Kwa kweli haihusiani kabisa na hg... ni ya mimi na wewe. Ambapo baada ya kuzunguka zunguka sana hapa chit chat nikitafuta mtu, mdada, mwenye siha, hiba na sifa njema awe kapo mwenzangu hapa, ghafla, yani ghafla kama vile parachichi linavodondoka juu ya mti wake puu... yani moyo wangu umedondokea kwako. Kwa sentensi hii moja, na
kiwatengu akiwa shahidi na mshenga, ninayo furaha, heshima na taadhima, kuwasilisha maombi hayo matukufu mbele ya uso wako mpole, nikiamini, kama ambavyo umekuwa mwema daima, utayachukulia kwa uzito unaofaa, na kunipa jibu litakalonihakikishia furaha kuwa umenikubalia...
Jawilat. .. napenda kuwasilisha...