This article about Dodoma becoming a capital city will rock you!

This article about Dodoma becoming a capital city will rock you!

Mbona sasa watu wanatokwa na mapovu kuhusu kuhamia Dodoma wakati hao hao ndio waliokuwa wanakejeli kwa Serikali kushindwa kuhamia Dodoma?

Au walikuwa wanazungumza kwa utani tu na wanaumia kwa kuwa imekuwa halisi?

Someni hiyo article vizuri! Haipingi kuhsmishia makao makuu ddm. Inaquestion planning yake na philosophy behind that planing! Article ina mambo ya msingi sana na somo zuri kwa wanasiasa na planners wetu! Hakuna anayepinga kuhamia ddm bali tunapinga modalities za utaratibu mzima unaoonesha dalili za kukurupuka.
Tusije tukalazwa njaa eti kwa sababu ya kutekeleza mradi wa kuhamia ddm fastafasta!
Je kuhamia huko fsstafasta ndio kutatupunguzia watz ukali wa maisha na umaskini? Ndio kutakoharakisha ujio wa tanzania ya viwanda?

Kwani miaka yote tangu uhuru ikulu nacserijali imekuwa Dar mbona hakujawahi kutokea tishio la usalama? Huo usalama uliopo ddm unatokana na nini?

Copy &paste jf

SIKU moja baada ya Rais John Magufuli kutangaza Serikali kuhamia Dodoma ifikapo 2020, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana amesema tayari mkoa huo umejipanga kufanikisha azma hiyo ndani ya kipindi cha miaka mitano.

Pamoja na Mkuu huyo wa Mkoa, pia wasomi kadhaa wamempongeza Rais Magufuli kwa kuonesha dhamira ya kutimiza ndoto ya muda mrefu ya kuhamishia makao makuu ya Serikali Dodoma na kusisitiza hatua hiyo, itajenga zaidi umoja wa kitaifa.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana, Rugimbana alisema tayari mkoa huo wa Dodoma umeainisha mikakati ya kufanikisha azma hiyo ikiwemo kutenga maeneo kwa ajili ya huduma mbalimbali.

Alitaja maeneo hayo kuwa ni eneo la Ihumwa ambalo ni maalumu kwa ajili ya kujenga nyumba za Serikali zikiwamo wizara na makazi ya watumishi wa Serikali.

Alisema kabla ya Rais Magufuli kutangaza rasmi azma ya kuhamishia Serikali Dodoma, tayari Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alitoa agizo la mkoa huo wa Dodoma kutenga eneo la bandari kavu na kituo cha biashara.

Alisema bandari kavu itakuwa inahudumia mikoa inayoizunguka Dodoma na hivyo kuiongozea uwezo Bandari ya Dar es Salaam kutokana na kupunguziwa kwa kiasi kikubwa msongamano wa bidhaa na makontena.

Aidha alisema Serikali ya Mkoa wa Dodoma inaendelea kujipanga kupanua huduma za kijamii kama vile afya na elimu ili kukabiliana na ongezeko la watu watakaohamia katika mkoa huo.

“Tunatarajia pindi serikali itakapohamia hapa, kutakuwa na ongezeko kubwa la mahitaji ya afya lakini pia elimu kwani kutakuwa na idadi kubwa ya wanafunzi. Hili nalo tumeanza kulifanyia kazi,” alisema Rugimbana.

Hata hivyo, Rugimbana alisema japokuwa mkoa huo unajiandaa kupokea Serikali haizuii wizara na taasisi za Serikali kuhamia mkoani humo na kuendelea kutumia vituo na wizara zilizopo wakati wakisubiri eneo rasmi kukamilika.

“Namhakikishia Rais na serikali yake kwa ujumla, mkoa umejipanga kikamilifu katika kutekeleza hili na ndani ya miaka mitano litakuwa limekamilika,” alisisitiza Rugimbana.

Tayari Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Jenista Mhagama amebainisha kuwa serikali imeanza kutengeneza sheria ya kutambulisha Dodoma kama Makao Makuu ya nchi na inatarajiwa kupelekwa bungeni ili kuondoa changamoto ya migogoro baina ya Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) na wananchi.

