The road towards 2010 Elections

Kati ya hawa nani atafaa kutuongoza 2010-2015?

  • Edward Lowassa

    Votes: 0 0.0%
  • Dr. Slaa

    Votes: 7 38.9%
  • Prof. Lipumba

    Votes: 0 0.0%
  • Mizengo Pinda

    Votes: 5 27.8%
  • Samwel Sitta

    Votes: 0 0.0%
  • Jakaya Kikwete

    Votes: 2 11.1%
  • Mark Mwandosya

    Votes: 2 11.1%
  • Harisson Mwakyembe

    Votes: 2 11.1%
  • None of The above

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    18
  • Poll closed .
- Wakishamtoa rais wa sasa, ni nani anayefaa kushika nchi naona hili swali halijibiwi, vipi?

William.

Wapo wengi wanaofaa, ni vile hawana majina na hawategemewi kugombea ndio maana huwezi kusema ni huyo au ni yule. Si kila anayefaa kuongoza lazima ajulikane na kila mtu. Kumbuka pia kiongozi unayemuona anafaa anaweza asiwe kiongozi bora kwa mwingine kutokana na kuwa na vigezo tofauti!
 

Kama utatafuta nani anayefaa kati ya hawa waliopo utahangaika sana. Mimi naamini kuwa kizazi hiki kimeharibika chote, ni ubatili mtupu uliopo. Tunahitaji kizazi kipya kutuokoa
 




Watu wa namna hii hawatufai kwani si wagombea bali ni Maruhani (Kama wale wa Pemba)
Ikiwa viongozi wanashindwa kujitambulisha na kukaa mafichoni na kungojea mwaka 2010 ndio waanze Mapambano ya ufisadi. Hivyo Mkuu wangu BUBU tuwaamini watu hao wasiokuwepo? Mbona kina Dr. Slaa wameyaanza zamani mapambano na hawajifichi? Naogopa kuwaaamini watu wanaongojea sijui wakati gani wakati Watanzania tunaendelea kuumia.
 


swali: MAGUFULI akifanya mkutano na waandishi wa habari na kutangaza kugombea?
Unadhani hawa wajumbe wataweza kumzuia. Hawawezi kutoa jina lake. Soma nyakati.

Hawawezi kuzui democrasia isitokee. wataiba kura wakati wa mkutano mkuu.
Ndio maana hawa viongozi hawapendi vyombo vya habari, na ndio maana wana katisha tamaa mtu yoyote asitangaze kugombea.


INAONEKANA WATU MNATAKA KUJUA BUBU ANAMFIKIRIA NANI, NA SIO KAMA MNATAKA MABADILIKO. NA BUBU KASHAWASOMA NDIO MAANA HATAKI HATA KUTOA JINA.
INGAWA UKITAKA UNAWEZA KUIWEKA WAZI LAKINI KURA NI SIRI.
WALA USIWAPE JINA BUBU KAA KIMYA TU.
 
Nashukuru Mkuu bubu na kwa mujibu wa majibu yako ya kipengele hadi kipengele nafikiri bado hujakataa kuwa kwa CCM hakuna anaeweza kutuongoza na maadam kama ulivyosema hapo awalli kuwa LAZIMA TUONGOZWE na CCM basi ni bora tuendelee na zimwi tulijualo.

Mambo ya Zimwi likujualo yamepitwa na wakati. Yalikuwa ni ya mwaka 47 sasa hivi tuko 2009 hivyo hatuna haja ya kuogopana au kuoneana haya. Mtu kama hawezi kazi basi ni lazima aambiwe kazi imekushinda kaa pembeni.

Bubu nilijaribu kukueleza kuwa ndani ya CCM tunashindwa kumpata alie safi kutokana na kuwa waliingia madarakani kwa jasho letu kupitia ufisadi wa EPA.

Ni lini mmejaribu kumpata liye safi ndani ya CCM na kushindwa kumpata msafi huyo? Je ni watu wangapi katika idadi ya wanachama millioni 4 wa CCM ambao walfanyiwa tathini ili kujua kama ni wasafi au la!?


Narudia tena Kikwete kashindwa kazi na hiyo ni sababu tosha ya kutomrudisha madarakani.
 

- Mkuu wangu hivi unajua jinsi Kikwete, alivyotishiwa kabla ya kugombea mwaka 2005? Wabongo tuache uoga, mbona Shibuda amesema wazi kwani amefanywa nini so far?

