The Only Thing We Have to Fear is Fear itself

Nashukuru mh. Mbowe na wewe unapita humu.Mimi hoja yangu hapa nataka niongelee mambo mengine muhimu,na sio majina.Watu wanasababu mbalimbali kutumia majina bandia,maana wengine ni waajiriwa nk. Mimi concern yangu hasa ni Chadema,kwanza nianze kujitambulisha kama mpenzi mkubwa wa chadema na mkereketwa halisi,nadhani ukipitia comments zangu utajua hilo.Concern yangu kubwa ninaona kama chama kinadorora sana sasaivi.Hasa hili suala la toka Lowassa aingie chadema,imekuwa kana kwamba tumemuachia chama,yaani chama kinapata umaarufu kwasababu yake,yaani yeye ndio chama na chama ndio yeye,nikiri kuwa ninampenda sana lowassa,lakini linapokuja suala la yeye kuwa mkubwa kuliko chama,hilo nakataa.Hatuwezi kama chama kuwa chini ya mtu,umaarufu wa mtu.Inabidi ajue yeye ni kama mwanachama mwingine ndani ya chama,taasisi kwanza mtu mmoja mmoja baadae.Kwanza nimeshangaa juzi anawaambia wabunge na madiwani wasipo achieve watafukuzwa!Najua yupo sahihi,lakini yeye ni nani kuwaambia hivyo?Mi nafikiri ni muda sasa ajue kuwa hii ndo chadema bana,hata akitoka tutasonga kama kawa.Amuulize Dr Slaa. Jambo la pili,inakuwaje waziri mkuu Majaliwa anakataza shughuli za siasa,tena akikiuka sheria na katiba halafu mnanyamaza kimya?Hakuna hata kumfungulia kesi mahakamani kwa kukiuka sheria? Tunaenda wapi Chadema?!!
 
Bravo Mwanasiasa,

Point well said, na umekuja across kama wewe ndiye mwenye kiti wa Chadema, badala ya Mzee Freeman na JJ, isipokuwa tu hebu fafanua maana ya militarism ndani ya CCM na Upinzani, hapo sijakupata?

Mzee Freeman,

Respect kwamba finally, baada ya kuangalia kila siku kwa pembeni, umeamua kuja mwenyewe, off course ninajua kuwa siku zote ulikuwa upo hapa maana watu wako fulani ninawajua wapo hapa kila siku haiwezekani kuwa hukuwepo, anyway heshima mbele kwa kujitokeza kwenye hii forum, hii inapaswa kuwa ni clear message kwa bwana Ukimwi kwamba hii forum inafanya kazi yake inavyotakiwa ingawa katika maizngira magumu lakini, hey! it is better than noithing,

Mzee Freeman,

I have a problem na ujumbe wako kuhusu majina ya bandia ninaona unataka kupoteza lengo pamoja na nia yako njema ya kuja hapa, do not tell us what to do bro!, wewe jibu mapigo tu, tena please we have nothing to apologize for kwa kutotumia majina yetu, wote hapa tunajua what time is hatuhitaji kukumbushwa na mtu yoyote, kilichokuleta hapoa na sio forum zingine ni kwa sababu the message is powerful na clear understandable, njia zote tunazozitumia humu ndio hasa nyinyi politician wa bongo mnazozielewa vizuri, na ndio maana hata magazeti mnayoyamiliki, on this I mean wote CCM na Upinzani huwa hamuaandiki majina, WHY? take this thing ya majina back bro! no more lectures kwenye hilo, next time you come just deal with the message,

