The Real Hidden World

The Real Hidden World

1. Kwanza kabisa unahitaji kuisoma tena post yangu hapo juu maana ni wazi tayari uko katika realm hiyo ya kinguvu za giza unayolazimisha iwe legitimate ingawa haiwezi kuwa hivyo kamwe.
2. Mwanadamu ameumbwa na Mungu lakini kwa uasi na kushawishiwa na bwana giza akatafuta hayo unayoyaita marital ya ziada etc. hakubaki kama alivyo. He dies. There was a chance for him to live forever. Kufa hakukuumbwa ndani ya mwanadamu mpaka alipochagua kufa akitumaini kupata maarifa ya ziada. Namna pekee ambayo mwanadamu angeweza kukiepuka kifo ilikuwa ni kuamini kuwa asingekufa kwa kumtii Mungu na uhai wa milele ungehakikishwa pale. Kutafuta kwake maarifa unakotuconvince hapa kuwa kutatufanya kuwa bora zaidi ndiko kulikoanzisha ujinga wake unaodumu mpaka Leo. Hakumwamini Mungu tu!
3. Hakuhitaji maarifa mengine yoyote zaidi ya kuamini kuwa Mungu angeshughulikia mambo mengine yote. Mungu bado anasisitiza hayo hayo leo kuwa watu wamwamini yeye. Hakuna haja ya kutafuta the third eye, machale au sijui giza gani. Yeye ndie machale, yeye ndie third and fourth and nth eye kama umepitia maths.
4. Uchawi na kuzaliwa kwenye uchawi ni Kamba na minyororo inayomfunga mtu kwa utashi wake. Anaweza kuvikata ingawa ni kwa gharama kubwa ya kimwili (ambao unakufa anyway). Sikia kwa nguvu zinazotoka kwa Mungu na utashi wa muhusika uchawi unatoka.
5. Mwanadamu ahitaji kujua Siri zaidi ya ukweli kuwa yeye ni mnyonge na anaweza kusukumwa pepo mbalimbali na kuwa Mungu muumbaji anao uwezo wote wa kumpitisha katika pepo hizo salama.
6. Soma tena post yangu huku ukiitafakari.
Yap nikweli
Wala hakuna anayelazimisha hapa kwamba nilazima hiki kitu kifuatwe
Hata katika Mungu Kuna Mhubiri(japo Kila mtu anaweza kuwa mhubiri)Kuna Mwombaji(Japo kila mtu anapaswa kuwa mwombaji)Kuna Mwalimu(Japo kila mtu anapaswa kuwa mfundishaji)
Unapokuwa Unakutana Na Mfundishaji jinsi aakavyoizungumzia Biblia Ni Tofauti kabisa na Mhubiri.
Napia Kwa msikilizaji/Mfundishwaji sio lazima afuate kile ambacho Anafundishwa na kuhubiriwa
Anapaswa kuchuja na kutafakari kwa umakini zaidi.
Sasa Mungu ndiye anaweza kukujaalia hayo maarifa ya utambuzi lipi jambo baya au lipi jambo zuri.
Lakini hayo maarifa Mungu hayaweki kwa ku-force akilini mwako anaweka kwasababu wewe umeonyesha unayahitaji(Umeyatafuta Kwakwe)
Ndio maana kuna wahubiri wewe mwenyewe kutokana na jinsi anavyohubiri unajua na kutambua hapa Hakuna Mungu wakweli Na wakati huohuo anakuwa anawaumini ambao hawatambui kweli unayoijua wewe.
Kwahiyo Ukweli unapaswa kuwekwa hadharani atakayeuchukua sawa atakaye uacha sawa pia.
Ukisoma Vizuri kila Mda yangu hapo juu Na vitu nakupa tahadhari kabisa kwamba hapa unaweza kupotea ama hapa unaweza kuokoka.
Kuna Jambo La Ziada Kila Mtu anapaswa kulijua japo sio lazima kulijua.
Nimekuelewa vizuri sana pale juu maoni yangu ilikuwa ni Nyongeza tu wala sijapingana nawewe
 
