african yanamlenga nani vile vile.
 
Kuna kipindi – “This week in perspective” - kinarushwa na TBC1.

Kipindi hiki nakipenda kwani hua na mijadala mizuri ya kuelimisha jamii. Ila kwa upande wangu naona yanayojadiliwa hayawafikii watu wote, si kwa sababu watu hawana runinga, bali kwa sehemu kubwa lugha inayotumika ni ya kiingereza na watu wengi hawajui lugha hiyo.

Sasa sielewi kama kimewekwa kwa ajili ya watu wanaojua kiingereza tu au ni kwa ajili ya watu wote, kama ni kwa ajili ya watu wote, ingefaa watumie lugha ya Kiswahili ili kila mtu anayekisikiliza/tazama apate kile kilichokusudiwa.

Ndugu Ulimbo, unaki-idea kuhusiana na TV programming? Huwa kuna vipindi vinaandaliwa maalumu kwa ajili ya kundi fulani la watu, ndio maana ktk Broadcasting and Announcing Skills kuna kitu kinaitwa "Audience Characteristics"
 
TBC 1 wana kipindi hiki mara 3 kwa week.

Aisee ni kipindi cha hovyo sana. Ni bora hata wangetumia huo muda kuonyesha Bunge Live.

Kipindi hakieleweki japo naelewa kiingereza vizuri sana.

View attachment 1094040
20190511_145516.jpeg
 
Hembu kuwa hadhiri, unasema unaelewa Kiingereza bado hukielewi kivipi? Kuelewa kwako Kiingereza kungekusaidia kuelewa kipindi. Labda ubainishe wazi nini kinakusumbua!
 
Mkuu hebu jazia nyama kidogo ili tuchambue vizuri,mada zinazojadiliwa hazieleweki au waalikwa hawavutii? au kiingereza chao ni colloquial?
 
Back
Top Bottom