Kichwamaji,
I do not underestimate Wapinzani, however they are underestimating CCM and Wananchi.
Mfano, wakati listi ya mafisadi ilipotoka, jambo la Kwanza Serikali na CCM walilifanya ni kujiuliza, je jambo hili lafungika na laweza kufika mahakamani? Jibu likawa hapana (do not ask for my source on this!), next CCM wakaanza technical mashambulizi na kuzima moto baada ya Mafisadi watajwa kudai watakwenda mahakamani (Mgonja, Ruta, Karamagi). Ukiangalia majibu ya Mkono, yalikuwa tofauti sana na alitumia technicalities and absence of subsance materials kuhusiana na tuhuma hizo.
Kilichotokea ni kuwa ile "Sensetion" ya orodha na mikutano ya hadhara ikatapakaa, lakini hakuna lililofuata.
Sisi Watanzania, tumeanza kukosoana ni nani ana haki kukemea ufisadi, huku mafisadi wakipeta na mkuu wao akitangaza rasmi ana imani na serikali yake.
Suala la BOT lina pembe tatu. EPA, Majengo na pesa za Meremeta, Tangold, Deep Green and Mwananchi. Kama kawaida, politicians wa Upinzani wakakimbilia majukwaa wakiwa na facts nusu nusu zisizo na misuli, CAG na Meghji wakasema tunafanya uchunguzi wa BOT, kila mtu akakaa kimya kusubiri ripoti binafsi ya CAG ambayo haiwi a Public thing mpaka Meghji na Kikwete waipitie.
Ripoti ya EY kwa CAG kuhusu BOT ni kuhusiana na EPA pekee na si zile pembe mbili zilizobakia. Sasa kama Uinzani ulikuwa na nondo za kutosha na kutaka kufanya hili ni jambo la Taifa, wangekuwa wajanja kumwaga habari hizi kama Udako na ushahidi wote, waache CCM wakihangaika kutafuta mchawi (kama ile barua ya Jitu Patel), halafu Upinzani ukawasilisha hoja Bungeni kuchunguza hayo mambo matatu ya BOT!
Ninachojaribu kufanya ni kusaidia Upinzani kutumuia nguvu zake katika Bunge kushikisha adabu CCM na mafisadi na si kuuza magazeti halafu 2010 unasikia Chadema ina viti 6, CUF 20 (vyote vya Pemba), TLP, UDP na NCCR wana viti 2 kila mmoja jumla ya viti 32 katika Bunge la viti 250!
Kesi za Mtikila za Wagombea huru na hata hii ya sasa ya Kadhi, Serikali na CCM wanaziogopa. Infact alishinda kesi ya Wagombea Huru, Tume ya Uchaguzi ikakiuka uamuzi wa Mahakama (Uchaguzi Tunduru) na hakuna hata mmoja kwenye Upinzani ameshinikiza suala la Ugombea Huru kufuatilia tamko la Mahakama (ingawa bado si Sheria, lakini tamko la mahakama halifutiki)!
There are better ways to play the game, so if some of us see a better way to win why not share? We are not looking for methods on how Opposition gather the facts, but it is how to use those facts effectivelly to your advantage!