Madame S
JF-Expert Member
- Mar 4, 2015
- 17,187
- 34,498
RIWAYA…..THE MAGIC RING ( 01 )
MTUNZI….. HUSSEIN O. MOLITO
TRANSLATION….. GIFT KIPAPA
Upepo mkali ulioambatana na radi huku rangi ya mawingu ikizidi kuwa nyeusi . muwako na muungurumo mkali unasababisha maporomoko ya mawe yatokayo mlimani na kudondoka kwa kasi chini yalizidi kutetemesha mlima huo.
Juu ya mlima huo kulikua na viumbe wawili waliokua wakirumbana na kutoleana maneno kwa ukali. Ilisikika sauti ya kike na kiume huku kila mmoja wao akiwa hataki kuwa chini ya mwenzake. Marumbano hayo yaliishia baada ya msichana kutoa pete yake na kumrushia mwanaume ambaye hakuijali zaidi aliiacha tu hiyo pete ianze kubiringita kwa kasi kuelekea chini ya mlima.
Baada ya tukio hilo, Yule mvulana alibadilika na kua kama popo mkubwa na kupaa angani kwa kasi. Haikuchukua muda mrefu, na Yule msichana alibadilika na kuwa jamii hiyo hiyo ya popo mkubwa na kupaa angani kwa kuelekea upande wake.
Utengano huo wa majini waliokua wapenzi kwa muda mrefu na wakiwa katika hatua za mwisho kufunga ndoa,ulikua gumzo kwa jamii yote ya majini aina yao.
Hiyo ilikua na mara ya kwanza kutokea katika historia za majini ambao daima hua waaminifu na hua hawaachani mpaka kifo kinapo watenganisha.
Taarifa za ugomvi huo zilifika kwa mkuu wa majini na kuwaita kwa ajili ya usuluhishi, ila jini la kiume liligoma kuripoti hivyo zoezi hilo likafeli.
Uzito wa mahaba ya jini la kiume ulianza kuonekana baada ya kutengana kwa muda wa wiki moja tu. Jini la kike lilishindwa kula wala kupata usingizi mzuri. Alishindwa hata kuyafurahia maisha japokua alikua na uwezo wa kutembea ardhini na kupaa angani pasipo mipaka. Mateso ya moyo yaliyo muonyesha udhaifu wake juu ya mwanaume huyo aliyeziteka hisia zake, ndizo zilizomshawishi awe mpole na kukubali makosa yake.
***********************************
Baada ya jogoo la kwanza kuwika, niliamka huku nikifungua dirisha ili kuhakikisha kama kweli kulikua kumekucha. Niliindea ndoo yangu ya maji na kukuta imebaki nusu ndoo kutokana na kuoga nusu ya maji yaliyokua humo kwenye hiyo ndoo jana yake usiku nilipokua nimerudi kutoka kwenye mahangaiko yangu.
Muwako wa simu yangu ambayo mlio wake ulikua mdogo sana, ndio ulionifanya niichukue haraka na kuangalia kibox kilichoashiria kua message ilikua imeingia. Kabla sijaifungua hiyo sms, mtu aliyenitumia hiyo sms alinipigia simu. Nilipokea haraka sana kwakua siku zote huyo mtu hua hanipigii simu kama hakuna dili ya maana ambayo tunaweza kufanya.
“uko wapi we boya.” Alinisalimia salamu ambayo haikuniumiza. Japokua kama mtu mwengine akiniita hivyo naweza kugombana nae kama si kushikana nae kutokana na kutolipenda jina hilo.
“nipo geto joh” niliitikia huku kidole changu nikikielekeza sehemu iliyoandikwa LOUD ili mradi niweze kumsikia kutokana na udogo wa sauti ya simu yangu.
“njoo Tabata bima muda huu… kuna mzigo tunatakiwa tuupeleke Morogoro.” Aliongea na kunifanya niitikie haraka bila kuuliza ni mzigo gani huo.
“sawa mkuu.” Niliitikia na kuchukua shati langu na kuanza kuvaa haraka huku simu nikiwa nimeishikilia mkononi.
