Ncha Kali
JF-Expert Member
- Sep 19, 2019
- 14,537
- 27,073
Ndio maana mnadanganyika kununua sukari yake hata kama kwetu hakuna uhaba, nashangaa wengi wanachanganya kati ya uhaba wa sukari na bei ya sukari.
Tanzania hakuna uhaba wa sukari tatizo lililopo ni bei ya sukari kuwa juu, na hili linasababishwa na wafanyabiashara kupandisha bei kiholela ili kutimiza malengo yao, serikali kama regulator ilitakiwa itoe bei maalum ya kuuzwa sukari na hao jamaa waifuate.
Lakini kwasababu hao wafanyabiashara ndio wafadhili wa CCM uchaguzi ukifika, serikali inajikuta imefungwa mdomo matokeo yake tunazidi kuumizwa kwa bei ya juu, na ule uamuzi wa Samia kuagiza iingizwe sukari toka nje, ndio utaua viwanda vya ndani na watu wanaweza poteza ajira zao, japo kwa upande wa mtumiaji kwake itakuwa nafuu.
Kwanini serikali isiingilie kati upandaji holela wa bei ya sukari at the same time ivihamasishe viwanda vyetu viongeze uzalishaji kwa kuvipunguzia baadhi ya kodi kama itabidi?
Kama hakuna uhaba bali tatizo ni wafanyabiashara, wanaweza kuagiza sukari na bado wasipunguze bei vile vile…. na hakuna kitu kibibi atafanya.