This FRIDAY ON Star TV TUONGEE ASUBUHI - By Paul Mabuga (HOST) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

This FRIDAY ON Star TV TUONGEE ASUBUHI - By Paul Mabuga (HOST)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Yahya Mohamed, Dec 23, 2010.

 1. Yahya Mohamed

  Yahya Mohamed Verified User

  #1
  Dec 23, 2010
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kwa nini watanzania wananyimwa fursa ya kuwa na Nishatiya uhakika?

  Michango, maoni ya wanaJF inakaribishwa katika mjadala huu
   
 2. Yahya Mohamed

  Yahya Mohamed Verified User

  #2
  Dec 23, 2010
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  [​IMG] Re: Star tv mijadala.

  '' Kwa nini watanzania wananyimwa fursa ya kuwa na Nishati ya uhakika ya Umeme'' IJUMAA WIKI HII - 24.12.2010

  Muongozaji,
  Taifa letu hili ni changa na lenye changamoto lukuki katika ukiaji wake, tunazo changamoto hasi na chanya.
  • Taifa halina misingi/mipango endelevu juu ya janga hili la umeme.
  • Taifa haliwezi kusonga mbele kimaendeleo pasipokuwa na nishati kamilifu na yenye kuvutia hata wawekezaji.
  • Kwa nyakati tofauti taifa limeshuhudia tatizo la nishati bila ufumbuzi wa kudumu, tunarithisha tatizo hili kwa vizazi pasipo kulitafutia ufumbuzi yakinifu.
  • Nishati ya umeme inadidimiza wananchi kwa kushindwa kuendeleza hali zao za ujasiriamali na kukuza uchumi wa taifa letu.
  • Maendeleo yahitaji nishati, hapa namaanisha maendeleo ya rasilimali watu-KIELIMU, maendeleo ya nchi-KIVIWANDA etc,,vyote vyategemea nishati hii adhimu ya umeme. kinyume chake kumekuwa na mipango mibovu na isiyo na dira ya janga la umeme kuwa ni historia walau tu kwa kizazi hiki.
  • Katika kipindi hiki cha mitikisiko ya uchumi duniani, tungetegemea kutoweza kuona janga la umeme kuikumba nchi yetu...bali matokeo yake tumeruhusu kuuyumbisha uchumi wa nchi tena kwa tatizo la nishati.
  nadhani ifike wakati sisi wananchi wa kawaida tuangaliwe vema na wakuu wetu wa nchi,

  REPPLIED BY MPEVU c/f from MIJADALA STAR TV THREAD
  Yahya M
   
 3. chokambayaa

  chokambayaa JF-Expert Member

  #3
  Dec 23, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 528
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Hakuna mipango thabiti ya nchi ya kupambana na janga hili
  viongozi wamekalia kula na kusahau wapiga kura wao
  aliyeshiba hamtambui mwenye njaa

  Nadhani wanataka kuuza generator zao kwanza we fikiria
  ukianzisha umeme wako tanesco wanakuletea zengwe
  Hakika wajinga ndio waliwao(wananchi)
   
 4. Nicky82

  Nicky82 JF-Expert Member

  #4
  Dec 23, 2010
  Joined: Mar 14, 2009
  Messages: 939
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tatizo la umeme Tanzania ni matokeo ya kuleta siasa kwenye sehemu ambazo hazitakiwi siasa. Umeme imekuwa ni kama zawadi kwa watu kumchagua mtu fulani, ndio maana Slaa kwa mfano wakati wa kampeni zake hakuwa akitaja kupeleka umeme sijui kijiji au mji gani kwa sababu umee ni huduma muhimu kwa jamii na serikali yoyote ina wajibu wa kusambaza umeme.

  Tatizo linapokuja pale CCM wanapotumia umeme kama karata ya siasa na kuombea kura na wananchi aitha kwa ujinga au kwa kutotambua wamekuwa wakichukuliuia hivyo, umeme kama zawadi badala ya umeme kama huduma ya lazima kwa jamii.