“chukua boda boda , hela yake nitampa huku huku.” Aliniambia hivyo ili nijue ni jinsi gani alivyokua na haraka.
“nimekuelewa mkuu.” Nilijibu hayo maneno na simu yangu ikakatika.
Nilighairi kuoga, nilivaa suruali yangu haraka na kuufunga mlango wa chumba changu na haraka nikawahi kituoni ambapo nilichukua pikipiki fasta na kumuelekeza ni wapi ambapo tunatakiwa twende.
Baada ya kufika, hakukua na story zaidi ya kuingia kwenye gari kubwa lililokua na shehena ya mzigo ambao hata mimi sikua naujua wa nini na wala sikutamani kuhoji.
“tutakunywa cha kibaha dogo.. naona mdmo umekukauka.” Aliongea BOSCO na mimi sikujibu chochote. Aliwasha gari na safari ilianza hapo. Kwakua nilikua namuamini bosi wangu hyo,wala sikuulizia maswala ya mshiko, ila nilijua tu mshiko nitakaupiga siku hiyo, nitaweza kulipia hata chumba ninachodaiwa kwa mwezi mmoja sasa.
Gari ilipamba moto huku gesi ya gari hiyo ikiendelea kulalamika. Mafuta yaliendelea kuchomeka na kusababisha matokeo ya spidi ya gari kuwa kubwa huku muendeshaji akitikisa kichwa kutokana na mziki uliokua unalia humo ndani.
“kama bado una usingizi, lala huko nyuma.” Aliongea Bosco huku akitabasamu.
“niko poa tu.” nlijibu huku nikiwa na hofu kidogo ya usalama wangu kutokana na uendeshaji mbaya wa gari aliokua nao Bosco.
Tulifka kibaha na tukapaki gari na kuingia kwenye mgahawa mmoja mkubwa.
“kula kama mwanaume ambaye anatarajia kushusha mzigo wa tani tatu peke yake. Sasa we agiza chapati mbili halafu uniambie eti huna spidi ya kazi.” Alinitania na kumuita muhudumu ambaye alikuja kutusikiliza.
Kwakua aliniruhsu mwenyewe, wala sikufanya hiyana, niliagiza msosi wa nguvu bila kujali gharama yake na kumfanya Bosco atabasamu.
“yeah… mi nataka majembe ya kula na kufanya kazi pia.. kama wewe Deo.” Aliongea maneno hayo huku na yeye akikandamiza supu ya mguu wa mbuzi uliolala pale mbele huku seheni nyingine ikiwa imejaa chapati takribani tano.
Baada ya kupiga msosi huo, tuliingia kwenye gari na kuanza safari kwa mwendo kasi zaidi wa ule wa mwanzo kutokana na kutokua na foleni wala msongamano wa magari ya hapa na pale.
Sikua napajua ni maeneo gani, ila kulikua na milima mirefu na juu ya milima hiyo ilikua kama inafuka moshi kutokana na baridi na hali ya hewa iliyokua huko juu.
Sehemu hiyo ndipo gari yetu ilipopata hitilafu na kulazimika tupaki pembeni kwa ajili ya msaada kutoka kwa mafundi ambao tumeshawapigia simu.
“ushenzi gani huu… mi nilitaka tufike leo leo na tugeuze leo hii hii ili tuje kula gambe dar usiku. Ila usijali mdogo wangu, lazima watulipe muda wote tutakao upoteza huko.” Aliongea Bosco na kuonyesha ni jinsi gani alikua amekasirika.
Baada ya muda kama wa nusu saa hivi, kila mtu alichoka na kujikuta tunatamani kunyoosha nyoosha miguu. Mimi nilitembe kwa mwendo wa kama mita hamsini hivi, ndipo nilipoona kitu kinang`aa na baadae muwako wake ukazima. Nilishawishika kujua kilikua na kitu gani huko. Nikakisogelea na nilipoyatuliza macho yangu, niliiona pete nzuri iliyokua na chata ya sura ya kinyago Fulani hivi.