- Kubalini tu kwamba hata nyinyi hamna uhakika nani anafaa, na huku ndani ya CCM kumejaa waoga wengi wanaotegemea msaada kutoka mbinguni, ndio maana mtu anayejiweza na asiye muoga kama Kikwete ndiye atakayeendelea, na mwishoni mwa kumaliza kwake ataamua nani awe mrithi wake maana tumekuwa waoga mno.

Respect.

FMES!
 

William, Pamoja na mfumo wa chama kimoja nakumbuka Mwalimu Nyerere alipotangaza kuwa angeng'atuka na asingegombea tena nafasi ya Uraisi, hali ya wasi wasi iliikumba nchi na kuna watabiri walioona hali ya machafuko ikiinyemelea Tanzania. Hali hii ilisababishwa zaidi na kujengeka kwa imani na hofu ya Tanzania bila Nyerere !!

Baada ya kuingia kwa mfumo wa vyamam vingi hali ya hofu kama hiyo iliigubika nchi tena na imetumiwa sana kama mtaji mkubwa na chama tawala hadi leo - hofu ya Tanzania bila CCM !!. Sababu zinazotolewa ni zile zile zinazoendeshwa na wasioitakia mema taifa kama vile CCM ina hatimilki ya amani Tanzania na wasiwasi wa wapinzani kusababisha machafuko na vita.

Katika msingi huo huo Raisi JMK pamoja na mapungufu yake yote, kuna wanaojaribu kutumia hoja hiyo hiyo kuwa Tanzania bado inamhitaji na nia yoyote ya kumtoa ni kuchokoza hali ya utulivu na amani. Ndani ya CCM kwa sasa haitarajiwi yeyote ajitokeze kumpinga na atakayethubutu ni adui na mvurugaji kama inavyoanza kuenezwa na mitume bandia.

Naamini kwa dhati kuwa kama JMK, kwa mapenzi yake kwa taifa, ataweza kung'amua mapungufu yake mapema, atajitoa katika kinyang'anyiro cha mwaka 2010. Ambacho sina hakika ni kama ataweza kuwa hata na ujasiri huo na hii inatokana na tabia yake ya kukumbatia ushikaji katika utawala wake na kushindwa kufanya maamuzi mazito.

William, leo hii JMK akitangaza kuwa hatagombea, mtu/watu a/watajitokeza na nakuhakikishia wapo wengi tu na wenye uwezo na ushawishi mkubwa. Kutokujitokeza kwa sasa hivi ni kwa sababu ya woga wa katiba inayotoa nafasi kwa vyombo vya dola kufumbia macho uvunjaji wa sheria kwa kuangalia sura, itikadi, wadhifa na nafasi katika jamii.

Kujitoa kwa JMK kutatoa nafasi kwa taifa kupata wigo mpana na huru wa wagombea. Kujitoa kwa JMK kutaleta neema katika ushindani kwa kutoa nafasi sawa kwa wagombea watakaoingia ulingoni. Kujitoa kwa JMK kutaidhoofisha CCM kwa kiwango fulani lakini hili naamini ni jambo jema kwa taifa - CCM is too fat and it needs to diet. Kujitoa kwa JMK kutamjengea heshima katika jamii kuwa angalau aliweza kuwa na ujasiri wa kufanya hivyo kwa maslahi ya taifa.

JMK, jitoe uinusuru Taifa !!
 
Mtu kama hawezi kazi basi ni lazima aambiwe kazi imekushinda kaa pembeni.Narudia tena Kikwete kashindwa kazi na hiyo ni sababu tosha ya kutomrudisha madarakani.

- Ni kweli kabisa, ila dawa ni kumumbia tizama umeshindwa kazi, tizama flani alivyoweza, ni vyema umpishe na kumuachia huyu flani, au?


william.
 

Mambo ya kisiasa si rahisi kuyatabiri, ndiyo maana hakuna alitabiri kwamba Obama angekuwa mgombea wa Democrats na hatimaye kuwa Rais wa Marekani.

Hivyo hivyo si rahisi kutabiri ni nani anayefaa kumreplace Kikwete maana kutabiri mambo haya si rahisi hata kidogo.

