The Law School of Tanzania: Maoni, Ushauri, Dukuduku

L

LENDEYSON

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2013
Messages
2,944
Points
2,000
L

LENDEYSON

JF-Expert Member
Joined Sep 27, 2013
2,944 2,000
Hii ni Shule ya Muhimu sana katika Sekta ya Sheria. Hata hivyo, Shule hii haijawahi kupewa Umuhimu unaostahili katika Jukwaa hili. Ni katika muktadha huo, kumeonekana umuhimu wa Shule hii kupata Fursa hapa Jukwaani, ikiwezekana kupewa maoni,ushauri, ili kuiboresha shule hii. Karibuni Wadau
 
Dragoon

Dragoon

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2013
Messages
7,075
Points
2,000
Dragoon

Dragoon

JF-Expert Member
Joined Nov 24, 2013
7,075 2,000

Hii shule ilifunguliwa kabla haijapevuka. hadi sasa bado haijapevuka. Kabla ya hii shule mtu akitaka kuwa wakili ilimlazimu aende internship. Mawakili wa internship ni wazuri zana. Mawakili waliopitia law school ni wabovu (sio wote tafadhali). kuna wengine wanatia aibu mahakamani hadi utawaonea huruma, hawajui chochote
 
L

LENDEYSON

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2013
Messages
2,944
Points
2,000
L

LENDEYSON

JF-Expert Member
Joined Sep 27, 2013
2,944 2,000
Hii shule ilifunguliwa kabla haijapevuka. hadi sasa bado haijapevuka. Kabla ya hii shule mtu akitaka kuwa wakili ilimlazimu aende internship. Mawakili wa internship ni wazuri zana. Mawakili waliopitia law school ni wabovu (sio wote tafadhali). kuna wengine wanatia aibu mahakamani hadi utawaonea huruma, hawajui chochote
Nakubaliana na wewe ingawa si kwa kiwango kikubwa. Nimeona Mawakili wengi wale wa Internship waki recommend kazi nzuri inayofanywa na vijana waliopita hapo. Kwa wanaoaibisha,tatizo ni shule au watu wenyewe?
Ni kweli pia naona Shule bado ipo kwenye Try n Error, sijui hadi lini. Maoni yako, nini kifanyike.
 
Dragoon

Dragoon

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2013
Messages
7,075
Points
2,000
Dragoon

Dragoon

JF-Expert Member
Joined Nov 24, 2013
7,075 2,000
Nakubaliana na wewe ingawa si kwa kiwango kikubwa. Nimeona Mawakili wengi wale wa Internship waki recommend kazi nzuri inayofanywa na vijana waliopita hapo. Kwa wanaoaibisha,tatizo ni shule au watu wenyewe?
Ni kweli pia naona Shule bado ipo kwenye Try n Error, sijui hadi lini. Maoni yako, nini kifanyike.
Nchi za wenzetu kila chuo kinachotoa shahada ya sheria kina shule yake ya sheria (law school). hata hapa tanzania kulikuwa na haja hiyo, tena ingerahisisha zaidi. mwanzo ungekuwa mgumu lakini hadi sasa hali ingekuwa imestabilise
 
M-bongotz

M-bongotz

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2010
Messages
1,734
Points
1,225
M-bongotz

M-bongotz

JF-Expert Member
Joined Jan 7, 2010
1,734 1,225
Kuna mapungufu makubwa kwenye sharia iliyoanzisha LST, kwanza muda wa mafunzo ni mfupi sana, muda huu hata ungerefushwa mfano kuwa mwaka mmoja na nusu kama Kenya bado isingetosha kuwafanya wahitimu kuwa mawakili wabobezi mara tu baada ya kuhitimu mafunzo yao. Tofauti na hapa kwetu, sehemu nyingi na mfano wa karibu ni hapo kwa jirani zetu Kenya, mhitimu wa Law School akumaliza bado ni lazima akae na wakili (pupilage) kwa kipindi Fulani kabla hajaruhusiwa kuanza practice, kwa Kenya ni miaka miwili. Walioandaa sharia hii wangeiga kinachofanyika kwenye fani nyingine mfano uhasibu ambapo mfano mtu aliyehitimu CPA hawezi kufanya Public Practice mpaka baada ya kipindi Fulani kupita ambapo katika kipindi hicho anakuwa anaendelea kujifunza toka kwa waliomtangulia.

