The Real Hidden World

The Real Hidden World

Asante kwa mrejesho wako, Ukipata mda viweke hapa kwa faida ya wengine maana mimi sina soft copy za hivyo vitabu.
Pia naona leo nakutana na watu wachache miongoni mwao.
Ambao wamekutana na nondo hasa hicho kitabu na akakisoma akabakia the same.
Kweli Ni ajabu.

Ila katika yote vema ukajifunza haya Tunaishi kwa Imani Tu.
Iwe Muovu anaimani hata Mwokovu anaimani pia.
Hata yule asiyeamini uwepo wa Mungu naye ndiyo imani yake sambamba na mtu ambaye anaamini Uwepo wa Mungu.

KWa faida yako Na wengine Hata Biblia tu sio Uthibitisho Juu ya uwepo wa Mungu(Japo tunaishi kwa kukaririshwa kuwa Biblia yaweza Kuthibitisha Hayo)
Ndio Maana Kupinga hoja au kuiwekea ukinzani kwa jinsi unavyoelewa wewe sio jambo la kujitosheleza hata siku Moja.
Nikiwa nasoma kitabu kimoja kinaitwa How To Handle Difficult People Nilijifunza jambo moja kubwa na lamsingi jinsi ya kujiepusha na migogoro yakuwa mbishi.
Kwanza unapaswa binafsi usipinge Hoja(hata kama hoja hujaikubali maana unataka ujifunze na kuweka ukweli pasipo ubishi) baada ya hapo unapaswa kuondoa ule ukweli ulionao katika akili yako na kuuweka pembeni kwanza(Hii inakufanya jambo lile usilione kikwazo kwako)Kisha ingia katika hilo jambo jifunze kama geni Hii itakufanya ulijue kwa uhalisia wote pasipo kuwa na ukinzani wowote utajua vizuri wapi udhaifu wake upo na wapi ukweli wake upo.
Inakuwa ni kama mtoto Uliyemlea wewe mwenyewe binafsi kama hana tabia ya wizi hata akiiba utaamini ni baati mbaya tofauti na wale ambao hawajamlea.
Kisha sasa unarudia ile kauli yako na kuime-merge hapo sasa ndipo unafikia mwafaka juu ya hoja mbili zilizo za tofauti.

Kubishia jambo na kulipinga haina maana kusema linakuwa la uongo la Hasha
Ukweli ni Uongo Na Uongo Ni Ukweli Pia.
Ukweli Unakuwa Ukweli pale unapokuatana na watu wanaoamini ukweli huo,
Na uongo unakuwa uongo pale unapokutana na wale wasioujua kama ni ukweli.
Mfano kuna mtu anatoa ushahidi wa uongo ambao haukuwepo kabisa na unakubalika kuwa ni ukweli.
Na hauwezi kupotoshwa hata siku Moja.
Wewe ni Mkristo namimi ni Mkristo Tunaamini katika Yesu Kristo lakini wakati huohuo wengine hawaamini hata neno lake moja sababu ni kwamba ukweli waYesu Kisto Uligusa mahali ambapo hawauamini Ukweli(Wajazwa na lile wanalolijua wao kua ni kweli hawawezi kuongeza lingine)
Naweza ongea mengi sana Broo Ila acha niishie hapa.
Mkuu nimekusoma vizuri..naomba usichoke kutoa hizi nondo..
 
NItakuja Kutoa Somo Kwanini Mchawi Ni Vigumu Kuokoka
Napia Kuna Stage za Uchawi Na Aina Za Uchawi
Leo Namalizia Mada ya Iliyoko Ya Wachawi Kisha Nitaleta huo ufafanuzi juu ya wachawi.