Kikwete ni muoga sana ndiyo maana pamoja na recommendations za kamati ya Mwakyembe ameshindwa kuchukua hatua zozote dhidi ya Hosea na Mwanyika, pamoja na ushahidi wa kutosha kuhusu ufisadi wa Rada ameshindwa kuchukua hatua dhidi ya chenge na Idrissa Rashid, pamoja na ushahidi wa kutosha dhidi ya Richmond/Dowans, Kagoda ameshindwa kuchukua hatua zozote dhidi ya Rostam. Pamoja na ushahidi wa kutosha kuhusu uuzwaji wa kifisadi wa Kiwira ameshindwa kuchukua hatua zozote dhidi ya Mkapa na Yona. Pamoja na ahadi chungu nzima kuhusu kuipitia upya mikataba ya uchimbaji wa madini yetu hadi hii leo ikiwa ni mwaka wa nne tangu aingie madarakani ameshindwa kufanya lolote ili kuibadilisha mikataba hiyo kwa maslahi ya Watanzania. Rais muoga na ambaye haweki mbele maslahi ya nchi na Watanzania HATUFAI na hili siyo siri.
 
- Ni kweli kabisa, ila dawa ni kumumbia tizama umeshindwa kazi, tizama flani alivyoweza, ni vyema umpishe na kumuachia huyu flani, au?


william.

Obama hakuwa na record yoyote ya maana alipoamua kugombea lakini waliweza kumuamini na kumkabidhi aiongoze nchi. Hivyo nasi tunaweza kumpata Mtanzania ambaye anatimiza masharti yote ya kugombea Urais na kumkabidhi nchi na akafanya kazi nzuri na kuweka maslahi ya nchi mbele zaidi ya Kikwete.
 

- Mkuu naona hoja tatu muhimu, nazo ni uoga wa baadhi ya wana-CCM, ushikaji, na kujitoa kwa rais mapema.

- Well, kwenye hili la uoga unakuwa sio mstaarabu unaposema kwamba hoja usizozikubali za baadhi ya wajumbe wa CCM, basi zinatolewa na mitume bandia kwa nini usiruhusu hoja yako hata siku moja isimame bila this kind of abusive language? Wao wametoa tamko lao la nani wanamtaka na sababu zao, sasa labda na wewe utoe zako na ushinde hoja zao, maana otherwise, unaonekana kuongelea kutoka kwenye corner ya defeatism na that is scaring kwa sababu ni haki yao kikatiba kuona wanavyosema.

- Umesema pia hoja ya Ushikaji kama moja ya pungufu kubwa la rais wa sasa, sawa lakini tizama mzizi wa ushikaji na uongozi wetu wa taifa, utaona kwamba huyu rais wa sasa, anajaribu kufuata nyayo zilizowekwa kabla yake na ni tabia iliyoko kwenye kila kona ya uongozi katika taifa letu, ukabila, udini, na ushikaji, sasa kweli unaamini hili kuwa ni kosa lake au anaendeleza tu aliyoyakuta?

- Mwisho unaongelea yeye kujiuzulu voluntarily, kwa sababu gani hasa? Kwa sababu ningeelewa kama ungesema kuwa tizama huyu kiongozi X wa CCM anayefaa, katika miaka mitano ya utawala wa awamu ya nne, amefanya one, two three as opposed na rais Kikwete, kwa hiyo ni bora ampishe kiongozi X, au? Otherwise, sioni hoja ya msingi ya rais wa sasa kujiuzulu au kama ipo lakini haikusemwa!

Kwa kumaliza ninasema hivi, wa-Tanzania tuache uoga, tuache ku-assume na tuheshimu mawazo tofauti na yetu.

Ahsante.

William.
 
...mimi naamini kuwashinda CCM lazima kuanzie kwenye viti vya ubunge la sivyo kuwaondoa hawa jamaa itakuwa ndoto na wataendelea kutufisadi na kututia umaskini wa milele,siamini chama chenye wabunge wasiozidi 20 kati ya 400 kinaweza kushinda uraisi,battle zote zipo bungeni na kule ndio kelele zinaweza make sense sio za kina Mrema kule manzese wanaonekana wendawazimu tuu!
 
- mkuu wangu hivi unajua jinsi kikwete, alivyotishiwa kabla ya kugombea mwaka 2005? Wabongo tuache uoga, mbona shibuda amesema wazi kwani amefanywa nini so far?