Kwenye macho yake kulikua na vitu kama vichupa ambavyo mimi nilihisi itakua ni almasi. Niliokota haraka na kuiingiza mfukoni kwangu.
Niliporudi, nilimkuta Bosco akijarbu kuwasha tena gari. Nilipofika tu, gari ikakubali kuwaka na tukaendelea na safari………..
Tulifika morogoro na kuingia kwenye duka moja kubwa la nafaka. Nilishuka na kwenda nyuma ya hilo gari. Nilifungua turubai na kuuona mzigo mkubwa wa nafaka ukiwa umepangwa vizuri kwenye magunia.
“sasa wewe kazi yako ni kuwahesabia tu hawa maboya watakaokuja kubeba. Wacha mimi nikapate mambo yangu. Hakikisha wanashusha magunia mia mbili tu. Ishirini yabaki humo humo.” Aliongea Bosco na kunifanya kuikubali hiyo kazi.
Walishusha mizigo na baada ya hesabu kutimia, nilimpigia Bosco simu na nusu saa baadae alikuja huku macho yake yakiwa yameshabadilika. Alinuka pombe na muda huo alikua na chupa ya bia mkononi.
Tulienda hadi kwenye hilo duka na kukabithiwa hela.
“zihesabu kama zimetimia.” Aliniambia na mimi nikafanya hivyo.
“zimetimia bosi.” Nilimjibu baada ya kumaliza kuzihesabu zile hela.
“sawa, tuondoke kabla hawa wachawi hawajatuteka.” Aliongea na kuwafanya watu waliomsikia kuanza kucheka.
“wewe unaweza kuendesha kidogo?” aliniuliza baada ya kuingia kwenye gari.
“naweza lakini sijawahi kuendesha gari kubwa.” Niliitikia kiuoga.
“liwe kubwa liwe dogo, gari gari tu. Kama unajua kuendesha dogo basi hili halitakushinda. Maana najiona kama nitalitupa hili gari.” Alongea na kunipisha mimi kwenye kiti cha dereva.
Kwakua gari ilishawaka, alinielekeza jinsi ya kutia gia na kupangua. Baada ya kukariri, nilianza kulitaoa gari taratibu huku majasho yakiwa yananitoka.
“tunaelekea wapi?” niliuliza baada ya kuona uelekeo tuliokua tunaelekea ulikua wa kuendelea mbele na si kurudi Dar.
“kwenye duka la mpemba. Hii mifuko iliyobaki ndio cha juu chetu.” Aliongea Bosco na kunifanya nitulie. Maana kwenye hiyo mifuko ishirini niliamini sitakosa hata laki tatu nje ya posho yangu.
Nilifanikiwa kufika dukani kwa mpemba. Baada ya kuishusha mizigo na kuchukua chetu, tulienda hotel ya karibu na kuchukua chumba kwa ajili kulala.
“fedha zote utalala nazo wewe, maana mimi sijielewi muda huu.” Aliniambie na kunikabidhi zile hela.
Zilikua nyingi sana. Ila nilizichukua na kulala nazo huku mawazo yangu yakikinzana usiku kucha. Kuna wakati niliwaza kukimbia nazo, ila kwakua sikua napenda maisha ya mashaka na kukimbizana na askari, nikaona bora nitulie tu kama mjinga.
Asubuhi alikuja Bosco chumbani kwangu nilipolala na tukaelekea bar kunywa supu. Baada ya hapo, mida ya saa tatu asubuhi, tulianza safari ya kurudi Dar huku yeye akiwa ndio dereva baada ya kuwa fresh.
Tulifika Dar mishale ya saa tisa alasiri. Tulienda kupaki gari na kukabidhi hesabu. Baada ya kugaiwa chetu, alinifuata na kunipa shilingilaki tano.
“najua kwa mtoto kama wewe zinakutosha hizo kwa kugongea mademu. Maana nawajua nyie mkizikamata.” Aliongea na kunifanya nicheke.
Nilifurahi sana baada ya kuzichanganya na laki moja na nusu ambayo ilikua ujira wangu wa ile safari kama tani boy.
