FRANC THE GREAT
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 5,500
- 8,065
Maswali yako ni ushahidi tosha kuwa uelewa wako katika masuala ya anga ni mdogo sana. Unahitaji maarifa!THE EARTH HAS PRESSURIZED AIR AND EMPTY SPACE HAS VACUUM OR IS A VACUUM,THEN WHAT IS THE BARRIER BLOCKING AIR FROM THE VACUUM?
Nakurudisha shule;
Air pressure ndiyo husukuma hewa kuelekea katika eneo lenye vacuum. Hili linafahamika!
Let's say, box ambalo hewa iliyopo ndani yake imeondolewa na kufanyika vacuum, pale box hilo linapopasuka au kupasuliwa, air pressure inayolizunguka box ndiyo huisukuma hewa ndani ya box ili kujaza ile vacuum.
Sasa, katika anga kitu kikubwa kinachoathiri air pressure ni altitude ama urefu wa kutoka katika uso wa dunia na kuelekea opposite ama mbali na uso wa dunia.
Kwa lugha nyingine ni kwamba; Air pressure is inversely proportional to the altitude ambapo kadri unapoelekea mbali zaidi kuachana na uso wa dunia ndipo air pressure huwa ndogo zaidi ama hupungua kidogo kidogo.
Katika kiwango hiko cha air pressure kupungua kidogo kidogo kadri umbali unapoongezeka, hupelekea mpaka kufikia kipimo cha air pressure kutokuwepo kabisa katika umbali wa kiwango cha juu zaidi cha tabaka la anga (atmosphere).
Hivyo kutokuwepo kwa air pressure katika umbali huo, hakutokuwa na msukumo (force) utakao wezesha hewa kusukumwa kuelekea katika space.
Hicho ndicho kinachozuia hewa kuingia katika space.
Maswali unayouliza ni mepesi sana na kama si mvivu wa kutafuta maarifa, hayawezi kukushinda. Pia kama hukusoma Sayansi hususani Physics, ni ngumu kuweza kuelewa haya mambo.COMBUSTION NEEDS AIR TO PUSH KAMA KWENYE ROCKET NINI KINAPUSH ROCKET KWENYE VACUUM,CAUSE THERE IS NO AIR?
Jibu ni, nishati zitumikazo na hizo roketi (Rocket Fuels).
Nakurudisha tena shule;
Kulingana na Newton's Third Law of Motion, every action produces an equal and opposite reaction, ama kwa maneno mengine; "action and reaction are equal and opposite." Hiyo ni Physics nyepesi kabisa!
Katika vacuum ambapo chombo kinapokuwepo, rocket fuel hutumika kuisukuma roketi mbele pale nishati hiyo inaposukumwa nje kutoka upande mmoja wa nyuma wa roketi. Hakuna hewa inayohitajika hapo!
Ndiyo maana missions hizo huwa na gharama kubwa sababu nishati nyingi hutumika kufanya hilo zoezi.
Ukitaka kuthibitisha hilo, fanya utafiti mdogo tu;
Chukua viatu vya matairi, kisha vivae na usimame na kitu kizito mathalani gunia lenye mzigo wa kilo zisizo pungua 10, kisha lirushe kuelekea mbele yako.
Ile force ya kulirusha gunia mbele itakusukuma wewe pamoja na viatu vyako kuelekea nyuma na ndicho kitokeacho katika space ambapo nishati itolewayo kwa force kubwa (thrust) kutokea nyuma ya roketi, inatumika kuisukuma roketi kuelekea mbele ama sehemu inapohitajika kwenda.
Mfano mwingine;
Ukiendelea kuwa na viatu vyako vya matairi miguuni, chukua bunduki (Shortgun) kisha simama nayo upige risasi moja kulekea mbele yako, nguvu ama msukumo utakaokurudisha nyuma utaenda kusimulia katika kile kijiwe chenu cha kahawa pale mtaani!
Nina maana ya kwamba, nguvu inayokurudisha nyuma au kinyume nyume ndiyo hiyo inayotumika kuisukuma roketi kuelekea mahala inakotakiwa.
Hakuna kitu kama hicho!Kuta za barafu tafuta helicopter fata compass yako uelekeo wa south ukikuta ukuta wa barafu anza kuuzunguka ,huwezi tafuta kazi zingine za utumwa endelea nazo.
Hao flat-earthers wameshindwaje kutafuta hiyo helicopter na kuelekea huko "south" unakosema ili kuthibitisha na kuipa nguvu nadharia yao?
Anayepaswa kuuthibitisha kwa ushahidi ni yule asemaye huo "ukuta" upo na si vinginevyo. Tunahitaji utafiti wao na si porojo!