But baada ya kusema yote hayo, ninasema heshima yetu kwako kwa kukubali hatimaye kuingia kama ulivyo kwenye hii froum, na ninakuomba uendelee kuwepo hapa ili tufundishane siasa na tuulizane maswali ya kweli kwa faida ya taifa letu, taifa letu liko njia panda, we know that, sasa hii sio forum ya upinzani kama some of us walivyoshauri, hapana hii ni forum ya wananchi wanaoelewa ukweli wa kinachoendelea bongo, na wangependa kusikia majibu au marekebisho, sasa tunategemea wewe na wenzako mje hapa mtupe majibu mnayoyafahamu, bila siasa nyingi tumesikia siasa za kutosha sasa tuongee majibu tu bro, hizi habari za majina ni irrelevant,

hebu tulonge issues Mzee Freeman wote hapa ni watu wazima, tuseme issue, na the hot one sasa hivi ni Richmond na IPTL, hebu tuwekee msimamo wa chama chako, utakapoingia tena, pia kama unaweza hebu gusa kuhusu hii NONESENSE ya unga? Halafu hebu gusia kuhusu elimu yako mpya, maana kuna tunaoiona kama kuna u-KIHIYO! kihiyo! ndani yake, hebu tuwekee usawa?

Wasaalaam wazee wote wa hii forum, na karibu wazee wa Chadema Freman na JJ, na we are ready for you ila please do not tell us how to write, Thank you! na Forum idumu!
JF ya enzi hizo,kulikuwa na vichwa sio Jf ya sasa yakina Mmawia.
 
Nashukuru mh. Mbowe na wewe unapita humu.Mimi hoja yangu hapa nataka niongelee mambo mengine muhimu,na sio majina.Watu wanasababu mbalimbali kutumia majina bandia,maana wengine ni waajiriwa nk. Mimi concern yangu hasa ni Chadema,kwanza nianze kujitambulisha kama mpenzi mkubwa wa chadema na mkereketwa halisi,nadhani ukipitia comments zangu utajua hilo.Concern yangu kubwa ninaona kama chama kinadorora sana sasaivi.Hasa hili suala la toka Lowassa aingie chadema,imekuwa kana kwamba tumemuachia chama,yaani chama kinapata umaarufu kwasababu yake,yaani yeye ndio chama na chama ndio yeye,nikiri kuwa ninampenda sana lowassa,lakini linapokuja suala la yeye kuwa mkubwa kuliko chama,hilo nakataa.Hatuwezi kama chama kuwa chini ya mtu,umaarufu wa mtu.Inabidi ajue yeye ni kama mwanachama mwingine ndani ya chama,taasisi kwanza mtu mmoja mmoja baadae.Kwanza nimeshangaa juzi anawaambia wabunge na madiwani wasipo achieve watafukuzwa!Najua yupo sahihi,lakini yeye ni nani kuwaambia hivyo?Mi nafikiri ni muda sasa ajue kuwa hii ndo chadema bana,hata akitoka tutasonga kama kawa.Amuulize Dr Slaa. Jambo la pili,inakuwaje waziri mkuu Majaliwa anakataza shughuli za siasa,tena akikiuka sheria na katiba halafu mnanyamaza kimya?Hakuna hata kumfungulia kesi mahakamani kwa kukiuka sheria? Tunaenda wapi Chadema?!!
Endeleeni kuwambia viongozi wenu ukweli ndio wanabadilika.
 
mi pia mgeni hapa naiepnda Chadema na nina mambo kadhaa nataka kuongea:

1. eti ni kweli anna komu bibi yako ndio maana akawa mgombea mwenza baada ya kufa yule mzenji na vilevile akawa kwenye nafasi ya kuwa mbunge viti vya wanawake chadema

2. naomba maelezo kuhusu sakata la wagombea viti maalum chadema manake kamati kuu yenu ilitaka kukuondoa lakini wazee wa busara kina makani, mtei na wengineo wakaingilia wanasema eti mmechagua mabibi zenu tu zitto na muhonga, wewe na anna komu na kiwelu na halima mdee na yule binti wa ndesamburo. what happened?

3. je unadhani wanaosema huna haki ya kuongelea mapambano ya kumkomboa mnyonge wakati umekuta kila kitu kwenye silver plater na dingi wako alikuwa mtu pekee aliyeruhusiwa kununua benzi na mchonga wanakuonea?