  Tatizo lingine ni viongozi kukosa vision na mipango ya muda mrefu. Pamoja na ukweli kuwa idadi ya watanzania inaongezeka na mahitaji ya umeme kuongezeka lkn vyanzo vya umeme vimekuwa haviongezeki kulingana na kasi ya mahitaji ya umeme.

  Hadi hapo viongozi watakapokuwa na nia ya kweli ya kutatua tatizo hilo vinginevyo tatizo litabaki kila siku na wimbo utakuwa huo huo
   
 5. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #5
  Dec 23, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Uzembe, ufisadi na umimi umejaa; ondoa monopoly ya Tanesco; Tanesco ibaki na kazi ya Power Generation tu; Distribution na Transmission iwe privatised na makampuni mengi binafsi yatoe huduma hizo
   
 6. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #6
  Dec 23, 2010
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,229
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  hivi Mnyaribombo ina maana gani Yahya?
   
 7. m

  masoudmwevi Member

  #7
  Dec 23, 2010
  Joined: Aug 5, 2008
  Messages: 53
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Tunapozungumzia maendeleo ya taifa lolote lazima kwanza lifanye mapinduzi kwenye viwanda, lakini huwezi kuwa na viwanda bila ya kuwa na umeme Endelevu(sustainable) hivyo basi kwa kuwa viongozi wetu hawako tayari kuleta maendeleo kwa wananchi wake wao wanadhani maendeleo ni kutuongezea majengo ya kuhifadhia bidhaa (warehouse) ambazo zinajaa bidhaa toka nje na kuigeuza nchi yetu soko la mitaji ya watu wa nje kwa kujaribia bidhaa zao.
  1) Kuna sababu gani wanashindwa kujenga kituo cha kuzalisha umeme mto Malagarasi au ndo ile hadithi alohadithia Kafulila kwenye mchakato majimboni kuwa kuna vyura muhimu sana pale watapotea?
  2) Umeme wa upepo inashindikana nini
  3) Wakati nikiwa nasoma kuna mwalimu mmoja alikuwa anatokea Molecular biology and bio-technology pale UDSM alisema wao (nayeye) walifanya utafiti kuhusu taka zinazotupwa dsm kuwa ipo namna ya kuzitumia kumaliza tatizo loa umeme dar, je wanasiasa hawaoni haja ya kutumia tafiti hizo za kisomi ?
   
 8. D

  DENYO JF-Expert Member

  #8
  Dec 23, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 699
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Asante kwa mada hii muhimu -awali ya yote nianze kwa kuwapa shime star tv -mzee diallo ameamua kutokuwa mnafiki big up

  tatizo la umeme ni matokeo ya haya yafuatayo

  1. Tuna watawala sio viongozi wenye mipango, viongozi wenye nia ya dhati kuona mabadiliko, viongozi wanaochukia umaskini, viongozi wanaokerwa na huduma duni za watanzania tumewakosa -na wanapojitokeza viongozi kama hao wanachakachuliwa. Tuna watawala ambao wapo kwa maslahi yao wasiokuwa na mipango, wanyonyaji na wasiowajibika.

  2. Wataalamu waliokabidhiwa majukumu nao wamezika utalamu wao na kuwa wanafiki -wanachofanya sasa ni kuwafurahisha watawala. Tanesco ikipata watu wenye msimamo wasio yumbiswa na watawala nchi tunaweza kuweka umeme kila kona. Lakini watawala wetu wemeingia huko na mikataba mibovu kama iptl, dowans, richmond huu ni umbumbu mkubwa. Hatuna watendaji kuanzia katibu wa wizara hovyo, wakuu wa tanesco hovyo -wanashindwa kukusanya malipo kinachokusanywa analipwa iptl lini tutapiga hatua?? Nchi itakuwa giza siku zote kwa sababu hakuna anyeweza kufikiri kati ya hao watawala na watendaji ni unafiki na matanuzi ya hovyohovyo tuuu

  3. Tatizo la umeme ni ujinga wa watanzania tunaoendekeza umbayuwayu -hawa watawala na watendaji wanatuona watanzania mabwege na ambao hatuna maamuzi. Watu wameshindwa kazi wanachakachua wanarudi madarakani badala ya kufanya kazi wanaendelea kupiga wabunge kwenye chaguzi za mameya -hii ni hatari kubwa. Watanzania tumeonewa sana na watawala wetu hawaoni aibu kutunyanyasa.