Alisema kuanzishwa kwa sheria hiyo kutarahisisha kuhamia Dodoma pamoja na kuondoa migongano ya kisheria kati ya taasisi mbalimbali inayosimamia masuala ya ardhi mkoani Dodoma, ikiwa ni pamoja na kueleza mipaka ya CDA.

Alisema watahakikisha migogoro yote inaisha kwa kufuata sheria na maridhiano kwa kuwapatia wananchi haki, na pale sheria inapowataka wananchi waipe haki serikali waoneshe ushirikiano. Waziri huyo alisema mji wa Dodoma utajengwa kisasa na kuonesha kweli ni makao makuu kama ilivyo miji mingine duniani kwa kuwa kioo cha nchi ilivyo.

Wasomi waeleza utekelezaji wake

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na mchambuzi wa masuala ya siasa, Dk Benson Bana, alisema kauli ya Rais Magufuli katika Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM juzi, imedhihirisha azma ya Serikali ya Awamu ya Tano katika kuhakikisha serikali yote inahamia Dodoma kwa gharama yoyote.

Alisema suala hilo limeanza kuzungumziwa tangu miaka 40 iliyopita na marais mbalimbali walionesha dhamira ya kulitekeleza bila mafanikio. Hata hivyo alisema Serikali ya Awamu ya Tano imeanza kuonesha kwa vitendo utekelezaji wa suala hilo, kwani tayari hatua kadhaa zimeanza kuchukuliwa kwa ajili ya kufanikisha lengo hilo.

“Nampongeza Dk Magufuli ameonesha ni Rais wa vitendo na nina imani hili litafanikiwa. Hakuna sababu ya watu kutohamia Dodoma wengi hasa watendaji hawapendi hili kwa kuwa wanahofia kupoteza fursa ya kupata viposho lakini ki ukweli kuhamia Dodoma kutasaidia Serikali kubana matumizi,” alisisitiza Bana.

Alisema kwa sasa serikali inapoteza fedha nyingi kugharimia watendaji wanaohudhuria shughuli za serikali zinazofanyikia Dodoma ikiwemo Bunge, kwa kulipia mafuta ya magari yao, posho za kujikimu na malazi.

Dk Bana alisema endapo Serikali yote itahamia Dodoma, hata mji wa Dar es Salaam utaweza kutengenezwa na kuwa mji mkubwa wa kibiashara, majengo ya Serikali ya sasa yatapangishwa na kuiingizia serikali fedha nyingi.

Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bashiru Ally alisema kuna faida nyingi za kuhamishia serikali Dodoma, mojawapo ikiwa ni upungufu wa usalama jijini Dar es Salaam kutokana na msongamano wa watu na miundombinu mibovu.

Alisema wazo la kuifanya Dodoma Mji Mkuu wa Tanzania lilipitishwa kama Azimio mwaka 1970 na Tanganyika African National Union (TANU) lengo likiwa ni kuutumia mji huo ulio katikati ya Tanzania kuwa kituo cha kuhudumia Watanzania wote.

Alisema endapo serikali itahamishiwa Dodoma, itatoa fursa kwa Watanzania kutoka pande zote nchini kupata huduma za Serikali bila kusafiri umbali mrefu hadi Dar es Salaam kama ilivyo sasa.

“Niseme wazi kati ya mambo ambayo Dk Magufuli ameyazungumza jana hili la kuhamia Dodoma limenifurahisha sana kwani linaonesha dhamira ya kujenga utaifa. Ninaomba serikali ijipange kutekeleza agizo hili kikamilifu, lakini pia mji wa Dodoma ujengwe kwa tahadhari na kuepuka yanayotokea sasa Dar es Salaam,” alisema Ally.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Edwin Ngonyani, alisema kwa sasa miundombinu ya Dodoma iko tayari kuipokea serikali yote isipokuwa kama itahitajika marekebisho zaidi.

