ThinkTank ya Sheria na Haki za raia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ThinkTank ya Sheria na Haki za raia

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Ntamb, Aug 2, 2010.

 1. N

  Ntamb Member

  #1
  Aug 2, 2010
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wapenzi wa sheria,
  Napenda kujua kama kuna kikundi chochote nchini ambacho tunaweza kukiita ThinkTank katika mambo ya Sheria. Nadhani kuwepo kwa kikundi kama hicho kungesaidia sana katika mambo mengi. Yakiwemo
  - kutoa uchambuzi na ushauri wa maswala mbalimbali ya sheria, kwa serikali, NGOs na vitengo mbalimbali.
  - kuwepo kwa mtazamo wa kutokea nje kidogo, na hivyo kuweza kuzuia mambo fulani kabla hayajatoke. Mojawapo laweza kuwa kwa mfano namna ya kupambana na rushwa. Mara nyingine "kamata weka ndani", inaweza ikawa siyo jibu la muda mrefu.
  - kubuni namna ya kuwawezesha raia wa kawaida wazijue haki zao, wasiogope kudai haki zao kwa kufuata sheria, nk.

  Jioni njema,
  Thadeo.
   
 2. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #2
  Aug 3, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Kama ilivyo katika tasnia nyinginezo, wapo waliobobea katika specialisations mbalimbali mfano - Taxation, Human Rights, Intellectual property, Constitutional, Criminal law, Family Law, insurance etc. Most of them ama wana firms zao au wako kwenye tasisi za kitaaluma au NGOs.Ukitaka michango yao basi watafute humo.
   
 3. T

  Taso JF-Expert Member

  #3
  Aug 3, 2010
  Joined: Jun 12, 2010
  Messages: 1,652
  Likes Received: 458
  Trophy Points: 180
  Taasisi za kitaaluma na kampuni zao na NGOs sio specifically think tanks. Umfate mtu kwenye law firm yake au ofisi ya some faculty kumletea stori za kumwomba mchango wake kwenye athari za kikatiba kwenye mpasuko na mustakabali wa uongozi Unguja? Si atakushangaa.

  Afadhali useme tuwatafute kwenye makontena ya ulabu, ambako nako sio official, registered think tank.
   
 4. N

  Ntamb Member

  #4
  Aug 3, 2010
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nina maana ya organizations ambazo haziko ndani ya serikali, na ambazo watu wake wamejitolea muhanga kuyatetea hayo wanayoamini.
  Organization kama hizo hazisubiri ziombwe na mtu, ndipo zianze kutafakari jambo fulani.

  Mifano michache hapa:

  Centre for Conflict Resolution : South Africa
  Centre for European Policy Studies : Belgium
  Royal Institute of International Affairs: United Kingdom
  European Union Institute for Security Studies : France
  Baker Institute of Public Policy : US
  Brookings Institution: US
  Carter Center : US
  Center on Budget and Policy Priorities :US
  Heritage Foundation : US
  RAND : US
  Urban Institute : US
  United States Institute of Peace : US
  ..
  ..
   
 5. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #5
  Aug 3, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
 6. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #6
  Aug 3, 2010
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kaka

  Wana ushirikiano wowote hao na serikali au hata wana lobby kwa aina yoyote kwenye kuleta mabadaliko serikalini (kisheria) au hata kupendekeza kwa hao so called wabunge wapiganaji wapeleke hoja fulani bungeni.

  Mfano tumeona kumkosa Liumba, Zombe, Richmond, Kupotea kwa hela za EPA and so forth bila kumsulubu hata mmoja wa maana. Sasa kuna mapendekezo yoyote yametolewa na either of those bodies mentioned above nini kifanyike makosa yasijirudie (tusiwakose wahalifu wa juu serikalini) vinginevyo we shouldnt call them 'think tanks' kama hawa tumii muda wao ku-review laws through court cases whats the point then.

  Kama mleta mada alivyouliza kuna watu gani wakutusaidia tufanye nini na tujue nini katika masuala fulani ya kesi zetu za kitaifa au hata locally. To make matters worse the same scenario are likely to be repeated na tutapata matokeo yale yale kutoka mahakamani amna ushahidi. Je wanaushauri wowote kwa kesi zozote mbali ni hizo nilizoweka vinginevyo ni maloya tu wakutanao hila sio 'think tanks' na wanahitajika kwa kweli kutoa ushauri sasa. Yote hayo yatakua magumu nimekuja gundua under viongozi aliotuachia Mwalimu.

