The story of my interview failures and lessons learnt

The story of my interview failures and lessons learnt

Dr. Wansegamila

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2012
Posts
2,995
Reaction score
8,273
Nimeamua kuandika huu uzi ili kuwatia moyo vijana watafutaji waliopo JF. Naona vijana wengi sana wahangaikaji na watafutaji humu JF, wengine wakiwa wamekata tamaa kabisa na kujiona kama hawana bahati katika maisha haya. Kwenye huu uzi nitaelezea interviews kadhaa ambazo niliitwa, nikafanya interview, lakini sikufanikiwa.

1. Ocean Road Cancer Institute (ORCI), Dar es Salaam.

Hii ilikua ni interview yangu ya pili katika career yangu, nakumbuka nili apply for this post nikiwa Moshi (niliona tu kwenye gazeti). Then nikaitwa kwa ajili ya interview Dar es salaam. Nakumbuka nafasi ilikuwa ni moja tu, na nilipofika pale nilikutana na wenzangu wanne, so jumla tulikua watano. Mmojawapo alikua ni mdada ambaye tulisoma nae medical school, ila alikua mwaka mmoja mbele yangu, alikuwa ni kichwa kweli kweli (kipanga).

Nikagonga interview fresh na interview kiukweli ilikuwa ya kawaida. Siwezi kusema kuwa i really nailed it, ilikuwa normal tu, baadhi ya maswali nilishindwa, ila mengi nilijibu vizuri. Kwa bahati mbaya kwangu, sikupata ile nafasi, ila aliipata yule mdada niliyesoma nae chuo, nikasonga mbele nikaendelea kupambana.

2.Tanzania Food and Drug Authority (TFDA), Dar es Salaam.

Hii pia as usual, walitangaza nafasi, nikatupia nikaitwa Dar for the interview. Nakumbuka nafasi nilizo apply walikuwa wanahitaji watu kama watano hivi. Kati ya interview nilizodunda hii iliniuma sana, kwa sababu niligonga interviews mbili (written then oral).

Interview ya kwanza (written) tulifanyia DUCE, people zilikua nyomi aisee, halafu nafasi zenyewe 5 tuu!! Niligonga ile pepa (ilikua imeshiba, ila nilikomaa), after that nikarudi zangu Arusha (kipindi hicho nilikua nafanya kazi Arusha). After like 2 weeks hivi, wakanigongea simu niende for oral interview. Nakumbuka hii oral tulifanyia pale TFDA makao makuu. Tulikuwa tumebakia mtu kama 12 hivi. Nikafanya ile oral interview, haikwenda vizuri sana, but i managed kujibu maswali kadhaa vizuri, kwa usahihi and confidently.

Kwa bahati mbaya sana, baada kama ya mwezi hivi nilipata barua from TFDA ikiniambia kuwa i was not selected for the post!! This was one of the saddest news i received, but kama kawaida yangu sikufa moyo, niliendelea kupambana!

3. Mradi fulani wa HIV/AIDS mikoa ya Southern Highlands Zone (Sitautaja kwa sababu maalum ambazo nitazieleza hapa chini)

Hapa ndipo ambapo nafanya kazi kwa sasa (ndio maana sijapataja, ili kuretain my anonymity). I have a history with this place.

Encounter ya kwanza nimeitwa for interview, i could not attend, at that moment nilikuwa nimesafiri kikazi, nipo Dar es salaam (hii organization makao makuu ni Mbeya). So, nilijaribu kuweza kuhudhuria hiyo interview, ila ilishindikana kabisa.

Encounter ya pili sasa ndio ambayo nilidunda!! Hiyo nafasi ilikua ni nafasi moja tuu, nikaitwa interview fresh, kufika nikakutana na wenzangu watatu. Niligonga ile interview, i felt that i did great, nilijibu maswali vizuri, ila kwa bahati mbaya after two weeks nikapata a regret email kunieleza kwamba i was not successful.

Encounter ya tatu sasa ndio iliyonipatia hii position ninayoitumikia sasa. Kwanza, its a higher position kuliko ile ambayo nilidunda (Siku zote Mungu huwa ana mipango mizuri zaidi kwa ajili yako,usikate tamaa mlango mmoja ukifungwa). Ilikua ni nafasi moja tuu, na tulikua mtu kama 8 hivi, ila nilipambana na Mungu alinisaidia.

SOMO:

1. Usiogope kutuma application au kwenda kufanya interview eti kwa vile hakuna unaemfahamu kwenye hiyo organization. Apply kila nafasi ambayo unadhani unaweza kufit. Bado zipo nafasi ambazo kweli ni merit based na sio kwa kujuana. Otherwise, mimi nisingeitwa kwenye interview hata moja, i come from a humble family, i started from scratch, bila kumjua yeyote kote nilipoomba kazi na hata kuitwa for interview, na baadhi hadi kupewa ajira.

