Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,638
- 697,938
Kwa mazoea vijana ndio tegemeo la taifa kwa
Mawazo mapya
Mawazo chanya
Kwa utayari
Kwa nguvu kazi
Kwa uchapakazi
Weledi
Uzalendo Nknk
Bongo bado ziko timamu, damu zinachemka na miili imejaa nishati.. Kwa muktadha huo na kwa miongozo sahihi na misingi imara vijana ni hazina kubwa kwa maendeleo ya taifa...
Kwa bahati mbaya sana sehemu kubwa ya vijana wa taifa lefu wamekumbwa na utapiamlo mkubwa wa fikra yakinifu, fikra chanya na maono yenye kujenga
Sehemu kubwa ya vijana kwasasa fikra na maono yao kikomo chao ni
Kuwa chawa
Teuzi
Kuendesha ndinga kali
Kuvaa vizuri
Starehe na show offs zisizo na maana yoyote
Kumiliki mali kwa njia za mkato, kuonesha mafanikio feki mitandaoni huku mijadala mikubwa inayowatikisa ni kuhusu kujadili watu na umbea wa kila aina, uzushi na ujinga mwingine
Swala la teuzi serikalini linatengenezewa mijadala ya kila aina na yote si kwa ajili ya kujadili dhana za teuzi husika na manufaa yake la hasha bali nani kateuliwa na kwanini kateuliwa (serikali nayo inapaswa kujitafakari kwenye hili maana teuwa tengua zimekuwa nyingi mno)
Mjadala wa wiki hii ni kuhusu mtangazaji mtanzania aliyerejea nyumbani baada ya kutumikia chombo cha habari ughaibuni kwa miaka mingi.. Wengi wanasema karudi ili kupata uteuzi wa juu serikalini
Kwenye teuzi za hivi karibuni hajateuliwa popote. Hili ndio sasa limekuwa mjadala kwamba kaingizwa mjini, kwamba kaliwa pesa yake kwamba ana bifu na chama chawala nk
Jamani kwani kama taifa hatuna vijana wanaoweza kushika nafasi za juu mpaka tuokoteze watu waliokwisha tumika na kuchoka huko watokako?
Wameteuliwa wangapi waliofanya vizuri sana ughaibuni na hapa wakaboronga mbaya? Hawa hawana maajabu yoyote na si kwamba wana akili kutuzidi la hasha
Mifumo imara, nidhamu ya kazi, masharti, kanuni na miiko ya kazi ndio viliwapaisha na kung'ara.. Wakirudi huku hata wapewe nafasi zilezile zilizowang'arisha kama mifumo yetu ni mibovu wanakuwa wa kawaida mno..
Tuachane ni haya mawazo kimo cha mbilikimo kwamba kila aliyefanya kazi ulaya atafaa kufanya kazi serikalini kwa fikra kwamba anajua na anaweza zaidi yetu tuliobaki nyumbani
Sent using Jamii Forums mobile app