Wakuuu Leo Tunaendelea Tena Na Mada yetu
Sawa nasubiria
 
Nianze kwa kusema nakumbuka nikiwa bado mdogo mdogo, nilikuwa na sifa moja kubwa sana mtaani kwetu ya ubishi.
Hata kama ulete fact za kiwango gani lakini niki-stickkatika msimamo wangu ni hapo hapo hamuwezi kunibandua hata mngekuwa mia.
Lakini kuna jambo moja aliligundua mzee mmoja siji kumsahau katika maisha yangu yote ningali bado mdogo kabisa miaka 8.
Aliniita na kuniambia
""Nikiamua kuwa na maarifa naweza kuwa nayo, nakuambia hivi si kwamba nimekuona unamaarifa bali nimegundua unaweza kujaza maarifa ukitaka, sasa nakupa kazi jifunze ulimwengu uliofichika ulivyo hautapata nafasi ya kubishana na wengine kamwe'''
Mzee nilimuelewa japo kwa ufupi sana, labda kutokana na umri wangu ulivyokuwa na kuambiwa jambo lililokuwa juu ya uwezo wa frikra zangu.
Nikiwa na miaka 14 ndipo mzee aliweza kunipa kitabu kilichokuwa na Tittle Hii
"Comfort That Kills" Nikitabu chenye page 36 tu lakini ndicho kikabadili ukurasa wangu wa maisha na kunipa hamu zaidi ya kuujua ulimwengu uliofichika.
Nilikisoma kwa kufanya mirejeo mingi sana katika kamusi ya kufasiri maneno ya Kiingereza kwenda kiswahili,
kwanza kilikuwa na maneno mengi ya kiingereza cha zamani sana, kilinipa shida kidogo lakini niliweza kukielewa na kufunguliwa ukurasa mpya wa kusoma Maandishi.
Si kwamba sikuwa msomaji toka mwanzo ila nikwamba usomaji wangu uliegemea sana katika kusoma hadithi za nadharia zaidi zilizoandikwa na waandishi mbalimbali mahiri.
Sasa hapo ndipo nikaaznza kuufukunyua ulimwengu uliofichika kwa fujo zote.
Sio katika Upande wa Dini au Historia tu, bali niliweza kuyajua mabo mengi sanakwa muda mfupi.
Na kadri nilivyozidi kusoma ndivyo nilivyozidi kujua na kutambua ya kuwa katika asilimia 100% huenda nimeijaza asilimia 0.001%(Kwa wasomaji wavitabu wananielewa vizuri hapa maana kadri unavyosoma ndivyo unaona hauna kitu na unahitaji kujaza vitu)

Nilikuwa napitia Thread Za mtu mmoja humu(jina kapuni)
Niligundua jambo moja wengi wanaompinga katika thread zake ni wale wanaoangalia muvi na video za youtube juu ya uhalisia wa ulimwengu tunaoishi, lakini hawezi kuwa na mrejesho hata mmoja juu ya maandishi aliyoyasoma.
Huyu jamaa ameandika vitu vingi ambavyo huenda sikujua kama naweza kukutana na mtu kama huyo hapa, lakini ndipo nikajua kumbe JF ina watu wengi sana wa kila namna (Viva JF)
Sijaja Hapa kuueweka hadharani ulimwengu uliofichika ila ukihitaji kuujua unajulikana kabisa, tena kwa urahisi sana.

Labda unaweza ukakosa Mzii mahala pa kuanzia lakini nakupa kidogo jambo moja.
Jaribu kujifunza mambo kama haya hapa.

Kwa watu wa Imani hasa wakristo na waochimba masuala ya tulikotoka,kwanini iko hivi,kwanini iko vile,imekuwaje,ilikuwaje,jaribu kupitia mambo haya.
-Ni vitabu gani vilimeondolewa katika Biblia
Unaisoma Biblia Leo lakini inavitabu zaidi ya vitano havijawekwa humo
Tafuta kwanini havimo, vinafundisha nini, nk

-Ni nani alikuwa mmiliki wa kwanza wa America(Usiniambie wahindi wekundu nabaadhi ya maneno yaliyopo kajifunze ulimwengu uliofichika)

Naomba niishie hapo kwa Leo, lakini nikipata mda mzuri na nafasi nitaweza kuleta hoja mbalimbali juu ya ulimwengu uliofichika kwa kadiri ya jinsi nitakavyokuwa na muda.