Nakubaliana kabisa na hoja kwamba baadhi ya mawakili waliopitia LST hawapo kwenye viwango stahiki, hii kwa upande mmoja inasababishwa na nilichokieleza hapo juu lakini pia tukubali au kukataa kumekuwa na shida sana ya ubora wa mafunzo ya shahada ya kwanza ya sheria yanayotolewa na vyuo mbalimbali hapa nchini, hii inapelekea kuwepo kwa utofauti mkubwa wa uelewa wa wanafunzi, na kwa sasa kuna tabia kwamba waalimu wanaburuza tu wanafunzi na kuwaambia kuwa mtajifunza zaidi mkienda Law School bila kujali kwamba mtu anayesajiliwa Law School anapaswa kuwa na uelewa wa kutosha wa nadharia, na pasipo kuwa na msingi mzuri wa nadharia ni ngumu sana kujifunza kwa vitendo.

Natambua kwamba si wanafunzi wote wanaokwenda Law School of Tanzania wanakwenda kwa sababu wana malengo ya kupractice sheria, wengi wao wanakwenda kwa kuwa mfumo umewalazimisha kwenda huko, ingekuwa vyema Law School ingebaki tu kwa wale wanaotaka kufanya kazi ya uwakili wa kujitegemea au labda wanaoutazamia uwakili wa serikali na wengine wote wasingelazimishwa kwenda Law SChool.

Law School of Tanzania bado ipo katika changamoto za ukuaji, naamini kabisa baada ya muda Fulani changamoto hizi zitaoungua kama sio kwisha kabisa, ikumbukwe kuwa mpaka sasa ni takribani miaka 7 tu tangia ilipoanza kupokea wanafunzi, lakini kuna mengi mazuri yaliyofanyika ambayo yanapaswa kupongezwa. Ni rai yangu kuwa uzi huu utumike kuainisha changamoto zinazokabili Taasisi hii zaidi kuliko kutumika kama ubao wa kumalizia hasira za wale ambao kwa bahati mbaya hawajafanikiwa kumaliza mitihani yao.
 
Umenena vyema kabisa mkuu, sina cha kuongeza wala kupunguza
 
gwa myetu

gwa myetu

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2014
Messages
4,390
Points
2,000
gwa myetu

gwa myetu

JF-Expert Member
Joined Aug 18, 2014
4,390 2,000
Pia vyeti vya kuhitimu hawavitoi kwa wakati , kuna watu wameapishwa tangu mwaka Juzi June hadi leo hawana vyeti , wakienda wanaambiwa bado havijaandaliwa sijui tatizo nini?
 
rodney jr.

rodney jr.

Senior Member
Joined
Feb 12, 2014
Messages
143
Points
225
rodney jr.

rodney jr.

Senior Member
Joined Feb 12, 2014
143 225
Suala la muda nafikiri pia lizingatiwe....vitu ni vingi and should be handled ndani ya miezi 4
 
jaji mfawidhi

jaji mfawidhi

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Messages
5,542
Points
2,000
jaji mfawidhi

jaji mfawidhi

JF-Expert Member
Joined Feb 20, 2016
5,542 2,000
Law School imepokea maagizo toka juu ifaulishe wanafunzi 70 tu kwa cohort moja," ndoto tu naota"
 
joshydama

joshydama

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2016
Messages
3,557
Points
2,000
joshydama

joshydama

JF-Expert Member
Joined May 10, 2016
3,557 2,000
Hii shule ilifunguliwa kabla haijapevuka. hadi sasa bado haijapevuka. Kabla ya hii shule mtu akitaka kuwa wakili ilimlazimu aende internship. Mawakili wa internship ni wazuri zana. Mawakili waliopitia law school ni wabovu (sio wote tafadhali). kuna wengine wanatia aibu mahakamani hadi utawaonea huruma, hawajui chochote
Mkuu Dragoon,

Suala la kuwa wakili mzuri ni suala la mtu mwenyewe yani juhudi zako ndiyo zitakufanya uwe competent au uwe wakili mwenye uwezo wa chini.
 
jaji mfawidhi

jaji mfawidhi

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Messages
5,542
Points
2,000
jaji mfawidhi

jaji mfawidhi

JF-Expert Member
Joined Feb 20, 2016
5,542 2,000
Wateja mahakamani wanalalamikia sana mawakili waliosoma vyuo vya MIAKA MITATU ,tofauti na St .Augustine(RUCO)-Iringa & Udsm ambapo wanasoma MIAKA 4 na wapo vizuri upstairs!

Kwa mwenemdo huu hata ajira imekuwa hawapewi hawa wanafunzi wanaosoms miaka 3.

Ndalichako tuokoe na hivi vyuo vya miaka mitatu!
Take action madame,please rescue us,we humbly pray so!
 
Rai Pazzy

Rai Pazzy

JF-Expert Member
Joined
Jul 6, 2015
Messages
453
Points
250
Rai Pazzy

Rai Pazzy

JF-Expert Member
Joined Jul 6, 2015
453 250
Wateja mahakamani wanalalamikia sana mawakili waliosoma vyuo vya MIAKA MITATU ,tofauti na St .Augustine(RUCO)-Iringa & Udsm ambapo wanasoma MIAKA 4 na wapo vizuri upstairs!

