How?In the future your advised to prepare yourself well in advance otherwise do not post anything!
Be ready now naendeleza naandika hapaMbn huendelezi somo toka majuzi watu tunachungulia tunaona kimya why?!
[HASHTAG]#mwendelezo[/HASHTAG] The Real Hidden WorldHabari Zenu Ndugu?
Kitabu Chenye Utata (Kina Uwezo Wa Kujua Wakati Wako Ujao)
Naamini kila mtu ameweza Kusherekea Vizuri Na tunajiandaa kupokea sherehe zingine za kuukaribisha mwaka mpya Kwa amani kabisa.
Kabla sijaanza kuweze kueleea hiki kitabu cha leo naomba nianze kwa kusema kuna kitu kimoja ni hatari sana katika maisha ya mwanadamu endapo kikiweza kuamshwa.
Hiki kitu kinaitwa Jicho La tatu(Third Eye) kazi ya hili ni kwamba unaweza kuona mambo ambayo hayawezi kuonekana kwa macho ya kawaida(baadhi ya wahenga husema jicho la kisogoni)
Mara nyingi unaweza ukakutana na watu ambao wao ni wanajimu/mtabiri/waganga/manabii(hasa false prophet) na wengine wengi sana.
naweza ukaiba kisha ukaumbuliwa ukapewa dili nzima ulivyoicheza kama ulikuwa unaangaliwa vile na CCTV.
Lakini haina maana kuwa kila mwenye uwezo huo anakuwa anafanyia kazi hilo jicho la tatu la hasha Bali ni kwamba wengine huwa wanatumia nguvu fulani yaweza kuwa ya Mungu au ya kishetani.
Ndio maana waweza kuta mtu anamapepo/mashetani akipandisha anamuongelea mtu fulani mamabo ambayo yeye mwenyewe hakuwepo na inakuwa ni sahihi.
Au wengine ni watu wanaotumiwa na Mungu kwahiyo Mungu anawawezesha kuweza kujua jambo ambalo limefichika.
Sasa uhalisia wa jicho la tatu ni kwamba unafunguliwa mlango wako wewe mwenyewe moja kwa moja wa kuweza kufanya hivyo(Kila mtu anauwezo huo ila ni lazima ile nguvu iweze kuamshwa""Activation"")
Hii ni ile tunaita nguvu ya asili(Super Natural Power) sasa ubaya wake ni huu hii kitu ikifunguliwa haiwezi ikafungwa kamwe hata ukiokoka ni kwamba haiwezi kufungwa kamwe.
Ndio maana ni vigumu sana kwa mchawi kuacha uchawi sababu kuna milango inakuwa imefunguliwa ambayo ni vigumu kufungwa.(Nitaleta somo kwanini mchawi ni vigumu kuacha uchawi hata akiokoka wasomaji wa Biblia wanaelewa fika hili)
Nimeanza kwa utangulizi huu kwa ufupi ili tuweze kuwa sawa juu ya jambo hili ninalokwenda kulieleza hapa usije ukatamani sana kujua mambo yako ya wakati ujao kunamadhara makubwa sana(Omba Mungu akujulishe ila usiforce wewe binafsi kujua)
Kuna mambo mengi sana ya kujifunza ila acha tuanze kidogo kidogo.
Wakati wa zamani miaka ya 1769 Alizaliwa jamaa mmoja Aliyekuwa ni mpiganaji mahili sana huyu jamaa aliitwa NAPOLEON BONAPARTE(unaweza uka-google kumjua zaidi)Alizaliwa nchini Ufaransa japo waazi wake walikua ni watu wa kutoka italia na asili yake inabakia kuwa huko.
Katika mojawapo ya vita ambayo aliweza kushindwa Ilikuwa ni katika mji wa Leipzip(huko ujerumani) ambapo walicha vitu vyao vingi sana huko na mojawapo ya kitu kilichokuwa kimeachwa ilikuwa ni "The Book Of Fate" na hiki ndicho kilikuwa kikimilikiwa na huyu jamaa hata ikapelekea kikaitwa Napoleon Book/Napoleon The Book Of Fate.
Kwa uasili hiki kitabu kilikuwa kinamilikiwa na watu fulani ugirikiambao walikua wakiabudu miungu fulani (Search google oracle in Greece utapata kuelewa mengi sana juu ya watu hawa)sasa hiki kitabu walikuwa wakikitumia katika kutatulia matatizo mbalimbali yaliyokuwa yanawakumba watu na Kilikuwa na nakala si zaidi ya tano japo mpaka sasa kumeweza kuwepo kwa nakili nyingi sana katika lugha tofauti tofauti duniani.
