prince john john
JF-Expert Member
- Aug 31, 2016
- 2,293
- 3,650
Duuuh hatare
Mh sijui hapa kutakua na style ya kukung’uta siafu ya mtoto Khumbu.


mkuu kwani na wewe uko interested !?May be...ni mtazamo wako piaI can simply conclude kwamba ulikua hujui unachotafuta kwenye mahusiano na ni mtu unaefanya maamuzi kwa kukurupuka
Ni upuuzi mambo ya itaendeleaKwa uzi huu nitaandika meeengi sana,kwa wote ambao tuliwahi ku-date but hatukufikia malengo ya kujenga familia, Kati ya watu nilio- date nao, wawili wapo humu (mmoja tulifika mbali sana na mwingine hatukuwa na mahusiano ya kiviiile) ila wote naamini watasoma uzi huu, kama kuna mahali nitakuwa nimemsingizia mtu ruksa kunikosoa...
1. Bertha...
Huyu alikuwa msichana wangu wa kwanza kabisa, tukiwa kidato cha tano, (alikuwa Iringa girls na mimi nilikuwa MINAKI) tulipendana sanaaa, I felt to be loved and I submitted all of my emotional strength
Nakumbuka wakati wa likizo tulikutana hostel za UDSM zilizopo ubungo nyuma ya NBC BANK, (bro aliniacha hapo nikiwa tution yeye akiwa masomoni nje ya nchi), kwa mara ya kwanza tulichezeana sana,lakini hatukufanya mapenzi kwa mimi kuwa na hofu sana ya UKIMWI, nayeye pia alikuwa mwenye hofu sana tukaishia hivyo, she was a very good girl,baada ya shule kufungua maisha yaliendelea, tulipofanya mitihani ya kidato cha sita mahusiano yalipungua na hatimaye yakapungua hatimaye kupotezana....
2. Grace...
Alisoma Ruvu girls, tulianza mahusiano baada ya kumaliza kidato cha sita, (tuli-date kwa muda mfupi lakinitulifanya Mambo mengi sana,kwa mara ya kwanza nikajua mpaka kulala lodge..
Baada ya muda kidogo nikagundua Grace anakunywa pombe ile mbaya, moyo wangu uliumia mno, nikahisi na-date na mti asiyefaa kabisa kuwa mke wangu tukaachana, (tulipokutana Udsm tukawa marafiki wa kawaida as if hatukuwahi kuwa na mahusiano) kwa sasa sijui yuko wapi hata...
3. MARIAM
Huyu nilikuwa na uhakika wa asilimia 80 kuwa nitamuoa, tulianza mahusiano mwishoni mwa semista ya kwanza, tukashibana sana,mwaka wa pili tukaamua kukaa Chumba kimoja (anapika anafua boom tunaweka pamoja na kufanya mipango mingi ya maisha yetu baada ya shule) eeeeh bwana wee, kumbe alikuwa na mahusiano mengine na jamaa alikuwa anasoma Duce...(nilijuaje? ni story ndefu ila nitaifupisha kwa kadri niwezavyo)
Ilikuwa siku ya Alhamis, (tukiwa mwaka wa pili) nilikuwa na ratiba ya practical nayeye alikuwa anajua, so aliniaga kwamba angeenda kumtembelea rafiki yake anaitwa Mariana, sikuwa na shaka hata kidogo,bahati mbaya kwake siku hiyo practical ikaahirishwa, nikawahi kutoka, ile nafika utawala (packing ya UDSM) naona Mariam anaingia kwenye gari ya mawasiliano, nikaamua kumfuatilia bila yeye kujua, alipofika mawasiliano alimfuata mshkaji mmoja wakaongozana kuelekea njia ya sinza, nikawa nawafuatilia na kuwapiga picha pasipo wao kujua, wakaingia moja ya lodge maeneo ya Mugabe, niliumia kwa viwango vizivyoelezeka nilisubiri kama nusu saa baada ya wao kuingia lodge nikaingia pia, nilipofika mapokezi nikachukua kitabu Cha wageni nikaandika majina yangu bandia lakini lengo ikiwa kutaka kujua chumba walichoingia Mariam na mshkaji, nikapiga picha ile daftari, (jamaa aliandika na namba yake ya simu) nikadhani atakuwa ameandika namba ya uongo lakini kwa bahati alikuwa ameandika namba yake halisi, nilichukua information zake nikaishia...
Ilipofika jioni narudi home nokamkuta Mariam anapika, nikamuuliza habari za rafiki yake Mariana akasema ameenda na ameonana naye ananisalimia...(nilikuwa na hasira muda huo asikwambie mtu, lakini sikutaka kumwonyesha kuwa nina hasira, though chakula sikuweza kula.
Baada ya siku mbili,niliamua kumtafuta jamaa bila Mariam kujua, nikaongea naye meeengi na hatimaye tukaamua kila mmoja ambwage Mariam (akili za shule shule bhana...)
Niliporudi home nikamuuliza Mariam ana wapenzi wangapi, like swali lilizua tafrani za hatari, alilia Mariam asikwambie mtu, akanituhumu kuwa namuonea kwa kutokumwamini ilhali yeye amejitoa kwa moyo wote kufanya maisha na mimi, hapo nilijifunza kitu kikubwa sana kwake.
Wakati wote akinishambulia kwa maneno makali nilikuwa na hasira mno,nilijizuia kwa kiwango cha juu kumpiga hata Kofi moja kwani nilijua kufanya hivyo kungepelekea madhara mengine makubwa zaidi, nilimwambia najua kila kitu kuhusu yeye na jamaa, nikamtajia lodge waliyokwenda na chumba walichoingia nikamtumia na picha za siku ya tukio, hapo ndiyo akaanza kuniomba radhi, SIKUWEZA KUMSAMEHE, nilimuacha, alinitafuta sana baada ya miaka 2 kupita sikutaka tena kumrudia.
ITAENDELEA....
Sent from my Z9 using JamiiForums mobile app
Kuna wakati ili uwe huru unalazimika kutoa dukuduku zilizo ndani,na mbaya zaidi huwezi kusimulia physically,angalau huku unajimwaga na kupunguza sumu bila hofuNaona members mmekuja na muamko wa kuhadithia history za maisha yenu Sasa hii ndio trending iliyopo Sasa hapa Jf
Safi Sana endeleeni kutupa story hizo tunajifunza mengi Sana kupitia nyinyi
Hahahaaa, kila mtu na lake mkuu, unaingia tu...hizi mada zenu zinatufanya wengine tuzidi kuyaogopa Mapenzi faken


