Ole wenu nyie viongozi wa Dini, Maaskofu, Mapadre na Wachungaji na wale wa ngazi za chini yenu, kwa kutopaza sauti zaidi na zaidi kupinga UDHALIMU katika Nchi yetu.
Kristo mnayemhubiri alipinga udhalimu kwa nguvu zote kutoka kwa watawala wa wakati ule. Alifanya hivyo mchana kweupe, jicho kwa jicho, uso kwa uso bila kupumzika siku zote kutwa nzima.
Wengi wenu mnaogopa kupaza sauti, wengine mmekuwa sehemu ya wadhalimu. Ole wenu. Kama UDHALIMU unaendelea mlipaswa kuendelea kupiga kelele popote pale mnapokuwepo tena pigeni kelele bila kuchoka.
Kuna haja gani ya kuhubiri mambo ya kwenye Biblia tena ni mambo yaliyopita huku tukiacha kuhubiri mambo yanayowasibu waumini wetu kwa wakati huu?
Lipi jema, uhubiri habari za Mtume Paulo au uhubiri habari za Mwumini wako anayekabiliwa na changamoto zinazosababishwa na ukengeufu wa viongozi wetu?
Mimi nadhani bado tuna nafasi. Tutumie muda na pumzi tuliyopewa na Mungu kuwapigania kondoo wetu tuliokabidhiwa na Mungu kuwachunga ili wasikamatwe na MBWAMWITU.
Kukaa kimya bila kuwatetea kondoo wanapokamatwa na MBWAMWITU wewe ni sehemu ya hao MBWAMWITU.