4. biashara zako: inasemekana hakuna nidhamu katika uendeshaji biashara zako ndio maana una madeni mengi na una-reschedule kila mara. wanasema kuna ushahidi kwamba uamuzi wa mahakama kuku-liquidate unausogeza mbele for legal technicalities. nssf, remember? sasa kama huwezi kuendesha biashara zako, utaweza kuendesha nchi?

5. hiyo hapo juu inaeleweka ila natoa ushauri kwamba umejiingiza kwenye siasa kama mfanyabiashara it is really trick kwasababu biashara in bongo is synonimuos with scandal. there is no clean businessperson in bongo. wanasema washikaji zako ccm ndio kwasababu ya biashara. basically you have been compromised na unayosema yote kuhusu ukombozi ni rhetoric tu.

6. magwanda. wakati wa kampeni yale mavazi yalikuwa interesting. ulisema eti kwasababu uko vitani. sasa huoni kufananisha kampeni na vita haileti ujumbe mzuri kwa nchi yetu ya amani? niliona mnyika na zitto na jamaa wengine nao walikuwa wanayavaa. tena mnyika na kamwili kake kadogo ndio ilikuwa kituko. did you force them to wear the gear? au walilazimika kwa kuona unayavaa?

7. mwakagenda v. baregu. kwanini mlimuengua mwakagenda an incumbent member wa EALA na kumweka baregu kama mgombea? mwakagenda haku-perform? au ni tishio kwa mbowe?

8. tanzania daima. kwanini usije tu hadharani ukasema you own the paper, and free media inc. na unawatumia kina ansbert ngurumo na waandishi wengine kama ambavyo ccm inawatumia wengine. nadhani itakuwa jambo la heshima kuwa mkweli kwenye hili.

9. ushauri: siasa sio environmental movement. you win if you play dirty. wadau bongo wanajua you play dirty, na tatizo ni the limited impact of your dirty politics, ila kinachokera ni kujifanya clean hadharani. you will never win an election kwa frame hii. i think you have a good team: zitto is bright, but reactionary. mnyika is wise, but naive. mzee mtei is a management guru is still bitter about mwalimu and the lost glory of machame empire. makani is witty but as useless as a TV wrestler. yourself is really good, but as ethically compromised as those you condemn. mwakagenda is good, but he is feared therefore underutilised. kaburu was good, but he was feared and underutilised, therefore left. slaa is my man, a legal and constitutional matador, i hope he won't be feared and underutilised and leave. the ladies of chadema bungeni, well, what can I say?

10. ushiriki wako hapa forum. a strategic mistake, ungekuwa unasoma tu. this place is addictive and you and your team will be bogged down here badala ya kufanya homework yako hapo shuleni. i think you have potential but you are a very naive politician.

aisee hivi ilikuwaje ukatoa bastola na kutishia yule mhuni kule karatu wakati wa kampeni. hauni ile incident inaku-disqualify kama kiongozi. tofauti na ditto ni kwamba yeye alifanya kweli.
Kuna masuali baadhi bado yanahitaji majibu humu.
 
KWANZA KARIBU MWENYEKITI, PILI NAOMBA SOMA MAWAZO WANGU KUHUSIANA NA ISHU YA MWIGAMBA NA MIENENDO YETU YA KUTUMIA MITANDAO YA KIJAMII.



Tuhuma alizozitoa Mwigamba dhidi ya chama nimezisoma vizuri JF, nasikitika kwa kiongozi wa nyadhifa yake kutumia mtandao wa kijamii kuyasema yale mbaya zaidi kwa kutumia jina la bandia. Wenzetu waliokuwa kwenye vikao vya maamuzi wanakikosoa chama kwa kutumia mitandao, je, sisi tusiokuwa kwenye hivyo vikao tutatumia nini?

