nimetafuta sana kazi bira mafanikio tukaamua mimi na mchumba wangu tuwe tuna amshana saa9 usiku kwa maombi maalum,ndugu zangu Mungu kajibu haraka nimeitwa kama sehemu tatu amakweli binadamu anateseka kwa kukosa maarifa kidogo,try the power of lord
bwana yesu asifiwe...
Muhusika kasema Amemuomba "MUNGU" akapata kazi.
We unamsifia yesu!
kwanini usiseme "MUNGU ASIFIWE?
Yohana 14:1 Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu,niaminini na mimi. 14;7 Yesu akamwambia,mimi ndimi njia,na kweli na uzima; mtu haji kwa baba, ila kwa njia ya mimi. 8 kama mngalinijua, mngalimjua Baba; tangu sasa mnamjua, tena mmemwona.10 Husadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba na Baba yu ndani yangu? Hayo maneno niwaambiayo mimi sisemi kwa shauri langu;lkn baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake.
Umeweka andiko hilo kuonyesha kuwa YESU NDIO BABA SIO!?
Sasa soma hili hapa halafu ujiulize huyo BABA umeshamuona! Au kumsikia??
YOHANA 5:37
-Naye Baba-aliyenituma-hunishuhudia. Ninyi hamjapata kamwe kusikia sauti yake, wala kuuona uso wake.
Mshukuruni MUNGU sio YESU!
Na msimfanye Yesu kama Dalali wa kukaa ktkt baina yenu na MUNGU!
Muombeni MUNGU moja kwa moja.
Sipo kwaajili ya kubishana na wewe ndugu samahani....nilikuwa najaribu kufafanua tu maana hata huyo aliyeomba nina hakika ameomba kwa jina la Yesu.....sasa kama tunaomba kwa jina lake na tunapata kile tulichokiomba where is the problem?.....mutuwache...!!!
Nimehamasika! Sina kazi mpaka nanuka shida!
sasa basi, mbele za Mungu naahidi! Nitafanya maombi kuanzia sasa mpaka napata kazi na sitachoka kamwe! Daima
Kwa ratiba ya kabla ya kulala usiku na saa 9 usiku halafu baada ya kuamka asubuhi
Nadhani ntaleta ushuhuda hapa hapa
Ni kweli ndugu.nakumbuka mm pia nilikuwa nimemaliza chuo katika shahada ya uzamili na nilikuwa nimefanya vizuri sana.nikawa naomba kazi hadi kwenye taasisi za kawaida sana lakini wananizungusha.
Basi mchumba wangu akaamua kuingia kwenye maombi ya mzigo sana juu ya swala langu na mm nika mwamini Mungu kuwa ameshafanya.
Ndugu zangu kweli Mungu alinihurumia nikaja kupata kazi nzuri sana ambayo nilikuwa nikiiota kwa siku nyingi. Yaan nikiitwa kwenye taasisi kubwa mbili za serikalini na nikaamua kuchagua moja
Nimeona nami niwashuhudie ndugu zangu kwan najua kuwa kuna watu pia wanapitia wakati mgumu katika maisha. Muamini Mungu kuwa hata km huna mtu anayekujua bt Mungu ambaye Yeye ni baba wa yatima anaweza kuwa referee wako kwenye ofisi yeyote hile.
ila naona si kwa wote kuna watu nahisi amewachagua
Muhusika kasema Amemuomba "MUNGU" akapata kazi.
We unamsifia yesu!
kwanini usiseme "MUNGU ASIFIWE?
Ni kwa kila anayemuamini. Yote yanawezekana kwake yeye aaminiye
mungu huwa ameshapanga mtiririko mzima wa maisha kuanzia ukiwa tumboni hadi utakufa lini na matukio katika maisha ni kopi ya kile alichokipanga ili neno litimie mfano yuda hata ingekuwa vp ilikuwa ni lazima amkane yesu