The Real Hidden World

The Real Hidden World

Mkuu, mbona unapiga danadana nyingi Sana katika Bandiko lako. Huenda unajambo lenye manufaa unalotaka kuliwasilisha. Lakini Shaka yangu na watu wenye fikra Kama zangu ni kuwa, Bandiko lako halina mshikamano unaowiana wa hoja.

Aidha, katika bandiko lako hujaelezea huo ulimwengu halisi ambao unadhani umejificha.

Kwa ufupi, unatumia nadharia za waandishi walioamua kuuelezea ulimwengu uliomo katika fikara zao.

Maisha haya ndio maisha halisi, mengine ni porojo.
 
Nikweli ndugu usemalo
Ila Kumbuka Unaposoma History haina maana ukiwa kazini utafanya kai ya history
Kuna vitu tunaita ujuzi kuna vitu tunaita maarifa napia kuna cha ziada kinaitwa hitaji.
Vyote hivyo vinasababu hadi uweze kuvitambua na kuvizingatia, bila sababu huwezi kuvijua na kuvitambua ni lazima uwe na sababu yako ya msingi itakayokupelekea kujua.
Mfano Mmoja mzuri sana ni huu
-Kwanini Unajua Ubatizo umewagawa wakristo?
-Je Unaweza Kushika Sheria Ambazo Hazina Hukumu(Utawashangaa Wasabato Hapa)
-Je unajua yakuwa Biblia haithibitishi uwepo Wa Mungu?(Wanaoamini Mungu Yupo ndio wanawaamini biblia ila asiyeamini Mungu Yupo hata Biblia hawezi iamini)
-Je nikweli baraka unaweza zipata kwa kuibariki Israel?(Wakristo hapa wengi wanafeli kwakuwa wamekaririshwa neno ila hawajataka kujifunza na kulielewa neno)
Maswali machache hayo hapoo juu ukijiuliza utatambua yakuwa ni jambo limefichika ambalo hakuna mtu atakupa majibu sahihi usipoamua wewe kujifunza.

Kwahiyo mambo yaliofichika si kukupeleka shimoni ila yatakufanya ujitambue na kuzijua haki zako zaidi za msingi
broda hicho unachozungumza ni shauku yako ya kujua usichokijua. so swali langu lilikuwa hv. baada ya kujua inakuongezea nini kufanikisha ndoto zako? au unafikir kila aliyefanikiwa alipitia huko. mi nafanya biashara huku nalima nawakat mwingine nadeal na ujenz so unaponiambia nisome ulimwengu usioonekana unataka nikishaujua niuweke kwenye mishe zangu au. broda hii dunia ina mmiliki wake cc tulijikuta tupo tayar so ukitaka kuujua sana unapoteza muda we tafuta hela jiwekee mipango komaa kila mwaka uhakikishe umetoka hatua moja kwenda nyingine. hayo unayotaka kujua ukishayajua utataka kujua zaid mwisho unapotea coz tunaish mara moja tu tutumie muda wetu vizur aisee hatuna muda ndugu yangu. mimi kwenye kusafir kwangu sana nimekutana mpaka na watu wanamuabudu mbwa na ni wasomi wakubwa sasa ukiniambia mimi nikae chin nimfikirie huyo mtu ili iweje. kuna vitabu vingi vya kusoma bana kuna watu wamefanya mambo mengi makubwa soma mawazo yao njia walizopitia upate huko cha kumrithisha mtoto achana na hadithi za alfu lela ulela nanii pambana jombaa uzee unakuja fasta kuliko unavyofikir.
 
KijanaHuru ukijuwa utakuwa na uhuru, Ebu nitupie hivyo vitabu PM.
Napenda sana vitabu niko tayari kununua kitabu hata cha elf 80 ndiko kwenye maarifa.