Vijana wengi waCHADEMA tumekilaani na kukoseshwa raha na kitendo cha Mwigamba, pamoja na hayo, hoja alizokuja nazo hadharani Mwigamba si za kubezwa hata kidogo. Tulaani kwa upande mmoja na tujikite kwenye maudhui ya hoja zake kwa upende wa pili.

Tunaomba viongozi wetu wakuu wa CHADEMA waangalie namna wanavyopokea mawazo mapya, namna wanavyowasikiliza wachache, namna ya kutekeleza maamuzi ya wengi(wengi wape) na namna ya kutekeleza maamuzi na maagizo ya vikao vikubwa vya kichama. Moja ya hoja ya Mwigamba kuwa vikao na maamuzi yake haviheshimiwi na viongozi wakuu aliowataja, sitaki kuamini kuwa hizo kasoro alishawahi kuzisema kwenye vikao sema tu hao viongozi kama alivyosema hawasikilizi maamuzi ya vikao, kama hawasikilizi maamuzi ya vikao wataweza kumsikiliza mtu mmoja anaye wakosoa? kama ndivyo basi hii ndio sababu iliyopelekea kutoka hadharani.

Huenda namna ya hizo nilizozianisha hapo juu zikawa hazifanywi katika namna ya kuridhisha na kupendeza, kama ndivyo, majukwaa ya ndani ya chama yatakuwa yananyima fursa ya kupokea mawazo mapya na kukosoa utendaji wa ofisi za viongozi wakuu. CHADEMA ijitathimini kwa hili, isiishie kumchukulia hatua za kinidhamu tu Mwigamba bila kuzifanyia kazi hoja alizokuja nazo hadharani.

Nimefurahi kusikia kuwa ametakiwa kudhithibitisha tuhuma alizozitoa dhidi ya viongozi wakuu wa chama, natoa rai kama tuhuma hizi zikithibiti basi Dr.Slaa, Mbowe, Zitto, Arfi na viongozi kama hao wa upande wa Zanzibar wajiuzulu nyadhifa zao. Wabaki kama wanachama wa kawaida na tuingize uongozi mwingine, uongozi utakaokuja kuendeleza mazuri ya watu hao na kuacha mabaya ya watu hao.( kama hayo mabaya yapo na yakithibiti). Endapo haya mambo yakithibiti na wasipojiuzulu basi itakuwa ni ndoto kwa CCM kutoka ikulu na ni ndoto kwa CHADEMA kuingia ikulu.

Kama Mwigamba akishindwa kuthibitisha hizi tuhuma alizozitoa dhidi ya viongozi wakuu wa chama, asiishie kuvuliwa uongozi tu, lakini pia afukuzwe uanachama na ikibidi ashitakiwe mahakamani kutokana kitendo hichi kibaya na kichafu ili iwe fundisho kwa watu wote wenye tabia kama hii ambao bado hawajajulikana, kwa kufanya hivi hao wengine ambao bado hawajulikana wanaweza kuacha tabia hii kwa kuchelea kukutwa na kitakachompata Mwigamba. Nafikiri hii ndio itakuwa njia ya pekee ya kulinda nidhamu na heshima ya chama mbele ya wanachama na watanzania kwa ujumla ambao kimsingi ndio wanunuaji wa sera zetu. Tukilea ujinga huu watatokea wengi wa kutuvuruga kisa tu waliona Mwigamba kapewa adhabu ndogo au onyo la kulaza ukope.

Hata hivyo sisi tulio nje ya ya vikao tunaweza kujiuliza operesheni ya M4C imepotelea wapi? Au tumeicha mara baada ya kutokea tukio la Iringa na vurugu za gesi Mtwara? Hivi ni kweli CCM wanatuandalia matukio bila kujua? Je, wakiacha kuandaa hayo matukio kisa tu Mwigamba kawashutua ndio CHADEMA bai bai? Pia tunaweza kujiuliza uchaguzi wa chama utafanyika lini ikiwa ilisemekana hadi desemba mwaka huu uchaguzi ungekuwa umekwisha malizika kwa ngazi zote, tunajiuliza hili la uchaguzi nalo limepotelea wapi? Hizi ni baadhi ya hoja chache alizokuja nazo Mwigamba hadharani. Je, sisi wanaCHADEMA tuishie kuona usaliti wa Mwigamba bila kuzingatia hoja hizi? Kwanini viongozi wasizijibu hoja za Mwigamba?

