Kuna aina ya watu, nashindwa jina gani zuri la kuwapa. Naomba mnisamehe, ila ili kukipa maana hiki ninachokiandika hapa, nitawaita Wajinga au Wapumbavu.
Aina hii ya watu ni wale ambao either hawajasoma kabisa au wana elimu ya msingi na wapo very little informed kuhusu mambo yanavyoendelea Tanzania na duniani!
Ninachokipenda kwa watu hawa, wana furaha muda wote! Yaani utawakuta wanatabasamu na kucheka all the time, hawana stress kabisa mioyoni mwao na ikifika usiku wanalala kwa amani kabisa.
Kadiri unavyojiongezea maarifa, unavyojua mengi zaidi na kuwa well informed kuhusu kila kitu kinachoendelea, huzuni moyoni inaongezeka. Inaongezeka kiasi kwamba moyo unakuuma mchana na usiku hulali kwa raha.
Kadiri unavyozidi kujua zaidi, unapata maswali mengi zaidi yasiyo na majibu!
Ule mstari unaosema "Kwenye wingi wa maarifa kuna wingi wa huzuni, na yeyote ajiongezeaye maarifa anajiongezea huzuni" ni wa kweli kabisa. Na leo nimejua kwamba, the less you know, the happier you are!
Bora niwe mjinga kwa kweli, nimevurugika na huu mchakato wa uchaguzi! Nahisi nitapasuka.