The world's greatest last place finisher ever

The world's greatest last place finisher ever

Super Sub Steve

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2011
Posts
17,723
Reaction score
11,336
Katika Michezo ya Olympics ya Mwaka 1968 iliyofanyika Mexico City kulikuwa na mwanariadha aliyetumia muda wa saa nne na nusu kumaliza mbio za Marathoni.

Wanariadha wengine walikuwa wamemaliza mbio katika muda wa saa mbili kabla.Muda ambao mwanariadha huyu alifika mstari wa mwisho wa kumalizia riadha,wale maofisa wanaotunza muda walikuwa wameshakabidhi stopwatches kwa waendesha mashindano na sherehe za utoaji tuzo zilikuwa zinaendelea.

Waendesha mashindano walipoambiwa kuwa kuna mkimbiaji mmoja bado yupo kwenye track za kukimbilia na anaendelea kukimbia,taarifa hii ilitangazwa kwenye redio na mashabiki wakarudi kumwangalia mwanariadha huyo ni nani.

Mwanariadha huyo aliyezua maswali vichwani mwa mashabiki alikuwa MTANZANIA JOHN STEVEN AKWARI.(30).Kila mtu alimshangilia mita chache za mwisho alivokuwa anakaribia kumaliza.

Badaye ikaja gundulika kuwa kuna wanariadha wengine 78 walishia njiani baada ya kujua kuwa wasingeweza shinda.

John alivyoulizwa kuwa kwanini aliendelea kukimbia wakati ye alishakuwa wa mwisho? Akajibu kuwa nchi yake haikumpeleka mashindano umbali wa zaidi ya maili 5000 ili kwenda kuanza ila kumaliza.

Mwaka 2008 akiwa na miaka 78 alialikwa na kamati ya kimataifa ya Olimpiki. Beijing,China kushiriki katika Ufunguzi wa mwaka wa Olimpiki.

Mwaliko huo ilikuwa ni kutambua ujasiri na moyo wake wa kupigana alioonesha miaka 40 iliyopita.

Ameelezewa kama ni "THE WORLD'S GREATEST LAST PLACE FINISHER EVER"


Source:
Gazeti mwananchi 29/10/2014 uk.15

Tafsiri sio Rasmi.
 
Dah! na huo ndio uzombi wa wazungu. wanachokifanya ni kurikodi tu hata kama ni record ya ulaza. mwee.
 
Dah! na huo ndio uzombi wa wazungu. wanachokifanya ni kurikodi tu hata kama ni record ya ulaza. mwee.

Inabidi tujivunie hiyo record hiyo kama kushinda hatuwezi.Ila jamaa alikuwa mvumilivu si mchezo
 
hahahaha safi ... kyumana kwa kutukumbusha historia hii mimi nlikuwa sifahamu kabisa
 
Last edited by a moderator:
hahahaha safi ... kyumana kwa kutukumbusha historia hii mimi nlikuwa sifahamu kabisa

Tujivunie chetu,hata kuwa wa mwisho sio mbaya,jamaa hope alipopatA trip ya China alipata visenti
 
Last edited by a moderator:
Tujivunie chetu,hata kuwa wa mwisho sio mbaya,jamaa hope alipopatA trip ya China alipata visenti

ni kweli ingawa hajashinda lakini alimaliza hakuishia njiani.....safi sana
 
Uvumilivu muhimu
 

Attachments

  • 1414663825715.jpg
    1414663825715.jpg
    18 KB · Views: 85
Muhimu hapo la kujifunza ni moyo wa kuto kata tamaa.
 
Back
Top Bottom