Kwa vyovyote vile watazijibu, wakati Mwigamba akithibitisha hizi tuhuma, subira ndio kila kitu katika hili, kama katakiwa kuthibitisha na kwa vyovyote vile nasi twakiwa kusubiri, kama ndivyo huu wimbo wa usaliti usaliti unapata uhalali gani katika kipindi hichi cha kusubiri? Na wale wanawalaumu Mbowe na viongozi wenziwe waliotajwa katika bandiko la Mwigamba pia wanapata uhalali gani wa kufanya hivyo ikiwa bado Mwigamba hajathibitisha katika vikao halali na uthibitisho huo kukubalika? Tuvute subira kwani siku zote ndio huvuta heri, kinyume chake labda tunataka maamuzi ya chama juu ya hili yazingatie mbwembwe zetu badala ya uthibitisho wenyewe.

Pamoja na hayo, Mwigamba kama aliona mawazo yake hayasikilizwi na kutekelezwa, na kama aliamini mawazo yake ni sahihi na yako kwaajili ya kujenga chama, basi ni vema MOSI angejiuzulu; hakuna umuhimu wa kufanya kazi na watu usiowaamini na kuwakubali au wasiokusikiliza au wanaokubeza. Pili, angetoka hadharani, tena si kwakutumia jina bandia, bali angetumia jina lake halisi, angetangaza kujiuzulu kwake na mapungufu aliyoyasema angeyataja kama sababu ya kujiuzulu huko.

Kitendo cha kuusifia uongozi wa Dr.Slaa na Mh.Mbowe kwenye kikao halali cha chama, na kisha kwa kutumia jina la bandia akawa anaukandia huo uongozi kama vile hakuusifia muda fupi uliopita kwa wakati ule, ni usaliti kwa uzalendo wake kwa chama, usaliti kwa weledi wake ambao wengi wetu tunaujua na mwisho ni usaliti kwa uanaume wake; kwani hatutaraji kwa mwanaume kusema vitu sahihi na anavyoviamini kwa kutumia jina la bandia kisa tu asijulikane. Nitaendelea kumlaumu Mwigamba kwa hili haijalishi alichokisema ni sahihi au la!

Halafu hili suala la viongozi na wanachama kutumia mitandao vibaya na bila ridhaa ya CHADEMA yenyewe limekuwa kama vile limeota mizizi fulani vilee. Kipindi fulani tulishuhudia Naibu Katibu mkuu wa CHADEMA akitupiana maneno na wajumbe wa kamati kuu kisa tu namba yake lilikuwa kwenye tamko la wajumbe hao walilolitoa kwa niaba ya chama, wengine tunajiuliza, kama lile lilikuwa tamko la chama lililobarikiwa na kamati kuu iweje Naibu Katibu mkuu alipinge hadharani ikiwa na yeye ni mjumbe wa kamati kuu ikiwa kimsingi na kikatiba yeye ni zao la tamko? Nimelitaja hili kwa lengo la kuonesha hii tabia ya kutumia mitandao ya kijamii kwa namna mbaya na chafu kwa Mwigamba si wa kwanza na limbuko.