Kuna vitu unataka kueleza juu wakati ni vya muhimu sana kwa sisi tunaotaka kuwa Huru. There are light we need to follow it
 
A book of Napoleon sijaelewa jinsi ya kukitumia, kama mtanusaidia muongoza itapendeza
 
Nikweli broo ni kitu fulani adimu sana
wachache wanajua, muhimu kuujua vyema ni mpaka ujitose uweze kwenda nao sambamba
mambo yake mengi tunayajua kama sumilizi za paukwa na pakawa ila ukweli wake
huenda mtu ukaogopa hata kutembea nje sometimes
ila madhara yake pia yapo inaweza kukufanya ukawa mwana dini sana
ama ndio ukaamua kukengeuka mazima.
sometimes unaweza ukawa kama mwehu maana unachokijua unataka kila mmoja ajua awe salama.
anything can happen
wengine huwafanya kuwa wapole sana na huongezeka busara zaidi na maarifa.
a lot of things utagundua.
but also humfanya mtu ajitambue kwa usahihi zaidi
ukweli sikuujua kwa kusoma vitabu bali niliutambua baada ya kufanya meditation kwa kutumia weed,
 
Hicho kitabu unacho nirefer nimeshakisoma bahati mbaya nipo far na access ya PC ningekutumia na hivo vingine kama vya ester na Magdalene!..
All in all good luck on your expedition, only don't forget your grounds!..
Dah!hivi hiko kitabu cha Mary madgalena kinahusu nini sana sana??
 
Umenigusa Sana, Ni Kama vile nakuona, kitabia/haiba .. samahan lkn imefikia elimu level ipi
Kwauhalisia nilikuwa nasoma sana vitabu ila ilikuwa ni vitabu vya hadith na masimulizi sana kidogo nilikuwa nagusia vile vya documentary hii ni kutokana na kuwa baba yangu ni mmsomaji mzuri sana wa vitabu.
Na anamaktaba yake nyumbani hivyo baada ya kujua kusoma tu tangu nikiwa mdogo basi kila maandishi nilipenda kuyafakamia na kusoma ili mradi tu nivutiwe na kilichoandikwa,
Kuhusu huyo mzee ilikuwa ni kwaajili ya mada tuliyokuwa tunabishana na wenzangu kwa uhalisia nilikuwa sahihi ila ikukubalika kwasbabu usahihi wangu haukuwa sawa nawao na wala haukuendana nao kabisa sasa yule mzee alinielewa toka mwanzo hadi mwisho alitambua nikoje,
Ndipo akanimwagia sumu kali ambayo imeniweka mahali hadi sasa,
Umuhimu mkubwa ni kwamba kwasasa naweza kujua wapi nisahihi kujenga hoja au wapi sio sahihi,Najua hapa nikae kima hapa niongee.
Kwa ufupi inasaidia sana kujijua wewe ni nani, wajibu wako, kwa wakati gani, kwa manufaa gani.
Faithcally unaweza kuwa juu zaidi ama ukashuka zaidi.
Inaetegemeana na jinsi ulivyoweza kuzi-adopt hizo mambo
 
Nianze kwa kusema nakumbuka nikiwa bado mdogo mdogo, nilikuwa na sifa moja kubwa sana mtaani kwetu ya ubishi.
Hata kama ulete fact za kiwango gani lakini niki-stickkatika msimamo wangu ni hapo hapo hamuwezi kunibandua hata mngekuwa mia.
Lakini kuna jambo moja aliligundua mzee mmoja siji kumsahau katika maisha yangu yote ningali bado mdogo kabisa miaka 8.
Aliniita na kuniambia
""Nikiamua kuwa na maarifa naweza kuwa nayo, nakuambia hivi si kwamba nimekuona unamaarifa bali nimegundua unaweza kujaza maarifa ukitaka, sasa nakupa kazi jifunze ulimwengu uliofichika ulivyo hautapata nafasi ya kubishana na wengine kamwe'''
Mzee nilimuelewa japo kwa ufupi sana, labda kutokana na umri wangu ulivyokuwa na kuambiwa jambo lililokuwa juu ya uwezo wa frikra zangu.
Nikiwa na miaka 14 ndipo mzee aliweza kunipa kitabu kilichokuwa na Tittle Hii
"Comfort That Kills" Nikitabu chenye page 36 tu lakini ndicho kikabadili ukurasa wangu wa maisha na kunipa hamu zaidi ya kuujua ulimwengu uliofichika.
Nilikisoma kwa kufanya mirejeo mingi sana katika kamusi ya kufasiri maneno ya Kiingereza kwenda kiswahili,
kwanza kilikuwa na maneno mengi ya kiingereza cha zamani sana, kilinipa shida kidogo lakini niliweza kukielewa na kufunguliwa ukurasa mpya wa kusoma Maandishi.
Si kwamba sikuwa msomaji toka mwanzo ila nikwamba usomaji wangu uliegemea sana katika kusoma hadithi za nadharia zaidi zilizoandikwa na waandishi mbalimbali mahiri.
Sasa hapo ndipo nikaaznza kuufukunyua ulimwengu uliofichika kwa fujo zote.
Sio katika Upande wa Dini au Historia tu, bali niliweza kuyajua mabo mengi sanakwa muda mfupi.
Na kadri nilivyozidi kusoma ndivyo nilivyozidi kujua na kutambua ya kuwa katika asilimia 100% huenda nimeijaza asilimia 0.001%(Kwa wasomaji wavitabu wananielewa vizuri hapa maana kadri unavyosoma ndivyo unaona hauna kitu na unahitaji kujaza vitu)