Updates Ipo Page #30 Kitabu Chenye Utata (Kina Uwezo Wa Kujua Wakati Wako Ujao)

Upadates Ipo Page Ya #95 Nguvu Za Asili Alizonazo Mwanadamu Kumshinda Mchawi
Wewe ni muuza Vitabu tu huna lolote jipya..!
 
Nguvu Za Asili Alizonazo Mwanadamu Kumshinda Mchawi SEHEMU YA PILI NA MWISHO

Kwanza nianze na kuwapa pole ya kukaa muda mrefu pasipo kuleta mada yoyote, shuguli za kimaisha na kupambana kupata riziki vinanifanya nisiwe hewani mda mrefu,
Tuwekane sawa, Mimi siuzi vitabu kama jamaa Mmoja alivyosema wala siuzi maarifa kwamba nitasema mlipie sijui, hapana natoa kwa ridhaa yangu binafsi ndio maana nakuja kupost nikipata mda wala siendeshwi na mtu ila najitahidi sana tuwe tunapata hoja za karibu karibu ndugu zangu.
Mengi Nimeyajua kwa usomaji wavitabu tu, nasasa nitakuja na mada hizi Mbili baada ya leo kukamilisha hii
1.Kwanini Ni vigumu Kwa Mchawi Kuokoka Au Kuacha Uchawi?
Tutajua viwango vwa wachawi,athari zauchawi,tutajua habari za ushirikina, kitu gani kina mpa nguvu mchawi na udhaifu walionao na jinsi wanavyopata nguvu n.k
2.nguvu ya Uponyaj iliyoko Ndani ya Biblia Ambayo Watumishi Wengi Hata Hawawafundishi watu.
Tutajua namna yakujiongezea mvuto wajambo(kama bahati vile)namna a kupata kazi,kulipiza kisasi,umevamiwa na vibaka au majambazi wakuache bila kukudhuru wala wasichukue chochote,namna yakuweka baraka katika biashara,mtu kushinda kesi, kutolewa gerezani hata kama kafungwa kifungo cha maisha, n.k ila katika haya nitatoa dondoo tu, maana habari hizi wakizijua wenye roho mbaya wataweza kuzitumia vibaya(Kumbuka Mungu Akasema Na Tumuumbe Mwanadamu Kwa Mfano Wetu) Ukijua nini maana ya mfano utaelewa namaanisha nini na utaelewa mfano huwa sawa na swali husika mfano hufungua uelewa. Nitaongea Mengi Mda wa Mada Ukifika.