Mfano Mmoja Mzuri ni huu Hapa.
Nilikuwa napata shida sana kujua Maswali Haya
Israel Ananafasi gani katika Maisha Yangu a Ukristo?
Baraka na Ukombozi kupitia israel unahusianaje na kupitia Yesu?
Je Nikweli Israel bado yupo Utumwani hadi Sasa?
Kama ndio hao waliopo Je wanaenda sawa na Maandiko?
Hayo ni baadhi ya maswali nilikuwa najiuliza sana, kila nikiuliza naumizwa kichwa tu, Wala hakuna aliyeweza kunipa majibu yakutuliza moyo wangu.
Ila nilipoamua kuchimbua mwenyewe ndipo nikafanikiwa kujua mambo ambayo kwa uhalisia hakuna mwanadamu angeweza kunieleza kwa ufasaha nikaelewa namna ile.
Na wakati huohuo wapo wakristo hawajajua na wengine wanajua pia, Lakini bado haijadhuru ukristo wao.
Kwahiyo kuna mambo si a msingi kuyafuatilia na kuyajua ikiwa mhusika haujaona um-singi wake na umuhimu wake
 
Umesema Vema Broo Nikweli kabisa na ndivyo kupitia Biblia inavyosema na ndio uhalisia wenyewe.
Ila kuna jambo nilazima ulijue
Kupitia shetani ni lazima ujifunze na kupitia Mungu nilazima ujifunze
Lakini ulazima wakujifunza upo nikwawale ambao hajazaliwa moja kwa moja na bahati hiyo yakuwa activated
Mfano Kuna mtu anazaliwa akiwa tayari ni mchawi na kuna mtu anazaliwa akiwa tayari ni chaguo la Mungu.
Akizaliwa akiwa mchawi hana msaada wa kujifunza uchawi tena bali atazidi kukua katika hali ya uchawi hadi uzeeni na kifo chake.
Na mtu akizaliwa katika hali ya kuchaguliwa na Mungu moja kwa moja utashangaa jinsi ambavyo anakuwa anatembea katika utukufu wa Mungu pasipo hata kufundishwa na mtu wa kupitia madarasa ya mafunzo ya biblia.
Atalieleza vyema neno la Mungu hata kuzidi wachungaji na maaskofu.
Lakini sasa tofauti na hapo ni lazima mtu mwingine achukue nafasi ya pekee kutafuta ile iliyo kweli ya Mungu au shetani.
Mfano Mtu unapaswa kusoma Neno la Mungu kila Siku, Kuomba Kila Siku tena pasipo Kukoma.
Kwahiyo Zile nguvu za Rohoni Zipo katika Nyanja Kuu Mbili Kuzaliwa nazo katika Asili Ya Pili Kujifunza.

Angalia Uhalisia Wa Kibinaadamu Hapa Ambao shetani anautumia na Mungu anautumia Pia.
Kua kitu kinaitwa Hisia
Mtu ambaye anaweza kuzimosa vizuri sana hisia zake ndio wale tunasema anamachale(Au Anandoto)
Unaweza ukawa unataka kwenda mahali lakini nafsi yako ikawa nzito sana ukaamua kulazimisha baadaye unapatwa na jambo baya huko kisha unajilaumu ""halafu moyo ulisita kweli kwenda huko lakini nilipuuzia""
Sasa vitu kama hivi nizawadi ambazo mwanadamu anapewa na Mungu bure kabisa ila sasa niwewe ujue kuitumia ipasavyo.
Kuna mahali Unasoma katika Biblia Anakuambia "Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa" Maana yake wokovu tunao nguvu tunazo Uzima tunao lakini maarifa ya jinsi gani utembee katika hayo yote ndio inakuwa vigumu.
Ndio maana kuna mtu anaweza kuomba kwa siku saba akajibiwa na mwingine dakika tu na akajibiwa.
Kinachokuwepo hapo ni viwango vya jinsi gani maarifa yako yamefunguka kujua namna ya Kumtafuta Mungu.
Kwahiyo Kuna upana sana namna ya kujua na kutafuta mambo ya sirini.
Hata katika dini Sio wote watafanikiwa kuzijua siri za wokovu japo kila mtu anaweza kuokolewa
Ni lazima mtu uwe na juhudi za ziada tena ndipo unaweza kuujua ukweli halisia nini Mungu anataka tufanye.

Kuna wakati hatuishi kwa kuzijua na kuzitambua sheria bali tunaishi kama watumwa tukiwa tumejibebesha sheria(Na hata katika Neno la Mungu Vivyo Hivyo)
Moyo wako upo huru Sana
Ubarikiwe
 
Cool Bro Ila anza kwa na hili Who Is Lilith?
Cheza na google a lot of data you will have
Lilith kaingiaje na mada yako mkuu!?...
Me nilizani umebase kwenye fates kumbe umegeneralize kwenye mystical histry!..
Sawa basi awagoogle na Titans, Olympians, Nike, Caerus, Ores, Amnet, Isis, Holy grail, Mayans, Atlantis, Oddysesius, Cronus!!..
Should i continue listing?...
 