Kwa mwenemdo huu hata ajira imekuwa hawapewi hawa wanafunzi wanaosoms miaka 3.

Ndalichako tuokoe na hivi vyuo vya miaka mitatu!
Take action madame,please rescue us,we humbly pray so!
Mwenye kitabu cha anson's law of contract katika soft copy anisaidie
 
cheguevara

cheguevara

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2012
Messages
1,131
Points
1,500
cheguevara

cheguevara

JF-Expert Member
Joined Apr 30, 2012
1,131 1,500
Swala siyo wingi wa miaka bali kukamilisha unit zinazotakiwa,kama unaweza kusoma unit zote kwa miaka miwili na ukagaulu haina shida,mbona shule za msingi wanarushwa madarasa na wanafaulu?
 
jaji mfawidhi

jaji mfawidhi

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Messages
5,542
Points
2,000
jaji mfawidhi

jaji mfawidhi

JF-Expert Member
Joined Feb 20, 2016
5,542 2,000
... UnaishI Gongo la mboto. Unaamka saa 11 alfajiri. Unapambana na foleni. Kesi (ya mteja wako) iko High Court. Imepangwa kusikilizwa saa 3 asbh. Unafika nusu saa kabla. Unapiga soga na mawakili "wasomi" kwenye corridor, huku kesi zikiendelea kuitwa....

.... saa 4. Kesi (ya mteja wako) bado haijaitwa. Unaendelea na soga, malumbano na majuzano ya sheria na kesi....

.... saa 5 asubuhi. Wenye kesi za madai kwa Mheshimiwa Jaji Kanyabayonga waende kwa msajili chumba nambari 65 kuahirisha kesi. Jaji Kanyabayonga yuko safarini. Amepata safari ya ghafla. Kesi (ya mteja wako) inaahirishwa kwa siku 14 mbele...

.... saa 6 mchana. Hukunywa hata chai. Unaanza safari ya kurejea ofisini kwako, mbali kidogo na katikati ya jiji. Safari inaanza...

.... mteja wako alikulipa tshs. 50, 000/= (fukara tu, hata kesi yake ni dhidi ya benki inayotaka kupiga mnada nyumba anayoishi baada ya kushindwa marejesho ya mkopo) apate uwakilishi. Huruhusiwi kumkataa eti kwa kuwa hana pesa. Cab rank rule. Justice for all...

.... Mawazo tele kichwani. Unafika mataa ya Selander bridge unavuka na taa ya njano ukiwahi ofisini. Afande anakusimamisha kwa shangwe na furaha kuu. Anakulima makosa 2: i. kutoheshimu alama halali (na taa) za barabarani, NA ii. kuzuia watumiaji wengine wa barabara. Unapigwa faini ya tshs. 60, 000/=. Huna hiyo pesa. Unaandikiwa "kifurushi cha wiki." na unapewa risiti ya kielektroniki. Ulipe ndani ya siku 7. Jua kali sana, unamwomba afande akusamehe lakini kumbe alishaingiza nambari ya gari na leseni yako kwenye kile kimashine kabla hata ya kuongea na wewe...

... unaondoka. Unawaza sana. Una njaa. Huna pesa. Ada kubwa za TLS zakusubiri. TRA, Manispaa, landlord wa ofisi na nyumba unayoishi nao pia. Wakili msomi.

Lakini umevaa suti. Na unaijua vyema sheria. Na unaamini kesho itakuwa afadhali ya jana na leo.
 
jaji mfawidhi

jaji mfawidhi

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Messages
5,542
Points
2,000
jaji mfawidhi

jaji mfawidhi

JF-Expert Member
Joined Feb 20, 2016
5,542 2,000
Wanafunzi wa Law school wanalia matokeo ya Cohort ya 19 hasa supp hayatoki,means wasubirie mpaka mwakani june.

Pia wanapinga ada ya dola 50 kwa EALS
 
soskeneth

soskeneth

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2016
Messages
583
Points
250
soskeneth

soskeneth

JF-Expert Member
Joined Jul 2, 2016
583 250
Jamaniii naomba tuanzishe na group la whatsapp kwa ajili ya msaada wa Kisheria tuu ukiafik weka no
 
cheguevara

cheguevara

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2012
Messages
1,131
Points
1,500
cheguevara

cheguevara

JF-Expert Member
Joined Apr 30, 2012
1,131 1,500
Kwanini mtu anasoma mwaka mmoja anakuja kuapishwa baada ya miaka 2 wakati kunauwezekano wa kumaliza law school na kuapishwa hapohapo?
 
Forum statistics

Threads 1,336,422
Members 512,614
Posts 32,538,950
Top