Pia tulishuhudia vijana wakimtuhumu Zitto kuwa ni msaliti na mengi yalisemwa, vijana waliokuwa wanasema Zitto msaliti ni wanachama na wanajulikana vizuri, lakini hadi leo hii na kwa vyovyote vile hawajaitwa kuthibitisha usaliti wa Zitto na wanaendelea hadi sasa katika mitandao kumuandama Zitto. Hotuba aliyoitoa Zitto katika mkutano wa CHADEMA Tabora hivi karibuni aliwaasa vijana waache kuwagombanisha viongozi wakuu wa chama, alisema vijana wanashinda kwenye mitandao kugombanisha viongozi, kwa vyovyote vile Zitto alisema hivi huku akizingatia mambo yanayofanywa na baadhi ya vijana kwenye mitandao. Hili la Mwigamba ni matokeo ya CHADEMA kushindwa kuwadhibiti baadhi ya vijana wa CHADEMA wanaotumia mitandao kukichafua chama na inaonekana mwindelezo tu wa tabia za watu kudhani kuwa CHADEMA iko kwenye mitandao ingawa kiukweli CHADEMA iko kwenye mioyo ya wananchi.

HITIMISHO:
Mara nyingi tunaambiwa wagawe kisha watawale. CCM inafanya kila hali kuhakikisha Viongozi wa CHADEMA na wanachama wao wanakuwa wanagawanyika ili wapate kutushinda na kututawala kwa muda mrefu watakavyo. Tunavyowakosoa viongozi wetu hadharani, kwa vyovyote vile CCM watajifanya kama vile wanaunga mkono ule upande unaokosolewa, lengo la kufanya hivyo ili wale wanaokosoa waone wale wanaowakosoa kuwa ni wasaliti kisa tu wanaungwa mkono na CCM. Hivyo sitoshangaa kuona CCM wakimuunga mkono Mwigamba kama vile wanavyojifanya wanamuunga mkono Zitto.

Hitimisho langu linalenga kwa sisi wanaCHADEMA tulio nje ya vikao vikubwa vya maamuzi, tuwaunge mkono viongozi wetu wote, kukiwa na ulazima wa kuwakosoa, basi tufanye hivyo kwa kuzingatia hoja na kwa kufuata utaratibu(kinyume chake vurugu na usaliti); kwa kufanya hivyo tutaweza kujadili hoja kwa kuzingatia maudhui ya hoja yenyewe na si kwa kuzingatia wasifu wa mtoa hoja ambao hausiani na hoja yake(upo wasifu wa mtoa hoja wenye kuhusiana na hoja yake) lakini kubwa tutaweza kujitoa kwenye ulimwengu wa macho ya nazi na ushabiki wa kichamchunga.

Hitimisho langu linalenga kutukumbusha kuwa hakuna wakati ambao CHADEMA yahitaji mshikamano na utangamano kama wakati wa sasa; wakati ambao CCM imeshagundua iko chumba cha wagonjwa mahututi na inajiandaa kisaikolojia kwa kushindwa uchaguzi ujao(Rejea hotuba ya Kikwete aliyoitoa tar 24 mjini Dodoma). Ili tuwe na mshikamano na huo utengamano ni lazima viongozi wakuu wa chama wakaonesha njia na kuwadhihirishia umma kuwa wao ni wamoja na hakuna matatizo miongoni mwao na wawatake watu wasiamini kuwa wao viongozi wakuu na migogoro kama watu wanaoshinda kwenye mitandao wanavyojaribu kuaminisha umma kuwa CHADEMA iko na migogoro. Tusipofanya hivyo, CCM itajiandaa kisaikolojia kwa kupokea ushindi badala ya kujindaa kupokea kipigo toka kwa CHADEMA.


Hitimisho langu linalenga kuwa si kila mwanaCHADEMA anayeikosoa CHADEMA na viongozi wake ni msaliti na katumwa na CCM hata kama huyo mkosoaji anaungwa mkono na CCM(Zingatia sababu za CCM kuwaunga mkono wakosoaji wa CHADEMA waliomo ndani ya CHADEMA), bali ifike mahala tukubali kuwa chama kimekua kikubwa na kina watu wengi na kila mmoja wetu yuko na uwezo wake wa kufikiri na kuyatazama mambo, kwa kuzingatia hilo, ni sahihi msimamo yetu na maoni yetu kutofautiana kama vile uwezo wa kufikiri kwetu unavyotafautiana. Ni hivi, lile ambalo waliona "sahihi" kwa uwezo wako wa kufikiri na mwingine kwa uwezo huo huo anaweza kuliona "si sahihi" kwa hivyo kuheshimiana, kusikilizana na kufuata mawazo ya wengi yaliyozingatia hoja za wachache ndio kila kitu katika maisha ya seti kuu iitwayo chama cha siasa, kinyume chake ni vurugu kama si udikteta uliodhahiri.