Alisema katika kufanikisha azma hiyo ya kuhamia Dodoma, wizara yake imeanza mchakato wa upanuzi wa uwanja wa ndege ili kuwezesha ndege kubwa zaidi kutua. “Mji huu tayari una master plan yake na utakuwa unaendelezwa kwa kufuata mpango huo,” alisisitiza Ngonyani.

Naye Mbunge wa Dodoma Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu; Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde, alimpongeza Dk Magufuli kwa hatua yake hiyo ambayo inatekeleza ahadi aliyoitoa katika kampeni.

“Wakati wa kampeni moja ya ahadi nilizotoa ni kuhamisha serikali Dodoma, nimefurahi sana na ninajisikia faraja kuona ahadi yangu imeanza kutekelezwa. Ni kweli suala hili ni la miaka mingi, lakini kupitia Serikali hii ya Awamu ya Tano naamini sasa litatekelezeka kwa vitendo,” alisema Mavunde.

Aliwataka wafanyabiashara na wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kutumia fursa hiyo na kuwekeza zaidi katika mji huo wa Dodoma ambao ndio Mji Mkuu wa Tanzania.

Juzi mara baada ya kukabidhiwa kijiti cha uenyekiti wa CCM Taifa, Dk Magufuli pamoja na mambo mengine alitangaza rasmi kuwa kabla ya kumaliza kipindi chake cha miaka mitano, serikali yote itakuwa imeshahamia Dodoma.

Alisema pamoja na miundombinu ya Dodoma sasa kuwezesha serikali kuhamia huko, yeye mwenyewe atakuwa mfano kwa kuhamia Ikulu ya Chamwino ambayo ina kila hitaji analotaka huku akisisitiza anatarajia Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Mawaziri na serikal inzima itamfuata

Habari Leo

Someni hiyo article vizuri! Haipingi kuhsmishia makao makuu ddm. Inaquestion planning yake na philosophy behind that planing! Article ina mambo ya msingi sana na somo zuri kwa wanasiasa na planners wetu! Hakuna anayepinga kuhamia ddm bali tunapinga modalities za utaratibu mzima unaoonesha dalili za kukurupuka.
Tusije tukalazwa njaa eti kwa sababu ya kutekeleza mradi wa kuhamia ddm fastafasta!
Je kuhamia huko fsstafasta ndio kutatupunguzia watz ukali wa maisha na umaskini? Ndio kutakoharakisha ujio wa tanzania ya viwanda?
Kutapunguza foleni katika jiji la Dar es salaam
Sekta mbalimbali zitakuwa kwa upana wake.

Moja ya sababu kuu ya kuhamia serikali Dodoma ni Usalama na pili ni katikati ya nchi yetu.

..nakubaliana na hizo sababu.

..lakini nadhani awamu hii ijikite kutekeleza ahadi alizotoa JPM wakati wa kampeni hususan ujenzi wa viwanda.

..kwa mtizamo tatizo letu wa-Tz ni kuwa na vipaumbele vingi mno matokeo yake tunatekeleza mambo mengi kidogo-kidogo.

..suala la kuhamia Dodoma liachiwe awamu zinazokuja baada ya JPM.

Kasi ya maendeleo na miundo mbinu ni kubwa ili kugeuza manispaa ya Dodoma kuwa jiji.
Miundo mbinu,maji safi na salama,viwanda vya wastani vya kutengeneza vifaa vya ujenzi.kilimo cha umwagiliaji kwa tekinologia ya kisasa kwa vijiji vinavyozunguka mji,kuhamasisha benki kubwa za mitaji za kigeni ili kuwezesha makampuni mbali mbali kujenga au kuwekeza katika mji mpya.