  For gods sake 'Mwakembe' is a lawyer despite his noises he cant tie Lowassa with Richmond directly doesnt he see the flaws that interpret embezzlement my law knowledge is limited, but i know someone has to be responsible for the loss of those funds. We need those 'think tanks' to function honestly in every sector of the social and not just into law. Watu wenye akili timamu hawawezi kuja na kilimo kwanza bila kujua namna kufanikisha hiyo sera kwa ufanisi mara matrekta, mara mbolea mara hiki kimepotea ni tabia hizi za kipuuzi serikali kujiendea bila ya 'think tanks' ndio chanzo cha sera mbovu. Na huko ndio vijana wa leo wanatakiwa kwanza waanze kabla ya papara za ubunge, watumie hiyo mi Phd yao huko kwanza kusaidia taifa kabla ya kukimbilia 'per diems' za wabunge.
   
 7. N

  Ntamb Member

  #7
  Aug 3, 2010
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Juma Kontena na Ngoshwe,
  Nashukuru sana kwa mchango wenu.
  Naona tunaelewana vizuri. Nimependekeza vilevile hilo pendekezo la Ngoswe kwamba inabidi kuwe na Think Tanks zinazogusa kila sehemu ya maisha.

  Angalieni hapa :< https://www.jamiiforums.com/habari-na-hoja-mchanganyiko/68575-too-few-thinktanks-in-tanzania.html>

  Labda mnaweza kuchangia vilevile kwenye hiyo mada, na huwenda wakapatikana watu watakaojitolea katika fani zao na kuziunda.

  Kweli, inabidi thinktanks ziwe ni za watu wanaojitolea muda wao wa ziada, kujaribu kutatua matatizo yanayotukabili, proactively, na siyo kusubili eti serikali itafanya nini. Kama samadi ukiirundika mahala pamoja, itamnukia kila anayepita, na hiyo inakuwa ndiyo faida pekee. Lakini samadi hiyo hiyo ikisambazwa shambani, tunajua jinsi mazao yatakavyoshamiri, tutafaidika sisi pamoja na watu tutakaowauzia mazao hayo. Nailinganisha samadi hiyo na elimu na ujuzi tulivyonavyo. Tutafaidika zaidi kama tukiwawezesha wengine kuitumia. We can extend our hand through thinktanks, I think.

  I welcome more opinions.
  Thadeo.
   
 8. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #8
  Aug 4, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Wakuu Konte na Ntamb,

  Binafisi nakubalina nanyi kwa 100%. Ni dhairi kuwa vyama vingi vizivyo vya kiserikali vimekuwa na mwelekeo wa kimaslahi zaidi kuliko kutimiza malengo ya kuanzishwa kwake. Hii inechangia sana raia wengi kupoteza imani na hivyo vyama hasa pale inapofika katika kuvihusisha kutatua matatzio ya wananchi. Kwa mfano, zamani kulikuwa na watu binafsi wanaojitolea kusaidia moja kwa moja kutoa ushauri na pia kuanzisha halakaki za kuibua hoja ambazo ziliifanya Serikali iamke na kuona uwepo wa dosari katika utendaji wake. Watu wa jinsi hii walifanyakazi kwa kujitolea kupitia mashirika hayo yasiyo ya Kiserikali au kwa binafsi zao. Kwa mfano kama akina Tundu Lissu na Rugemeleza Nshala wao binafis au kupitia Lawyers' Environmental Action Team (LEAT) katika sakata la Mradi wa Bulyanhulu.

  Nakubaliana nanyi 100% kuwa fedha za umma ambazo zinatengwa katika bajeti za Serikali kila mwaka zinapotea kutokana na kukosekana kwa uadilifu na mfumo wa kuwafanya watendaji katika Sekta ya umma wawe waadilifu (accountability of Government to its people). Ni dhairi kuwa uwepo wa "Think Tank" zenye nguvu kunaweza kuifanya Serikali yetu iweze kutimiza mema kwa wananchi wake kwa kupitia uibuiaji wa hoja na kuzifuatilia kwa kina mapka mwisho. Tumeona jinsi ambavyo nchi za wenzetu, Mashirika yasiyo ya Kiserikali yalivyo na nguvu na sauti ya kuweze "kuhamisha Milima na kufukia mabonde". NGOs hizi au watu binafsi wameweza kuzifanya Serikali zao ziwe makini katika kila jambo na hata kuwajibika kwa watumishi wa umma pale mambo yanapokwenda kinyume na matarajio iwe kwa kutumia dhamana kwa maslahi binafsi au kwa Uzembe, kila senti inamwajibisha kiongozi.