Nilirudi numbani na laki sita na nusu. Nilifurahi na kuzimwaga geto. Nikawaza nini nifanye ili kukibadilisha chumba changu ili kivutie. Cha kwanza kabisa nikaona ni bora niondokane na adha ya kulala kwa shida. Nikaamua kuleta kitanda na godoro lake.
“kila kitu kinahitaji uzindizi…. Na hivi nizindue na nanii?” niliwaza baada ya kufunga kitanda change na kutandika shuka jipya lililokubali vizuri na kuonekana thamani ya chumba changu kupanda ghafla.
Nilichukua simu yangu na kutafuta jina lililoandikwa Martha na kupiga.
“helloo.” Niliongea huku nikitabasamu baada ya kuweka loud speaker.
“niambie.” Aliitikia bila kuonyesha kuifurahia kuipokea simu yangu.
“safi tu wangu, umenisusa?” niliongea huku nikiwa nimekaa kwenye kiti huku nikikangalia kitanda changu kilichopendeza kutokana na upya wake.
“sijakususa wangu, mambo mengi.”
“njoo basi home.” Niliongea na kusikilizia jibu lake.
“sasa hivi nataka niende kwa mjomba adamu ili anipe hela ya kusuka. Na baadae siwezi kuja huko usafiri ni shida.” Aliongea bila kujua kua muda huo nilikua nimejaa kimtindo.
“chukua boda boda mpaka huku mi nitalipa na hela ya kusuka nitakupa pia.” Niliongea na kumfanya Martha acheke.
“usichekeshe walionuna babu wee, kama kweli unaweza kufanya hivyo nitumie kwanza elfu tano.” Aliongea na kuonyesha wazi kua alikua ananipima imani.
“subiri nikutumie.” Niliongea na kukata simu. Niliingia kwenye menyu ya tigo pesa na kumtumia shilingi elfu kumi. Haikupita hata dakika, simu yangu ikaanza kuita huku jina lililosomeka kwenye screen ikiwa ni Martha.
“niambie wangu.” Niliitikia kinyonge.
“thenks baby,… hivi hii ulionitumia ndio ya bajaji au utamlipa huko?” aliuliza huku akionekana akiwa na furaha zaidi ya mwanzo.
“hiyo nime test tu kama nikituma hela inaruka.. ukinifurahisha leo utapata hata kumi kama hizo.” Niliongea huku nikiwa najiamin na kitu niongeacho.
“nakuja sasa hivi baby.. mmmmwwwwaaaah” aliongea na kunibusu busu ambalo toka nimeanza kuwa nae hakuwahi kunibusu kama hivyo.
Baada ya dakika ishirini, nilisikia mlio wa bajaji ikiwa nje ya dirisha langu, nilitoka na kumlipa Yule dereva hela aliyotaja bila kubishana nae.
Tuliingia ndani huku nikimuacha akishika mdomo baada ya kuona kitanda na godoro vikiwa vinameremeta pale kwangu.
“kweli mpenzi wangu umekua.” Aliongea hayo maneno na kujitupa kitandani.
Hatukuongea maneno mengi baada a mimi kupanda kitandani zaidi ya kuanza kumpapasa na kuanza kula vyangu alivyokua ananibania muda mrefu.
Baada ya kumaliza, niliiendea suruali yangu na kutoa waleti mpya niliyoinunua. Hapo ndipo ile pete ikadondoka chini na kuelekea upande aliokua Martha.
Martha aliiokota na kuivaa.
“pete nzuri sana hii, umeinunu shilingi ngapi?” aliniuliza Martha na kunifanya nishindwe kumuambia ukweli.
“nimeinunua hela nyingi sana , naomba tu unipe pete yangu.”
Niliomba pete lakini Martha hakua tayari kunipa. Baada ya kumlazimisha sana anipe na kuona kua alikua ameamua kuing’ang’ania sana, niliamua kumuachia huku moyo wangu ukiwa haujaridhika Martha kuondoka na pete yangu niliyoiokota mbali.
ITAENDELEA