The Real Hidden World

The Real Hidden World

Hiko kitabu naomba unisaidie na kama una vitabu vingine nisaidie nisome tu ili niongeze maarifa!nakuPM bro!
Mkuu hicho kitabu nakifahamu na nilipewa na jamaa yangu bure kabisa miaka ya 2004. Nilikisoma jinsi ya kukitumia. Lakini niliogopa baada ya kuambiawa na mzee fulani aliyekua ni mchungaji mkogwe kwamba kila unapokitumia unapunguza umri wako wa kuishi. Ilibidi nimtafute alienipa nimrudishie. Bila mafanikio kwa sababu alihamiswa kikazi kweda mkoa mwingine nilikificha kabatini mpaka 2012. nilipoonana nae na kumrudishia. lakini kiuhalisia ni kama kitabu cha kupigia bao. hakifai kwa mtu mwenye imani yake ya Dini. kina mambo mazito. Wala mtoa mada hujakosea. Nilikua nawakusanya jamaa zangu kwenye Kahawa tunaanza tunaanza kutazamiana namba na maelekezo yake kwenye majedwali yake, hakikosei. yaani jioni tumetoka tu shuleni tayari dakika sifuri kundi la majamaa wananisbiri nje tuende kijiweni. Leo nikikumbuka dah !!
Nianze kwa kusema nakumbuka nikiwa bado mdogo mdogo, nilikuwa na sifa moja kubwa sana mtaani kwetu ya ubishi.
Hata kama ulete fact za kiwango gani lakini niki-stickkatika msimamo wangu ni hapo hapo hamuwezi kunibandua hata mngekuwa mia.
Lakini kuna jambo moja aliligundua mzee mmoja siji kumsahau katika maisha yangu yote ningali bado mdogo kabisa miaka 8.
Aliniita na kuniambia
""Nikiamua kuwa na maarifa naweza kuwa nayo, nakuambia hivi si kwamba nimekuona unamaarifa bali nimegundua unaweza kujaza maarifa ukitaka, sasa nakupa kazi jifunze ulimwengu uliofichika ulivyo hautapata nafasi ya kubishana na wengine kamwe'''
Mzee nilimuelewa japo kwa ufupi sana, labda kutokana na umri wangu ulivyokuwa na kuambiwa jambo lililokuwa juu ya uwezo wa frikra zangu.
Nikiwa na miaka 14 ndipo mzee aliweza kunipa kitabu kilichokuwa na Tittle Hii
"Comfort That Kills" Nikitabu chenye page 36 tu lakini ndicho kikabadili ukurasa wangu wa maisha na kunipa hamu zaidi ya kuujua ulimwengu uliofichika.
Nilikisoma kwa kufanya mirejeo mingi sana katika kamusi ya kufasiri maneno ya Kiingereza kwenda kiswahili,
kwanza kilikuwa na maneno mengi ya kiingereza cha zamani sana, kilinipa shida kidogo lakini niliweza kukielewa na kufunguliwa ukurasa mpya wa kusoma Maandishi.
Si kwamba sikuwa msomaji toka mwanzo ila nikwamba usomaji wangu uliegemea sana katika kusoma hadithi za nadharia zaidi zilizoandikwa na waandishi mbalimbali mahiri.
Sasa hapo ndipo nikaaznza kuufukunyua ulimwengu uliofichika kwa fujo zote.
Sio katika Upande wa Dini au Historia tu, bali niliweza kuyajua mabo mengi sanakwa muda mfupi.
Na kadri nilivyozidi kusoma ndivyo nilivyozidi kujua na kutambua ya kuwa katika asilimia 100% huenda nimeijaza asilimia 0.001%(Kwa wasomaji wavitabu wananielewa vizuri hapa maana kadri unavyosoma ndivyo unaona hauna kitu na unahitaji kujaza vitu)

Nilikuwa napitia Thread Za mtu mmoja humu(jina kapuni)
Niligundua jambo moja wengi wanaompinga katika thread zake ni wale wanaoangalia muvi na video za youtube juu ya uhalisia wa ulimwengu tunaoishi, lakini hawezi kuwa na mrejesho hata mmoja juu ya maandishi aliyoyasoma.
Huyu jamaa ameandika vitu vingi ambavyo huenda sikujua kama naweza kukutana na mtu kama huyo hapa, lakini ndipo nikajua kumbe JF ina watu wengi sana wa kila namna (Viva JF)
Sijaja Hapa kuueweka hadharani ulimwengu uliofichika ila ukihitaji kuujua unajulikana kabisa, tena kwa urahisi sana.