Mada iliyopita nilieleza namna ambavyo unawea ukamuona mchawi akiwa ameingia ndani mwako paipo hata kutumia dawa yoyote bali ni kwa uweza wa asili ambao Mungu ameweza kumjalia mwanadamu japo si wote waojua jambo hili pia unaweza ukamuua mchawi bila hata kuwa wewe mchawi ukisha muona anapokuwa kaingia ndani kwako,
Inakuwa hivi ukimwambia tokea mlangoni anakufa,ukimbonda na kitu cha aina yoyote hata punje ya harage au mchanga yaani anakufa tena anakufa kabisaaaaa.
Kumbuka hapo wewe sio mshirikina wala sio mchawi wala haujapewa dawa yoyote ni ule ujuzi wa asili tu Mungu kamjaalia mwanadamu.
Sasa turudi kumuonamchawi aliyeko nje, kuna aina nyingi za dawa watu wanasema ukitumia unaweza kumuona mchawi nasikia ukijipaka mate ya mbwa(sina hakika wala sijawahi jaribu) saa twende katika jambo ambalo unatumia ukawaida wakibinaadamu.
Kwanza lazima ujue yakuwa mchawi anatembea kwamiguu katika baadhi ya shuguli zao anaweza kutoka magomeni hadi stand ubungo au kimara kwa miguu,Njia zao huonekana kwa macho ya kawaida ila hutegema sana aina na aina za maeneo.
Mfano makaburni hapa najua umewahi jionea ukienda makaburini achana na ya hapa mjini kule vijijini ambako watu huzikwa mara moja moja sana maana yake watu hawaendi makaburini mara kwa mara ukifika unakutana na vinjia fulani hivi ambavyo kama vimeacha kutumiwa na watu yaani vinaanza kufutika ila kila ukipita makaburini au mkienda kuzika vinji ahivyo vipo tu.
Wala haviondoki wala kufutika, sasa hivi ndio vinjia mojawapo vywa wachawi vinaonekana kwa macho ya kawida na hayo ndio maeneo rahisi unaweza kuona, najua sasa unasema ahaaaaa kimoyo moyo umekumbuka huko makaburini.
Sasa mbali na hapo pia huwa tunapishana nao njiani kila siku toka utotoni hadi tunakuwa mfano ushawahi kutembea njiani mpo na wenzako afu mlikuwa mejieneza njia nzima lakini gafla mnajikuta wote mpo upande mmoja?
Au unatembea peke yako pembeni ya barabara afu gafla unenda upande wapili hauchukui hata sekunde 30 unarudi tena upande wako wa mwanzo?
Au unatembea usiku sehemu ulipo sio joto wala hakuna upepo ila gafla unapishana na joto la gafla tena zito likiambatana na ka utulivu fulani kama sekunde 4-6 hivi kisha kanapotea?
Kama ulishawahi kukutana na mazingira hayo basi jua ulipishana na wachawi ndugu ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha.
yaaani wale wasioonekana kirahisi kwa macho ya nyama umepishana nao(japo unaweza kuwaona ukiwajulia) Sasa miminakuleta kwa hawa wa usiku hasa unapokuwa unapishana na kijoto hicho, nikiwa mdogo iliwahi ambiwa nabibi ikitokea hivyo umepishana na mchawi,
Mimi nikajua stori za kufnunda watoto tusifanye upumbavu fulani lakini kunasiku nilikutana na kitabu kimoja hivi (Sitokitaja Jina Kwa sababu zangu binafsi) Ila nilikipata nikiwa nasoma Shule ya sekondari IMae Ipo Mkoani Iringa Shule ile hupokea sana vitabu vya misaada toka nje ambavyo ni ufahamu wa ziada tu vinakuwemo vitabu mbalimbali sana na hapo nilivifaidi mno kwa ujuzi na maarifa ya aina mbalimbali hasa.
Wanavitabu vingi sana ajabu mnoo naikumbuka sana ile shule ina elimu kubwa japo nakumbuka kma watu watatu tu ndio tulijua hilo.
Sasa kinaeleza yakuwa mchawi akiusana na mtu akiwa anatembea basi yeye hudhurika na mtu hudhurika zaidi kwahiyo hutumia mbinu na kanuni zakukufanya wewe usigusane nae.
Sasa hi hutokea sana katika vinjia vidogo vigodo au watu mkiwa wengi kwamba akiwakusanya upande mmoja mtamjulia au kanjia kadogo hawezi kukufanya umpishe.
Sasa anachokifanya anajirefusha miguu anatengeneza kitu kama goli hivi (tobo) unapita katikati ya miguu yake.
Sasa ukipita hapo ndio unakumbana na hilo joto sasa mkiwa wenginlinadumu kidogo hata kama sekunde 30-45 hapo sasa ndio mnapopita katikati ya tobo lake au katikati yamiguu yake nio unahisi joto na upepo ule wa utuluvu.
Nini Kinatokea Hapo dawa yake haiwezi kumficha tena ukipita katikati ya miguu yake kinachotkea mkishapita nilazima ageuke kisha anasonya, akifanya hivyo anarudi ukawaida wake na hamuwezi kumuona tena.
Sasa ukimuwahi kabla hajasonya he he he heeeeeeeeeeeeeeeeeee, ushamuona Ila huyu aakuwa na uwezo wakukimbia na kujigeuza katika umbile lingine ila hawezi kukudhuru wala kuyeyuka, anaweza kukimbia akajigeuza mti au paka au mbwa ili mradi msijue kaenda wapi ila anakuwa yupo hapo hapo au ndio anaondoka mdogomdogo kama mbwa au paka au chochote kile anachojua yeye.
Sasa mimi nilikuwa naijua hiyo siri mda sana sijawahi kuprove tu siku nakumbuka tumetoka mahali kwenye semina mida ya saa mbili usku tulikuwa watu kama 12 hivi sasa si unajua vinjia vya kijijini?
Basi nilipoona ile hali mie hata sikujiuliza ikamwambia mwenzangu unaitwa nyuma si akageuka?
WEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE! hizo kelele zake sio za nchi hiii nakumbia mie hata sikugeuka nikaangalia tu njia yanyumbani ni ipi nakukaza mbio nisijibamize katika miti ya kokoa(zinalimwa sana kwetu)
Kuja kukutana ni asubuhi tulivyotawanyika hakuna ajuaye, sasa maelezo ya watu walioona walikuwa wanne yaani wansema wameona jini refu hatali afu limetanua miguu yake ila tumeshindwa kujua sura uhalisia wake.................................
Hapo Ndio Nilijua Nikweeli.