Endelea...Kuna wakati ili uwe huru unalazimika kutoa dukuduku zilizo ndani,na mbaya zaidi huwezi kusimulia physically,angalau huku unajimwaga na kupunguza sumu bila hofu
Sent from my Z9 using JamiiForums mobile app
Maamuzi ya kukurupuka hapo juu ni kama yepi best yangu au unekuwa wewe ungeamuaje kuanzia huyo namba moja mpaka tano...I can simply conclude kwamba ulikua hujui unachotafuta kwenye mahusiano na ni mtu unaefanya maamuzi kwa kukurupuka

Naam nakuelewa Sana Tuko pamojaKuna wakati ili uwe huru unalazimika kutoa dukuduku zilizo ndani,na mbaya zaidi huwezi kusimulia physically,angalau huku unajimwaga na kupunguza sumu bila hofu
Sent from my Z9 using JamiiForums mobile app
Aaahh now days tunaingia huko kwaajili ya sex tu nothing more

Weka vitu Mkuu.![]()

Ukiweka story nzima kwenye ukurasa mmoja inakuwa ndeeefu mno, sio lazima usome yote, unaishia panapokutosha tu..Ni upuuzi mambo ya itaendelea
Kwahiyo story imefikia mwisho !?
Hiyo hatua niliifikia ila pia nikafeli...Aaahh now days tunaingia huko kwaajili ya sex tu nothing more
Mambo ya kupigwa matukio Kama hayo Mimi nataka Sasa![]()



SawaUkiweka story nzima kwenye ukurasa mmoja inakuwa ndeeefu mno, sio lazima usome yote, unaishia panapokutosha tu..
Sent from my Z9 using JamiiForums mobile app