The Richest Man In Africa: Kila Utajiri una Ukafiri nyuma yake

Habibu B. Anga

Habibu B. Anga

Verified Member
Joined
May 7, 2013
Messages
6,407
Points
2,000
Habibu B. Anga

Habibu B. Anga

Verified Member
Joined May 7, 2013
6,407 2,000
cl9jz-xwiaasy_n-jpg.815633The Richest Man in Africa: Kila utajiri una ukafiri nyuma yakePREMIERE


Nimekuwa kimya sana, nimejikita sana katika tafakuri. Tafakuri juu ya masuala yaliyo bayana lakini hayasemwi... masuala yaliyo dhahiri lakini hayaonwi. Pengine kuna sababu kwa nini hayasemwi na pengine kuna juhudi ya kufanya yasionwe.

Nahisi imefika zama kwa wale ambao tumeamua kufanya kalamu kuwa maisha yetu labda tuthubutu kuoneshwa visvyoonwa na kusema yasiyosemwa. Ni hatari, nafahamu. Lakini hatuna fursa nyingine ya kuweka alama juu ya uso wa dunia zaidi ya fursa ya maisha haya tuliyonayo sasa.


Moja kati ya vitu vibaya zaidi na vya kukaraisha kuishi katika nchi za ulimwengu wa tatu si umasikini wake tu bali ni namna ambavyo tumejiwekea mifumo ya kudumaza uthubutu wa kuwaza na kujenga fikra mbadala. Pengine mifumo hii dumavu ndio sababu hasa ya kufanya umasikini usikome katika nchi zetu hizi.
Utete wa kiwango cha kujiamini (fragile egos) cha viongozi wetu wa nchi hizi umefanya watu kuwa na mawazo mbadala liwe ni mwiko kabisa. Na siongei tu kuhusu ukosoaji, la hasha bali najenga hoja pia juu ya utamaduni wa nchi zetu kuijenga jamii yetu kuwa na mawazo ya 'kundi la ng'ombe'. Mawazo mfanano. Utamaduni wa kuona kwamba tukiwaza sawasawa ndiyo inatufanya kuwa jamii bora tukisahau kuwa maendeleo duniani yameletwa na uwepo wa watu waliofikiri kinyume na mawazo yaliyojengeka kwa muda mrefu kwenye jamii. Watu wenye kufikiri nje ya mawanda yaliyozoeleka.

Utete wa viwango vya kujiamini vya viongozi wetu unafanya hofu na woga kutamalaki kwenye jamii yetu kiasi kwamba hata wenye kujua kidogo tu hawakisemi na kuogopa kuifumbua macho jamii juu ya machache wajuayo. Matokeo yetu jamii zetu za kiafrika zinaishi katika ukimya, ukimya wa wanaojua wakiacha jamii ukifungiwa gizani na hata watoto wetu mashuleni kulishwa historia iliyokobolewa na kupembuliwa na kubakia makapi wasijue ukweli halisi.

Ni muda muafaka nadhani kwa viongozi wa kiafriaka kutambua kuwa mawazo mbadala hata yale ambayo wanaweza wasiyafurahie ni mbolea katika ustawi wa jamii. Jamii inakua kwa mawazo yenye kukinzana. Kukinzana kwa dhamira ya kuisukuma mbele jamii.

Mwaka jana nilifurahishwa sana na makala kinzani ambayo ilikuwa imekuja na wazo mbadala lenye kukinzana na jarida la Forbes ambalo hutoa orodha ya watu matajiri zaidi duniani. Makala ile ilimuainisha Vladmir Putin Rais wa Russia kama mtu tajiri zaidi duniani akiwa na utajiri wa zaidi ya dola bilioni 200. Kwa haraka haraka baadhi ya watu walihisi ni propaganda za magharibi kumjengea picha Putin kama kiongozi mwenye kujilimbikizia mali na mlafi.
Yawezekana ni kwelil lakini watu wanaruka ukweli kwamba ukiwatazama maswahiba wa karibu wa Putin kama vile Roman Abramovich wana utajiri mkubwa kuzidi ule ambao unatajwa na jarida la Forbes. Lakini pia ukitazama kwa mahesabu ya kihasibu kuna kiwango kikubwa sana cha fedha ambacho hauwezi kukisema kilienda wapi katika kipindi cha mwishoni mwa miaka ya tisini na mwanzoni mwa miaka ya elfu mbili kipindi ambacho kinatambulika nchini Rusia kama kipindi cha 'alluminium war'.