Hitimisho langu lanalenga kutoa waasa kwa vijana, kwa kuanzia mimi niliyeandika haya na kwa wenzangu wote, tusimamie misingi ya chama na tujenge hiyo misingi kwenye mioyo yetu, tuwe wanachama wa kumaanisha na si wanachama kadi au vumbi. Wanachama wa CHADEMA wa kumaanisha ni wale ambao hata kama Dr.Slaa akirudi CCM wao wataendelea kuwa CHADEMA, haturajii kwa mwanachama wa kumaanisha kuingia CCM kisa tu Zitto Kabwe kajiunga na CCM. Mwanachama aliye na msingi wa CHADEMA katika moyo wake hawezi kuwakosoa viongozi wake kinyume na taratibu na katu hawezi kuwatetea viongozi wake wabadhirifu kisa tu yuko na mahaba na hao viongozi.

BILA CHADEMA IMARA MAFISADI WATATAMBA MCHANA WA JUA UTOSI.

MIMI NA WEWE TUIFANYE KUWA IMARA.


MwanaCHADEMA.
SIHASA HIZI?
 
Mh Mbowe karibu saana ktk jukwaa hili,wengine mara nyingi tunapenda kusoma michango na mada mbalimbali za wanajukwaa,Nakupongeza kwa kujiunga humu karibu sana kinacho mata humu ni hoja ya mhusika mwenyewe na si jina lake
 
Raisi wa 32 wa marekani FDR kwa utafiti wangu ndie mwanasiasa aliyeutambulisha msemo huu maarufu fear fear itself kwenye ulimwengu wa siasa na tangia hapo umevuka boda na kusambaa kwenye tansia zote,mabara yote,nchi zote adi jana pale Protea Hotel mh Nape alipoendeleza kusambaza alichokisema FDR march 1933.What's fear?
According to cambridge english dictionary fear is an unpleasant emotion or thought that you have when you are frightened or worried by something dangerous, painful, or bad that is happening or might happen.Tangu awamu ya 5 ichukue hatamu wapinzani wamekuwa wakisisitiza kuwa kuna uoga/hofu ndani na nje ya serikali,Lissu,Msigwa,Lema,Zito, Mbowe kama vinara na Bashe kwa mbali.
Baada ya uvamizi wa CMG,wakemea uoga/hofu wamepaza sauti sana na Bashe sio kwa mbali tena na sio tena wanasiasa tu kwani adi Ruge wakati anahojiwa alikemea uoga na kusisitiza vijana wa TZ tusiwe waoga hasa katika kuhoji na kutetea haki zetu,jana emotional Nape kakemea uoga baada ya kutengulia uwaziri.
Najiluliza hivi hapa muoga ni nani? na ni uoga kweli au vijana hawako aware na kinachoendelea, sio kila mtu huku mtaani anayaona mambo kama wanasiasa wanavyoyaona na kuna wengine hawajui waanzie wapi,kwa nini wasitoe suluhisho badala ya kuhoji uoga/hofu iliyotanda kama ipo.
 
Bado natafakari maneno ya Nape-
"nchi haiwezi kuendeshwa na maamuzi ya watu wachache waliojufungia huko" (hawa watu ni akina nani?ni kweli sizonje hataki ushauri?je ni kweli siku ile ya movie walikuwa wote?wale askari wa kikosi maalum cha ulinzi alikabidhiwa na nani?)
 
Back
Top Bottom