Nilikuwa napitia Thread Za mtu mmoja humu(jina kapuni)
Niligundua jambo moja wengi wanaompinga katika thread zake ni wale wanaoangalia muvi na video za youtube juu ya uhalisia wa ulimwengu tunaoishi, lakini hawezi kuwa na mrejesho hata mmoja juu ya maandishi aliyoyasoma.
Huyu jamaa ameandika vitu vingi ambavyo huenda sikujua kama naweza kukutana na mtu kama huyo hapa, lakini ndipo nikajua kumbe JF ina watu wengi sana wa kila namna (Viva JF)
Sijaja Hapa kuueweka hadharani ulimwengu uliofichika ila ukihitaji kuujua unajulikana kabisa, tena kwa urahisi sana.

Labda unaweza ukakosa Mzii mahala pa kuanzia lakini nakupa kidogo jambo moja.
Jaribu kujifunza mambo kama haya hapa.

Kwa watu wa Imani hasa wakristo na waochimba masuala ya tulikotoka,kwanini iko hivi,kwanini iko vile,imekuwaje,ilikuwaje,jaribu kupitia mambo haya.
-Ni vitabu gani vilimeondolewa katika Biblia
Unaisoma Biblia Leo lakini inavitabu zaidi ya vitano havijawekwa humo
Tafuta kwanini havimo, vinafundisha nini, nk

-Ni nani alikuwa mmiliki wa kwanza wa America(Usiniambie wahindi wekundu nabaadhi ya maneno yaliyopo kajifunze ulimwengu uliofichika)

Naomba niishie hapo kwa Leo, lakini nikipata mda mzuri na nafasi nitaweza kuleta hoja mbalimbali juu ya ulimwengu uliofichika kwa kadiri ya jinsi nitakavyokuwa na muda.


Updates Ipo Page #30 Kitabu Chenye Utata (Kina Uwezo Wa Kujua Wakati Wako Ujao)

Upadates Ipo Page Ya #95 Nguvu Za Asili Alizonazo Mwanadamu Kumshinda Mchawi


Upadates Ipo Page Ya 128 Nguvu Za Asili Alizonazo Mwanadamu Kumshinda Mchawi Sehemu Ya Pili Na Mwisho
Dunia hii ni kongwe kuliko wengi mnavyofikiri, kuna watu tumemuona Mungu hiyo moja pili kuna watu hawajamuona Mungu wala kumskia hivo wanaamini ahakuna Mungu,kabisa kabisa tena mnaweza kukosana kwa hilo.hao Mungu hajawapenda kama alivo mchukia Esau. na yeye hajifichi anasemaga tu nakuchukia, sikupendi waziwazi. siyo kama sheitwani yeye akikuchukia hakupnyeshi wazi wazi.
 
Dunia hii ni kongwe kuliko wengi mnavyofikiri, kuna watu tumemuona Mungu hiyo moja pili kuna watu hawajamuona Mungu wala kumskia hivo wanaamini ahakuna Mungu,kabisa kabisa tena mnaweza kukosana kwa hilo.hao Mungu hajawapenda kama alivo mchukia Esau. na yeye hajifichi anasemaga tu nakuchukia, sikupendi waziwazi. siyo kama sheitwani yeye akikuchukia hakupnyeshi wazi wazi.

Duh
Kwa iyo kama Mungu anamuumba mwanadam anamleta duniani alafu anampenda huyu na kumchukia mwingine huo si ubaguzi???
 
