Kuna watu wameongea issues za muhimu hapo juu.
Kama serikali haitavunja mkataba wake na Celtel, haya yote ni vichekesho tu. Sasktel walijitahidi sana kwa miaka miwili kutafuta mikopo toka kwenye mabenki. Ugomvi wa serikali na Celtel umewafanye waonekane si mali kitu, kwani wabia hao walishindwa kuwadhamini.
Celtel wanashika handbreak kuhakikisha kwamba TTCL haikopesheni kwa namna yoyote ile.
Tatizo jingine la TTCL ni aina ya wafanyakazi waliopo. Wapo vijana wasomi wazuri tu waliajiriwa kwa mikataba ya muda mfupi, halafu wapo shikamoo jazz wanaosema walikuwapo tangu enzi za East African Community! Matokeo yake ujima ni mwingi kuliko vitendo
Mpingo1,
Muhimu kwa sasa kwa TTCL ni kuandaa strategy mpya ya kukabilia na competition na pia kulitumikia taifa letu katika karne ya 21. Ni ngumu sana kupambana na hizi mobile companies kwenye voice market maana capital inayotakiwa huko sio kubwa sana hivyo threat of new entrants (Porter five forces) ni kubwa sana. Ndio maana kila siku makampuni mapya yanajitokeza.
Watanzania wanataka internet services kwa maana ya broadband ambayo ina speed ya kutosha kuweza kufanya shughuli zote za uzalishaji. Hili ndilo tatizo la Tanzania na mobile companies hawawezi ku provide speed and bandwidth required for 21st century ICT services. Wakitaka kufanya hivyo watahitaji network kubwa zaidi nje ya mtandao wao.
Binafsi naona hapa ndipo penye soko; kwanza soko la moja kwa moja kwa mlaji ( end user) na pia soko la jumla (whole sale market). Soko la jumla nina maana makampuni kama ya mobile yatataka customers wao ambao hawana landline au cables au fibres kwenye nyumba zao watumie huduma zao kupatia reliable ICT services.
Technology kwasasa ipo (kwa mfano fibre to home or business FTTX), kinachotakiwa ni strategy kwanza na pili uwezo wa ku raise fund kwa ajili ya kutengeneza network kama hiyo. Ni muhimu kuanza kidogo kidogo kwa kuunganisha makampuni ya binafsi na ofisi za serikali ili hao wafanyakazi waonje matunda ya internet ya kisasa na wakirudi nyumbani watataka wawe na speed kama hiyo hiyo.
Nikiwa TZ nikitaka kufungua internet inakuwa kasheshe, jamaa yangu huwa ananiambia hapo kwao ndio speed kubwa lakini hata kufungua website ya kawaida tu inakuwa kasheshe. Niko convinced mobile companies TZ hawana uwezo wa ku compete na TTCL kwenye hiyo area kama TTCL kweli wataamua.
Waachane na kupoteza muda wao kwenye PSTN maana wakifanikiwa kuwa na broadband ya kisasa hata hiyo voice (VOIP) itakuwa included tena at a very affordable price. Pia ni kupoteza muda kuanza kuhangaika kuanzisha kampuni nyingine ya mobile maana watakutana na competition kubwa na ili kupata customers itabidi watumie pesa nyingi sana kwa kupunguza bei au matangazo. Wakifanikiwa kutengeneza a reliable broadband network, hapo ndipo wanaweza kuingiza na mobile ambayo itakuwa inatumia network hiyo hiyo ya broadband. Pia network hiyo hiyo inaweza kutumika kutoa services za TV kwa mfano IPTV or on demand television au wanaweza kuform partnership na TBC au kampuni nyingine ya utangazaji na kuanza kutoa huduma bora za on demand television.
Kuna mambo mengi sana ambayo TTCL wanaweza kufanya. Aliyesema opportunities favour prepared minds hakukosea; innovation yoyote inakuja kwasababu kuna mambo mawili; kwanza kuna demand ambayo watu wa kawaida hawajui kwamba kuna njia zingine zinaweza kutumika ku satisfy hiyo demand na pili kuna watu ambao wanaweza kuliangalia jambo nje ya their comfort zone (inventors) na wakaweza kuja na solutions mbalimbali. Kwa mfano TZ kila siku viongozi wetu wako kwenye motion huku na huku kuhudhuria mikutano; je ni kweli ni muhimu wao kuwa pale physically? Je TTCL wakiamua kuwa na centers zao zenye video conference facilities, bado hao watu watataka wawepo pale physically? Kwa mfano sasa kuna bunge Dodoma, je hao watendaji wote wa wizara husika, wanahitaji kuwepo pale Dodoma? Ukiwa na reliable ICT service unaweza kuanza kufikiri mabadiliko kama haya ambayo sio tu yanaokoa muda lakini pia yanaokoa pesa.
TTCL imepoteza muda mwingi kwenye migogoro, labda hii ni nafasi ya kuanza upya na kufanya yale ambayo wengine tumekuwa tukiwashauri au kuwaombea wafanye. Huko nyuma nilikuwa na mawasiliano ya karibu na baadhi ya watendaji wa TTCL wakati wa CEO Mkumba na niliweza kuwashauri kwenye mambo mengi. Japo walikuwa slow lakini walikuwa wanaelewa na happy kutaka kujifunza. Walipokuja Wacanada hao jamaa wakawekwa pembeni.
Hata leo mimi niko tayari kabisa kuwashauri TTCL tena bure ili mradi kama hainichukulii muda wangu mwingi (sina uwezo wa kutumikia mabwana wawili). Aidha kuna Watanzania wengi sana kwenye telecom nje ya nchi; watumieni watu kama hao kwa ushauri na wengi ninaowajua mimi wanaweza kuishauri serikali au TTCL bila hata kuhitaji kulipwa senti tano.