Lilith kaingiaje na mada yako mkuu!?...
Me nilizani umebase kwenye fates kumbe umegeneralize kwenye mystical histry!..
Sawa basi awagoogle na Titans, Olympians, Nike, Caerus, Ores, Amnet, Isis, Holy grail, Mayans, Atlantis, Oddysesius, Cronus, Cronus!!..
Should i continue listing?...

Asanthe sana Bro
Unajua shida ni hii hapa kutambua ipi ni mystical history na ipi sio.
Laba kwa nyongeza Tafuta kitabu cha mtu anaitwa Enoch Kama wewe ni Mkristo nadhani utakuwa unamjua ama umewahi kusikia habari Zake.
Huyu jamaa kuna kitabu alikiandika lakini havipo katika biblia
Ukipata Kitabu chake ukikisoma unataelewa nini nimeongelea na hapo utakutana na Fates haswaaaa.

nikweli kwa jinsi ulivyoongea lakini mtu asipojua zinakuwa nikama hadithi ambazo tulihadithiana utotoni kama baba wa taifa aliweza kubadilika kuwa umbile alilotaka wakati wa vita.
Ila Ukizidi kukua kwa kuangalia hizo hadith huwezi kuujua ukweli, ila ukiamua kuutafuta ukweli ndipo utajua kwanini nasema kuna ugumu kupata tofauti katika fates history na mystical history
 
Laba kwa nyongeza Tafuta kitabu cha mtu anaitwa Enoch Kama wewe ni Mkristo nadhani utakuwa unamjua ama umewahi kusikia habari Zake.
Huyu jamaa kuna kitabu alikiandika lakini havipo katika biblia
Ukipata Kitabu chake ukikisoma unataelewa nini nimeongelea na hapo utakutana na Fates haswaaaa.
Kinaitwa THE BOOK OF ENOTH kama sijakosea, tafuta na THE BOOK OF ESTER.
Ila Ukizidi kukua kwa kuangalia hizo hadith huwezi kuujua ukweli, ila ukiamua kuutafuta ukweli ndipo utajua kwanini nasema kuna ugumu kupata tofauti katika fates history na mystical history
Kwanza hakuna Fates history lkn kuna mystical history!..
Lakini ukiongelea FATES ni kama hiko kitabu ulichosema ushawahi kiona hapo unakua haujaongelea historia tena ni kitu ambacho umekiona na kupitia chenyewe unaweza angalia yatakayokuja mbeleni!..
 
Kinaitwa THE BOOK OF ENOTH kama sijakosea, tafuta na THE BOOK OF ESTER.

Kwanza hakuna Fates history lkn kuna mystical history!..
Lakini ukiongelea FATES ni kama hiko kitabu ulichosema ushawahi kiona hapo unakua haujaongelea historia tena ni kitu ambacho umekiona na kupitia chenyewe unaweza angalia yatakayokuja mbeleni!..
The Book Of Enoth Sijajua Na Sina Uhakika sana maana sijawahikukitafuta Pia The Book Of Ester Kipo Katika Biblia Hakikutolewa Na Nimekisoma Mara Nyingi sana Kwa Nyakati tofauti tofauti.
Ila Muhimu Kitafute The Book Of Enoch Kipo Wala hakiuzwi Na ni bure kabisa na ndicho ambacho hakikuwekwa katika biblia vipo na vingine kama nane hivi.
Ila ukianza na hicho itakuwa vema sana.

Ila Nimejifunza sana Watu wengi ambao wanasoma Theology Huwa wanafaidi sana kuzidi sisi tunaoisubiri Biblia tu mda wote.
Kuna Kitabu Kinaitwa Outline Studies in Christian Doctrine Kiliandikwa na Rev.George P. Pardington, PH.D Ukikipata hiki kitakupunguzia mzigo wa kuisoma Theology.
Ila Kumbuka Dini Na Theology ni Vitu Viwili
 
The Book Of Enoth Sijajua Na Sina Uhakika sana maana sijawahikukitafuta Pia The Book Of Ester Kipo Katika Biblia Hakikutolewa Na Nimekisoma Mara Nyingi sana Kwa Nyakati tofauti tofauti.
Ila Muhimu Kitafute The Book Of Enoch Kipo Wala hakiuzwi Na ni bure kabisa na ndicho ambacho hakikuwekwa katika biblia vipo na vingine kama nane hivi.
Ila ukianza na hicho itakuwa vema sana.