-
fmes!

shibuda has got nothing to loose, he is not regarded as a threat to kikwete. Its a win win situation for him.
Kikwete is so nervous of standing against anyone.
 

Hili la kutoa jina la nani anayefaa mimi sikubaliani nalo na mfano wangu tena ni kwa Obama, maana kama Democrats wangeamua watote majina ya wanaofaa kuwa wagombea wa chama hicho jina la Obama lisingekuwemo kwa sababu hakuwa na umaarufu mkubwa ndani ya chama hicho, ni mweusi na tulishasikia mara nyingi kwamba America is not ready for a black president, he has a funny name na his middle name is Hussein and also no big accomplishments in politics or leadership to show off. Ndiyo maana napingana na wenye dhana ya kutaka watu wataje majina. Maana kwa mantiki hiyo leo hii Obama asingekuwa Rais wa Marekani.
 

Ndio maana tukasema bora huyo JK. Uko serious kweli na unayoyasema?
Unataka maendeleo yalyokosekana miaka 50 uyapate kwa kipindi cha miaka mitano na huku unakaa kwenye Forum na kuanika pumba ukitaka Jk akuletee maendeleo? Maendeleo huletwa na watu sio mtu binafsi.

Unaijua Ilani ya CCM? Ni kujinufaisha na hilo lilihakikishwa kabla Mkapa hajaondoka Kwa Fedha zetu. JK anatekeleza vizuri na ndio maana wanamgangania
Tangu aingie Kikwete angalau mauwaji ya Polisi yanafanyiwa kazi. Hata hivyo si kazi ya Rais kufatilia Kesi na ukichungua hivi sasa ndio wakati ambao haki mara nyingi zinafuatwa.
Na hizi harakati za wanaojipendekeza nazo umbebeshe yeye? Lini katika hotuba zake ukamsikia kama Rais wetu aliepita akisema kila wakati " Nilpoingia madarakani nchi ilikuwa hivi .............,vile.........?
Tumekuwa tukiomba kupatiwa mbadala wa Kikwete na tutaendeleza kudai hivyo, wewe la!
 

Akina nani Mkuu? CCM au kina BUBU?
 

Mkuu jina lako liheshimike. Kikwete alijitangaza tukajuwa kuwa anajiona anaweza, basi na hao wengine mpaka watakapojulikana ndio watapata nafasi, sio scientific ilivyo kuwe na substance?
 


Hongera angalau umeonyesha njia. Lakini usiwabebeshe watu wengine failure yake. Hebu tupe ushahidi wa kikwazo cha Mkapa kwa Magufuli na Baadae tupe kikwazo cha JK kwa kushindwa kufanya kazi zake.
Mambo mawili kama umezingatia moja ni kuwa Wizara alizopita Magufuli kazikuta na uozo wa rushwa na huondoka akiziwacha bado katika hali hiyohiyo au zaidi. Sasa wizara mojamoja ni hivyo atakapopewa jinchi lililooza kwa rushwa itakuwaje?
Jambo la pili kwa kigezo cha ushujaa wa humu JF hafai kwani hapambani na Mafisad ndani ya CCM.
Ama kwa data nafikiri akichaguliwa Urais kutakuwa hakuna haja ya Seketeri wa kumwandikia data atakuwa nazo kichwani.
 


Mkuu Bubu hebu kuwa na msimamo unaoeleweka. Namna unavyoelezea mfumo mbaya ulioko CCM na baadae kufikiria kuwa huyo mwanachama alieko Manzese tawini ataweza kupata nafasi ya kuteuliwa nafasi ya urais Duh! nafikiri hii ndio aninacha sio hiyo unayoiona wewe.
Be realistic nani kwenye CCM alitokea tawini tu akawa mjumbe wa halmashauri kuu sembuse kamati kuu na nafasi ya kugombea urais.
Mfano wako wa Obama does nt hold water na hali hii tunayoizungumza. Obama alipitia nafasi zote na ilikuwa stahiki yake kupanda hapo alipo na kwa mfano huohuo wa Obama na sisi tunawapima wana CCM walikokuwa tayari kufikia kiwango hicho cha kugombea urais na tunashindwa kumuona na hasa kwa kigezo chako mwenyewe kuwa wote si safi kwa vile wamebebwa na Chama kilichokuwa si safi.
Kama unakubali kuwa CCM ina mizizi katika ufisadi utawezaje kutegemea mmoja wa wajumbe wa mafisadi kupigana na ufisadi. Ni miaka minne sasa tangu CCM iingie madarakani kwa pesa za EPA ni nani katika CCM,awe mbunge, Waziri,Mwenyekiti wa Mkoa au mjumbe aliekikana Chama kwa ufisadi wake?
Mapambano tunayoyaona si mapambano ya kukisafisha chama bali ni kulipizana kisasi kwa wanachama binafsi. ingekuwa vita hivyo ni dhidi ya shina hasa CCM basi tungesema kuwa anaweza akatokea mtu alietofauti na wenzake ndani ya CCM na kwa hivyo huyo alieko mwache amalize muda wake, kwani si hatuna Chama chengine cha kushika Madaraka.?
 