Upuuzi mtupu hakuna kitu kisichowezekana.Sioni kama tafiti hiyo imekamilika,kitu kimmoja kimekosekana ni upungufu wa utashi wa waasisi,ukigeugeu wa serikali na chama tawala.Pammoja na hayo Mkoa wa Dodoma una changamoto nyingi,ikiwemo ukame wakati water table ipo juu,ni jinsi gani ya kutumia ground water.Pia ni upandaji wa misitu kupunguza vumbi.Kilimo cha tekinogia ya kileo yaani smart agrotec katika vijiji vilivyopakana na mji wa Dodoma.Faida zake tutatengeneza ajira kubwa za ujenzi kwa muda mrefu.
Dodoma ni tatizo tu. Kuna watu kwa kuwa Dodoma ni kwao wanadhani ni muda wa kufaidi, lakini dodoma haina maji yanayofaa kwa matumizi ya kawaida. chini ya ardhi kuna maji, lakini ni machafu, kwa ujumla hayafai kunywa kwa population inayotegemewa. Maji hayo pia siyo mengi kama inavyodhaniwa. Mzakwe imeshazidiwa na idara husika inafahamu. Kwa maamuzi mazito kama hayo, lazima sasa maji yaletwe toka L.Victoria. sijui kama hilo linaweza kufikiwa ktk miaka 5 ijayo kama inavyozungumzwa, maana mbona hata shinyanga yenyewe bado haijafaidika na maji hayo?

Kwa miji yetu kama ilivyo kawaida, kama ukuaji wa mji utafikia 5% basi ujue wataoga mara moja kwa wiki.

Kutapunguza foleni katika jiji la Dar es salaam
Sekta mbalimbali zitakuwa kwa upana wake.
Ah wapi sahau la foleni kupungua. Dar ni jiji la kibiashara. Foleni haitapungua kws serikali kuhamia ddm bali kwa kuboresha miundo mbinu!

alieandika hiyo article naye ni kilaza tu. alitaka mji mkuu wa kijamaa uweje? kwani kutoa planner nchi za magharibi kuna ubaya gani? hao si ndiyo mabingwa wa kuplan miji?. ajue mipango miji na huduma za kijamii vinaenda sambamba.

alieandika hiyo article naye ni ****** tu. alitaka mji mkuu wa kijamaa uweje? kwani kutoa planner nchi za magharibi kuna ubaya gani? hao si ndiyo mabingwa wa kuplan miji?. ajue mipango miji na huduma za kijamii vinaenda
sambamba.
Hujaelewa vixuri content ya article. Kwani wewe kidato cha ngapi?

....Kwa maoni yangu Dodoma inatakiwa iandaliwe ili iwe na Miundombinu inayofaa, barabara hazipo, miundombinu ya maji haipo!. Foleni inaanzia Chamwino! Wajenge Flyover za kutosha kwanza ili kufanya jiji la kisasa. Nafikiri maamuzi ya kuhamia yafanywe baada ya kuweka miundombinu ya kisasa! Tusikurupuke....

Monkey business kila kitu wanarukia. Sasa budget imepita hatujasikia waziri mkuu kutengewa pesa na taasisi zake zote kuhamia dodoma, pia mawaziri wanatakiwa kuanzia jana wahamie Dodoma. Matamko mengine bhana sijui mzuka au nini.

Kuna vitu hatuzingatii katika mipango yetu hasa Priorities na Opportunity cost.
Kuhamia Dodoma ni muhimu, but is it a priority ? Na je, hizo fedha za kuhamia dodoma zingejenga vyuo vikuu vingapi ili kuendana na Tz ya viwanda?

Hii ni article moja yenye sababu za kitaalsmu kwa nini dodoma capital project has proved a failure. It is a fantastic article worth spending your precious time to read! Mtaona jinsi mipango yetu ilivyo disconnected from uhalisia wa mazingira yetu!

Happy reading!

The burden of being planned. How African cities can learn from experiments (...) - INTI - International New Town Institute
Siasa...Dodoma
Biashara...Dar....kama ilivyo uvuvi.....