Kwakweli huu ndo ulimwengu uliofichika hakuna aujuae wachache wanaujua nitajitahidi kuwaletea mapema hizo mada hapo mbili juu.

Mimi Sio Mchawi Wala Sio Mshirikina Mmi Nimkristo Ninaye Mwamini Yesu Krsito Niliyekombolewa Na Kuoshwa Kwa damu Ya Yesu Kristo Na Ninamwamini Si kwasabau Nasoma Biblia Hapana Nikwasababu Ya Jinsi Alivyojifunua Katika Maisha Yangu Na Kuonekana.
Sipo Kumthibitishia Mtu Ila ndio Imani Na Yangu.
Namaarifa Amenijaalia hayo
Msije niona Mie Ni Mtu Mzee Sana wa zamani Hapana Nsio Kwaaanza April Natimiza Miaka 24, Nimekuwaje Hivi?
NIkutokana ana Msingi Wa Wazazi Wangu Na Jamii Iliyokuwa Imenizunguka Na Maisha Ambayo Nimeyapitia Yamenifanya Niwe Hivi Leo.
Pia Mimi ni Mfundishaji Tu Wa Habari Njema Za Wokovu Sio Mhubiri Mie Ni Mwalimu Tu.
Najua Ni Karama tu Mungu Aliyonijaalia Kuwa nayo, Hata nijistaajabia Wakati Mwingine, Kunamda Nilikuwa Najiona Wakawaida Kawaida, Ila Namshukuru Mungu Kwa Hapa Nilipo Na NItajitahidi Kulea Yote Niyajuayo.

Asantheni Sana Wana Jamii Wenzangu
Hot Thread Zile Pale Juu Nazita Kwenu Soon
Mengine Nitakayoleta Baadaye.
1.Namna Ya Kuikuza Imani.
Mfano zamani mtu anasali kwa mti au kinyago, au kwa mamba, au katika mto ana mambo yanakuwa inawezekanaje ?
2.Proof Ya Kusema Mungu Yupo Pasipo Kutumia Biblia.
Wakristo Wngi Ukiwauliza Swali thibitisha Kwamba Mungu Yupo Ha ha ha h Kimbembe Anaanza kupekua BIblia na kukuambia analia vyote viijileta vyenyewe? Na watumishi hawafundishi haya nitaileta mada.
3.Je Israeli Niani?Katokea Wapi?Anafanya Nini?Yuko Wapi?Umuhimu Wake?nk
Yaani Hapa Ndio nimeona WEngi Wamechemka sana hata Wahubiri Na waumini wao wanaanza Kutishana Mizigo Ya Kuiombea Israel Hata Hawaeli Israel ni Nani Hata Hawaelewi Israel+Yesu=? hawajui baraka Inapatikanaje Yaani Wanaendeshwa Tu Na Hawataki Kujifunza.
Mimi NItaleta Mada Inayofundisha Namna Dunia Itakakavyoisha Na mtiririko Wa Matukio ya Kiama Kwa Uthibitisho Wa Uhalisia Nanyi Mtaona NI Kitu Gani Kimefichika Mda Mrefu Watu Hawakijui Hapo ndipo Mtashangaa Biblia ile Ile Lakini Maneno Kila Siku Ni Mapya