Vigogo waanza kukorogana

Mwandishi Wetu Aprili 8, 2009

Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo

Baadhi wawabeza Ndejembi na wenzake

Wengine: Kuna mbio za kumuwini Kikwete

Wasema hoja ya msingi si urais, ni ufisadi

BAADHI ya wanachama waandamizi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamesema uamuzi wa kumuunga mkono Rais Jakaya Kikwete kuwania tena urais mwakani si jambo la msingi bali jambo la msingi ni hatari iliyopo ya dola kuelekea kutekwa na kikundi cha matajiri.

Kwa mujibu wa wana-CCM hao, kuna msukumo mkubwa kwa matajiri nchini na hasa wenye maadili yanayotia shaka, kuwekeza katika siasa kwa kuwania nafasi za uongozi lakini kwa malengo ya kulinda maslahi yao.


Maelezo ya viongozi hao waandamizi wa CCM yanakuja siku chache baaa ya baadhi ya wenyeviti wa mikoa wastaafu wa chama hicho kufanya mkutano na waandishi wa habari na kutangaza pamoja na mambo mengine kumuunga mkono Rais Kikwete katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Katika mkutano wao huo uliofanyika Aprili 5, mwaka huu, wazee hao Pancras Ndejembi ambaye ni mwenyekiti mstaafu mkoa wa Dodoma, Tasil Mgoda (Iringa), Jumanne Mangara (Pwani) na Hemed Mkali (Dar es Salaam), walisema wanamuunga mkono Kikwete na kukemea tabia inayojitokeza ya baadhi ya viongozi kutumia vita ya ufisadi kama mtaji wao wa kisiasa hata kama wameshindwa kutekeleza wajibu wao kwa wananchi.

“Tupigie kelele rushwa lakini turudi kwenye kuitaka Serikali iimarishe taasisi na vyombo vya kupambana na rushwa. Huko ndiko watuhumiwa wa rushwa wanachunguzwa, wanakamatwa na hatimaye wanahukumiwa.

“Baada ya kuhukumiwa na mahakama ndipo tunawaita mafisadi. Kumuita mtu fisadi kwenye gazeti au kwenye mkutano wa waandishi wa habari peke yake hakutoshi kama tunataka kushinda mapambano haya. Ni lazima vyombo vya na taasisi za kupambana na rushwa viwe imara,” alisema mzee Ndejembi kwa niaba ya wenzake.

Alidai pia kwamba kila wanachama wa CCM wanachukia rushwa kwa kiwango sawa na kwamba vita dhidi ya ufisadi ni ya chama hicho na si ya kikundi kidogo cha wana-CCM ambacho kinatumia mwanya huo kama mtaji wa kisiasa.

Kutokana na maelezo hayo ya akina mzee Ndejembi, viongozi wengine waandamizi wa CCM wamezungumza na Rai Mwema wakijaribu kutafuta kiini hasa cha kuibuka kwa wazee kuzungumza mapema kumuunga mkono Kikwete na matatizo ya msingi yanayokizonga chama chao, ambayo hayajafichuliwa.

“Baadhi katika kuhakikisha wanawekeza katika siasa hususan ndani ya CCM wamehakikisha wanakuwa wafadhili wakubwa wa chama na ndiyo maana baadhi ya misaada yao aliyowahi kupokea Rais Jakaya Kikwete imezua maswali mengi,” alisema mmoja wa viongozi wa kitaifa wastaafu.