Kipindi Napoleon anashindwa vita ndipo kilipatikana hiki kitabu japo kuna uvumi pia unaonyesha kilianza kupatikana miaka kumi kabla ya hapo.
Nimeanza na Napoleon Bonaparte ili tujue kwanini kiliitwa Napoleon maana aliweza kukitumia kitabu hiki kushinda vita kila mara na vita ya mwisho anapigwa hakuwahi kusimama tena.(Uki-google utajua Mengi)
Sasa twende kwenye pointi
Kwa hapa tanzania naamini zipo nakala nyingi sana japo nikwamba kila aliye na hizi nakala anakuwa ni mtu wa kujificha nayo sana.
Nikiwa na miaka 16 nakumbuka baba aliwahi nipa simulizi ya ndugu yetu mmoja aliyeweza kumsaidia jirani yake kujua nini hatima ya watoto wake waliokuwa wanaumwa.
Alisumbuka sana kuwatibia hata ikampekelekea kumdhorotesha sana kiuchumi, Siku moja huyu ndugu angu akamfuta jirani yake akimwambia anaweza kumsaidia kutambua hatma ya watoto wake.
Jirani alikubali japo hakujua nini ataweza kuambiwa, huyu ndugu alichukua kitabu chake (Napoleon Book) Akafanya hesabu zake kama kilivyokuwa kinamuongoza huku akimuuliza maswali yule jirani.
Mwisho wake akaambiwa huyu mtoto aliye mahututi atakufa hataweza kupona, ilichukua siku moja tu maneno yale yakatimia.
Baada ya mda kidogo ikatokea mtoto mwingine kazidiwa jirani kabla ya kwenda hospital japo hakuwa na uhakika kama ataweza kupata msaada maana hawakuweza kutatua tatizo toka mwanzo, Ikabidi amuulize ena ""Kitabu chako kinasemaje juu ya huyu tena?"
Baada ya mahesabu ya mda kidogo ndipo akaambiwa na huyu yatampata kama yule wa mwanzo, wakiwa njiani akaaga dunia pia,
sasa huyu jirani akabeba panga na kumfuta huyu jamaa akisema ndiye mchawi wake juu ya wanae.
Kwa miaka ile kashfa hii ilikuwa ni mbaya sana maana ingeweza hata kumpelekea mtu kifo, akaamua kuondka na kuhamia eneo jingine.
Sasa nilivutiwa sana juu yakukijua hiki kitabu nikaamua kuomba likizo kwa baba nikamsalimie huyu ndugu yetu(Mimi namwita Babu)
Kwake anamaktaba kubwa sana ya ndani nikiwa huko nilipakanyua karibu maktaba nzima sikuweza kupata hiki kitabu(Lakini kumbe yeye alisha nishitkia akiniona kuna kitu cha ziada nakitafuta)
Hakutaka kuniamsha akaniacha ajue nini hatma yangu kila nikienda maktaba yeye anakaa mahali ambapo yeye angeweza kuniona pasipo mimi kujua.
Wiki iliisha nikiwa nimekosa tumaini na tayari nikaanza kukata tamaa lakini niliogopa kuuliza sababu ya kutokana na maudhui ya kitabu husika.
Siku nikaamua kunyata na kuingia chumbani kwake kupekua.
NIlipekua sana tena sana pasipo kukiona lakini kumbe babu yupo bafuni (Chumba chake self) akiniona mda wote nafanya pilika pilika zangu.
kama baada ya lisaa hivi nikaweza kuvuta sanduku moja la mboa lilikua zito sana kwakweli likiwa limejaa vitabu vingi mno na hapo ndipo nikawa nimevutika na sanduku husika.
Nakumbuka nilikaa juu ya kitanda chake huku nikiwa naangaliana na mlango wa bafu jambo lililofanya anione vema sana nini nilikuwanafanya.
Nilitoa kitabu kimoja baada a kingine na kila kitabu nikikipitiaContent zake
Hamadi macho yalitua moja kwa mojaa juu ya kitabu chenye ukubwa kama tenzi za rohoni(wakristo wanazijua) kikiwa na ujazo wa kadri, niliganda kidogo bila kuelewa nini nafanya huku jasho zikinichuruzika,
Gafla babu akakohoa Sikushitushwa wala sikuogopa akaja hadi kitandani nilipo akaniambia umeisha kiona najua utanisumbua sana na sasa nakichoma moto mbele yako usije nisumbua tena,wakati wote huo sikuongea akakibeba na kwenda kukitia moto.