Ila Nimejifunza sana Watu wengi ambao wanasoma Theology Huwa wanafaidi sana kuzidi sisi tunaoisubiri Biblia tu mda wote.
Kuna Kitabu Kinaitwa Outline Studies in Christian Doctrine Kiliandikwa na Rev.George P. Pardington, PH.D Ukikipata hiki kitakupunguzia mzigo wa kuisoma Theology.
Ila Kumbuka Dini Na Theology ni Vitu Viwili
Hicho kitabu unacho nirefer nimeshakisoma bahati mbaya nipo far na access ya PC ningekutumia na hivo vingine kama vya ester na Magdalene!..
All in all good luck on your expedition, only don't forget your grounds!..
 
Hicho kitabu unacho nirefer nimeshakisoma bahati mbaya nipo far na access ya PC ningekutumia na hivo vingine kama vya ester na Magdalene!..
All in all good luck on your expedition, only don't forget your grounds!..

Asante kwa mrejesho wako, Ukipata mda viweke hapa kwa faida ya wengine maana mimi sina soft copy za hivyo vitabu.
Pia naona leo nakutana na watu wachache miongoni mwao.
Ambao wamekutana na nondo hasa hicho kitabu na akakisoma akabakia the same.
Kweli Ni ajabu.

Ila katika yote vema ukajifunza haya Tunaishi kwa Imani Tu.
Iwe Muovu anaimani hata Mwokovu anaimani pia.
Hata yule asiyeamini uwepo wa Mungu naye ndiyo imani yake sambamba na mtu ambaye anaamini Uwepo wa Mungu.

KWa faida yako Na wengine Hata Biblia tu sio Uthibitisho Juu ya uwepo wa Mungu(Japo tunaishi kwa kukaririshwa kuwa Biblia yaweza Kuthibitisha Hayo)
Ndio Maana Kupinga hoja au kuiwekea ukinzani kwa jinsi unavyoelewa wewe sio jambo la kujitosheleza hata siku Moja.
Nikiwa nasoma kitabu kimoja kinaitwa How To Handle Difficult People Nilijifunza jambo moja kubwa na lamsingi jinsi ya kujiepusha na migogoro yakuwa mbishi.
Kwanza unapaswa binafsi usipinge Hoja(hata kama hoja hujaikubali maana unataka ujifunze na kuweka ukweli pasipo ubishi) baada ya hapo unapaswa kuondoa ule ukweli ulionao katika akili yako na kuuweka pembeni kwanza(Hii inakufanya jambo lile usilione kikwazo kwako)Kisha ingia katika hilo jambo jifunze kama geni Hii itakufanya ulijue kwa uhalisia wote pasipo kuwa na ukinzani wowote utajua vizuri wapi udhaifu wake upo na wapi ukweli wake upo.
Inakuwa ni kama mtoto Uliyemlea wewe mwenyewe binafsi kama hana tabia ya wizi hata akiiba utaamini ni baati mbaya tofauti na wale ambao hawajamlea.
Kisha sasa unarudia ile kauli yako na kuime-merge hapo sasa ndipo unafikia mwafaka juu ya hoja mbili zilizo za tofauti.

Kubishia jambo na kulipinga haina maana kusema linakuwa la uongo la Hasha
Ukweli ni Uongo Na Uongo Ni Ukweli Pia.
Ukweli Unakuwa Ukweli pale unapokuatana na watu wanaoamini ukweli huo,
Na uongo unakuwa uongo pale unapokutana na wale wasioujua kama ni ukweli.
Mfano kuna mtu anatoa ushahidi wa uongo ambao haukuwepo kabisa na unakubalika kuwa ni ukweli.
Na hauwezi kupotoshwa hata siku Moja.
Wewe ni Mkristo namimi ni Mkristo Tunaamini katika Yesu Kristo lakini wakati huohuo wengine hawaamini hata neno lake moja sababu ni kwamba ukweli waYesu Kisto Uligusa mahali ambapo hawauamini Ukweli(Wajazwa na lile wanalolijua wao kua ni kweli hawawezi kuongeza lingine)
Naweza ongea mengi sana Broo Ila acha niishie hapa.
 