Labda unaweza ukakosa Mzii mahala pa kuanzia lakini nakupa kidogo jambo moja.
Jaribu kujifunza mambo kama haya hapa.

Kwa watu wa Imani hasa wakristo na waochimba masuala ya tulikotoka,kwanini iko hivi,kwanini iko vile,imekuwaje,ilikuwaje,jaribu kupitia mambo haya.
-Ni vitabu gani vilimeondolewa katika Biblia
Unaisoma Biblia Leo lakini inavitabu zaidi ya vitano havijawekwa humo
Tafuta kwanini havimo, vinafundisha nini, nk

-Ni nani alikuwa mmiliki wa kwanza wa America(Usiniambie wahindi wekundu nabaadhi ya maneno yaliyopo kajifunze ulimwengu uliofichika)

Naomba niishie hapo kwa Leo, lakini nikipata mda mzuri na nafasi nitaweza kuleta hoja mbalimbali juu ya ulimwengu uliofichika kwa kadiri ya jinsi nitakavyokuwa na muda.


Updates Ipo Page #30 Kitabu Chenye Utata (Kina Uwezo Wa Kujua Wakati Wako Ujao)
 
Kiukweli mimi kama mimi lugha ya wazungu haipandi sasa mkuu jaribu kushusha baadhi ya nondo umu na mimi nifaidi kidg,naona mnatoleana mifano tu page zinasonga shusha maarifa bosi daah.
 
Kiukweli mimi kama mimi lugha ya wazungu haipandi sasa mkuu jaribu kushusha baadhi ya nondo umu na mimi nifaidi kidg,naona mnatoleana mifano tu page zinasonga shusha maarifa bosi daah.
NIlipata Shida Kidogo Mkuu mambo Ya kuhangaika na uchumi wetu sasa nimekosa mda wakuwa free kidogo
ila soon nakuja hapa na kitu kipya baadaye au jion nitaleta mkuu.
pole sana kwa kusubiria
 
Wakuu, kwa anaye hitaji softcopy ya Kitabu hiki cha Napoleon, hii hapa link ya kudownload kwenye Google drive kuna mshkaji wang mmoja anayo softcopy amekuwa mwema kushare link :

Sijui iko sahihi:
 
Wakuu, kwa anaye hitaji softcopy ya Kitabu hiki cha Napoleon, hii hapa link ya kudownload kwenye Google drive kuna mshkaji wang mmoja anayo softcopy amekuwa mwema kushare link :

Sijui iko sahihi:

Weka link vizuri
 
Nguvu Za Asili Alizonazo Mwanadamu Kumshinda Mchawi

Habari ndugu zangu?
Poleni kwa ukimya na kunisubiri kwa muda mrefu sana pasipo kuja na mada mpya yoyote.
Leo wacha tuweze kuzungumza juu ya mda hii kwa ufupi tofauti hasa na mda niliyoahidi kuileta, Kwanza nilazima ujue nakutambua ya kuwa mwanadamu ananguvu za asili ambazo Mungu amemuumba nazo, Japo kunawakati unaweza ukazichochea ziweze kufanya kazi na wakati mwingine zinajichochea zenenyewe pasipo kuchochewa na jambo lolote, Hii inatokana na jinsi ambavyo ni nguvu ya uapnde gani ambayo yaweza kutumika mara kwa mara kwa mtu husika.
Mfano nakumbuka nikiwa mdogo nikichelewa shuleni kuna rafiki yangu mmoja kila nikichelewa naye tulikuwa tunaingia salama kabisa shuleni pasipo shida yoyote,
Ila siku nikichelewa peke yangu yaani nilikuwa nakung'utwa hatari sana ikabidi sasa niwe nikichelewa lazima nimpitie jamaa maana yeye hakuwa mtu wa kuwahi sana shule.
Kuna jambo lingine ilikuwa kuna siku moja tunakutana na bibi mmoja hivi(nilikuwa nimesindikizana na baba yangu mdogo wakati wa likizo kuchunga ng'ombe)yule bibi alikuwa anatupa matunda fulani hivi kikwetu yanaitwa Maswisa sijajua kiswahili maana yapo unyakyusani pekee. tunapoanza kuyapokea tu jamaa yetu mmoja alikuwa mbali kidogo akapiga kelele akiuliza we bibi unawapa nini hao(kwa lugha yetu) yule bibi kumuona tu rafiki yetu yule akaacha hata kutupa yale matunda akaondoka zake haraka japo hata jamaa yetu hakujua nini kimetokea.
Kuna jambo lingine hili nina kaka yangu mmoja tangia utotoni amewahi kukanyaga nyoka zaidi ya mara sita au saba ninazokumbuka mimi lakini hakuna nyoka aliyewahi kumdhuru hata siku moja.
nijambo la kushangaza sana ukiangalia baadi ya matukio hayo hapo juu, sasa nini huwa kinasababisha?
Hiyo ndio nguvu ya asili aliyo nayo kila mtu kwa jinsi alivyoumbwa na Mungu.
Nakupa mfano Mwingine,
Bibi yangu mzaa mama yeye ni mke mkubwa maana babu alioa wake watatu alikuwa pia ni chifu ila alikwisha fariki mda sana, sasa kuna siku moja bibi alikuwa ameamka mtu mwenye huzuni sana nikamuuliza bibi vipi mbona uko hivyo?
Akasema kuna msiba unakuja nikamuuliaz msiba wa nani akasema hajui nikamuuliza tena
Umejuaje kuna msiba?
Akaniambia ameota gari linagonga nyumba yake
Mmmmh nikahamaki kidogo nikamuuliza hilo ndilo linakuambia kuna msiba?
akanipa ushahidi wamisiba kama minne ilioikumba familia ambayo aliota ndoto hivyo hivyo na msaba ukawa kweli, then jion kuna taarifa ya msiba ikaja ndugu yetu amefariki so means msiba unatuhusu lazima uwe hapo kwa bibi.
jambo linalokuja nikuwa kunamuunganiko fulani juu ya nguvu ya asili na maisha a kawaida ila uhalisia ni kwamba je unaweza kutambua kuwa nguvu zako za asili zinazungumza nini?
hapo ndio kimbembe sasa.
Mfano mwingine Ni huu mwili kusisimka,kichwa kuwasha,jicho kucheza,kusisimka kichwani tu kiupande nk.
Ni matokeo ambayo yapo yanaonyesha ile nguvu ya asili inakuwa inafnaa kazi ila sasa je utajuaje inafanya kazi kwa jambo gani? ndio hapo sasa shida kujua.
Twende sasa kwenye Mada.
mara nyingi wachawi huwa tunawafumania sana ama kukumbana nao katika mazingira tofauti tofauti pasipo kutambua sisi wenyewe binafsi.
Kuna wakati mnaweza mkawa mnatembea njiani na kisha gafla mnajikuta wote mpo upande mmoja tu,
Ama unakuta mlikuwa mnaongea na gafla mpo kimya,
Ama unatembea usiku peke yako au kundi na kisha kunajoto la gafla unapishana nalo na unaona kabisa hapo kuna hewa nzito ila unaendela pasipo kujua mazingira yaliyokuzunguka yanaashiria nini.
Wengine wanashituka toka usingizini gafla anamuona mtu na akipiga kelele ama kukemea(Kwa wakristo) mtu yule anatoweka gafla.
