Kumbe unamsifu kwa balagha tu, nilidhani unatuambia kizito zaidi. Na hata hivyo, si kweli amepandisha viwango. Kina hayati Kambarage walikuwa weledi mahsusi wa balagha, na wanafunzi wake, kina Benjamin na Edward, marehemu, Allah amrehemu. Na haikusaidia. William katuuza, Edward "kauliwa," Kambarage kang'atuka (kilugha, Kiswahili kakimbia), kachaniwa Azimio la Arusha Zanzibar, kafa, kasahaulika, kapita, ufisadi umerudi kwa kwenda mbele, funika kombe mwanaharamu apite. Lakini kwa kuongea humshindi Kambarage, John Mnyika hajaleta viwango vipya.
Hatutaki balagha na porojo, kina Magufuli wanatosha, na wametuchosha, tunataka vitendo.