  Wengi walitarajia uwepo wa vyama vingi vya siasa (Political Parties) na vyama visivyo vya kiserikali (NGO) Tanzania kunaweza kusaidia mabadiliko na wanachi wakayaona hayo. Lakini hakina ukifuatilia kwa undani utaona jinsi siku zinavyosonga, biashara ya vyama hivi imekuwa ni porojo na ushindani wa kutafuta mazingira "mema ya ulaji tupu" (uongozi na maslahi binafsi) kuliko watu wao yaani watanzania. Vingi ya hivyo vyama havina mwamko, wasomi wengi wanaibuka kila kukicha lakini hawapendi kutumia muda na elimu zao kwa faida ya Taifa kama walivyofanya wenzetu huko nyuma mpaka leo nchi hii ikawa huru.

  Wasomi wengi hawapendi kushiriki katika tafiti za kuibua hoja za msingi, wengi hawapendi kuandika wala kusoma..wengi wamekuwa wakitumika au kutumikishwa kwa maslahi ya mfumo tulionao wa kunufaisha wachache badala ya kujitumikisha kwa maendeleo ya walio wengi. Tunaibua tabaka la utengano mkuu, wa walionazo na wasio nazo...wenye nguvu na wasio na nguvu..

  Kama nikiangalia tafakairi ya Mzee Konte, waweza kuona pia hata hiyo sekta ya Kilimo ndio imekuwa ikitumika zaidi ya miaka kumi iliyopita kuhamishia na kufichia rasilimali nyingi (fedha za umma) ambazo hazina matokeo kwa walengwa. Bajeti za kisekta zimekuwa zikiongezeka kwa silimia kadhaa mwaka hadi mwaka, wabunge wetu na wasomi hawana muda hata wa kupima matokeo ya ongezeko la bajeti na utekelezaji kwa vitendo wa yale yaliyodhamiriwa katika bajeti husika ( kwa mfano, ukifuatilia mfumo wa mijadala Bungeni, waheshimiwa wakiambiwa Serikali imenunua matrekta kadhaa, hoja inakuwa imefungwa bila hata kuuliza wala kutaka kuona yapo wapi na yanafanya nini na yameongeza tija kwa kiasi gani kutokana na kuwepo kwake sambamba na uwepo wa rasilimali nyingine zinazoigharimu fedha za Umma kama Ruzuku za Pembejeo, Wataalamu wa Kilimo, Miradi ya Maendeleo nk)...

  Hizo kauli mbiu kama "KILIMO KWANZA" sasa imekuwa wimbo wa siasa..na walioibua unaweza kuona ni "wafanyabiashara" ambao kimsinigi hata hicho kilimo kwao ni wimbo wa zamani. Zitihada zilizofanyika kuleta Kauli Mbiu ya KILIMO KWANZA ni kuunganisha Sera na Mikakati ilivypo tu lakini ikija kwenye utekelezaji wake, hakika hata baadhi ya wakuu wetu wa nchi hawajui tutokako wala tuendako (kwa wale mliofuatilia kongamano la "WEF" lililofanyika miezi michache iliyopita - Dar es Salaam, mliweza kujionea jinsi ambavyo hata Mhe. Rais alivyoshindwa kabisa kuelezea kwa kina mikakati ya kimaendeleo katika Sekta ya kilimo nchini sambamba na dhana ya "KILIMO KWANZA".

  Hakuna anayeweza kubainisha kwa nini Kilimo kina kufa pamoja na historia ya miradi ya wafadhiri mingine ambayo ipo na imewahi kuwepo kuwalengwa kwa watu hao hao (wakulima))!!!!.

  Sasa kuna Jitu kuu linaitwa "THE FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETIES" hiki chombo kilianzishwa takribani miaka saba iliyopita kikiwa na malengo makuu ya kusaidia jitihada za Serikali katika kuwakwamua wananchi kijamii na kiuchumi ikiwemo kuwafanya wananchi wajue haki zako na kujitambua, na kujiletea maendeleo kupitia Sera na Mikakati iliypo kama Tanzania Development Vision (TDV -2025); MKUKUTA nk.


  Kwa muda sasa kupitia vyombo vya habari, hiki chombo kimeonekana kikiibua mijadala mbalimbali kupitia nfumo wa "majadiliano ya hoja" (debates). Hata hivyo, inaonekana kana kwamba hitimisho ya yale wanayoyajadili wadau yamekuwa yakiishia kwenye mitandano au makabati ya vyombo kama hivi.