Leo nazungumza mambo mawili ambayo nayajua unaweza ukamuona mchawi pasipo kuwa na dawa wala ushawi wowote ule na ninaongea kwa ujasiri hivi maana sijajua sipinani na maandiko ni jambo la kawaida kama kuandaa fumanizi la mke au mwizi vile.
Sehemu ya kwanza ukiwa Ndani
Ukiwa umelala ukawa unakabwa ama ukiwa usingizini ukahisi kuna mtu chumbani kwako ukazinduka na gafla unamuona mtu na kisha ukipiga kelele anapote ama ukikemea.
kama imewahi kukupata basi jua bana ulishamfumania mchawi ila ulishindwa kumkamata tu, yaani umemwona mwizi nawewe umekimbia wakati kabambmwa laiti wangekuwa wanatusimulia wangesema leo nimefumaniwa kwa fulani chup chup kunaswa tu.
Sasa nini kinafanyika?
Unapokuwa umelala mchawi huwa anaoneka live pasipo kujificha maana anakuongezea na usingizi mzito zaidi ili usiamke kama uko umepigwa nusu kaputi vile, akisha fanya mambo yake anapoondoka tu nawe ndio unapata fahamu unazinduka, sasa nini kinatokea ukizinduka kabla hajaondoka?
Hapo ndio az Mwizi Arobaini yaani hapo ndio unakuwa umemnasa nini unatakiwa ufanye asipoteee?
Kwanza kabisa usipige kelele wala kukemea kaa kimya mwangalie tu jivike ujasiri sasa sio unaogopa tena ha ha ha ha
Yeye atafanya nini?
Yeye anaanza kukufanyia vituko ili upige kelele na ukishapiga hapo ndio njia umemruhusu yeyuka na anayeyuka, akishajua yakuwa umekaa kimya haujafnya lolote atazidisha mbwembwe kama kuvua nguo zao wanazovaa kama yuko uchi kabisa basi atafanya mambo mengi ya ajabu ili mradi wewe upige kelele ila kumbuka hapo hana nguvu hata chembe ya kukudhuru hata kidogo, na kumbuka wewe sio mchawi wala hujawahai kuchawia wala kunywa dawa ni namna tu asili ya kumkata huyu mchawi.
mwishowe anaanza hata kulia sasa hapo ndio utamuona akionesha ishara za kukuomba msamaha sijajua ni kwanini hapo hana uwezo wakuongea nawewe hata neno moja bali ni ishara tu.
ndi maana ukiwa unasituka kutoka usingizini unamuona mtu mbele unakuta anakuwa kama anataka aklushike vile ama anafanya jambo ambalo wewe utapiga kelele nayeye anapotea anaenda zake.
Yaani ndio upumbavu wa uchawi unamnasa pasipo wewe kuwa mchawi hiii ni nguvu tu ambayo Mungu kamuumba wanadamu ni ya asili haswaaaaaaa.
Ukishachoka umempiga na picha zakutumia wenzako whatsapp sasa mwambie tu haya nenda
weeeeee huo upepo chumbani kwako utajihisi upo baharini na imechafuka fasta anatembeaaaaaaaa.
Daaa wadau nimechoka sana kwakweli nimeona nisiiwaache bure ila kesho nitaongelea ukitembea barabarani lile jotona hewa nzito ni nini?
na utamnasaje unayepisha naye hapo ama tukio la hapo?
sasa hilo mimi mwenyewe shuhuda daaa nilikoma ubishi, kwakweli sema la nyongeza ukichukua kitu chochote hata punje ya mchanga ukambonda nacho ndio umemuua utapotea lakini ndio hataamka tena huyo yaani mchawi unaua usiye mchawi ha ha ha ha ha ha hatari sana.
Neno La Mungu Linatukataza Kuua Linatufundisha Lulipiza Ubaya Kwa Wema Kuua Ni Dhambi hata Ukiua Mwizi Ni Dhambi Pia.
Usihukumu Usije Ukahukumiwa

At first nilisoma kujua jambo hili katika kitabu kimoja hivi kinaitwa Versteckter Natur ni cha kijerumani lakini kinamekuwa translated kushoto kijerumani kulia kiingereza, maaana yake ni Hidden Nature.Sijawahi iafua soft copy ila kitabu kina fact ambazo unaweza soma kisha unabakia unacheka mwenyewe ila nitakuja kuwapa dondoo ninapomalizia hapa na niitajaribu kuitafuta soft copy yake kama ipo

Wadau niwatakie usiku mwema mlale salama kabisaaa
 
Kikubwa ni kuipata hii information na kuishi with all the confidence
Tuondokane na inferiority complex aliyo tuwekea mtu mweupe!
Binadamu anao uwezo wa ku create chochote !
Kutumia mawazo yake!
 
IMG_1687.JPG
IMG_1632.JPG
IMG_1687.JPG
IMG_1632.JPG
 
Back
Top Bottom