Nianze kwa kusema nakumbuka nikiwa bado mdogo mdogo, nilikuwa na sifa moja kubwa sana mtaani kwetu ya ubishi.
Hata kama ulete fact za kiwango gani lakini niki-stickkatika msimamo wangu ni hapo hapo hamuwezi kunibandua hata mngekuwa mia.
Lakini kuna jambo moja aliligundua mzee mmoja siji kumsahau katika maisha yangu yote ningali bado mdogo kabisa miaka 8.
Aliniita na kuniambia
""Nikiamua kuwa na maarifa naweza kuwa nayo, nakuambia hivi si kwamba nimekuona unamaarifa bali nimegundua unaweza kujaza maarifa ukitaka, sasa nakupa kazi jifunze ulimwengu uliofichika ulivyo hautapata nafasi ya kubishana na wengine kamwe'''
Mzee nilimuelewa japo kwa ufupi sana, labda kutokana na umri wangu ulivyokuwa na kuambiwa jambo lililokuwa juu ya uwezo wa frikra zangu.
Nikiwa na miaka 14 ndipo mzee aliweza kunipa kitabu kilichokuwa na Tittle Hii
"Comfort That Kills" Nikitabu chenye page 36 tu lakini ndicho kikabadili ukurasa wangu wa maisha na kunipa hamu zaidi ya kuujua ulimwengu uliofichika.
Nilikisoma kwa kufanya mirejeo mingi sana katika kamusi ya kufasiri maneno ya Kiingereza kwenda kiswahili,
kwanza kilikuwa na maneno mengi ya kiingereza cha zamani sana, kilinipa shida kidogo lakini niliweza kukielewa na kufunguliwa ukurasa mpya wa kusoma Maandishi.
Si kwamba sikuwa msomaji toka mwanzo ila nikwamba usomaji wangu uliegemea sana katika kusoma hadithi za nadharia zaidi zilizoandikwa na waandishi mbalimbali mahiri.
Sasa hapo ndipo nikaaznza kuufukunyua ulimwengu uliofichika kwa fujo zote.
Sio katika Upande wa Dini au Historia tu, bali niliweza kuyajua mabo mengi sanakwa muda mfupi.
Na kadri nilivyozidi kusoma ndivyo nilivyozidi kujua na kutambua ya kuwa katika asilimia 100% huenda nimeijaza asilimia 0.001%(Kwa wasomaji wavitabu wananielewa vizuri hapa maana kadri unavyosoma ndivyo unaona hauna kitu na unahitaji kujaza vitu)

Nilikuwa napitia Thread Za mtu mmoja humu(jina kapuni)
Niligundua jambo moja wengi wanaompinga katika thread zake ni wale wanaoangalia muvi na video za youtube juu ya uhalisia wa ulimwengu tunaoishi, lakini hawezi kuwa na mrejesho hata mmoja juu ya maandishi aliyoyasoma.
Huyu jamaa ameandika vitu vingi ambavyo huenda sikujua kama naweza kukutana na mtu kama huyo hapa, lakini ndipo nikajua kumbe JF ina watu wengi sana wa kila namna (Viva JF)
Sijaja Hapa kuueweka hadharani ulimwengu uliofichika ila ukihitaji kuujua unajulikana kabisa, tena kwa urahisi sana.

Labda unaweza ukakosa Mzii mahala pa kuanzia lakini nakupa kidogo jambo moja.
Jaribu kujifunza mambo kama haya hapa.

Kwa watu wa Imani hasa wakristo na waochimba masuala ya tulikotoka,kwanini iko hivi,kwanini iko vile,imekuwaje,ilikuwaje,jaribu kupitia mambo haya.
-Ni vitabu gani vilimeondolewa katika Biblia
Unaisoma Biblia Leo lakini inavitabu zaidi ya vitano havijawekwa humo
Tafuta kwanini havimo, vinafundisha nini, nk

-Ni nani alikuwa mmiliki wa kwanza wa America(Usiniambie wahindi wekundu nabaadhi ya maneno yaliyopo kajifunze ulimwengu uliofichika)

Naomba niishie hapo kwa Leo, lakini nikipata mda mzuri na nafasi nitaweza kuleta hoja mbalimbali juu ya ulimwengu uliofichika kwa kadiri ya jinsi nitakavyokuwa na muda.


Updates Ipo Page #30 Kitabu Chenye Utata (Kina Uwezo Wa Kujua Wakati Wako Ujao)
Ple tafuta muda urudi ujilipue hapa. Tunahitaji kujifunza
 
Mkuu mimi pia nimefurahi kukutana na mtu aliyeanza safari yake kitambo ya kutafuta yaliyo nyuma ya pazia.

Mimi sina mda mrefu ila najiona nikiendelea kuwa huru siku hadi siku.

Ila neno kufichwa kidogo linanipa shida,siamini kama kunakufichiana ila tu ni uwezo mdogo tulionao ndio unatufanya tusiuone ndio maana anayeuona anashangaa kweli jinsi mwengine asivyouona.

Nisaidie vitabu kadhaa ndugu niendelee kujifunza,maana safari bado changa sana japo mwakani nimedhamiria kupiga hatua ya KISHINDO.
Bro kuna vitu mob vinafichwa maana yake. Mfano unakuta tukio fulani linatokea ila maana yake ni tofauti kabisa na mnavyosikia media zikiripoti.
 
Back
Top Bottom