  4. Tatizo la umeme matokeo ya ufisadi kuanzia juu hadi chini

  nini kifanyike

  1. Nia ya dhati kwa watanzania kuwafanya hawa watawala wawe viongozi -kwa kuwasema saana, kuwatoa, kuwagomea na kuweka watu wenye uchungu na nchi hii sio wasanii tulionao, -nasikitikita sana kumchakachua slaa

  2. Watendaji waache unafiki na uoga -walitumike taifa kwa akili zao bila kumwogopa rais kikwete au pinda -bora kuondolewa kuliko kuwa mnafiki wafike sehemu waseme enough is enough -hawa watawala bila kufanya hivyo hakuna lolote. Kwahiyo mkurugenzi wa tanesco badala ya kulialia amekosa pesa kwanza akusanye pesa na aitumie pesa hiyo kuliinua shirika hilo siyo kulipia mikataba kandamizi kama iptl richmond na dowans-mhando asikimbilie kupandisha bei akusanye kwanza vizuri umeme mwingi unapotea, mapato mengi yanatumika kifisadi.

  3. Mikataba yote mobovu ivunjwe hakuna mkataba wa milele kama hauna tija -inatunyonya. Mfano unakuta mkataba wa kulipa kwa siku milion 500-hii kweli akili au matope??

  4. Anasa zimekuwa nyingi kwa serikali hii-waziri naibu waziri wa nini? Anakazi gani?? Tanesco iachwe huru bila kuingiliwa na hawa watawala.
   
 9. Kiresua

  Kiresua JF-Expert Member

  #9
  Dec 24, 2010
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 1,202
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Paul Mabuga, asante sana kwa kutuletea mjadala huu mzuri kuhusu umeme!
  Napenda kumuuliza Waziri maswali 1
  1) kwa nini serikali kama mdaiwa mkuu wa TANESCO asiwe mfano wa kulipa madeni yake, wanasema tuu lipeni madeni yenu.... wanatutwisha mizigo mikubwa lakini wao hata kidole hawaweki... ingawa kweli tunadaiwa. SERIKALI ilipe madeni yake kwanza
  2) Mhusika wa TANESCO anasema ongezeko la bei ni kidogo ambayo iko ndani ya uwezo wa wananchi. nimeshangaa sana kauli hii, watumiaji wa kati ndo wanalipa umeme kuliko watumiaji wengine wote kama viwanda n.k. sasa basi hivi wanatuona hatuna akili Watanzania? yaani kutuambia eti ongezeko ni kidogo sana, eti sh 11 tu, 28 tu, kama vile ni kodogo sana!!! mnasahau kuwa bei ya umeme itakavyopanda wenye viwanda wataendelea kuongeza bei ya bidhaa zao, na mwisho wa siku atakaye umia ni mtanzania wa chini, huyu unayemuambia eti tumeongeza sh 11 tu, fikiria kila kitu kitakacho zalishwa, au kuuzwa kitaongezwa bei.... nani atakaye umia????........ jamani msitufanye bado ss ni wajinga

  Mabuga tafadhali wasilisha hili
   
 10. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #10
  Dec 24, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Tunanyimwa nishati ya umeme kutokana na wanasiasa kuingiza siasa kwenye maswala ya umeme.

  Kitu kingine hawa wanasiasa wanalikamua mno shirika la umeme angalia mikataba ya kinyonyaji.

  Dili za kuingiza tenda za kuzalisha umeme zinatengenezwa na wanasiasa lengo kujipatia ulaji.

  Kupandisha bei ya umeme si suruhisho ya kupata huduma bora ya umeme.

  Shirika hili litafute njia mbadala ya kuzalisha umeme sio kutegemea gesi na maji.
   
Loading...