  Nadhani ipo haja kuangalia upya mfumo tunao kwenda nao, tumeona jinsi tunavyopoteza wasomi kupitia siasa, wengi wanataka kuwa waheshimiwa ili walipo wengine waendelee kuwaheshimu tu hata kama hawana mchango mkubwa kwa Taifa. Sasa Bunge la Jamhuri ya Muungano limejaa wadaktari na maprofesa. Bunge kama chombo cha Serikali ambacho kinaundwa na asilimia kubwa ya wajumbe wa chama Tawala, limepoteza kabisa mvuto na meno ya kuiuma Serikali ya chama chao kwa hofu iliyojengeka miongoni kwa waliomo kuwa ni usailiti kwa Chama, usaliti ambao unaweza kukupoteza kabisa katika ulingo wa siasa...

  Hali inatisha...tunakoenda ni kiza kizito sana!!!

  NAUNGA MKONO HOJA..
   
 9. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #9
  Aug 4, 2010
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Wakaka

  Nashukuru for once we all agree on the importance of 'Think Tanks', kaka Ngoshwe sina tena mimi binafsi lakuongezea you said it all on the importance of these organisations. Hila swala la kujiuliza huko bungeni kwetu au raisi wetu huwa anajua vipi hii sera itafanya kazi au la? kabla kuipitishia mihela chungu mzima. Maana cha kushangaza kila mwaka tuna budget and it seems the situation is getting worse on the ground instead of improving.

  Ni hapo mimi ndio nina mashaka nako it seems tunapoteza hela nyingi kwenye secta nyingi za serikali through corruption, bado sera zenyewe sidhani kama zina theories ambazo zipo tested and proven to succeed based on social thinking and small scales experiments. Inaonekana mijitu inaamka tu asubuhi na kujiamulia haya wajomba 'Kilimo Kwanza' bila ya kuangalia tunalima nini, wapi, kwa faida ya nani, itasaidia vipi jamii, je wanajamii wapo tayari kuwa dedicated na hiyo policy, what pecentage of the land is a target, cost effectiveness, distribution of the produce, distribution of resources, application of the policy (private farming or communal farms), how is the government going to recoup some of its investment back. Yaani amna plan ndio tunapata matokeo ya wizi wa mbolea, kupeana contract za ajabu kwenda kununua mitrekta ambayo mibovu kesho yote tutaikuta hoi (mibovu) ataikishanunuliwa in this case we dont just make the social suffer but also waste alot of money for stupidness.

  Ni hapa kwanza hawa jamaa wanaojinadi wana madgree yao kwanza waanze, kwa kuisaidia serikali kuja na policy nzuri si tayari wameshafanya mi research yao wakati wanachukua hiyo mi Phd. Wawe vocal kwanza kwenye kukemea policies za serikali ambazo wanaona azina faida badala ya kukimbilia madaraka yenye faida. Na hili wala serikali haita kuwa na hasara sana kuweka 'think tank' katika kila wizara kwanza kuna malaki wanaenda makazini na kufanya nusu siku ya kazi na muda mwingine kupiga soga tu. Hivyo tukiwapa watu kazi za siku tutakuwa na excess work force ambayo inapata mshara wa bure tu hao wanaweza amishiwa huko kwenye hizo 'QUANGO'S' na kuwasaidia hao akina 'Mwambulukutu' kwenye jitihada zao za kutaka kuibadilisha Tanzania. Bila ya tamaa za Ubunge, this is costeffective and it would creat a usefulness to idle scholars.

  Hutaki kujua kuhusu 'corporatist' pressure groups ambazo zipo on the other side of the continent and how much these groups lobby in UN, IMF, In G8 summits and all other institution that can set us conditions for their gain hili tupate misaada kutoka kwao along the way kutuachia mishimo tu na kuchukua ardhi yetu.

  Yaani we can not afford to move without our educated masses in these times. We just cant afford not to create 'think tanks' on the side of the government to assist in home and foreign policies. The times of 'JK' as a president are done if they think about kuwapachika watoto zao in my times, they got another thing coming I have no problem na mtoto wa fisadi aliesoma kutaka madaraka but I have a big one kwa anayetaka kupachikwa without merit. Hao ndio matatizo ya baadae kama hawa waleo kwa kutokua much prepared na Mwalimu for his selfish motives.
   
Loading...