Akarudi kisha ndipo nikapata kujua uhalisia wa hicho kitabu ninini kwa masimulizi yake.
Nikitabu chenye mwongozo wa nyota na namba Na herufi
KInamaelezo fulani namna ya kukitumia
mfano.
Unaingia katika mtihani unataka kujua utafeli au utafaulu kina kupa majibu kama utafeli au unafaulu
Kama unafeli kuna kanuni tena namna ya kufanya ufaulu kinakupa majibu pia
Lakini nikwamba mwongozo wa hizo namba zinatoa jibu la namba ambalo ndilo ukipeleka katika kitabu tena utajua ile namba inamaana gani.
Kuna maswali hua najiulia mpaka kesho nakosa majibu ni nguvu gani ipo katika hizo namba?
Ni Mambo gani yanasababisha haswa iwe vile?
Sina majibu kabisa, hata kama unakesi unataka kujua ufanye nini ili ushinde kinakupa majibu kama huwezi kushinda kinakupa majibu.
Lakini jambo la ajabu nikuwa ni mwongozo wa namba tu.
Lakini pia ajabu yake kubwa sana ni Hii
Kuna Majira hakipaswi kusomwa kabisa, Na kila mwezi una siku kadhaa hakipaswi kusomwa kabisa
Sasa hapo ndipo pia nashindwa uelewa kwanini kinakuwa hivi.
Lakini ni Mengi sana unaweza ukayajua ukihitaji japo katika mitandao kumejaa nakala nyingi a uongo zinazouzwa.
Nami Naamini Hakiwezi uzwa kwa namna kama hiyo kutokana na jinsi kilivyo.
Huyu babu yangu mimi alikuwa ni Rastafalian kasafiri sana nci za wenzetu huko, na ndiko aiwea kukipata hiki kitabu japo aliniambia alikijua akiwa norway ila alikuja kupewa bure kabisa na mzee mmoja kutoka Egypt.
Kumbuka Sio Lazima Kuamini Mambo kama haya japo wale wanaojua ndio huwa wanajua.
Pia sipo hapa kufanya wewe uamini ninachozungumza (Fukua,Fukua,Tafuta mirejeo Utajua nawe)
Pia Mimi ni Mkristo ndio maana natumia baadhi ya maeneo ukristo maana ndio niujuao japo mada hizi hazihusiani na mambo ya dini.
Kumbuka Ulimwengu Uliofichika ni sawa na Propaganda tu Mara nyingi ukweli unakuwa hauonekani ila uhalisia upo wazi kabisa.
Nasisitia tena Sio Lazima wala silazimishi mtu kufuata jambo kama hili
Ila wanaohitaji kujua karibuni sana kujifunza.
Next Mada Itakuwa Kwanini Mchawi Ni Vigumu kuacha Uchawi hata akiokoka?
Pamoja broo I See you nilikuwa off kidogo am back Next chapter yaweza kuendelea kwa leoNiko pamoja nawe kaka...
Cool ThanksSubscribed...
Shukrani Mkuunakufuatilia mkuu shusha mondo hizo...
kama nakihitaji hicho kitabu cha napoleon .nitakipataje mkuu
maana Google umesema kuna wajanja wajanja wengi unaweza ukauziwa fake
okay...nitakufuata PmShukrani Mkuu
ka uhalisia mimi nilibahatika tu kukiona kwa macho hata sikuweza kufungua hata ukurasa mmoja kuweza kukisoma
Unaweza ukakipata ila sijajua connection zako zilivyo na watu mbalimbali.
Pia mtu anaweza akawa anacho ila akakana kama anacho maana kuna baadhi ya mambo wengi hawapendi kuweka hadharani haswa kwasababu binafsi na sana zikiwa zinahusiana na mada kama hizi
Kwauhalisia nilikuwa nasoma sana vitabu ila ilikuwa ni vitabu vya hadith na masimulizi sana kidogo nilikuwa nagusia vile vya documentary hii ni kutokana na kuwa baba yangu ni mmsomaji mzuri sana wa vitabu.Asante kwa makala zako!nikupongeze kwa kupenda kusoma vitabu ili kuongeza maarifa.ningependa kujua tofauti uliyopata (uliyokuwa nayo)na baada ya kusoma vitabu.je unadhani ubishi wako ndo ulimshawishi huyo mzee Akuambie utafute maarifa?pia naomba hardcopy ya moja ya kitabu chako nipitie pengine inaweza kuwa nuru kwangu kuujua ulimwengu uliofichika