Nisiwachoshe Sana Mtachagua Mada Ipi Nianze Nayo Jamani
 
NA MUNGU ALIWAWEKA WATU ILI WAFUNDISHANE NA KUELEKEZANA,ILA WAYACHUKUE YALIYO MEMA TU NDIO MAANA MACHO NA MASIKIO HAYANA PASSWORD YAPO WAZI TU.
Asanthe Kaka Amesahau Hata Suleiman Pia Alikuwa Mtu Wa Mungu lakini kuna wakati alichagua njia zisizo sahihi akautumia ujana wake wote kwa anasa akaja kuamka uzeeni.
Umemjibu Vyema Kwakweli
 
Nguvu Za Asili Alizonazo Mwanadamu Kumshinda Mchawi SEHEMU YA PILI NA MWISHO


Tutajua namna yakujiongezea mvuto wajambo(kama bahati vile)namna a kupata kazi,kulipiza kisasi,umevamiwa na vibaka au majambazi wakuache bila kukudhuru wala wasichukue chochote,namna yakuweka baraka katika biashara,mtu kushinda kesi, kutolewa gerezani hata kama kafungwa kifungo cha maisha, n.k ila katika haya nitatoa dondoo tu, maana habari hizi wakizijua wenye roho mbaya wataweza kuzitumia vibaya(Kumbuka Mungu Akasema Na Tumuumbe Mwanadamu Kwa Mfano Wetu) Ukijua nini maana ya mfano utaelewa namaanisha nini na utaelewa mfano huwa sawa na swali husika mfano hufungua uelewa. Nitaongea Mengi Mda wa Mada Ukifika
Kwanza ni kupongeze kwa kazi nzuri unayofanya ya kutuapatia elimu hii bure kabisa, pili naomba utupe hiyo elimu niliyo quote maana ni muhimu sana ili watu waache kwenda kwa waganga wa kienyeji kupata utatuzi wa matatizo yao.
Ubarikiwe sana mkuu.
 
Duuu hapo kwenye hako kajoto unageuka nyuma? Au sijaelewa? Maana Maelezo mengi lkn sijapata real concept
Ukisha lihisi tu hilo joto unageuka nyuma maana yake kama unatembea unaenda mbele angalia uliko toka
 
Kwanza ni kupongeze kwa kazi nzuri unayofanya ya kutuapatia elimu hii bure kabisa, pili naomba utupe hiyo elimu niliyo quote maana ni muhimu sana ili watu waache kwenda kwa waganga wa kienyeji kupata utatuzi wa matatizo yao.
Ubarikiwe sana mkuu.

Sawa Mkuu Mimi sijagusia katika upana wote bali nimeongelea baadhi tu ya uwezo mwanadamu aliojaaliwa kuwa nao
 
Sawa Mkuu Mimi sijagusia katika upana wote bali nimeongelea baadhi tu ya uwezo mwanadamu aliojaaliwa kuwa nao
Sawa mkuu lakini uliahidi utazungumzia hizo nukta kwenye post zinazokuja au nimekuelewa vibaya?
 
Mie nilianza kusoma vitabu vya spiritual na kusoma hadithi za busara ila ni spiritual na mara nyingi sina limiti katika iman yangu na usomaji kiasi flani kuna lock huwa nazifungua kwenye ubongo wangu kupitia mafundisho hayo. Kuna jamaa mmoja anasema siku ukiujua ukomo wako utaenda zaidi ya ukomo wako.
 
Mie nilianza kusoma vitabu vya spiritual na kusoma hadithi za busara ila ni spiritual na mara nyingi sina limiti katika iman yangu na usomaji kiasi flani kuna lock huwa nazifungua kwenye ubongo wangu kupitia mafundisho hayo. Kuna jamaa mmoja anasema siku ukiujua ukomo wako utaenda zaidi ya ukomo wako.

Wisely Broo
Niukweli Halisia
 
Back
Top Bottom