Ingawa kiongozi huyo hakuwataja kwa majina matajiri hao ambao maadili yao yana utata, mwaka jana Rais Kikwete aliwahi kupokea msaada kutoka kwa tajiri Tamil Somaia, kwa ajili ya kusaidia uchaguzi wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kitendo hicho cha Rais Kikwete kupokea msaada huo kwa ajili ya UVCCM huku ikifahamika wazi kuwa mhusika anahusishwa katika tuhuma za ufisadi wa rada kilizua mjadala mkali miongoni mwa wana-CCM na makundi mengine yasiyofungana na vyama vya siasa nchini, wakiwamo waandishi wa habari.

Kiongozi mwingine ambaye pia hakutaka kuandikwa jina lake gazetini ambaye pia ni mstaafu ngazi ya kitaifa, alisema hatua ya baadhi ya wenyeviti wastaafu wa mikoa wa CCM kutangaza kumuunga mkono Rais Kikwete imedhihirisha makundi yaliyopo ndani ya CCM hadi sasa.


“Unajua kuna siri moja. Mzee Malecela (John) bado ana heshima kubwa ndani ya CCM na kwa sasa wanachama wengi ndani ya chama wanamwona kama kiongozi wa kundi la viongozi wanaopinga ufisadi hadharani bila woga.

“Sasa kitendo cha Malecela kutoka hadharani na kuzungumza kumuunga mkono Kikwete mwaka 2010, maana yake ni kwamba kundi lake la wapambanaji wa ufisadi liko karibu na Rais Kikwete, lakini kwa upande wa Ndejembi (Pancras) huyu ni hasimu mkubwa wa kisiasa wa Malecela,” anasema kiongozi huyo na kuongeza kuwa;

“…pia Ndejembi mbele ya wanachama wengi wa CCM anajulikana kuwa katika kundi moja la akina Peter Kisumo, Kingunge Ngombale-Mwiru na wengine ambao kauli zao zinatafsiriwa na wanachama kama zinawaonea huruma mafisadi na kwamba kundi lao linaendeshwa kwa maelekezo ya waathirika wa ufisadi na rushwa ambao baadhi wamejiuzulu.”

Naye mbunge mmoja ambaye pia alishirikishwa na gazeti hili kutoa mawazo yake kuhusu hatua ya baadhi ya wastaafu kuzidi kujitokeza kumuunga mkono Rais Kikwete, alisema mashindano ya kila mmoja kujitokeza kumuunga mkono Rais mwakani ni kutaka kundi husika kujisogeza jirani naye.

“Haya mashindano si suala la msingi, lakini msingi hapa naamini kwamba ni kuwapo kwa juhudi na wasiwasi wa nchi kufikishwa katika hali tunayoweza kusema state capture…yaani dola kubakwa hasa na matajiri haramu.

“Hii ndiyo hali iliyojitokeza nchini Italy. Italy imejikuta ikiongozwa na kampuni kubwa na matajiri…wananchi hawana nguvu wala sauti. Nikupe siri moja hata hapa kwetu huo mkakati upo ingawa umesitishwa baada ya kulipuka kwa kashfa ya Richmond…lakini watu wachache walijipanga kutawala uchumi na siasa za nchi na hatimaye vyombo vyote vya dola yakiwamo majeshi yetu,” alisema mbunge huyo ambaye amejijengea heshima kubwa mbele ya jamii katika miaka ya hivi karibuni.


Katika kusisitiza maelezo yake alisema; “Walijipanga na kuhakikisha siasa inakuwa kwa ajili ya watu wenye pesa kuanzia ubunge lakini ule mchakato wa kwenda kwenye state capture umetingishwa na suala la Richmond na wanaonekana kukata tamaa na hizi vuruguru za hapa na pale kutoka kwao ni sawa na mateke ya mfumo unaoondoka,” alisema.

Mbunge mwingine aliyezungumzia mwenendo wa sasa katika CCM ambaye pia kama ilivyo kwa wenzake hakutaka kuandikwa jina lake, akihofia kuvuruga uhusiano wake na wazee hao wa CCM, alisema; “Jambo la kutia moyo ni kishindo cha nguvu ya umma kutokuwa upande wao."

Hata hivyo, alishangazwa na baadhi ya wazee wa CCM wanaojitokeza kukemea wanaopinga hadharani ufisadi huku wakishindwa kukemea watuhumiwa wa ufisadi ambao kwa mujibu wa mbunge huyo wanatumia fedha zao kuanzisha magazeti ya kuwachafua wana-CCM wenzao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…