Lakini pia ni ukweli ulio wazi kuwa jarida la Forbes halivutiwi na kuwaweka kwenye orodha ya utajiri viongozi wa kiserikali na wahalifu. Ndio maana utaona ma-Prince wa nchi za kiarabu licha ya utajiri wa kufuru walionao lakini hawapo kwenye orodha hizo. Vivyo hivyo na wahalifu wa daraha la kwanza kama akina Guzman El Chapo ambaye ana utajiri wa kutupwa lakini bado haorodheshwi kwenye orodha hiyo.

Ndipo hapa ambapo nataka kujadili juu ya mtu tajiri zaidi Afrika ambaye huwezi kumsoma kwenye jarida la Forbes. Lakini utajiri wake ambao nataka kuujadili si utajiri wa fedha pekee bali nataka kujadili namna ambavyo mtu huyu anavyo ratibu matumizi ya rasilimali katika nchi nne za ukanda huu wa Afrika mashariki na kati, yaani Tanzania, Rwanda, Burundi na Kongo.

Vuta pichani kichwani mwako akitokea mtu mmoja mahiri na kuweka rasilimali za nchi nne tofauti mikononi mwale. Vuta picha ya mtu mwenye uwezo wa kusema neno lolote na likatekelezwa kote ukanda mzima wa Afrika mashariki na nchi za maziwa makuu.

Kwa heshima na taadhima, leo saa kumi jioni nakukaribisha kusoma makala yangu mpya "THE RICHEST MAN IN AFRICA: Kila Utajiri una Ukafiri Nyuma Yake"


SEHEMU YA KWANZA BOFYA HAPA

SEHEMU YA PILI BOFYA HAPA


SEHEMU YA TATU BOFYA HAPAStay here and keep your eyes (and your mind) open!Habibu B. Anga "The Bold"
To Infinity and Beyond
 
M

Mshughulishaji

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2015
Messages
798
Points
1,000
M

Mshughulishaji

JF-Expert Member
Joined Sep 29, 2015
798 1,000
Mkuu Habib B. Anga, unatutupa tupa sana wafuatiliaji wa makala zako !
Lakini pole pia kwa vikwazo unavyokutana navyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
K

kashinje juma

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2017
Messages
709
Points
1,000
K

kashinje juma

JF-Expert Member
Joined Apr 20, 2017
709 1,000
The bold.ntafurahi km utaniunganisha kwenye list ya unaowatag kwenye simulizi zako.jina kashinje bulugu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
K

kashinje juma

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2017
Messages
709
Points
1,000
K

kashinje juma

JF-Expert Member
Joined Apr 20, 2017
709 1,000
Bingwa the bold.km itakupendeza naomba uniadd kwenye list ya unaowatag kwenye simulizi zako kali na za kusisimua..natanguliza shukrani mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
J

Joseph lebai

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2017
Messages
3,048
Points
2,000
J

Joseph lebai

JF-Expert Member
Joined Jul 19, 2017
3,048 2,000
Achana na matajiri wakubwa, anza na jamii yako, ukichunguza kwa makini , tajiri yoyote, namaanisha yoyote, kuna "kaukafiri " ndani yake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CANIMITO

CANIMITO

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2013
Messages
2,064
Points
2,000
CANIMITO

CANIMITO

JF-Expert Member
Joined Feb 12, 2013
2,064 2,000
Sehemu ya 4 na kuendelea inapatikana wapi?
 
Adolph hitler jr

Adolph hitler jr

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2016
Messages
1,833
Points
2,000
Adolph hitler jr

Adolph hitler jr

JF-Expert Member
Joined Nov 5, 2016
1,833 2,000
Mkuu naweza pata copy ya kitabu kwa bei yeyote ata online softcopy..?
 
Dunamist

Dunamist

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2018
Messages
255
Points
500
Dunamist

Dunamist

JF-Expert Member
Joined Aug 13, 2018
255 500
Naomba tag, Mara sehemu ya nne ikija hewani... Habibu B. Anga
 
M

Mbelajr

Member
Joined
Sep 14, 2018
Messages
14
Points
45
M

Mbelajr

Member
Joined Sep 14, 2018
14 45
Mkuu tudadavulie sehemu ya nne,vitabu vyako hatuvijavipata.Uko juu zaidi ya Antenna
 
K

kashinje juma

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2017
Messages
709
Points
1,000
K

kashinje juma

JF-Expert Member
Joined Apr 20, 2017
709 1,000
Kinauzwaje mkuu,na ntakipataje?
 

Forum statistics

Threads 1,333,944
Members 511,787
Posts 32,458,846
Top