Mbona mnalalamika? kijiji cha serikali kitakuwa Ihumwa ambayo ni nje ya mji sasa hiyo foleni mjini italewa kwa population gani iliyopo Dodoma? New York yenyewe peak hours kuna foleni sembuse Dodoma? inajengwa bypass ya Ihumwa - Udom - Kikuyu kupitia Njedengwa ambako kumewekwa miundombinu ya uwekezaji au watz sisi ni watu wa kulialia tu, toka 1973 wanafanya maandalizi mpaka leo waachwe waendelee? kabla hakukuwa na political will ya kuhamia Dodoma na ambayo ndio msingi mkuu wa utekelezaji, sasa tunaona political will tunaanza kulalamika, Dar mnaogopa ukiwa? karibuni ugogoni maisha yatasonga tu

....Kwa maoni yangu Dodoma inatakiwa iandaliwe ili iwe na Miundombinu inayofaa, barabara hazipo, miundombinu ya maji haipo!. Foleni inaanzia Chamwino! Wajenge Flyover za kutosha kwanza ili kufanya jiji la kisasa. Nafikiri maamuzi ya kuhamia yafanywe baada ya kuweka miundombinu ya kisasa! Tusikurupuke....

Kwa nini ninyi watu ni wajinga sana? Ni nani alikwambia kuwa Mji Mkuu lazima uwe over populated? Unataka tujenge flyovers Dodoma za nini? Ulishatembea wewe Dunia hii? Mimi nimefika Washington d.c Mji Mkuu wa USA hauna chochote cha maana ukilinganisha ni miji mingine ya USA zaidi ya kuwa makazi ya Raisi wa USA na mapartments za malobbyist, nimefika Pretoria AK Mji Mkuu wa AK, hauna chochote zaidi ya kuwa makazi ya Serikali ya AK, nimefika Bern, Uswisi ambao ni de facto Mji Mkuu wa Uswisi lkn hakuna chochote cha maana ukilinganisha na Miji mingine ya Uswisi!

Au mnafikiri wanavyosema Mji Mkuu unahamia Dodoma maana yake ni kwamba Dodoma lazima iwe Dar ya Pili? Acheni Ujinga na umbumbu Dodoma haiwezi kuifikia Dar na kamwe haiwezi kuwa Dar na wala hilo siyo lengo kwanza ukiniuliza mimi Dodoma haiwezi hata kuifikia Arusha City au Mwanza City na itabakia kuwa hivyo kwamba ni Mji Mkuu wetu na makao makuu ya nchi lkn Dar inabakia kuwa Mji mkuu wa Kibiashara Tanzania!

Watu kama ninyi ni mzigo kwenye hii nchi hata sijui ni kwa nini mlizaliwa hapa, mmejawa na negativity na kutwa kushinda kutafuta makosa tu badala ya kuwa msaada, watu kama ninyi hata mkipotea ni sawa tu hii nchi na jamii yetu haiwahitaji, mnaboa sana!

Ndalama Kwanza Kula like zakutosha.. siku mbili hizi kila nikipitia humu Jf kwenye thread za kuhamia dodoma inaonesha kabisa wanaopinga ni watu wanaogopa ukiwa... Miundombinu gani ambayo dodoma haipo? Natoa pongezi za dhati kabisa kwa CDA kwa jitihada upangaji Mzuri wa Mji.. Mie sioni tatizo Serikali Kuhamia dodoma... Mbona serikali ipo dar na foleni ni kawaida? kwa miundo Mbinu Gani ilokuepo Dar serikali ikae huko miaka yote? Tunawakaribisha saaaana Mkoani Dodoma.. na Kila kitu kitakua In Place..

Mbona mnalalamika? kijiji cha serikali kitakuwa Ihumwa ambayo ni nje ya mji sasa hiyo foleni mjini italewa kwa population gani iliyopo Dodoma? New York yenyewe peak hours kuna foleni sembuse Dodoma? inajengwa bypass ya Ihumwa - Udom - Kikuyu kupitia Njedengwa ambako kumewekwa miundombinu ya uwekezaji au watz sisi ni watu wa kulialia tu, toka 1973 wanafanya maandalizi mpaka leo waachwe waendelee? kabla hakukuwa na political will ya kuhamia Dodoma na ambayo ndio msingi mkuu wa utekelezaji, sasa tunaona political will tunaanza kulalamika, Dar mnaogopa ukiwa? karibuni ugogoni maisha yatasonga tu

.....Sio kulalamika...maandalizi ni muhimu....huwezi kuhamia wakati hata huna pa kukaa...wewe unawaza nini!!

Back
Top Bottom