Nikweli ndugu usemalo
Ila Kumbuka Unaposoma History haina maana ukiwa kazini utafanya kai ya history
Kuna vitu tunaita ujuzi kuna vitu tunaita maarifa napia kuna cha ziada kinaitwa hitaji.
Vyote hivyo vinasababu hadi uweze kuvitambua na kuvizingatia, bila sababu huwezi kuvijua na kuvitambua ni lazima uwe na sababu yako ya msingi itakayokupelekea kujua.
Mfano Mmoja mzuri sana ni huu
-Kwanini Unajua Ubatizo umewagawa wakristo?
-Je Unaweza Kushika Sheria Ambazo Hazina Hukumu(Utawashangaa Wasabato Hapa)
-Je unajua yakuwa Biblia haithibitishi uwepo Wa Mungu?(Wanaoamini Mungu Yupo ndio wanawaamini biblia ila asiyeamini Mungu Yupo hata Biblia hawezi iamini)
-Je nikweli baraka unaweza zipata kwa kuibariki Israel?(Wakristo hapa wengi wanafeli kwakuwa wamekaririshwa neno ila hawajataka kujifunza na kulielewa neno)
Maswali machache hayo hapoo juu ukijiuliza utatambua yakuwa ni jambo limefichika ambalo hakuna mtu atakupa majibu sahihi usipoamua wewe kujifunza.

Kwahiyo mambo yaliofichika si kukupeleka shimoni ila yatakufanya ujitambue na kuzijua haki zako zaidi za msingi
 
Kudadeki nimegundua kuna elimu kubwa sana kuhusu dunia na haina usiri wowote kuweza kuifahamu ila kutokana na baadhi yetu tumepewa elimu ya kutupumbaza kiukweli elimu tuliyo pewa imeacha maswali mengi sana yenye utata mkubwa sana.

Ila nilicho gundua wale wote walioigundua huu usiri wa ulimwengu ulijificha wapo huru sana.


Kuna siku moja nilikua shamba na mzee wangu akaniambia kata vigongo tukapute embe ya kuuingia mboga

Tukaenda kuputa embe nilikata Vigongo v3 mzee alikua anataka Embe moja tu Muembe ulikua katika kichaka kikubwa

Nikaputa cha kwanza sikufanikiwa kudondosha

Nikaputa cha pili sikufanikiwa kikabaki kimoja na ndo cha mwisho

Nikatuliza akili huku nikiputa katika utulivu wa hali ya juuu huku nikimuomba Mungu wangu anisaidia kwanizamu kubwa kweli kweli nikafanikiwa kudondosha Maembe 2

Bila Mzee kujua kama nilimtaanguliza mungu kabla sijakimalizia kile kilichobaki kaniambia mshukuru Mungu maana yani icho cha mwisho ndo umefanikiwa kuangusha nikamjibu Dah kweli Mungu amenisaidia


Basi tukafunga safari na kurudi nyumbani


Nilicho gundua Mungu yupo na imani yangu thabiti IPO katika kuamini Mungu na mmoja hajazaa wala hajazaliwa na wala hanamshirika.

MSIMAMO WANGU- Siamini katika Dini yoyote. Naaaamimi katika Mungu mmoja

Nitatenda mambo mazuri yenye kumpendeza Mungu.












Sent using Nokia 7 Plus
 
Duh
Kwa iyo kama Mungu anamuumba mwanadam anamleta duniani alafu anampenda huyu na kumchukia mwingine huo si ubaguzi???
Kwa akili yako kama mwanadamu utasema Mungu ni mbaguzi, ujue kuna wengine hamjaumbwa na Mungu bali matokeo ya shetani mpaka leo.utasikia watu wengine wanasema wanafanya mapenzi ndotoni, wananyonyesha ndotoni.wanatembelea sehemu wasizozijua ndotoni nk. inawezekana kabisa kuna watu tuna ishi nao wametoka kuzimu, ndo wanahoji uhalali wa uwepo wake yaani ile hofu yake hawanayo, ni rahisi kuwajua hawa watu ila ni somo la siku nyingine.........
kama shetani alivo mtengenezaa Cain katika bustani ya Edeni, lakini pia Mungu alimlinda Cain na kizazi chake wakawa wanamuziki wazuri wenye mafanikio, pia napenda ujue mwanamke ni mama wa viumbe vyote, halisi na visivyo halisi, ila baadhi hamjijui, ndo tunawafungua akili. hata ivo mtu kama wewe umepewa nafasi ya kutenda vyema ili ukubaliwe na Mungu.ujue shetani baada ya uasi alitengwa,zaidi ya yote akafukuzwa mbinguni lakini bado anaongea na anafanya bidii ya maombi usiku na mchana ya kukushitaki wewe kwa Mungu.
 
Back
Top Bottom