2. Usiweke vinyongo ukidunda interview (hata kama akili yako inakutuma ulifanyiwa figisu), usikubali kuruhusu hili litawale akili yako!! Jitathmini wewe mwenyewe, na jiulize ni kipi unaweza kufanya ili kuwa bora zaidi in the next interview. Ukishakua na tabia ya kuweka vinyongo na kuamini kuwa ukidunda interview basi umefanyiwa figisu, kwanza haitakusaidia kitu, pili kila siku utakua hufanyii kazi mapungufu yako,badala yako unalaumu tu kuwa 'kujuana kwingi'. Ni sumu kubwa sana.

3. Usiende kwenye interview kichwa kichwa huku hujajiandaa, upo upo tuu!! Huna hata taarifa za msingi kuhusu hiyo organization/kampuni, hujui hata mission na vision ya hiyo kampuni, hata ukiambiwa utaji kazi tatu za hiyo organization, hujui!! Jiandae, na ujinoe haswa kwanza, kuhusu technical part of kazi unayoomba, lakini pia kuhusu basic information ya hiyo organization.

4. Usiogope ku apply nafasi ya kazi au kwenda kwenye interview eti kwa sababu labda nafasi yenyewe ni moja tuu au mbili. Maisha ni mapambano, wewe endelea kusubiri hadi ukiona wanahitajika watu 10 au 20 ndo u apply, utazidi kuchina kitaa. Mimi nilikua na apply na nikiitwa interview natia timu, hata kama nafasi ni moja, najua huu ni mpambano na chochote kinaweza kutokea, nikipata mswano, nikidunda i collect myself, naendelea na kupambana. Na kiuhalisia sasa, nafasi nyingi zenye maslahi mazuri ni zile ambazo utakuta anahitajika mtu mmoja tuu!! Usikubali kushindwa, untill it's over!!

vvm
 
Asante mkuu kwa kutupa moyo nasi siku moja tutahadithia!
 
Asante kwa kututia moyo.Huu mwezi wa 8 sasa nasota kitaa nimepiga interview hadi sio vzur sambaza barua kbao mahospitali wapi!!!.Mungu atusimamie vijana kwa kweli tusife moyo.Maana mambo mengi tuliyokuwa tunaambiwa kuwa tukisoma tutayapata imekuwa mtihani si kama vile tulivotarajia tena.
 
Nimepiga interview 2 pale utumishi

1. hii ilikua haina written, ilikua ndio interview ya kwanza kufanya baada ya kutoka chuo 2016, nimefika pale watu wanakula kidesa kama wako wanaenda kupiga pepa, nimeingia sikushindwa swali hata moja katika maswali 10 niliyoulizwa nilikua najua yote NIKAKOSA nafasi, sikuumia

2. utumishi tena, nilianzia written, Maswali yalikua JIWE mtumishi nikaondoka na 55 nikaingia oral, cha ajabu maswali 90% yalirudiwa ya interview nilofanya kati ya 10 nilikosa 2(siyajui kabisa) , NIKAKOSA, hii NILIUMIA SANA

nikarudi kitaa.
 
Asante kwa kututia moyo.Huu mwezi wa 8 sasa nasota kitaa nimepiga interview hadi sio vzur sambaza barua kbao mahospitali wapi!!!.Mungu atusimamie vijana kwa kweli tusife moyo.Maana mambo mengi tuliyokuwa tunaambiwa kuwa tukisoma tutayapata imekuwa mtihani si kama vile tulivotarajia tena.

hakuna kukata tamaa
 
Nimepiga interview 2 pale utumishi

1. hii ilikua haina written, ilikua ndio interview ya kwanza kufanya baada ya kutoka chuo 2016, nimefika pale watu wanakula kidesa kama wako wanaenda kupiga pepa, nimeingia sikushindwa swali hata moja katika maswali 10 niliyoulizwa nilikua najua yote NIKAKOSA nafasi, sikuumia

2. utumishi tena, nilianzia written, Maswali yalikua JIWE mtumishi nikaondoka na 55 nikaingia oral, cha ajabu maswali 90% yalirudiwa ya interview nilofanya kati ya 10 nilikosa 2(siyajui kabisa) , NIKAKOSA, hii NILIUMIA SANA

nikarudi kitaa.
pambana
 
Asante kwa kututia moyo.Huu mwezi wa 8 sasa nasota kitaa nimepiga interview hadi sio vzur sambaza barua kbao mahospitali wapi!!!.Mungu atusimamie vijana kwa kweli tusife moyo.Maana mambo mengi tuliyokuwa tunaambiwa kuwa tukisoma tutayapata imekuwa mtihani si kama vile tulivotarajia tena.
Komaa mwanangu! Trust me one day you will be somewhere you did not expect. Mungu atakusaidia mkuu I know how it is
 
Back
Top Bottom